𝗠𝗔𝗟𝗜𝗣𝗢 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Ep 22
Ilipita dakika kama tano hivi lakini Katarina hakuona mwenzake akirejea, sasa kwa namna alivyokuwa mbea, aliamua kushuka kitandanI na kutoka chumbani akaangalie Manka anafanya nini….alipofika sebuleni alimkuta Manka ameketi kwenye kochi anachezea simu yake, muda huo Manka alikuwa ni mwepesi haswa, maana alikuwa amekwanguliwa zote kwenye mwili wake.
Manka alijua kilichomleta pale binti ni unafiki mtupu, aliinua kichwa akamtazama Katarina akatabasamu kwa kujishtukia kisha akasema “Nimejiuliza umeenda wapi”
Manka hakumjibu, alitulia kimya, mpaka Katarina akaondoka kwa aibu na kurudi chumbani. Lakini moyoni alikuwa ashahisi kuna kitu kinaendelea kati ya Erick na Manka maana aliona kama vile kuna kujaliana kulikopita kiwango cha ushemeji. Erick alimaliza kuoga kwani yeye chumba chake na mkewe kilikuwa na bafu humo humo ndani
Manka naye aliinuka pale sebuleni akaenda bafuni akajiogesha haraka haraka na kurudi chumbani akajilaza, ule usingizi ulikuwa ni wa hatari, yaani mzito balaa.
Lakini vile vile, saa kumi na moja na nusu, Aneth aliamka na kumtazama mumewe ambaye alikuwa kando yake, tena wala hakujifunika alikuwa na boxer halafu kifua wazi, huku mtoto akiwa kando yao amesinzia pia.
Aneth alipomtazama mumewe alijisikia vibaya, ni mwezi umepita lakini mumewe hana mpango naye, hajawahi kumuomba penzi kabisa, alijua mumewe kapata mwanamke mwingine ndio maana anamfanyia vile.
Aneth alimchukua mtoto akamuweka kando, kisha yeye akalala katikati, na kumsogelea mumewe na kumshika kifuani akaanza kumpapasa.
Aneth nia yake alikuwa anataka kujua kama kweli bado mumewe anahisia naye. Binti aliuchukua mkono wake akaupeleka taratibu kwenye boxer ya mumewe akauingiza ndani, lakini mjomba alikuwa amelala doro.
Alimpapasa papasa, lakini kulingana na shoo ambayo Erick alikuwa amempa Manka, wala mjomba alikuwa hataki penzi kwa usiku ule. Aneth alipapasa kwa muda mrefu ndipo Erick akashtuka usingizini na kumtazama
“Mume wangu” Aneth aliita huku akijaribu kuilegeza sauti na macho.
Erick alimtazama usoni, akaona unafiki mkubwa, hasira zikamzidi na kujikutana anasonya na kugeukia upande wa pili akajikunyata kuendelea kuinjoy usingizi wake.
“Baba Chris” binti aliita kwa hasira tena
“Usinisumbue mimi nina usingizi” Erick alisema kwa jeuri
Aneth alimtikisa kwa nguvu huku akilalamika “Kwanini umebadilika hivi? Hivi ni maisha gani haya ambayo unaishi na mimi Erick? Nimekukosea nini? Kama una mwanamke mwingine si uniambie tu niachane na wewe?” alisema kwa hasira mtoto wa kike na kujaribu kumvamia ili aweze kumkumbatia lakini Erick alimtupa kule kwa hasira akamdondokea mtoto
“Acha ujinga….usiniguse sihitaji ukaribu na wewe, au unataka nihame hiki chumba nikalale kule sio?” aliuliza kijana yule
“Daaah Erick….mtoto wangu analia” alisema binti huku akijaribu kumtoa mtoto ambaye alishtuliwa na mama yake baada ya kumdondokea
“Msssssiiieeew” Erick alisonya kwa hasira kisha akashuka kitandani na kusimama akavaa suruali ya traki suti halafu akaenda zake mpaka sebuleni akajilaza katika kochi moja la watu watatu halafu akaanza kuutafuta usingizi wa alfajiri
Kule chumbani Aneth alimnyonyesha mtoto huku machozi yakimtiririka, alimlaumu sana mumewe, alimlaumu Mungu kwa kumpa mwanaume msaliti bila kujua yeye ndo chanzo cha matatizo.
*
Saa kumi na mbili kamili, Erick alirudi chumbani akamkuta mkewe ameshika tama ameketi kitandani huku akiwaza mambo kibao. Machozi yamemkaukia mashavuni, alikuwa anajutia.
Erick bila kujali alivaa nguo zake safi, fulana na suruali ya kadeti halafu raba nyekundu, akaondoka zake huku akimuacha njia panda mkewe.
