CEO BIBI ATANIPIGA, TOA JAMANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 16
Kwetu wawili haikua shida kwani tuliamini kwenye wakati wa Mungu ndio wakati sahihi tutakaopata hao watoto, pressure ya wazazi ilikua kubwa sana ikabidi tuanze mchakato wa kutembelea hospitali, huko nilikutwa na tatizo la kuwa na uvimbe kwenye mfuko wangu wa uzazi, niliondolewa uvimbe kwa uwezo wa Mungu ndani ya miezi mitatu nilifanikiwa kupata ujauzito.
Mume wangu akufurahi sana nami nilikua katika furaha kuu kwani kuitw mama ilikua moja ya ndoto yangu, tulisubiri huyo mtoto kweli baada ya miezi tisa ya kutunzwa na kuhudumiwa vizuri kama mamq mjamzito nilijifungua salama mtoto wa kiume tulimwita Kelvin.
Wazazi wa Kendrick walisafiri kuja Tanzania kwa lengo la kumwona mjukuu wao, walikua wenye furaha sana, walituletea zawadi nyingi za kutosha, babu mtu alimpatia mjukuu wake fixed account yenye millioni mia, hiyo account mtoto angeweza kuifungua na kutoa pesa afikishapo miaka ishirini, wazazi wa Kendrick walikaa Tanzania kwa mwezi mmoja kisha walirudi marekani.
Miezi sita ilikatika, siku moja nikiwa na mume wangu tunazungumza mambo ya hapa na pale, aliniambia.
“Mke wangu najua tuna kila kitu hapa ila kuna haki yako inatapanywa mahali, nilikuahidi nitaishughulikia nazani muda umefika sasa wa kulishughulikia hilo jambo kwa ukubwa zaidi, nataka nimfungulie kesi mahakamani baba ako mdogo Peter nitazungumza na wanasheria wangu ili waliweke vizuri jambo hili na kulifikisha mahakamani ili uipate haki yako, jambo la pili nafikiria kumtafuta kaka ako Frank ili apatiwe matibabu stahiki popote pale duniani ili aweze kupona huo ugonjwa wake naamini kwa uwezo wa Mungu atarudi kwenye hali yake ya kawaida” mume wangu aliongea maneno mazuri hadi machozi ya hisia yalinitiririka alikua anawapenda sana ndugu zangu nilijisikia amani na furaha kuolewa nae
Mume wangu aliniaga kwamba anakwenda kuonana na wanasheria ili waweze kumsaidia katika hiyo kesi pia aliniomba nijiandae kwa mchakamchaka wa mahakamani, tumkimbize baba mdogo mpaka anirudishie mali zote za wazazi wangu. Mume wangu alipoondoka nilipokea taarifa yenye kusikitisha sana, ilikua taarifa ya kifo cha mama Hamida.
Sikuwa na sababu ya kuendelea kukaa nyumbani wakati msiba mzito umetokea tena wa jirani yetu wa karibu tulipokua tunakaa nyumba ya mwanzo. Nilimwomba mume wangu ruhusa ya kutoka ili niende msibani ili watu waweze kuniona, mume wangu aliniruhusu, tuliingia kwenye gari mimi na bibi, mtoto niliamua kumuacha kwa dada wa kazi kwakua mtoto hakua na tabia ya kulia lia hivyo niliona atakaa ae vizuri, tulifika msibani, tuliingia ndani walipowafiwa mimi nilikua karibu na ndugu yangu Hamida nikimtuliza na kumfariji japo apoe poe kidogo, na mimi majozi hayakuniacha salama kwani nilikua nalia kila nilipokua nakumbuka wema wa mama Hamida alikua mama flani hivi mwenye roho ya kizungu hakua na mawaa kabisa, alikua miongoni mwa binadamu wema waliokua wanaishi kwenye mgongo wa dunia.
Nikiwa msibani niliona simu yangu ikiita kwa fujo sana, nilijaribu kuipotezea ila mpigaji aliendelea kupiga si mwingine bali mlinzi wetu wa getini, niliamua kutoka nje na kumpigia ili niweze kumsikiliza vizuri.
“Boss mtoto tiii tiiiii tiiiii”
“Mtoto kafanyaje weee masai mtoto kafanyaje eti?” Niliuliza kwa sauti ya juu, masai hakua hewani tena simu ilishakatika. Nilijitahidi kumpigia simu tena na tena ila sikumpata Masai, nilimpigia dada wa kazi nae sikumpata kabisa hewani. Niliingia kwenye gari, nilikua kama nimechanganyikiwa mawazo mabaya baya yaliniandama nilijiuliza sana kipi kimemkuta mwanangu jamani, niliendesha gari nikiwa nafuta machozi na kuzuia mafua yaliyokua yanatiririka kwenye pua zangu.
