𝗠𝗔𝗟𝗜𝗣𝗢 𝗞𝗜𝗧𝗔𝗡𝗗𝗔𝗡𝗜
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 26
TULIPOISHIA
Manka alirudishia mlango kwa jazba kisha akachukua safari na kuelekea maeneo ya wazo kwa bajaj huku akilipia nauli ya shilingi elfu moja.
Alipofika nyumbani alimkuta dada akiwa anatumia jitihada za kuruka kupitia dirishani lakini akishindwa maana alikuwa ni mnene kidogo Manka alifungua mlango halafu akapiga magoti sebuleni
“Dada yangu naomba unisamehe…..nilidanganyika mimi” alisema kwa huruma na machozi
ENDELEA HAPA
Aneth alishuka dirishani kisha akasimama mbele ya mdogo wake, akamtazama kwa macho makali yaliyochanganyika na machozi kumlengalenga
“Manka” alisema kwa hasira Aneth
“Nisamehe dada” binti aliongea
Bado Aneth alizidi kumtazama sana mdogo wake, ndipo akaenda bafuni na kunawa uso kisha akaenda chumban na kujipaka mafuta, akaondoka kwa mara nyingine kuelekea kazini.
Katarina alirudi nyumbani, akamkuta Manka ameketi pale sebuleni ana msongo wa mawazo, simu imeshapasuliwa, alichokiokota ni laini tu.
Katarina alimcheka, halafu akamuambia “Pole kumbe wamekupasulia simu” lakini Manka hakujibu chochote, direct alijua binti ndiye aliyemuambia dada yake kwamba anatoka na mumewe.
Manka aliweka kinyongo, hakuwa na la kufanya.
Hata hivyo Erick alikuwa katika bafu la kulipia maeneo ya sinza, akaoga vizuri halafu akatupia jezi yake ya yanga halafu akaondoka moja kwa moja mpaka kwenye gari alilokuwa amelipaki kwenye maegesho yaliyoko kwenye kituo cha daladala cha Simu2000.
Alipoingia ndani ya gari, simu yake iliita alipoitazama ni Jonas anampigia simu. Erick aliipokea simu yake na kuongea
“Hallo” alisema Erick mara baada ya kupokea simu ya Jonas
“Vipi kaka mbona sikuoni online muda mrefu nimekutumia ishu fulani”
“ah kuna mambo yalikuwa yamenibana hapa, ngoja niingie sasa hivi”
“Poa”
Jonas alikata simu na kumpa fursa Erick ya kuwasha data aone kile alichotumiwa. Ni kweli baada ya kuwasha simu, Erick aliona jumbe nyingi sana, lakini aliitafuta iliyokuwa imetumwa na namba mpya ambayo sio ya Jonas
Jonas alikuwa akipenda kutumia namba za watu makusudi ili kuepusha ushahidi pale lolote litakapotokea.
Ilikuwa ni video yenye dakika kumi na tano na sekunde kumi na mbili, jumla ikiwa na ukubwa au ujazo wa mb 43. Hii haikuwa tatizo hata kidogo kwa Erick kutumia kiwango kidogo tu cha kifurushi cha mb 43. Aliipakua na kuanza kuitazama
Ilikuwa sio video nyingine bali ni ile video ambayo siku moja kabla, Haidali alimuonyeshea Jonas wakati wakiwa bar wakipata moja baridi moja moto. Kumbe Jonas alipojitumia ile link ya video ile, alienda kuipakua akiwa peke yake na hata kumtumia Erick makusudi ili aone uchafu wote wa mke wake.
Nia ya Jonas ni kulipiza tu kisasi kisa mwanamke yule alikuwa amemkataa kimapenzi, na hata kuamua kutoka na mtoto Haidali ambaye ni mtoto wa kufikia wa mmiliki wa kampuni ya AB Insurance Ltd.
Jonas alimshuhudia mkewe akimkatikia haswa Haidali, alikuwa akilia haswa, akionyesha ufundi ambao hata yeye mwenyewe licha ya kuwa naye kwa muda mrefu hakuwahi kuupata kabisa.
Erick alitikisa kichwa kwa sababu aliumia, ilikuwa ni jambo zito sana kwake, hata hivyo Erick aliificha kwenye programu ya calculator ambayo alikuwa akitumia kuhifadhi picha zake siku zote.
Alipomaliza aliondoka zake akaenda hadi kwenye biashara zake kujua zinaendeleaje.