Aneth alikaa pale kwa muda mrefu sana, alikuwa anawaza mambo mengi, alipanga nguo vizuri halafu akatoka mpaka sebuleni muda wa saa mbili asubuhi akamkuta Katarina akifuta futa meza sebuleni kwa kitambaa cha maji.
“Shikamoo” alisema Katarina
“Marahaba…umeamkaje?”
“Salama tu”
“Uji wa mtoto bado?” aliuliza mwanamke yule
“Upo jikoni dada”
“ Kwani Manka yuko wapi?” aliuliza Aneth
“Amelala”
“Amelala hadi saa hizi? Kakuachia kazi zote hizi?” aliuliza kwa hasira dada Aneth
“Ndio”
Aneth aliondoka pale, akaenda hadi katika chumba alichokuwa akilala Manka pamoja na Katarina, alipotazama kitandani Manka amelala fofofo amesinzia kabisa tena anakoroma kwa raha zake.
“We Janeth!!!!!” alifoka kwa hasira Aneth maana alikuwa ana mawazo yake tele yaliyokuwa yanapelekewa na ndoa yake kuwa na utata, lakini bado alikuwa hajajua mdogo wake huyo ndo mke mwenza na anahongwa pesa nyingi sana
Manka alishtuka usingizini na kumtazama dada yake kwa macho makali kwa sababu ya usingizi Aneth akafoka “Unalala lala nini mpaka saa sita??” alimuuliza kwa hasira
“Shikamoo dada” alisema binti
“Embu amka bwana ukasaidiane na mwenzako usafi we vipi?” aliuliza kwa hasira na kusonya halafu akatoka chumbani kule akaenda hadi jikoni
Aneth alipofika jikoni aliepua uji wa mtoto halafu akauweka upoe, ndipo akaenda chumbani akakuta simu yake inaita na alikuwa anapigiwa simu na Haidali, aliipokea
“Hallo”
Haidali akaanza kwa mbwembwe “Baby mbona nakupigia simu hupokei?”
Aneth akajibu “Samahani kuna mambo hayajakaa sawa”
“Sawa, kwanini hujafika kazini?”
“Nimeshakuambia Haidali kuna mambo hayajakaa sawa”
Haidali alipatwa na hasira akamfokea “kwa hiyo unalinganisha mambo yako na kazi zangu? Kama hutaki kuja useme atafutwe mtu mwingine”
Aneth alikata simu kwa hasira, yeye ana mawazo yake halafu Haidali anamletea mambo kibao. Alimbeba mtoto akaenda naye mpaka sebuleni akaketi bila kujua afanye kitu gani, ndipo akamuambia Katarina
“Katarina”
“Abee”
“Simuelewi baba Chris”
“Mh kwanini dada?”
“Amebadilika, wala hanijali, haachi tena pesa ya matumizi, sijui nimemkosea wapi” alisema dada Aneth
Katarina alikaa kimya, hayo ni mambo ya wakubwa yeye alikuwa hayawezi, aliendelea kupanga sebule, Aneth akaendelea kuongea “Ninahisi ana mwanamke mwingine, sijui kwanini lakini”
Katarina hakujibu chochote, lakini muda huo Manka alikuwa amesimama kwenye korido akiwa anasikiliza kile dada alichokuwa akikisema, alihisi anaenda kushtukiwa sasa. Alitoka kwa kujishtukia, mwizi ukimtazama tu usoni utamjua, hawezi kukuangalia kwa kujiamini.
“Shikamoo dada” alisema na kuketi
“Marahaba” alisema dada “kalete uji wa mtoto kule jikoni uje umnyweshe mtoto mi ninaenda kazini” alisema Aneth
“Sawa”
Manka aliinuka na kuondoka akaenda mpaka ndani ya jiko akarudi na uji wa mtoto kwenye kibakuli kidogo halafu akauweka chini naye akaketi chini kabisa kwenye zulia, ndipo akampokea mtoto na kuanza kumnywesha taratibu
Aneth alienda kujiandaa kisha akaondoka zake na kuondoka kuelekea kazini kwake. Siku ile hakwenda na gari yake, alichukua bodaboda mpaka kazini maana aliamini kwa msongo wa mawazo asingeweza kuendesha vizuri, hivyo ingeweza kupelekea kupata hata ajali
Alipofika kazini Haidali alikuja juu kwa kusema “Aneth……Aneth……Aneth” alikuwa akifoka huku akimnyooshea kidole lakini Aneth kwa jeuri wala hakujibu, alienda zake na kuketi huku akimtazama Jonas ambaye alikuwa anachezea compyuta mezani
“Unaniletea kiburi? Hujui hii ni kazi? Unajaribu kulinganisha kazi na mambo yako mengine? Unakuja kazini muda unaotaka, unataka uachishwe kazi?”
