NCHI ZILIWAHI KUWAFUNGA MARAIS WAO
Watu washajua unapopata madaraka unalewa, ukishalewa sasa unaanza kufanya madudu huku ukiamini utalindwa. Hiyo haipo kwenye nchi nyinginezo, wao hata kama umemaliza muda wako, wakigundua wakati ulipokuwa rais kuna madudu uliyafanya, wanakuweka ndani ukajifunze.
Hizi ni nchi ambazo ziliwahi kuwafunga marais wao.
BRAZIL: Jair Bolsonaro aliwahi kukutwa na dhahama hii baada ya kubainika alifanya mambo ya kibabe wakati wa uchaguzi kwa kuwatumia wanajeshi. Mwamba alihukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu gerezani. Hukumu hiyo ilitolea Alhamisi iliyopita ya Septemba 11 mwaka huu.
AFRIKA KUSINI: Aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia 2009 mpaka 2018, Jacob Zuma alikamatwa na kufikishwa mahakamani mnamo Julai, 29 mwaka 2021 kwa makosa kadhaa ya rushwa na hivyo kufungwa gerezani kwa muda wa miezi 15. Aliambiwa atestify, akakataa, akala nyundo zake za kutosha.
MISRI: Janga hili pia halikumuacha Bwana Hosni Mubarak ambaye aliingoza nchi hiyo kuanzia mwaka 1981 mpaka 2011. Alihukumiwa kwa kifungo cha miaka mitatu gerezani, hiyo ilikuwa Mei, 21, 2015. Huyu alichezea pesa za umma yeye na familia yake alipokuwa madarakani.
SUDAN: Unakutana na jamaa aliyeitwa Omar al-Bashir. Huyu jamaa aliichukua nchi hiyo kuanzia mwaka 1989 mpaka alipoondolewa mwaka 2019. Ilipofika Disemba 14, 2019 akakamatwa na kupelekwa mahakamani na kufungwa kwa miaka miwili kwa kutumia rushwa na matukio mangine ambayo yalikuwa ni kinyume na sheria.
KOREA KUSINI: Aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2013 mpaka 2017, mwanamama Park Geun-hye naye alikutana na kisanga hiki mnamo April 6, 2018 alikutana na kisanga hiki baada ya kugundulika alipokuwa rais alitoa sana hongo. Kwa makosa hayo na mengine, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 ila baada ya kukata rufaa, ikapunguzwa mpaka miaka 20 gerezani.
PAKISTAN: Rais Imran Khan ambaye aliiongoza nchi hiyo kuanzia mwaka 2018 mpaka 2022 alihukumiwa kifungo cha miaka 10 mnamo Januari 30, 2024 kwa kutoa siri za taifa hilo sehemu mbalimbali. Baada ya kupewa adhabu ya kifungo hicho cha miaka kumi, kesho yake akapelekwa tena mahakamani na kuongezewa kifungo mpaka miaka 14. Hii ilikuwa ni kwa makosa mengine ya rushwa.
MALAYSIA: Aliyewahi kuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 2009 mpaka 2018, Najib Razak naye alihukumiwa kifungo cha miaka 12 gerezani mnamo Julai 28, 2020 alipohusika kwenye mchongo mkubwa wa rushwa ulioibua kashfa kubwa nchini humo, hii ilijulikana kama 1MDB.
THAILAND: Thaksin Shinawara ambaye alikuwa waziri mkuu wa nchi hiyo naye alikutana na rungo la adhabu gerezani baada ya kugundulika aliyatumia vibaya madaraka yake. Huyu jamaa alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 2001 mpaka 2006. Alifungwa kwa miaka miwili mnamo Septemba 21, 2008.
MYANMAR: Mwanamama Aung San Suu Kyl, alikuwa kiongozi nchini humo kuanzia mwaka 2016 mpaka pale nchi ilipochukuliwa na jeshi mwaka 2021. Alikamatwa na kupelekwa kwenye mahakama ya kijeshi na kufungwa kifungo cha miaka 27. Kesi zake zilikuwa ni pamoja na rushwa, uchakachuaji wa uchaguzi na kuvunja sheria za nchi hiyo.

