Jamaa Baada Ya Kuua, Akawa Mchungaji, Tazama Kilichotokea
Story Ya Kweli
Miili ya wanawake wawili ilikutwa ndani ya gari moja huko Ozark, Alabama. Ni wasichana wa umri chini ya miaka kumi na nane, JB Beasley na Tracie Hawlett.
Polisi waliichukua miili hiyo na haraka sana wakaamua kufanya uchunguzi, walihitaji kujua ni nani ambaye alihusika kwenye mauaji hayo.
Walihangaika kwa kipindi kirefu, hawakufanikiwa kumpata muuaji. Hawakuchoka, waliendelea kufanya uchunguzi wao.
Muuaji ni nani?
Alikuwa mwamba fulani wa kuitwa Colley McCranery. Huyu mchizi baada ya kufanya mauaji hayo, akaenda kusomea uchungaji, aliendelea na maisha yake kama kawaida na kufungua kanisa.
Kilichotokea?
Kwa miaka ishirini muuaji hakugundulika hivyo polisi kuamua kuchukua vinasaba ambavyo vilionyesha muuaji hakuingizwa kwenye database na kuvipeleka Parabon Nanolabs, hiyo ni kampuni ya kuchukua vinasaba iliyokuwa huko Reston, Virginia. Hawa majamaa wanaweza kubashiri muuaji ni nani kutokana na vitendo vyake, muonekano na mengineyo.
Kwenye uchunguzi wao, wakagundua muuaji alikuwa Colley ambaye wakati huo alikuwa mchungaji, polisi wakaenda na kumtia nguvuni.

