π‘ππ πππ¨π£π π¨πππ ππ, πͺππͺπ π¨π ππ‘π’ππ§π
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 15
Kwanza mtoto akamuachia dada wa kazi halafu akatoka akapambane na hao visokolokwinyo, wanapewa kazi wanaichukulia kawaida.
“Enheee funga funga kila kitu hapo wateja nawaomba tutaendelea kesho kwasasa huduma imesitishwa nawaitaji wote ndani haraka” Patricia alitema cheche ya maneno halafu akaingia ndani.
Wateja wakatoka wafanyakazi wakaacha walichokua wanafanya wote wakakutana kwenye eneo la kikao.
“Sasa nataka kila mmoja ajihukumu mwenyewe kama umewahi kuiba chochote ndani ya hili duka sogea mbele pale” Patricia aliweka kituo hapo lakini hakuna hata mmoja alieweza kusogea mbele.
“Nahesabu mpaka tatu kama umewahi niibia sogea pale, moja, mbiliii, tatuuu” wote hawakusogea ni Annah peke ake ndo alisogea mbele.
“Enheee uliiba nini”
“Nimewahi chukua pea moja ya kiatu madam naomba unisamehe”
“Unanidai bei gani mwezi huu?”
“Kwakua leo ni mwanzo wa mwezi nimefanya kazi siku nne tu inakua elfu sitini.
“Haya chukua hii pesa uondoke hapa kuanzia leo hauna kazi kwa wizi uliofanya”
“Madam madaam nisamehe sirudii tena” Annah alijitetea huku anapiga magoti ili asiachishwe kazi kitendo cha kujitaja mwenyewe kimemlamba.
“Weeee usitie neno ondoka” Patricia alikua mkali kama pilipili.
“Huyo tumemalizana nae ninyi mliobaki kuna mwingine amewahi kuiba kwa nafasi ya upendeleo jitaje” ukimya ulitawala hakuna mtu hata mmoja aliejitaja.
“Sasa kila mmoja atazame hapa kwenye laptop yangu” Patricia alifungua Laptop na kuwaonesha ilikua ni video ambayo ilionesha kila mmoja wizi aliofanya ndani ya duka.
“Mungu wangu kumbe kulikua na Camera” Mfanyakazi mmoja alishika kichwa kwa kujua kumbe kulikua na camera za siri bila wao kujua.
“Ndo mmejua eeeh sasa mtajuta”
“Kuanzia sasa mko chini ya ulinzi kwa wizi mliofanya” askari polisi waliingia ndani na kuwakamata wafanyakazi wote, duka lilifungwa kwa pamoja walielekea kituo cha polisi.
“Afande hawa wasitoke wapelekwe mahakamani sina msamaha na wezi wakubwa hawa” Patricia aliongea na mkuu wa kituo.
“Bila shaka sheria itafuata mkondo wake wala usijali muhimu uniachie kidogo ya mafuta”
“Hilo halina shida nipatie namba” Patricia alichukua namba nakuweka chochote kitu halafu akarudi nyumbani kwake angalau moyo ulisuuzika.
Patricia alipofika nyumbani aliendelea na shughuli za kuandaa chakula ila mpaka saa saba usiku, mumewe hakua amerudi alimtafuta kwa simu akamwambia amekwama kwenye foleni mpaka saa kumi usiku ndo Damian anarudi nyumbani.
Patricia alimpokea mumewe kwakua alichoka sana hivyo hawakuongea juu ya jambo la kazini na asubuhi na mapema pia Damian aliwahi kuondoka kwenda kazini.
Alijaribu kumpigia waongee ila akamweleza kwamba bado amebanwa na kazi nyingi za ofisi.
Majira ya saa tano tano, Patricia aliwasha gari na kwenda mpaka kituoni.
“Afande naweza kuwaona wale waharifu wangu niliowaacha jana”
“Mbona walitolewa jana na mwanaume aliejitambulisha kwamba ni boss wao”
“Unasemaaa huyo boss wao anaitwa nani?”