“Boss” alisema Aneth lakini Haidali alimtazama tu usoni akaanza kumuhurumia kwani ni zaidi ya mwaka wapo kwenye mahusiano na anampenda sana tu.
Haidali aliondoka bila kujibu chochote, akaingia ofisini kwake na kuketi kisha akawa anawaza mambo fulani fulani.
*
Kule upande wa nyumbani Manka alikuwa chumbani anaangalia angalia nguo zake, ndipo ghafla akakumbuka kwamba simu yake ameiacha sebuleni. Alitoka kama mshale, kufika akamkuta Katarina kaishika simu anachezea
“wewe” Manka alisema huku akimrukia kama samaki akampokonya simu yake
“Khee shoga” alisema Katarina kwa mshangao
“Usishike simu yangu”
“Mh makubwa” alisema Katarina huku akigonga mikono (makofi) kwa mshangao “Hata mimi nitanunua tu ya kwangu” alisema binti huyo kwa hasira lakini Manka alienda nayo chumbani akaketi na kufuta message zote alizokuwa amechati na shemeji yake bwana Erick
Haikuishia hapo, wakati baadaye wakipiga story Katarina alimuambia Manka “Unajua mama Chris anasema kwamba anahisi mume wake ana mwanamke mwingine?”
Manka akashtuka na kusema “Sasa mimi inanihusu nini? Watajua na ndoa yao mi sihusiki”
Katarina akavuta chungwa na kuanza kulimenya halafu akasema “Manka nahisi unatoka na shemeji yako” alisema maneno ambayo yalimshtua sana Manka maana aliogopa akijua siri imeshafichuka
EP 23
Manka alimtazama mwenzake kwa mshangao, Katarina anatabasamu huku anamenya taratibu chungwa “Mimi nitoke na shemeji yangu?? Mimi huyo mimi kabisa??” binti aliuliza kwa mfululizo maswali hayo
“Ndio wewe, hapo”
“No siwezi nikafanya huo upuuzi kabisa”
“Mh haya” alijibu Katarina, bado Manka hakujua Katarina kaona nini mpaka akaanza kumtilia mashaka kwamba anatoka na Erick
Hii ilikuwa ni kweli lakini Erick alikuwa anajaribu kujipa furaha kwa kutoka na shemeji yake baada tu ya mkewe kumsaliti, na alifanya hivi kama malipo maana wanawake ni wengi lakini aliamua kufanya na mdogo wa mke wake akiamini atafarijika kabisa.
Manka huku moyo ukimdunda aliondoka pale sebuleni akaenda moja kwa moja hadi chumbani ndipo akamtumia ujumbe Erick
“Mume wangu” hii ilikuwa ni message kutoka kwa Manka akimtumia shemeji yake
Erick akajibu “Niambie mke wangu”
“Ninaogopa”
Erick akamuuliza “Unaogopa nini mpenzi?”
“Katarina ameanza kunishtukia….ananiambia eti mi natoka na wewe”
“Mh amejuaje?”
“Sijui, ila kuna muda alishika simu yangu, sijui alikuta message”
“Duuh”
“Ndo hivyo mume wangu, mimi nataka kuondoka hapa nyumbani naogopa dada akijua itakuwaje”
“Basi sawa ngoja nitawahi leo tutaongea sawa?” alisema Erick
“Sawa, si unipangie chumba nikae?” aliuliza
“Tutafanya yote hayo, sasa utamuambiaje dada yako kwamba unaenda kupanga chumba?”
“Sijui hata”
“Basi nakuja”
Erick alikuwa ameshakolea kwenye penzi la shemeji yake, hakutaka jambo lingine kabisa, na huwezi amini, Erick alipompata Manka hukuwahi kulala na mwanamke mwingine, alikuwa muaminifu kwake kabisa.
*
Baadaye muda wa saa tisa alasiri, Erick alimtumia ujumbe Manka ukiwa hivi “Nimeshafika hapa Tegeta kibaoni, njoo tuongee”
Manka akajibu “Sawa nakuja”
Manka alitoka taratibu hakutaka kumuambia Katarina kwamba anatoka maana alikuwa hataki Katarina ashtuke kuhusu chochote juu ya mipango yake na Erick
Manka alipofika kibaoni alikuta gari ya shemeji imepaki kwenye sheli moja, akaifuata na kuzama ndani ya gari halafu wakaanza kupanga mipango ya binti kuondoka pale nyumbani awe na uhuru na penzi lake kwa raha zao
“Nataka nikununulie nyumba ukae huko unizalie watoto wawili….sitaki tena kuzaa na dada yako”
“Mh ila naogopa mpenzi” alisema binti
“Usiogope hakuna mtu atakayejua, nataka nikutoroshe kabisa uende mbali wasijue uko wapi, yaani nakuja tunafanya yetu halafu unakuwa kama mke wangu sawa?” alisema huku akimuwekea mkono begani “Halafu nakufungulia duka kubwa” alisema mtaalam na kumpapasa maziwa binti akakaa kimya kabisa
Wakiwa wamekaa pale papasana ikazidi mpaka wakajikuta washaanza kupeana ndimi taratibu.