Siku ile Erick hakurudi nyumbani, vile vile Aneth jioni alichelewa kurudi na alipofika nyumbani alikuta Manka amelala kitandani na Katarina anaandaa chakula jikoni ndipo akamuuliza Katarina
“Huyu mpuuzi yuko wapi?”
Katarina naye akamuuliza swali badala ya kujibu “Yupi? Manka au?”
“Ndiyo….yuko wapi mbwa huyu?” aliongea kwa jazba Aneth
“Amelala”
Kwa hasira Aneth aliondoka huku akifoka “Anajiona yeye ndo mama mwenye nyumba sana kulala saa hivi halafu wewe akuachie kazi zote? Anachojua kutembea na mume wangu tu si ndio?” alifoka mwanamke huyo halafu akasonga mbele mpaka chumbani kwa wasichana hao wawili akazama ndani
“We malaya” alisema Aneth ndipo Manka akaketi kitandani kwa huzuni, na dada yake akatupa tiketi ya basi aina ya BM juu kitandani
“Dada” binti aliita kwa huzuni machozi yakimtiririka tayari
“Amka ujiandae, kesho saa kumi na moja unatakiwa uwe ndani ya basi, sitaki maswali mengi…..na pia sihitaji kukuona kwangu”
Manka alishuka chini akapiga magoti “Dada nisamehe”
“Wewe” Aneth alisema kwa jazba akiwa amemnyooshea kidole “Usiniambie ujinga wako….panga kilichokuwa chako…kesho mapema uko umbwe…mshenzi wewe” alifoka halafu akatoka na kuubamiza mlango paah huku akimuacha binti akilia mwenyewe ndani, ameshalikoroga zege, hawezi tena kulirudisha likawa saruji
Alilia kwa muda mrefu sana, lakini ilibidi afanye kama ilivyokuwa.
Saa kumi kamili kesho yake, binti aliamshwa, akaoga na kupanda gari ya dada yake mpaka Shekilango ambapo kulikuwa na ofisi za basi hilo zuri zaidi la kusafiria.
Binti aliondoka Dar, na kiswaswadu chake mkononi. Alipofika maeneo ya Bagamoyo alimtumia ujumbe shemeji (Erick) yake na kumuambia
“Shemeji kwa heri dada kanifukuza, nashukuru kwa yote”
Erick kusoma ule ujumbe alishtuka na kumuambia “Amekufukuza?”
“Ndio”
“Lakini nilikuambia usirudi kwake jana, ningekutafutia sehemu ya kuishi ule maisha”
“Hapana shemeji, roho iliniuma nikajuta, lakini najua, Katarina ndiye aliyemuambia”
“Katarina ndiye alimuambia kwamba tuko wote?”
“Ndio shemeji”
“Haya poa, wasalimie, tutawasiliana, ukihitaji kurudi utanitaarifu nikutafutie kabisa sehemu ya kushukia”
“Sitoweza tena, naenda kutafuta maisha mengine”
“Ok poa, good bye”
“Ok”
Ilikuwa ni mwisho wa mahusiano kati ya Erick na shemeji yake, Janeth au Manka, kwani alimsababishia matatizo na kusababisha kufukuzwa kabisa.
EP 27
Erick wala hakujali, tena cha kushangaza kabisa alitabasamu kwa kuona mke wake anaumia kwa kile kitendo alichokuwa amefanya.
Ilipofika muda wa saa tatu asubuhi Erick alimpigia simu Katarina binti wa kazi, na kumuuliza yuko wapi
“Niko nyumbani boss” alisema binti
“Okay….. Aneth yupo?” aliuliza mtaalam
“Hapana ameenda kazini”
“Okay….sawa”
Erick alikata simu yake.
Muda huo Katarina alikuwa sebuleni akicheza na mtoto kwenye zulia, wanacheka kweli maana yule binti alikuwa amezoeana sana na Chris, alikuwa anajua mno kulea.
Ghafla alisikia sauti ya Erick nyuma yake mlangoni ikisema “Wooow”
Katarina aligeuka kwa mshtuko ndipo akamkuta boss wake amesimama mlangoni huku akimpigia makofi akasema “Baba Chris umerudi?”
“Yeah…..ila unajua sana kumlea mtoto” alimsifia huku akisogea na kuketi kwenye sofa moja la watu wawili halafu akawaangalia, lakini muda ule Katarina alikuwa ameshapoteza kujiamini.
Erick akasema “Anyway, naonau umekosa confidence, ila nikuambie kitu kimoja”
“kitu gani kaka?”
