Pastor Aanguka Baada Ya Kumeza Viagra
Kakuyuni, Kaunti ya Makueni
Mchungaji kutoka kanisa la Jesus is Coming Tomorrow Ministries aliyetambulika kwa jina la kyoneka nanengwe alikimbizwa hospitali baada ya kuzimia, kwa madai kuwa ni kutokana na kuzidisha dozi ya vidonge vya kuongeza nguvu zinazojulikana kwa jina la Viagra.
Kulingana na ripoti, ambao wanahudumu katika tawi la kanisa la Kakuyuni, walikuwa wamepanga mkutano wa faragha na mchungaji mwanamke wa kanisa hilo. Kabla ya kisa hicho, inasemekana pasta alimtuma mchungaji huyo katika soko la Voi kununua chakula na vinywaji kwa kile alichotaja kuwa “kipindi cha maombi maalum” katika makazi yake.
Muda mfupi baadaye, majirani walitahadharishwa na kelele zisizo za kawaida kutoka kwa nyumba hiyo. Walipochunguza, walimkuta mchungaji akiwa amepoteza fahamu. Inashukiwa kuwa alikuwa amekunywa tembe nyingi kupita kiasi, jambo ambalo lilizua hisia kali na kumfanya kuzimia.
Watu walioshuhudia tukio hilo walimkimbiza katika hospitali ya karibu ambapo alilazwa akiwa katika hali mbaya. Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinaonyesha kuwa mchungaji huyo anaweza kuwa na matatizo ya moyo yanayohusishwa na overdose ya kichocheo.
Juhudi za kumpata Mchungaji Kyoneka ili atoe maoni yake hazikufaulu, na viongozi wa kanisa wamejizuia kutoa taarifa zozote kwa umma, wakisema wanasubiri ripoti ya matibabu kabla ya kutoa jibu rasmi.
Chanzo: thecountydiary