“Anaitwa Damian, alisema hawezi kuendelea na hiyo kesi hivyo tuwaachie na akaenda mbali zaidi akasema ni mumeo, mmeshaongea vizuri nyumbani”
“Kubabake, us*nge gani huu afande”
“Eeeeeeh eeeeeh binti hapa ni kituo cha polisi ukileta ujinga wowote tunakusweka ndani” mkuu wa kituo alikua katika sura nyingine tofauti na aliyomwona nayo siku iliyopita.
Patricia aliondoka kituo cha polisi akiwa amenuna kweli kweli, alijaribu kumpigia simu Damian, simu haikupokelewa alienda nyumbani akasubiri mwanaume arudi usiku ili wasemezane vizuri, muda nao ulienda kasi kasi kama mimi nawewe tunavyosubiri kuona timbwili lao π.
Saa nne kamili usiku mwanaume alirudi, picha linaanza akakataa kula msosi wakati Patricia alitaka kusubiri kwanza ale chakula ili waongezee vizuri pazito hapo….
EP 16
“Kwanini hautaki kula chakula Damian?”
“Leo nimekuwa Damian na sio mume wangu tena?”
“Usigeuzie kesi hiyo kwangu nambie shida nini”
“Nakula chakula mke wangu wala usichukie”
“Sawa kaa pale ule”
“Hauji kunilisha kwani”
“Hapana sitaki kula mwenyeweπ” Patricia aliona kama Damian anamchanganya yaani alivyokasirika halafu anamletea letea matani ya kijinga.
Kuzima shida, Damian akaamua kula zake chakula, baada ya hapo wakaelekea chumbani na huko ndipo Patricia alitaka kuongea vizuri na huyo mwanaume.
“Jana ulienda polisi?”
“Ndio mke wangu, kwanza naomba unisamehe nilienda polisi kuwatoa wale mabinti bila kukwambia, nimekosa sana mke wangu naomba unisamehe”
“Niambie sababu iliyokufanya ukawatoe”
“Nimewaonea huruma tu, kwakua wamefanya wizi, tunaweza kuwafukuza tu dukani bila kuwafunga hiyo itatusaidia hata kuendelea kumfurahisha Mungu, hebu fikiria sisi tuwe uraiani, tunafurahia maisha. Halafu huko nje kuna familia zinaumia kwasababu sisi tumewafunga ndugu zao, hizi pesa na mali ni vitu vya kupita tu malkia wangu, hebu tumuepushe shetani tufanye maisha yetu sawaa mamaaaa mwaaaaah” Damian aliongea maneno kisha akayasindikizia na busu la shavuni.
Lilikua busu moto moto kweli na liliweza kumlainisha Patricia.
“Sawa mume wangu ila wakati mwingine usifanye maamuzi bila kunambia”
“Hapo hapo ndo nilitaka nikukumbushe na nilifanya makusudi ili ujisikie vile nilijisikia jana umefanya maamuzi makubwa bila hata kunishirikisha wife kweli”
“Nisamehe mume wangu”
“Yes namna hiyo sasa msamaha unajenga sana familia tuendelee kuishi hivyo na tuzeeke pamoja, najua tumeombana misamaha ya juu juu ngoja nikaoge halafu nikirudi tuombane msamaha wa kiutu uzima sasa”
“Mmmh wee bwana hushibi”
“Vyakula vyote duniani naweza kinai ila sio mwili wako, utamu wake siwezi kuelezea ila elewa tu siwezi shiba kabisa”
“Sawa babaa nenda kaoge utanikuta nakusubiri kwa hamu zote” Patricia aliachia tabasamu ambalo lilizidi kumzuzua Damian, kuna ile unakua na mtu kwenye mahusiano namna alivyomzuri na wakupendeza mpaka unajiuliza mara mbili mbili kweli huyu ndo wangu au ni upendeleo tu π.
Kuna watu ni wazuri duniani hatari sana najua hata wewe unawajua hao malaika wanaoishi duniani.
Tuendelee sasa.
Damian akiwa bafuni kuoga, simu yake ilionesha notification ya kuingia ujumbe, Patricia hakua na kawaida ya kukagua mara kwa mara simu ya mumewe ila awamu hii akaamua kutazama ni kipi kinaingia.