Chapter 17
Nilifika nje ya geti la nyumbani hapo nilikuta gari la mume wangu kumbe nae alifika muda huo huo baada ya kupigiwa nae na masai, nilipoingia ndani nilikuta mtoto kabebwa na baba ake. Mdada wa kazi alikua chini kwa kumtazama alikua kachezea kipondo cha kuchapwa kutoka kwa Masai.
“Mwanangu jamani upo salama baba angu aaah nilimchukua mwanangu Kelvin na kumkumbatia kwa nguvu baada ya kumkagua mwilini na kumwona yupo sawa ndipo nilianza kuuliza nini kilitokea
Masai alitueleza kwamba alimwona mdada wa kazi anatoka na begi kubwa kitu ambacho sio kawaida yake, alipotaka kukagua begi hilo ndipo waliingia kwenye ugomvi, Masai alisema kwamba alimzidi nguvu na kukagua begi akihisi kuna vitu muhimu vimeibiwa ndani ya begi alimkuta mtoto kwa maana mfanyakazi alikua anatoroka na mtoto wangu. Hasira zilinipanda nikampiga vibao viwili vitatu vya moto, tuliamua kumpeleka polisi huko alihojiwa kwa kipondo cha kushtua mwili si mnajua polisi wanavyojua kuupa mwili mateso yaani unakula virungu vya maungio mpaka unatema siri zote.
Mfanyakazi aliongea mambo mazito ambayo sikuamini kweli binadamu hawaaminiki hatal kidogo. Mfanyakazi alikiri kwamba ni kweli alikua anataka kutoroka na mtoto kwani aliahidiwa kupewa pesa nyingi sana kama millioni kumi endapo atafanikisha kumuiba mtoto na kumpeleka kwa Rose. Kumbe Rose ubaya ambao alitaka kutufanyia ni kutuibia Kelvin wetu, mwanamke alikua mbaya sana yule, roho mbaya na visasi dhidi yetu vilikua vinaendelea. Kwa uwezo na mbinu za polisi walitumia simu ya mdada wa kazi kuweza kumkamata Rose aliekua anamsubiri mfanyakazi karibu na uwanja wa ndege, Rose alikua na tiketi kabisa yaani alitaka kuchukua mtoto na kukimbia nae nje za nchi ili tusimwone milele, kufanikiwa kumweka mtoto salama dhidi ya mikono miovu ya Rose, ilikua furaha kwetu haikupita hivi hivi tulikwenda kuitolea sadaka kanisani maana ni Mungu mwenyewe ndie alimwongoza masai kufungua begi la mdada wa kazi kama asingefanya hivyo tungekua kwenye sonona ya hatari kama mimi ningekufa kabisa maana sioni ambapo ningeponea maumivu yangekua makali sana, kitu ambacho kingekua. kigumu kukihimili, swala la kupoteza mtoto lisikie tu kwa mwenzako linauma balaaa. Baada ya wiki tatu za kuhangaika na kesi hiyo mahakamani, Rose alihukumiwa miaka saba gerezani kwa kosa la kutaka kufanya usafirishaji haramu wa binadamu, yule mfanyakazi wa ndani nae alihukumiwa miaka mitano gerezani kwa kuhusika kupanga na kutekeleza hila mbaya za usafiri wa binadamu.
Wakati wanapelekwa gerezani walikua wenye kulia sana, kibinadamu niliwaonea huruma kidogo ila nilipokumbuka watu hao hawakuweza kunionea huruma mimi labda ningekua katika hali gani ya kupoteza mtoto hivyo nilifuta hiko kipengele cha huruma na kuwaacha wakatumiekie miaka yao gerezani labda wakitoka watakua watu wapya wenye tabia njema hata kisasi kinaweza pukutika moyoni mwa Rose.
Tuliporudi nyumbani jambo ambalo tulilifanya ni kumpandisha cheo mlinzi wa getini alikwenda kufanya kazi ofisini kwa mume wangu, tuliona huyo alistahili kitu kikubwa kwani alituokoa na maafa.