Wakati wakifaidiana, kumbe Aneth naye ndio alikuwa ametoka kazini akapita na bajaji maeneo yale akaiona gari ya mumewe sheli imeegeshwa, wala hakutaka kuangaika nayo maana walikuwa katika ugomvi.
Aneth alipita zake mpaka nyumbani, hakujua kama mumewe yuko na Manka ndani tena wanakulana mate, ndipo akaondoka mpaka nyumbani na kuketi sebuleni huku akijipepea
Katarina alitoka chumbani akiwa amembeba mtoto ndipo akamkuta dada pale
“Dada umerudi?” aliuliza
“Ndio…..embu namuomba mtoto nimnyonyeshe” alisema na kujifuta jasho usoni
“Sawa” alisema Katarina kisha akasogea na kumpatia mtoto Aneth akawa anacheza naye kabla ya kumnyonyesha “Katarina leo nina hamu ya tambi na nyama ya kukaanga safi….embu nenda sokoni ukalete vitu vya kupika”
“Sawa ngoja nibadilishe mavazi” alisema binti
“Halafu Manka yuko wapi?” aliuliza Aneth
“Mi sijui, ameondoka hapa muda mrefu hajaniaga wala hajaongea chochote kuhusu kuondoka”
“Hivi huyu mtoto kashaanza kuharibikia kwangu ee? Sasa akija muambie hivi ajiandae kurudi kijijini asinizoee mimi mfyuuuu” alisema kwa hasira
Katarina hakuongea chochote aliondoka zake akaenda kubadilisha mavazi na baadaye aliondoka mpaka sokoni.
Sasa wakati anarudi kutoka sokoni alikuta na Manka njiani, na walirudi kwa pamoja mpaka nyumbani, Manka alikuwa amelowa kwenye nguo ya ndani haswa, hadi alitembea kwa shida, midomo yake ilionekana kukutana na cha mtema kuni kutoka kwa mwanaume huko njiani.
Kwa kuwa Katarina hakuwa na mamlaka yoyote kwa binti wala hakumuuliza chochote, waliingia ndani.
Walipofika ndani, alimkuta Aneth akiwa anacheza na mtoto sebuleni, ndipo akampokea kwa maneno mdogo wake
“Hivi Manka, wewe ni msichana wa aina gani? Umekuja kwangu kuja kunipa stress?” aliuliza maswali ambayo yalimshtua Manka akidhani ameshashtukiwa kwa kile alichokuwa akikifanya
“Dada” aliita kwa upole huku akichezea nguo yake kwa aibu
“Usiniite dada….ulienda wapi???” alifoka dada huku akimuweka mtoto pembeni halafu akainuka na kumsogelea “Nakuuliza umetoka wapi??”
Manka alianza kutetemeka “Nimetoka huko njiani nilikuwa natembea tembea tu kuujua mji” alisema
“Kuujua mji? Hivi wewe unaijua Dar es salaam ni mji wa aina gani? Unapafananisha na Kibosho si ndio? Mpumbavu wewe unafikiri ukipata mimba utalaumiwa wewe au mimi?” dada alifoka kwa hasira
“Nisamehe dada” alisema
“Nikusamehe kwa upuuzi gani? Sasa sikiliza, sitaki shida kwangu, mimi nilikuleta upajue Dar, basi umeshapajua, sasa ni muda wa kurudi nyumbani” alisema Aneth
“Dada nisamehe”
“Nimeshamaliza” aliongea kwa jazba Aneth, mama Chris halafu akambeba mtoto wake huyo akaenda chumbani
Manka alibaki na mawazo sana. Alihisi Katarina ndiye anayemchongea lakini Katarina alikuwa hajasema chochote kibaya kwa mtu yeyote yule.