“Kwahiyo baby usinambie kwamba yule mwanamke wako ana michirizi mingi mapajani na huipendi kama nini”
“Sio michirizi tu ila ana huo mtambi mkubwa kama pipa, hata ungekua wewe mwanaume akivua nguo huwezi kumtamani”
“Hahahahah kwahiyo baby mimi je”
“Wewe uko na umbo matata, kifua kinajulikana kipo wapi, tumbo wapi, kiuno wapi sio yule kipipa wangu”
“Baby bhana usinichekeshe ila niambie umeenjoy penzi la jana lakini”
“Mnooo nimeenjoy”
“Si uje tu sasa huyo kibonge unalala nae wanini atakupa nini zaidi ya kukuzeesha” hiyo ilikua meseji ya mwisho kuingia kwenye simu ya Damian, alitazama hizo meseji vizuri Patricia alihisi kutetemeka hakuamini kwamba mwanaume ambae humsifia kila akisimama mbele ya macho yake.
Huko pembeni humuita majina ya ajabu, aliomba Mungu ampe uvumilivu maana hayo maumivu yake yalikua yanakata kata kama kisu. Alivyopata nguvu kidogo akachukua namba ya huyo mwanamke na kuirudisha simu ya mumewe pale pale kama hakuna kitu kilichotokea.
“Mke wangu mzuri huyoo, hapendi kuvua nguo mwenyewe mpaka mumewe nimsaidie haya malkia wangu nipo hapa kukusaidia deka utakavyo” Damian alishusha maneno mengi yenye kuchombeza ila Patricia aliendelea kumtazama tu ila huo moto uliokua unafuka moyoni ni zaidi ya jehanamu.
“Baby nini tena mbona kama haupo sawa vile”
“Nahisi tumbo linaniuma sana mume wangu yaani sielewi” Patricia alidanganya hakujisikia kufanya chochote na mumewe.
“Ooh mke wangu pole sana, pumzika tu bhasi kesho nayo siku” walilala na siku mpya ilipoingia kama kawaida Damian alienda huko kazini.
Patricia alishindwa hata kunywa chai kwa mawazo akaamua kumpigia huyo binti aliekua anachat na mumewe.
“Heee wewe si umenifukuza ofisini kwako kama mbwa unanipigia pigia simu unataka nini” bila hata salamu, sauti ya ukali ya Mimah iliuliza upande wa pili wa simu.
“Nimekupigia simu kukupa onyo uachane na mume wangu”
“Heee wewe kibonge mafuta unalazimisha au unaomba emu niombe uko mjinga wewe” Mimah aliendelea kutamba.
“Nimemaliza usinilazimishe kufanya jambo baya”
“Hahahaπ eti jambo baya unanijua au unanisikia utaingia kaburini hivi hivi unahisi mimi nyumbani kwetu nilitoka kwa kukurupuka mpaka leo nimekuonea huruma sanaaaaaa, ukisema fyokoo huyo bwana anahama mazima nyumbani kwako mpuuzi mmoja wewe” Mimah alimaliza maneno na kukata simu.
“Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii” Patricia alipiga ukelele mkubwa wenye maumivu makali π.
EP 17
“Mungu naomba uvumilivu nini hiki jamani mbona nateseka mimi aiiiiiiiiiiih, nimechoka kuteseka Mungu nichukue tu sasa nikapumzike mimi π” Patricia aliendelea kulia huku akisukumia na maombi, alilia sana.
Mchana akaamua kumpigia simu mama ake kumweleza kila kitu.
“Binti angu hao ndio wanaume, hata baba ako katika huu umri bado anaruka na vibinti vidogo ambavyo umri wao ni kama wewe, sisemi uzoee maumivu ila jitahidi kujikaza, usijidhuru ila fanya kuzungumza nae na ukiona umeshindwa kabisa omba talaka urudi nyumbani japo hiyo iwe hatua ya mwisho yaani utoke kwenye nyumba yako umwachie mwanamke mwingine aliekuja juzi tu, nakuamini binti angu unaweza kupambana na hii vita”
“Sawa ahsante mama nitajitahidi kwa hilo” angalau Patricia alipata nguvu, alikunywa chai na usiku ulipofika aliomba kuongea na mumewe.