Maisha yaliendelea siku moja mume wangu alirudi nyumbani akiwa na kaka angu Frank alikua kapendeza kwa mavazi kwani mume wangu alipomkamata huko kwa msaada wa watu alihakikisha anaogeshwa ananyolewa minywele na mindevu pia kuvalishwa nguo mpya kitu ambacho kilipungua kwa kaka ni kujielewa bado akili yake haikutulia, hali hiyo ya kuchekacheka ilitufanya tujisikie vibaya sana mimi na bibi angu siku iliyofuata alisafirishwa kupelekwa Marekani na masai alimpeleka kwenye hospitali kubwa ili kuona namna wanaweza kumtibia, niliombea sana siku hiyo ifike atakaporudi nchini awe amepona kabisa.
Chapter 18
Kesi yangu ya kudai mali za marehemu wazazi wangu ilishindwa kufikishwa mahakamani kwa haraka kwani wanasheria wote ambao mume wangu alikua anawapa kesi hiyo walikua wanamrudishia pesa na kudai hawataki kujihusisha kabisa na kesi hiyo kwani walikua wanapata jumbe mbalimbali za vitisho kwamba watarogwa na kupotea kama upepo, jumbe hizo zilipelekea kesi kushindwa mahakamani kwa wakati. kupelekwa
Mume wangu ilibidi asubiri kwa mwezi mmoja rafiki ake aliekua anamalizia masomo huko. uholanzi masomo ya sheria aweze kurejea nchini, waliweza kuiandika vizuri kesi hiyo na kuiwasilisha mahakamani. Baba mdogo alishtukia kupelekewa barua ya wito mahakamani alijilaumu sana kwa kutomjua mwanasheria mapema wa kesi hiyo, alipoulizia zaidi kuhusu uwezo wa mwanasheria Michael aliambia ni mwanasheria hatari ambae hajawahi shindwa kesi kabisa, kichwa chake kilikua chepesi kwa kushika sheria zote za nchi na zile za kimataifa pia alikua mtaalamu wa kutega mitego na kuitegua iliyotegwa akiwa mahakamani, baba mdogo aliulizia kama kuna uwezekano wowote wa kushinda kesi hiyo mbele ya Michael, aliambiwa ni ngumu sana kama atakua na plan B ya kufanya aweze kuifanya mapema maana atajikuta anapoteza kila kitu alichonacho na kuishiwa kuwa mfungwa gerezani ukonga.
Baba mdogo alipelekewa barua ya wito mahakamani, wito huo ulimtaka kufika mahakamani wiki ijayo yaani siku saba kutoka siku hiyo, maandalizi ya kisheria aliona yasingefaa kwa wakati huo hivyo aliamua kupita na plan b, nayo ni kuwatuma wazee wakazi, majambazi kuwateka mume wangu na mwanasheria Michael. Kwa upande wa Michael aliijua kazi yake vyema pia alijua ugumu wa kesi iliyokua mbele yaje hivyo alibadili eneo la kukaa akiwa anapambana na kesi hiyo hivyo majambazi walimsaka sana ila walimkosa kwa upande wa mume wangu alijisahau alihisi amani ni ile ile ya kila siku.
Siku moja kabla ya siku ya kesi alikua anatokea Gym kufanya mazoezi kwani nilimshauri akate kitambi, nikweli kilikua hakimuwashi ila niliona kufuga kitambi kwa umri wake ni sawa na kujizeesha mapema wakati anaelekea upande wa maegesho ya magari walitokea watu watatu walimteka na kuondoka nae. Mimi nikiwa nyumbani napika nilipokea taarifa ya kutekwa kwa mume wangu nilihisi kuchanganyikiwa, polisi walipambana kumtafuta usiku mzima, siku ya mahakamani imefika mume wangu hakupatikana kabisa. Nilihisi kama naota vile niliogopa sana, nilipokea simu kwa mtu ambae sikumfahamu aliniambia kwamba anae mume wangu nikisubutu kwenda mahakamani tu wanamuua, nilijikuta nachanganyikiwa, niliamua kutokwenda mahakamani ila niliwapa taarifa polisi ili waendeles kuifuatilia ile namba.
Kwa upande wa mahakamani shauri lilisomwa Ilipangwa siku ya kutoa ushahidi ambapo pia pande zote mbili zilitakiwa kupeleka ushahidi wa nyaraka muhimu ambazo zinathibitisha uhalali wa umiliki wa hizo mali kwa upande wangu sikua na nyaraka hata moja kwani kipindi hiko mimi nilikua mdogo na bibi hakuelewa chochote mambo yote yalikua chini ya ba mdogo, tulipewa wiki moja ya kwenda mahakamani.
Kwa upande wangu nilitamani kumpata mume wangu tu hizo mali hata akibaki nazo sawa tu, nilizidi kumchukia baba mdogo kwani niliamini ni yeye aliehusika kumteka mume wangu, wiki moja ilikatika na kweli nilipungua. Mwanasheria alinilazimisha kufika mahakamani nami nilienda nilikua na bibi angu tu kama shahidi wa pekee.