Alimtumia ujumbe Erick na kumueleza “Mimi nitafukuzwa muda wowote, ninaona visa vishazidi sasa jipange kunitafutia pa kwenda kukaa ndio tutakuwa na amani”
Ilifika mida ya jioni ndipo Manka akaanza kumchamba Katarina chumbani
“Wewe ni mbea sana….sikufichi, naona wivu wako kisa shemeji yangu alininunulia simu na nguo. Umeanza kunichongea, sasa nakuambia hata akinifukuza siondoki hapa Dar, mshenzi wewe” aliongea kwa jeuri Manka halafu akatoka zake na kwenda bafuni huku akiiacha simu mezani pale chumbani
Katarina alijisikia vibaya, japo ni kweli kununuliwa simu kulimuuma sana Katarina lakini hakuwa na namna yoyote ya kusema alipe kisasi maana ni upendo wa shemeji.
Katarina alishika simu ya Manka maana alikuwa akiijua password, lakini alipojaribu ilikataa kufunguka, akajua amekosea kuandika, ndipo akarudia tena na tena na bado ikamkatalia, kwani Manka alikuwa ameshabadilisha password
Aliirudisha mezani pale, halafu yeye akaketi zake kitandani, ghafla uliingia ujumbe kwenye simu ya Manka, na kwa kuwa Manka alikuwa hajui kuipangilia vizuri simu kumbe notification aliziweka ziweze kuonekana hata simu ikiwa kwenye funguo.
Binti alitazama kulikuwa na ujumbe pale kutoka kwa Erick ambapo namba aliiandika baba Chris
Ujumbe ulisema hivi
“Usijali, kesho sitaondoka hapo nyumbani asubuhi nataka tupange mipango yetu mizuri kabisa uondoke hapo halafu kingine ni kwamba saa ile uliniacha na hamu kweli kweli, kesho tutafanya mpango nimtume mbali Katarina halafu tufanye yetu kabla sijaenda kazini”
Katarina aliposoma huu ujumbe alishtuka na ndio alipata jibu kamili kwamba wale watu wanapeana raha na shemeji yake
EP 24
“Mh makubwa” alijisemea Katarina baada ya kugundua kwa uhakika kwamba kile alchokuwa akikihisi ni cha kweli kabisa.
Katarina alijifanya kama vile hajaona kitu, kimya alitoka akaenda zake sebuleni na kuanza kuangalia TV taratibu, lakini hata akili yake haikuwa kwenye TV ilikuwa kwenye lile suala aliloligundua kwenye message.
Upande mwingine, Jonas na Haidali walikuwa bar wakawa wanakunywa mbili tatu. Jonas akamtazama Haidali halafu akamuambia “Hivi wewe Haidali ni ustadhi gani ambaye unapenda pombe hivi?”
Haidali akatabasamu na kusema “Kwani wewe unaruhusiwa kunywa pombe na dini yako?”
“Hapana siruhusiwi kunywa pombe mimi sio mkatoliki”
“Sasa je? Ni starehe tu, ukishakuwa addicted basi…”
“Ila ni kweli hata uzinzi hauruhusiwi na dini yoyote lakini wewe mbwa ni malaya asee”
“Ahahaaa….acha ujinga wewe…mimi na umalaya wapi na wapi” alisema Haidali “Hivi unajua tangu nioe sijawahi kumsaliti mke wangu, isipokuwa na huyu demu wa kichaga mzee” alisema kisha akatafakari na kuendelea “Anajua mapenzi kinoma….sijui kama tutakuja kuachana labda nife au yeye afe kwanza”
“Hahahaaaahaa…..” Jonas alicheka sana halafu akasema “Nilishawahi kutembea na wachaga kadhaa ila sijaona bado wa kunichanganya….kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi katika kampuni moja huko arusha ndio nifanya interview niliwatafuna wote”
“Hahaha…ulishawahi kuniambia…hata Rebecca si ulimpata huko huko Moshi?” aliuliza Haidali
“Ndio…”
Haidali alitoa simu mfukoni kisha akaanza kutafuta kitu fulani huku akisema “Ngoja nikuonyeshe viuno vya Aneth ndo utaelewa nachokuambia”
“Mh” Jonas aliguna kwanza ndipo Haidali alipompa simu aangalie…
Kweli kulikuwa na video ambayo Haidali alikuwa amejirekodi akifanya mapenzi na Aneth, ilikuwa ni video ya takribani dakika 20. Ilionyesha yule mtoto kajifunzia mambo makubwa Pwani. Alikuwa anafanya muujiza.
Jonas alikuwa ni mtundu sana, aliichunguza ile video imehifadhiwa wapi ndipo akagundua Haidali kaificha kwenye Google Drive. Alichofanya cha haraka sana, ni kwamba alikopi kiungio (link) ya video ile akaituma kwenye simu yake kwa njia ya SMS halafu akaifuta ile message na kumpatia Haidali simu huku akisifia. Nia ya kukopi kile kiungio ni ili akaipakue kwenye simu yake.