“Mume wangu naomba unambie ukweli wote, usinifiche kitu hivi nikweli unatembea na yule binti Mimah, sitaki kuongopewa”
“Ndio natembea nae”
“Kwanini umenifanyia hivi mume wangu mimi nakunyima nini jamani si nipo nawewe kila siku ukitaka kula unakula mpaka bhasi wapi nimekosea mume wangu”
“Kwani hujioni, baada ya kuzaa umeruhusu huo mwili uwe hovyo hovyo, macho yangu yanaona na hii damu bado changa inachemka”
“Kwahiyo unaniambia hivyo kwani mwili huu mimi nimeupenda jamani”
“Bibi eeeh kwa mwili huo nani unahisi anakutamani bhana, nimechoka kukuigizia mimi hunivutii wala kunipagawisha tena”
“Jamani jamani hebu achana na huyo mwanamke wako tukuze ndoa yetu na maisha ya watoto”
“Kusema ule ukweli siwezi kuachana na Mimah hilo haliwezi kutokea kamwe”
“Kama ni hivyo siwezi kulala na wewe ten”
“Sawa tu kwani nitakosa kitu tutengane vyumba kama vipi mimi nitahamia kule chumba cha wageni , wewe baki na tumbo lako kama pipa” Damian hakutumia hata tafsida aliendelea kumpa maneno makali sana Patricia, ndoa yao iliingia kidudu mtu anaeitwa Mimah nakweli alijua kuivuruga katika miezi minne, Patricia na Damian hawakulala chumba kimoja.
Mapenzi ya Damian na Patricia yalizidi kumiminika mpaka bhasi tena wakapata na ujauzito, kuna siku Damian akawa naarudi nyumbani na wakati mwingine harudi anailea mimba. Duka ambalo walikua wanamiliki lilikufa kwani Damian alimkataza Patricia kusimamia kabisa, Damian aliua duka lake na kwenda kumfungulia Mimah duka lingine ambalo lilikua mara tatu ya duka la mwanzo na Damian alimwona Mimah ndie mwanamke wa kumfaa katika maisha yake.
Patricia alizidi kukonda ule ubonge wote ulipungua gafla akawa moja, alipoteza nyama zote, alizidi kuwa mbaya sanaa.
“Patricia mbona umekua hivyo”
“Weee acha tu ndugu yangu mwili unateketea wenyewe huu”
“Hapana Patricia wewe haupo sawa, yule mwanamke niliekua nampenda mbele ya macho yangu nikimwona naweweseka wala sio wewe Patricia” Doctor Ndunguru aliongea baada ya wawili hao kukutana hospitalini ambapo Patricia alienda kupima.
“Hata nikificha vipi haiwezi nifaa wala kunisaidia kitu, kama unanafasi naomba tukutane tuongee kidogo”
“Hamna shida kwaajili yako naweza kumwachia mwenzangu twende sehemu tukaongee” Dr Ndunguru aliacha kazi na kuondoka zake, licha ya kuoa ila bado upendo kidogo ulikua kwa Patricia, upendo wa kweli huwa haufi na kama itatokea ukafa bhasi hauozi na kama utaoza bhasi itakua mbolea ya kuneemesha maua mazuri na yenye kuvutia.
Walichagua eneo moja na kwenda kuongea vizuri. Patricia alimweleza mwanzo mpaka mwisho wa yale aliyokua anapitia kwenye ndoa yake.
“Pole sana Patricia ila ushauri wangu ni kwamba acha kuwapenda watu wengine na anza kujipenda wewe, moyo wako ufanye ujipende wewe, acha kuwaza juu ya watu wengine watakuonaje, mume wako atafanyaje, anza kujipenda wewe, usiruhusu mawazo yakutawale, fanya mazoezi, kula kwa wakati, jitengeneze na urudi kuwa yule Patricia asiejali wala kuwaza chochote”
“Unahisi hilo litasaidia?”
“Ndio ndio nakupenda na ndio maana nakwambia haya yote”
“Sawa nitafanya hivyo” wawili hao waliagana na kila mmoja kupita upande wake, Patricia akijipanga kuanza mwanzo mpya.