“Ulivyofanya sio vizuri”
“Nimefanya nini mimi?”
“Kwanini umuambie Aneth kwamba mimi natoka na mdogo wake?”
“Mimi???” binti alianza kukana
“Ndio ninajua ni wewe umemuambia”
“Akuu….sio mimi”
“Sawa kama unakataa” aliongea Erick huku akitoa simu mfukoni na kuanza kuitafuta ile video ya Aneth akiwa anafanya mapenzi na Haidali. Akasema “Embu shika hii simu angalia kile kilichopo” alisema mtaalam halafu akaiweka chini na kuisukuma ikateleza mpaka binti alipokuwa ameketi
“Kuna nini?” binti aliuliza huku akiikodolea macho anaona Aneth akikata viuno hatari.
Katarina alishika mdomo akaogopa na kuifunika simu kwa aibu.
Erick aliona binti anashindwa kujiamini yeye akiwa pale, ikabidi aondoke zake akaenda chumbani, sasa kiwa chumbani binti alipata uhuru akaiangalia ile video kwa muda mrefu jinsi mwanamke yule alivyokuwa anahangaika nayo ya Haidali.
Erick alirudi akakuta yule mtoto wa kike katoa macho hasa, haamini kile alichokiona. Aliiweka simu pembeni kwa aibu kisha akainuka na kumbeba mtoto anataka kuondoka. Ndipo mtaalam akamuuliza
“Unaenda wapi sasa?”
“Mh” binti alisema huku akisita na kumtazama boss wake
“Umeitazama vizuri umemjua aliyekuwa anafanya uchafu ni nani?”
Katarina alicheka kwa aibu lakini hakujibu, ikabidi mtaalamu aongeze swali “Huyo ni mama Chris si ndio?” Katarina akatikisa kichwa kukubali ni mama Chris halafu Erick akatabasamu na kusema “Sasa mimi niliona akinisaliti muda mrefu, ndio maanan iliamua kumlipiza kisasi, sasa nashangaa wewe uliona nafaiiiiidi”
“Mh mi sikujua” alisema binti
“Ungechunguza kwanza” alisema Erick binti akatulia na kuanza kupiga hatua ila Erick akamuambia “Subiri kwanza sijamaliza” binti akamgeukia na kusikiliza, Erick akaendelea huku akipiga hatua kumfuata taratibu “Huyo mwenzako nilimuahidi nyumba, na ndio nilikuwa namalizia kusaini mkataba, sasa ameondoka, halafu sina mwingine wa kumpa ile, nyumba…..” alivuta pumzi mtaalamu halafu akaendelea “Mama Chris sio mwanamke ambaye ananiheshimu hatak kidogo, ni msaliti, sihitaji kuwa naye tena, ninahitaji mwanamke mwingine mdogo mdogo kama wewe nimpe pesa, nitamlipa milioni moja kila mwezi, kazi yake akae hapo ndani anifulie na kunipikia na kunipa penzi, na kunizalia watoto wengine wawili wanatosha”
Katarina aliguna huku akitazama pembeni kwa aibu sana, Erick akaendelea “Kwa kuwa wewe umepeperusha njiwa wangu, kwanini nisiwe wewe ndiye ninakulipa uwe kama mke wangu wa pili kwa siri bila mama Chris kufahamu?”
“Mh baba Chris hapana” alisema binti kwa uoga.
Erick wala hakuongea, alitoa wallet na kuhesabu noti kumi nyekundu akampa, halafu akasema “Huu ni mwanzo tu, ninataka nikununulia iPhone yako safiii mpya kabisa na wewe uwe unaonekana mtandaoni”
“Hapana shika pesa yako” binti aliongea
“Kwa sababu umeshaipokea naomba ukae nayo, nataka nikutoe hapa ukawe bilionea mdogo zaidi mwenye biashara zake mjini”
“Mh” binti aliguna
Erick aliisogelea simu yake, akaibeba na kuondoka mpaka nje ya geti akapanda gari yake na kuondoka moja kwa moja,
Huku nyuma alimuacha binti na mawazo tele, binti hakujua aganye nini, hakika ilikuwa ni bonge la mtihani kapewa
EP 28
Ilikuwa ni vita imeanzishwa, tangu siku ambayo Aneth amemfumania mumewe akiwa na mdogo wake kitandani, hakika hakuwahi kumuona kwa macho kabisa. Erick alikuwa haji kuonana naye licha ya kuja mara kwa mara mchana kubadilisha nguo na kuondoka.