“We fala, ulimrekodi lini huyu mwanamke aisee?”
“Hahahaa hiyo ni moja tu…..zipo nyingi sana” alisema Haidali na kuikata ile video akaweka simu mfukoni halafu akaupalilia moyo kwa kupiga bia zake taratibu.
“Ila anaonekana ni mtamu sana, halafu kumbe analia hivyo wakati wa tendo?” aliuliza Jonas
“Hahaaahaa sasa ndo uniambie ninaanzaje kumuacha”
“Noma”
Walikunywa sana, mpaka saa tano usiku kila mmoja alishika njia yake kuelekea nyumbani ili kumalizia usiku pamoja na familia yake.
*
Asubuhi na mapema Aneth aliamka akajiandaa kama kawaida yake alitakiwa aende kazini. Alipomaliza kujiandaa aliondoka huku akimuacha Erick kitandani akiwa na mtoto Chris.
Hata salamu ya asubuhi haikuwepo baina ya wanandoa hawa wawili, lakini Erick alibaki kwa kuwa alikuwa na mipango yake thabiti yeye na Manka.
Hata hivyo Katarina naye alikuwa ameshaamka, na jukumu lake ni kuhakikisha mtoto anakula vizuri na usafi wa nguo na mwili kila wakati. Katarina alienda chumbani akamkuta Erick anacheza na mtoto wake, akamuamkia
“Shikamoo baba Chris”
“Marahaba, umefuata nini?” Erick alimuuliza
“Nimemfuata mtoto akaoge na kunywa maziwa pia” alisema binti
“Sawa….ngoja nicheze naye kidogo..nitamleta”
“Sawa kaka” Katarina aliongea kwa nidhamu kisha alitoka nyumbani na kwenda moja kwa moja hadi jikoni akawa anaandalia maziwa ya mtoto.
Kichwani mwake alipomuona Erick bado amelala na haikuwa kawaida yake, alijua kuna jambo litakalofuata, tena ni kwamba Manka alikuwa hajaamka, alikuwa mvivu sana, halafu alikuwa na kiburi kilichopitiliza ukijumlisha kwamba anatoka na shemeji ndio kabisa alijiona mtemi kama Inonga alivyojiona mtemi kwa Fiston Kalala Mayele, kwenye derby ya Kariakoo.
Kwa jinsi Manka alivyokuwa akimuachia Katarina kazi kila siku, ndio kwanza alikuwa akimkwaza na kuutengeneza uadui kati yao kwa kiasi kikubwa bila Manka kujua kuna tatizo linaweza kutokea.
Baada ya nusu saa Erick alitoka akiwa amembeba mtoto anacheza naye kwa kumtekenya tumboni mtoto anafurahi na kucheka sana.
Erick alimpatia Katarina mtoto kisha akamuambia, “ukishamaliza kufanya kazi zako uniambie, kuna sehemu ninataka nikuagize ukanichukulie mzigo fulani”
Katarina aliikumbuka ile message ndo akagundua ni kweli lile aliloandika jana linaenda kutokea, hakuwa na budi kukubali kwani yule ni boss wake na ndiye anayemlipa mshahara wa shillingi elfu hamsini kila mwezi “Sawa kaka”
“Ok”
Erick aliondoka zake akarudi chumbani halafu akamtumia ujumbe Manka “Hutaki kuamka?”
Manka akamtumia viimoji vya kucheka vikiwa na makopakopa machoni halafu akasema “Nimelegea sitaweza kutembea…labda uje unibebe”
Erick alitabasamu kisha akamuandikia “Usijali nitakuja kukubeba ila nikiwa nakubeba nitakuwa nimeichomeka ndani ikizidi kupata joto”
“Hahahaaa…unapenda!!! umenifanya hadi mimi nikawa napenda mpenzi wangu”
“Usijali ngoja akiondoka tu tuinjoy”
“Sawa”
Erick alijiachia, alijua atamtuma Katarina mbali ili ainjoy na shemeji yake, aliitamani shoo ya mdogo mke.
Baadaye mida ya saa tano na nusu, Erick alitoka chumbani akamkuta Katarina na Manka wakiwa sebuleni wanakunywa chai, ndipo akamtazama Katarina na kumueleza
“Katarina unatakiwa uende pale Bunju B sokoni, kuna mtu atakupatia mzigo wangu uniletee, nenda sasa hivi anakusubiri” aliongea na kutoa shilingi elfu kumi kwenye pochi akampatia “Nauli hiyo”
Katarina aliipokea na kuuliza “Si ninaenda na Manka?”
