Mke Alimuua Mume Arithi Mali, Tazama Kilichotokea
Simulizi Ya Kweli
Mali zinaweza kubadilisha kila kitu, mbaya kuwa mzuri na hata mzuri kuwa mbaya, ndivyo inavyokuwa.
Baada ya kuona tayari mumewe ana utajiri wa dola milioni 3.6 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 10 za Kitanzania, mama wa watotowatatu Kouri Richins mwenye umri wa miaka 33 akaamua kumuua mume wake ili arithi mali.
Mume alifariki dunia, akawa na uhuru wa mali zote na mpaka kuamua kuandika kitabu cha watoto iizungumzia maumivu makubwa aliyokuwanayo moyoni mwake.
Sio poa.
Ila baada ya wiki kadhaa akafuatwa na polisi na kukamatwa kwa tuhuma za kumuua mumewe kwa kumuwekea sumu iitwayo fentanyl iliyotengenezwa nchini Urusi, waliongeza kwamba aliitumia sumu hiyo mara tatu kwenye kinywaji cha mumewe.
Stori haikuishia hapo ila kabla ya mumewe kufariki, mwanaume huyo aliwaambia ndugu zake hakuwa na amani na mkewe, inawezekana kabisa mwanamke huyo atamuua kutokana na pesa alizokuwanazo, hivyo kwa siri akahamisha umiliki wa pesa hizo na kumuweka dada yake kwamba ndiye atakayekuwa msimamizi wa kila kitu.
Japokuwa Kouri alimuua mumewe lakini bado hakupata kitu, mali na pesa zote za mumewe zilikwenda kwa dada yake.


1 Comment
Hey, you used to write great, but the last few posts have been kinda boring… I miss your tremendous writings. Past few posts are just a little bit out of track! come on!