Mara nyingi alizoea kulala lodge au kwa marafiki zake. Matumizi ya nyumbani alikuwa hataki kutoa, alifanya makusudi kwa sababu alishaona usaliti mkubwa ukiendelea kwa mkewe, hadi kurekodiana video akiwa analiwa utamu kabisa
Siku nne zilipita, ndipo Erick asubuhi asubuhi alimpigia simu Katarina, ndipo Katarina akapokea
KATARINA: Hallo baba chris
ERICK: Umeamkaje?
KATARINA: Niko salama sana sijui wewe huko
ERICK: niko poa pia, vipi huyo mwanamke yupo au ameenda kazini?
KATARINA: Hayupo ameshaenda kazini
ERICK: sawa, vipi sasa mbona ulikaa kimya kuhusu ile ishu?
KATARINA: mh (Katarina aliguna hakujua amjibu nini)
ERICK: Mbona unaguna, nijibu basi mimi nitakugharamia kila kitu hadi mwenye utafurahi
KATARINA: Mi naogopa
ERICK: Unaogopa nini? Kumbuka wewe sio ndugu yake kabisa, hata ukimuambia unaondoka wala hatoshangaa maana nataka nikupangie chumba chako kizuri kabisa
KATARINA: Jamani
ERICK: usiogope
KATARINA: unanidanganya kaka halafu mi nitadhalilika
ERICK: Sikudanganyi haki ya Mungu, ninahitaji kufurahi na wewe, unajua kadri unavyozidi kukaa Dar ndo unazidi kuwa mzuri, mtoto mweupe ila nyie wambulu ni wazuri
KATARINA: hahaa hapana bwana….
ERICK: kwa hiyo huniamini, huamini kwamba nataka kukuoan? Au zile ahadi unahisi ni za uongo
KATARINA: ndio ninahisi ni za uongo
ERICK: Nifanye nini ili uamini ni za kweli
KATARINA: Ninunulie simu kubwa uniletee
ERICK: Anhaa, hilo tu? Basi hamna shida nitakuja nayo kesho asubuhi dada akishaenda kazini utaniambia sawa?
KATARINA: sawa ole wako unidanganye
ERICK: usijali
Kwa namna walivyoongea ilionekana kabisa Katarina hawezi kufurukutak wa Erick, Erick hakuna na nia nyingine zaidi ya kulipiza kisasi kwa mkewe ambaye alikuwa ni msaliti kwake kwa muda mrefu sana, roho ilikuwa ikimuuma kiasi kwamba hakutaka mwanamke mwingine isipokuwa wa pale nyumbani ili kuhakikisha Aneth anaumia.
*
Siku ile Aneth alikuwa ofisini na Haidali, uso wa Aneth ulikuwa umepoteza nuru, ndoa imeshatanga tanga, usaliti aliokuwa ameufanya ni sawa na kudandia mtumbwi wa kibwengo akidhani atavuka mto lakini kumbee vibwengo havivushi maji.
Jonas alimtazama binti anavyoweweseka, ndipo akapata furaha yake iliyo kamili, moyo wake ulitabasamu na kujiona mshindi kabisa, alitoka akiwa anapiga mluzi taratibu huku akiwaza mambo makuu mawili aliyoyafanya akiamini ndio yamevuruga ndoa binti kabisa, ikiwa jambo la kwanza ni kumfikisha katika hoteli aliyokuwa Aneth na mchepuko huku akidai mchepuko una UKIMWI halafu kingine ni kutuma video ya ngono kwa mume wake.
“Hahahaaaa Jesu” Jonas alijipongeza sana, kuliko kumkatalia Jonas ni bora angeacha tu kazi, ilikuwa ni hatari kwa afya yake, lakini kamwe Aneth hakujua Jonas ndiye adui yake mkubwa.
Binti akiwa ameinama ofisini, ameshika tama, anawaza mambo mengi, majukumu ya familia yamemzidi kabisa, alijikuta anatokwa na machozi.
Haidali alipita akamuona mwanamke akiwa katika mateso makubwa sana, akamuita “Aneth” ndipo Aneth akainuka kichwa na kufuta machozi machoni akamtazama Haidali “Vipi mbona una stress sana mpenzi? Kwanini siku hizi umebadilika sana?”