Manka naye akamjibu “Kheee…mimi nabaki na mtoto”
Erick akafoka “Ningekuwa nataka muende wote ningekuambia muende, lakini nimesema uende…maana yake wewe mwenyewe…najua mkienda wawili hapa mtachelewa kurudi halafu mtoto pia hatakiwi kupigwa na upepo”
Katarina kwa nidhamu akasema “Sawa nimeelewa”
Erick aligeuka na kuondoka zake, ndipo Katarina akamsitisha na kumuuliza “Lakini mimi huyo mtu nitamjuaje?”
Erick akamjibu “Ukifika utanipigia simu kisha nitakuelewesha”
“Sawa”
Ilikuwa ni mipango bubu, nia ya Erick ni kulifaidi penzi la shemeji yake kwa mara nyingine tena, wote walikuwa wamemissiana.
Katarina alianza kujiandaa, na ilipopita kama dakika thelathini hivi alimfuata Erick na kumuaga, halafu alirudi kwa Manka na kumuambia “Najua mna mipango yenu ndo maana ninaondolewa hapa…”
Manka alimtazama kwa dharau kisha akampandisha na kumshusha halafu akajibu “Kwendraa…hata kama yanakuhusu nini?”
Katarina alikuwa ana hasira sana kila alipoona kile kilichokuwa kinaenda kufanyika.
EP 25
Baada ya Katarina kuondoka alifika maeneo ya Tegeta Nyuki kituo cha daladala halafu akamtumia ujumbe Aneth akamuambia
“Kile nilichokueleza jana kinaenda kutokea, nimeagizwa bunju na kaka yuko na mdogo wanataka kufanya yao ambayo huwa wanayafanya mara kwa mara”
Aneth akiwa kazini alishtuliwa na huu ujumbe alisimama kama kichaa na kumtazama Jonas
“Vipi Aneth?” aliuliza
“Ngoja” alisema huku akihema na kuondoka akiwa ameshika simu mkononi. Alipofika nje alitaka kufungua mlango wa gari akakumbuka ufunguo upo kwenye pochi na kaiacha ndani ya ofisi.
Kwa kuchanganyikiwa Aneth alirudi akikimbia ndani, akamkuta Jonas na Haidali wanamchungulia binti akateleza na kudondoka
“Vipi Aneth?” aliuliza Haidali
Aneth akajikokota na kuinuka akaiwahi pochi ndipo akawa anatoka Haidali akamshika kumzuia “Unaenda wapi?”
“Niachie mshenzi wewe” alijikuta anamtukana ndipo Haidali akamuachia binti akaondoka haraka kuelekea garini.
Aliliwasha gari, akaondoka kwa kasi kubwa ya mia na 20.
Wakati akiparangana njiani kumbe Erick ndo anaanda chakula chake katika kitanda cho cha ndoa kabisa. Alikuwa ndo anamkoboa nguo ya ndani na Manka alibaki uchi wa mnyama.
“Naogopaaaa mpenzi”
“Usiogope” alisema Erick na kuvamia nyonyo akainyonya ila binti akamzuia
“Wait kwanza”
“Nini tena?”
“Katarina amesema kwamba anajua tunachotaka kufanya, unahisi hawezi kumuambia dada?”
“Hawezi bana” alisema Erick kwa kupuuzi na kumpanda binti akaanza kuparangana naye.
“Ossh….sheem…..auuuwii”
Aneth naye alikuwa amefika getini na licha ya geti kufungwa kwa ufunguo alilifungua na kuingia haraka maana naye alikuwa na ufunguo wake wa dharura pia, alipofika ndani alikuta pia mlango umefungwa kwa nje ndipo akakwama kuufungua ikabidi azunguke aende katika dirisha la chumba alichokuwa akilala Manka pamoja na Katarina.
Alipochungulia, alimuona Chris pekee akiwa amelala pale. Alizidi kunyata na kwenda kwenye dirisha la chumba chake na mumewe, akachungulia.
Alipotazama kwa makini, kupitia kando ya pazia, aliona binti akiwa amelazwa kifo cha mende, amemkumbatia shemeji yake, huku kiuno cha kila mmoja kikikatwa taratibu tena wamekumbatiana kwa nguvu
Ni kama vile alipigwa shoti ya umeme. Alirukia dirisha akalipiga kwa nguvu “Pah….pah uwiii uwiiiii”
Hii iliwashtu kina Erick na Manka wakaachana na kutazama dirishani.