Chapter 19 & 20
Jaji wa mahakama alipoingia na utambulisho ulipofanyika uliitwa ushahidi wa upande wa baba mdogo aliwasilisha nyaraka alizokua nazo kwa jaji.
Upande wetu hatukua na nyaraka, aliitwa bibi akaongea pale ila hakueleweka vizuri kutokana na uchungu kumzidia na kuanza kulia, bibi angu alikua na maumivu mengi moyoni mwake, nami nilijikuta nashindwa kujizuia nililia mpaka pale jaji alipotutaka tunyamaze, kesi ilionesha anakwenda kushinda baba mdogo, lakini alijitokeza mwanaume mmoja mzee aliomba nafasi ya kutoa ushahidi upande wetu, sura yake haikua ngeni kwangu ila sikujua ni wapi nilimwona mzee huyo, jaji kwa huruma alimpa nafasi atoe ushahidi wake, aliapishwa kwaajili ya kusema kweli akawa tayari kuongea.
“Mhe jaji naitwa Mathayo Petro, nilikua mlinzi wa getini wa familia ya bwana Justin Masika kabla hajafariki aligundua hila lizilokua zinafanywa na mdogo wake Peter za kutaka kumuua na kurithi mali zote alizonazo, aliamua kunikabidhi mimi hati halali za mali zote muhimu alizokua anazimiliki, aliniambia kama chochote kitamkuta bhasi niweze kusimama na familia yake, nilikubali na kumwahidi nitafanya hivyo.
Siku ya ajari ya boss wangu Justin Masika nilimsikia Peter akizungumza na bwana mmoja akimpa maelekezo ya mahali alipo kaka ake Justin, nilimrekodi kwa siri sauti yake alipokua anatoa maagizo ya kuhakikisha kaka ake anakufa, ushahidi ni wa sauti upo kwenye hii memory card na hizo hati halali ni hizi” Mathayo Petro aliweka kituo hapo, nyaraka zilipokelewa na kupelekwa kwa jaji na Mathayo Petro aliendelea kuongea
“Mhe Jaji na watu wengine mnaweza jiuliza kwanini nilikaa kimya muda wote huo na sasa ndio nimejitokeza, ukweli ni kwamba Peter alinitishia kwamba kama nitaropoka kwa lolote bhasi ataniua mimi na familia yangu kama baba na kiongozi wa familia sikutaka hilo litokes.
Nimekaa sana shimoni kama panya mwoga nimeamua kutoka nje na kutekeleza ahadi ambayo nilimuahidi boss wangu, nawasilisha mhe jaji ubao wa mahakama ulipinduka haraka Mathayo Petro alisawazisha na alikua anaongoza. Jaji aliandika kidogo kisha sauti ya ushahidi ilisikika, baba mdogo alivyokua anapanga hila ya kumuua kaka ake. Watu kidogo wapige makofi namna mwizi alivyokamatika kirahisi, nyaraka zilichunguzwa na kujulikana kwamba nyaraka alizoleta Mathayo Petro zilikua sahihi na zile alizoleta Baba mdogo Peter zilikua za kutengeneza.
Mahakama ilifanya maamuzi siku hiyo hiyo kwamba anatakiwa kuachia kila kitu anachokimiliki, mali zote zilitakiwa kuachwa kwangu na bibi. Tulifurahi sana kila mmoja ndani. ya mahakama alipiga makofi tulipotoka nje ya mahakama baba mdogo alikamatwa kwa makosa matatu, kosa la kwanza kughushi nyaraka na kujipatia mali kwa udanganyifu, mbili alihusika kwa mauaji ya baba angu Justin Masika na tatu kosa la kumteka mume wangu Kendrick kwani polisi walikweta kumpata kwenye moja ya ghala la mazao lililokua linamilikiwa na baba mdogo Peter tulirudi na ushindi mkubwa nyumbani.
Baada ya mwaka mmoja Kaka Frank alirudi Tanzania akiwa mzima mwenye afya tele, alimchukua mzee Mathayo Petro na kuwa nae kwenye kampuni za baba kama msaidizi wake. Mimi niliendelea na familia yangu tuliongeza watoto wengine wawili, maisha yamekua mazuri sana kwetu, hatukua na kiporo hata kimoja kwani tulirudisha mali zote za wazazi wetu. Nikushukuru wewe uliesoma mpaka hapa, nikukaribishe kwa kazi zijazo kwani ni burudani Juu ya burudani.
THE END.