“Haidali….please, naomba tuachane” alimjibu bila kupindisha
“Mh…umefikia huko? Kwani nimekukosea nini?” aliuliza huku akiketi kando yake na kumshika mgongoni
“Naomba tuachane, nahisi hii dhambi ndiyo inatembea na familia yangu…ni dhahiri kwamba kwa sasa sina ndoa, imekuwa ni ngumu nalia kila siku, majukumu yamenizidi mwenzako” alilia sana Aneth siku ile
“Unahitaji nini Aneth? Ni pesa?”
“Hapana sio pesa, ninahitaji furaha irejee… Erick hakuwahi kuwa hivi, sijui amekumbwa na nini…hataki mazoea na mimi kabisa, naomba nipe likizo niangalie itakuwaje”
“Pole sana, nilishakuambia wanaume wanaofanya biashara hizo za mikoani, sio watu, ni malaya watupu, kwanini nisikupangie nyumba uje uishi na mtoto wako humo?”
“Hapana Haidali, nina ndoa ya kanisani, ni mpya kabisa inatakiwa idumu, sijawahi ona ndugu yangu yeyote akivunja ndoa yake, mimi nitaonekanaje?”
“Kwa hiyo unahitaji kuteseka ili kuwafurahisha ndugu zako?” Erick aliuliza
“Daaaaah” binti aliumia sana, hakujua tatizo limeanzia wapi, hakujua anahitaji muda wa kufikiria sana.
Siku ile, Haidali alimpa ruhusa mapema sana, binti akaondoka na kwenda nyumbani kwake kupumzika, alipofika alijilaza kitandani huku akimtazama mtoto ambaye alimzaa na Erick, alikumbuka mbali, alikumbuka mwanzo wa mbali kabisa, ndipo akamtumia ujumbe mrefu na wa uchungu sana mwanaume wake huyo wa ndoa.
Ujumbe ule ulikuwa ukisema hivi
“ERICK MUME WANGU, MBONA KIMYA SANA SIKUELEWI? UMENIKOSEA SANA KUTEMBEA NA MDOGO WANGU, LAKINI BAADA YA TUKIO HILI SIKUWAHI KUKUONA, SIKUWAHI KUSIKIA HATA UKINIOMBA MSAMAHA, KUMBE ULIONA NI SAHIHI… UMEAMUA KUNITELEKEZA MIMI NA FAMILIA YAKO, NATESEKA NINA MAWAZO, HIVI KWANINI UMEAMUA KUFANYA HIVI? NATESEKA SANA, KILA SIKU NALIA KWA AJILI YAKO, NAOMBA URUDI NIMESHAKUSAMEHE MUME WANGU, NAOMBA UJE TUONGEE TUJUE TATIZO LINAANZIA WAPI” alituma binti kwa uchungu
EP 29
Erick aliutazama ule ujumbe akajikuta amecheka kwanza, halafu akatulia kimya hakutaka kumjibu, kila akikumbuka namna mkewe alivyokuwa anamkatikia Haidali, yaani ndo kabisa aliona kama vile anamkera kabisa, alikaa kimya kabisa mkali huyo.
Aneth alizidi kupata mawazo sana, ila alitumia sana busara, hakuwahi kumuambia mzazi wala ndugu kwamba alimfuma Manka na mumewe, alitumia busara kubwa sana, lakini maumivu yake yalikuwa sio ya nchi hii
Kule Kibosho Umbwe Manka alianza kuuza mboga zake safi kabisa, kwani alikuwa na pesa alizokuwa amezichuma kwa shemeji yake kwa muda mfupi. Kitu kingine ni kwamba binti alikuwa amenunua simu nzuri alikuwa anaosha vibaya sana mtaani kwao, aliwafanya watu wajue Dar kuna pesa kumbe ni mwili wake ulimuweka mjini hadi akawa na vyote hivyo.
*******
Erick hakuwa na dogo katika kulipiza kisasi, alitumia gharama kuhakikisha mke wake anazidi kuteseka, Erick alinunua simu nzuri kabisa aina ya Oppo licha ya kumuahidi Katarina iPhone lakini aliona ni gharama zisizokuwa na msingi.
Erick alichukua muda wake, akaondoka kuelekea nyumbani kwake taratibu huku simu mpya kabisa ikiwa kwenye box lake.