“Mbwa nyie mnanisaliti daaah auwii” alisema kwa hasira na kuchukua kipande cha tofalia kapasulia vioo vya dirisha halafu akafungua na kutazama ndani
“Erick…….Eriiiiick…..umeamua kunisaliti na mdogo wangu……gghgghgghghgg ……..Mankaaaa” alisema kwa hasira huku akijigonga gonga kwenye dirisha “Ninawachomea huko ndani mbwa nyieee…..uwiiii uwiiiiii jamani nifungulie nije niwaueee” alisema kwa hasira mwanamke huyo na kukimbia kule nje akausogelea mlango na kuudunda anajaribu kuuvunja lakini wapi
Manka alitetemeka alipata hofu kubwa, alihofia hakujua itakuwaje kama nyumbani wakipata taarifa kama ile
“Baba Chris…mimi ninakufa eti” alisema Manka kwa uoga huku akikimbia kuelekea nje ya chumba kile na kwenda chumbani kwake
“We mbwa, leo ndo utanijua mimi ni nani” alifoka kwa hasira binti huyo
Erick alimjua mke wake kwa kiasi kikubwa, alivaa kisha akachukua ufunguo wa gari akauti mfukoni na kumfuata Manka akamuambia
“Mi nina uwezo wa kumdhibiti…..ila wewe sasa kaa kwenye huo mlango wa nyuma nikishafungua huku ataingia ndani halafu nitamfungia wewe ukimbie sawa?”
“Sawa” Manka aliongea huku akitetemeka.
Alisogea kwenye mlango wa nyuma akasokota ufunguo, halafu Erick naye akafungua wa mbele. Kitendo cha kufungua hivi tu Aneth alizama ndani akiwa na jazba kali
Manka alitokea mlango wa nyuma akafunga kwa nje, halafu Erick alipambana na Aneth mpaka akamkalisha chini kwenye sakafu “Niachie mwanaume malaya sana wewe”
Erick alimchoropoka mke wake kisha akakimbia na kwenda mlangoni akatoka na kumfungia mkewe ndani halafu yeye akakimbia mpaka kwenye gari.
Aneth alilia sana, alitukana kila aina ya tusi, alitoa kila aina ya laana kwa mumewe na mdogo wake, wote walikuwa ni wasaliti lakini unaposalitiwa inauma zaidi.
Alipoona hakuna msaada binti aliingia chumbani akamchukua mtoto wake ambaye alikuwa analia na kuanza kumbembeleza chumbani kwa Manka na Katarina, alipotazama pembeni aliona simu ya mdogo wake, alisikia hasira maana alijua ile simu ilikuwa ni zawadi kutoka kwa mumewe na alikuwa amemletea kwa nia ya kumlaghai ampe penzi
Aliigonga ukutani kwa nguvu paaah, ikapasuka pasuka. Halafu akatukana “Mpumbavu wewe
aliongea kwa hasira
Muda huo, Manka na Erick walikuwa njiani wanaelekea njia ya madale, Manka amejifunga khanga na blauzi tu. Hawajui wanaelekea wapi.
Damu ni nzito kuliko maji, binti aliona huruma akajikuta anaanza kulia, anajutia kitendo alichokuwa amekifanya, ndipo akamuuliza shemeji yake “Ina maana dada umemfungia?” aliuliza
“Kwanini unauliza hivyo?”
“Naomba unirudishe kwa dada yangu nikamuombe msamaha” alisema binti kwa huruma huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamtiririka mashavuni
Erick alimshangaa yule binti anafuata kifo kwa dada yake
“Una akili wewe? Unataka kwenda kwa dada yako atakuua yule”
“Please nirudishe”
“Hapana haiwezekani” alisema Erick huku akipaki gari na kupokea simu aliyokuwa akipigiwa na house girl wake binti Katarina
“Kama hutaki mi ninashuka” alisema Manka kwa hasira halafu akashuka kwenye gari “Naomba nauli nipande bajaji”
Erick hakumjibu aliongea na simu akisema “Katarina rudi nyumbani yule mtu alinitapeli”
Katarina akajibu “Sawa” aliona kabisa mchezo umeshakamilika.
Erick alimtazama shemeji yake “Naomba urudi kwenye gari” alifoka
“Naomba nauli please naomba nikaongee na dada yangu”
“Okay” kwa hasira Erick alichomoa shilingi elfu kumi akampatia “Haya nenda”
Manka alirudishia mlango kwa jazba kisha akachukua safari na kuelekea maeneo ya wazo kwa bajaj huku akilipia nauli ya shilingi elfu moja.
Alipofika nyumbani alimkuta dada akiwa anatumia jitihada za kuruka kupitia dirishani lakini akishindwa maana alikuwa ni mnene kidogo Manka alifungua mlango halafu akapiga magoti sebuleni
“Dada yangu naomba unisamehe…..nilidanganyika mimi” alisema kwa huruma na machozi.
JE DADA YAKE ATAFANYA NINI?
INAENDELEA