Aliifika nje ya geti lake, akashuka kwa mbwembwe akiwa amebeba box la simu mpya mkononi, alipofika ndani ya geti alimkuta binti akiwa anafua nguo za mtoto
“Katarina” alisema Erick kimahaba huku akimtazama mtoto wa kike
“Abee” binti alisema huku akiinuka na kujifuta maji kwa kutumia khanga yake, halafu muda huo anakodolea mkono wa Erick ulioshikilia box la simu mpya
“Umeamkaje mamaa” aliuliza Erick
“Sakana tu, karibu”
“Ok usijali….shika…si upo mwenyewe?”
Binti aliruka fasta akapokea “Asante,,,niko mwenyewe”
“Sawa, sasa sikiliza, Aneth asiione hiyo simu, utafukuzwa kama mwenzako, itumie akiwa hayupo….halafu ichaji kwanza mpaka ijae ndo uanze kutumia”
“Sawa” alisema binti kwa furaha “Asante sana”
“Usijali”
Katarina aliingia ndani chumbani kabisa, akaifungua na kuweka chaji, halafu aliporudi alimkuta mtaalam akiwa ameshaketi sebuleni, binti akasita kidogo kwa aibu
“Mtoto yuko wapi?” aliuliza
“Amelala”
“Sawa. Kwa hiyo sasa??” aliuliza mtaalam binti hakujibu chochote.
Erick aliinuka na kumsogelea akamshika kidogo “Kwa hiyo umenikubalia?”
“Mh hamna shida” alisema binti
“Poa, kwa hiyo sasa tunaweza kufanya kidogo ili niondoke?”
“Mh, mi naogopa nitaumia”
“Utaumia? Hauwezi umia bwana”
“Hapana, mimi sijawahi kabla naogopa eti”
“Mh kweli?”
“Ndio”
“Tujaribu kidogo tu, sitakuumiza”
Erick alimbembeleza sana, huyu binti alikuwa ni mgeni kabisa kwenye mapenzi. Alichokifanya Erick alimbeba mzima mzima mpaka chumbani kwake yeye na mke wake, halafu akamlaza kitandani na kuanza kumchezea
“Naogopa eti”
“Usiogope”
Erick alijitahidi kuparangana na yule mtoto, haikuwa rahisi lakini kiukweli alikuwa hajawahi kufanya mapenzi kabisa yule binti, Erick ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza, yaani alimlaghai kirahisi sana, ilikuwa ni jambo la kufurahisha kwa Erick, hakuwahi kukutana na bikira kabla. Alimsifia sana binti
Erick alioga akabadilisha nguo safi halafu akaondoka zake.
**
Jioni Aneth aliporejea nyumbani alikuta ndani kwake kuna vitu vimebadilika, akajua lazima mtaalamu alifika pale ndani, akamuuliza Katarina
“Hivi baba Chris alikuja hapa mchana?”
Sasa kwa ushamba wa binti alijikuta anashtuka maana alikuwa amefanya mapenzi na boss wake na ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa
“Hapana hajarudi” alidanganya akihisi atashtukiwa
“Hajarudi? Embu niambie ukweli, nani kafungua kabati la nguo safi wakati wewe hauna ufunguo?”
“Ah…ni kweli alikuja” alisema binti
“Sasa kwanini unanidanganya?”
“Samahani dada”
“Acha upumbavu wewe….” alifoka mama Chris
Alihisi kuna mchezo mpya umeanza tena, alichokifanya mama Chris alitoka nje ya nyumba akaenda hadi kwa mama mmoja jirani, kuna kitu walikizungumza, halafu alirudi nyumbani na kukaa kama kawaida yake.
****
Siku zilizidi kusogea, mapenzi yalinoga zaidi kati ya house girl na boss wake, Erick Jackson. Kila mara mchana Erick alirudi na kumtawanya miguu mtoto wa kimbulu, mapenzi yalikuwa bam bam. Binti alianza kunawiri, alipewa matunzo aliyokuwa anayataka, hakuna stress, alijisikia faraja, hakika penzi lilimnogea hakutamani kitu kingine
Siku hizo yule jirani ambaye Aneth alimtembelea wakaongea jambo fulani mazoea kati yake na familia ya kina Katarina yalizidi, ndipo siku moja alikuja kwa kunyata baada ya kusikia mziki mkubwa ka baba Chris.
Alifungua geti taratibu akapenya mpaka katika dirisha la sebuleni akachungulia akamkuta binti akicheza mziki na Erick taratibu huku wakipapasana. Mdogo mdogo walijikuta wanaanza kunyonya ndimi bila kujua jirani alikuwa anawachungulia.
Walijikuta wanadondokea kwenye hamu na mihemko kwenye sofa wakaanza kupapasana na kuvuana moja moja. Mwishowe, Erick alimuinamisha binti kwenye sofa na kuanza kumtanika chuma tembele moja lililoenda shule.
Katarina alipiga kelele za mahaba huku akisema “Nataka unioe niwe mke wako, nakupenda sana, nakupenda”
Yule jirani akaondoka taratibu, na alipofika nyumbani alimtumia ujumbe Aneth ukisema hivi “Kile ulichokuwa ukikihisi ni kweli, nimewakuta leo wameinamishana sebuleni”
Huu ujumbe ulimshtua sana Aneth, hakusita, alilia machozi mazito, alijikuta anaumia sana. Alijiona kama mjinga, alilaumu sana kuingia kwenye mahusiano na mwanaume katili kama Erick.
Binti alitoka nje ya ofisi, akaingia kwenye gari halafu akawa analia kwa gadhabu kubwa, ndipo Haidali alipomfuata na kumuuliza tatizo nini
“Haidali naomba likizo ya wiki tu, mume wangu ananisaliti kila mara, ninakosa furaha ninalia kwa uchungu”
Haidali alimtazama, Aneth alikuwa amekonda, sura imemkakamaa, alikuwa hana furaha kabisa, alimuhurumia na kumuambia “Basi sawa kapumzike, ukiona mambo ni magumu sana, niambie nikutafutie sehemu ambayo utaishi kwa furaha”
“Sawa”
Aneth alienda nyumbani, alikuwa anajua siri zote lakini alipofika alimkosa Erick kwani alikuwa ameshaondoka kama ilivyokuwa kawaida yake.
Alimtazama Katarina amewaka, amependeza mashavu yamejaa, kalio nalo limeanza kubinuka, maziwa yamemjaa amekuwa mtoto mzuri hasa, alijua kabisa penzi ndio linamnogea
“Dada leo nipike nini?” Katarina aliuliza
“Chochote tu” alijibu Manka huku akiangalia kwa hasira.
Binti alipoenda jikoni tu, Aneth aliamua kuingia katika chumba chake kukagua, alipofika hivi alikuta chaja kwenye soketi, akaitazama ni mpya kabisa akajua binti ana ila anaificha.
Alianza kupekua chumbani mwishowe akaikuta kwenye begi la nguo binti alikuwa ameificha, aliitoa, simu haina hata password na jumbe zote zilikuwepo. Aneth akajua kabisa kwa Erick aliingia choo cha kike.
Aliirudisha simu kwenye begi hakutaka kumuambia binti kabisa kwamba amegundua chochote, alipomaliza aliingia chumbani akalia kwa uchungu huku akimkumbuka Mungu bila kujua kwamba yeye alikuwa ndiyo chanzo cha yote yale.
Alimtumia ujumbe mumewe
“ERICK BAADA YA KUTOKA NA MDOGO WANGU SASA UMEHAMIA KWA HOUSE GIRL? OOH ASANTE SANA, KWA HILI SITOKUSAMEHE TENA…NAOMBA NISIKUONE KWANGU” alituma kwa hasira, Erick akazidi kucheka ka dharau
EP 30
Masaa yalizidi kutembea, siku mbili za likizo zikapita Aneth akiwa nyumbani tu, alikuwa hana namna ya kufanya ila, kila alipokuwa akimuoan Katarina, alijikuta anakasirika, na alichokifanya alimfanyia surprise na kwenda kumpakia gari aina ya Lakrome akamrudisha kwao Karatu.
Erick zile habari zilimsikitisha kidogo, ndipo akaamua kwenda nyumbani kuonana na Aneth, alipofika alimkuta Aneth akiwa amejikunyata na katoto kake kachanga kwenye kochi, huku akiwa na mawazo, Erick alimtazama binti kweli amekomoka.
“Nilikuambia usirudi hapa, sasa umekuja kutafuta nini?” alimuuliza bila kumtazama
“Kwanini umemrudisha Katarina kwao?”
“Usiniulize maswali ya kijinga, niambie kwanini unaamua kuniumiza hivi? Hivi kwanini wanaume hamna huruma? Nimejitoa sadaka kwako, nimekuzalia hadi mtoto, nimetafuta hadi kazi ili kukupunguzia majukumu lakini leo ndo uliyonilipa kweli Erick? Kweli? Asante”
Alisema binti huku akilia
Erick akasema “Usilie, ngoja kwanza tusiongee sana” alisema na kutoa flash kwenye mfuko wa suruali halafu akasogea runinga iliyokuwa ukutani akaiwasha. Alipoiwasha tu hivi alichomeka flash halafu akachukua rimoti.
Alipoibonyeza mara mbili, ndipo mubashara video ya Aneth akimpa penzi Haidali ilionekana. Aneth alishtuka na kujikuta ananyanyuka huku akitetemeka. Erick hakuongea alitabasamu
“Erick!!!!!” aliita binti huku akimuwahi mtaalam amnyang’anye rimoti lakini Erick akamkwepa.
Binti aliogopa, jasho lilianza kumvuja, alisogea kwenye TV akachomoa flashi kisha akasogea nyuma
“Umeona uchafu wako?” aliuliza Erick “Halafu unajiona wewe ni msafi sana? Uliona ulichokuwa ukikifanya ni kitu chema sana ee???” Erick aliongea kwa jazba
Aneth alishuka akapiga magoti chini, kisha akasema “Mume wangu nisamehe……” alisema huku akilia
“Embu toka hapa, malaya mkubwa wewe…unafikiri mimi ni mjinga nianze tu kutembea na mdogo wako mimi bure? Toka hapa”
“Nisameheeee……..nisameheee Erick ninakupenda wewe…..sikujua kama ni….”
“Hukujua??? Wewe mtu mzima hukujua? Msaliti mshenzi sana wewe, hata Amidu alijiua kwa sababu ya umalaya wako hujui? Au ulifikiri sikujua? Nilikuvumilia tu kwa sababu tulikuwa tumeshafunga ndoa ila sasa hivi siwezi kuishi na mwanamke kama wewe tena, mbwa wewe”
“Erick” binti alilia sana, halafu kwa dharau Erick alitupa rimoti pembeni halafu akaondoka zake kutoka nje, binti anajaribu kumuwahi amshike miguu lakini Erick alimlamba kibao
“Usinishike nenda kamshike hiyo boss unayeona anakufaa sana” alifoka halafu akatoka
“Eriiiiiiick” binti aliita kwa uchungu, alijua kweli ni mkosaji alijuta.
“Sitorudi tena kwako, nimeamua kukuachia kila kitu acha nikaanze maisha mapya, hii nyumba atairithi Christian, japo ninahisi pia sio mtoto wangu pia” aliongea kwa hasira Erick
“Noooo…ni mwanao Erick….please nisaidie mwenzako sitokusaliti tena mume wangu”
Erick hakujibu chochote aliwahi gari lake, na kuondoka moja kwa moja huku akimuacha binti amejigaragaza chini kwa uchungu, alijiona mjinga kweli kweli
Erick aliamua kwenda kutafuta chumba chake kimoja tu masta, akaanza maisha mapya kabisa Erick huku akiitelekeza familia yake kabisa.
Dullah akamuuliza “Erick kwa hiyo hutaki kukaa na yule mwanamke tena?”
Erick akajibu “Sitaki kabisa, tena ninatakiwa nikapime niijue afya yangu na hii video sijui tuisambaze?” alisema kwa jazba
Elisha alimshika kifuani na kusema “Usiisambaze hiyo video nakuomba ndugu yangu, video ikisambaa hata wewe pia utadhalilika, pia kumbuka bado ni mama wa mtoto wako, muwekee kwanza mtoto heshima yake”
Erick aliyapokea yale maneno vyema kabisa.
Ilikuwa ni kwa kutetemeka lakini Erick alienda kupima virusi maana alikumbuka alishawahi kuambiwa yule boss mtoto ana UKIMWI na ametembea sana na mkewe.
Erick alipopima alipata majibu ya kwamba yeye ni mzima wa afya kabisa, ila lengo la Jonas kuivuruga ndoa yake likawa limeshafanikiwa
Yalikuwa maisha ya uchungu kwa Aneth, alijilaumu mwenyewe, alijua yeye ndiyo chanzo cha ndoa yake kubomoka. Alianza kutangatanga, akiwa na Haidali, mapenzi yalikuwa hayana furaha tena. Binti alikuwa kama kichaa…..aliwaomba marafiki wa Erick wamuombee msamaha lakini Erick alikataa kata kata.
MITHALI 14:1
“Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
MWISHO
Ninaamini umejifunza mambo mengi sana kupitia hadithi hii ambayo alihadithia ndugu yetu Aneth Massawe, hatukuwa na namna tuliielezea kwako, ili uelewe kwanini ndoa nyingi zinashindwa kudumu kabisa.