EP 18
Majira ya usiku Damian alikua nyumbani anacheza cheza na mtoto wake, mara kidogo mlio wa gari ukasikika kwa nje, Damian alisogea mpaka dirishani ili kutazama hiyo gari iliyokuja mahali hapo majira kama hayo.
Ilikua gari ya gharama sana Rolls Royce. Kuona gari hiyo Damian macho yalimtoka na kwenye hiyo gari alimwona mkewe anashuka.
Alipanic maana kwa vyovyote alijua kwamba mkewe ameletwa na mwanaume tena mwenye msuli mpana wa pesa. Damian akapania kweli akiingia tu amnyooshe vilivyo mpaka amtaje huyo mtu ambae amemrudisha usiku.
“Baby njoo najisikia uchungu baby nakufa mwenzako wahiiii” baada ya kupokea simu ya Mimah alimsikia mwanamke huyo akiongea hivyo kutokea upande wa pili wa simu.
“Sawa nakujaa usife mama angu” Damian alichomoka kuelekea kwa Mimah njiani alipishana na mkewe amependeza mno kwa nguo za mazoezi.
“Kesho nikirudi hapa uwe na majibu yule mwanaume ni nani aliekuleta usiku huu nyumbani kwangu mjinga wewe” Damian aliondoka haraka huku nyuma Patricia alimsonya na kumbeba mwanae.
Huko kwa Mimah alichukuliwa mpaka hospitalini na Mungu akamsaidia akajifungua mtoto wa kike, tena alifanana mno na Damian
“Naona umenizalia mama angu, nikimtazama sura amefanana sana na marehemu mama angu ahsante kipenzi na hongera sana” Damian alitoa sifa kedekede kwa Mimah.
“Sawa babaa unajua mwanamke akikupenda anakuzaa π” furaha ilitawala mahali hapo kwa wawili hao.
“Hebu mpenzi naenda kazini mara moja naona nimeitwa huko kuna kikao cha management nitakurudia badae hivi”
“Sawa mume wangu uwe makini huko si unajua tunakutegemea mimi na binti ako eeeh”
“Hilo nalijua nitarudi kwaajili yenu binadamu ninaowapenda zaidi duniani” Damian alichomoka na kuwahi kiwandani, kulikua na kikao kizito huko sababu kulikua na wageni kutoka nje ya nchi maana kampuni ilikua ya kimataifa.
“Engineer Damian utapita na wageni hao wafanye ukaguzi kwenye mitambo yote”
“Sawa sawa boss hakuna shida” waliongozana kufanya ukaguzi, hao wazungu wataalamu walipima mitambo yote huku wakiandika ripoti kamili ya mienendo ya mitambo walivyokamilisha sasa kikao kikakaliwa.
“Engineer Damian, ulikabidhiwa hii mitambo kwaajili ya kuichunguza na kuongoza ifanyiwe services mara kwa mara kwa hali iliyopo mitambo ni chakavu mpaka haiwezi kufanyiwa services nchini, hii ni hasara kubwa sana kwa kiwanda chetu kwa uzembe huu mkubwa uliosababisha mtu tuliekuamini, kuanzia sasa huna kazi”
“Boss yanazungumzika haya”
“Nimeongea kwa kiswahili kabisa nenda nyumbani kama kuna lolote utafahamishwa usionekane tena kiwandani sawa”
“Sawa mkuu” Damian aliongea kwa unyonge sana akaaga na kuondoka, hakukumbuka hata kwenda hospitalini alipomuacha Mimah.
Alivyofika nyumbanu, akakuta nyumba ina mfanyakazi na mtoto tu.
“Mama enu ameenda wapi”
“Sijui amekwenda wapi ila alinambia atarudi baada ya siku tatu, niwe makini na mtoto tu”
“Malezi gani haya ya mtoto huu ni upumbavu” Damian akaanza kumpigia simu Patricia lakini simu haikupokelewa, akaingia whatsapp akamkuta yupo online akatuma meseji, zilionesha tiki mbili lakini hazijibiwi.
Kutazama status ndo hapo Damian alianguka chini kabisa maana alichokua anakiona kizito……
EP 19
Alimuona mkewe amevalia nguo za kitalii anakula bata Ngorongoro anaenjoy kabisa kwa raha zake.
“Kwa vyovyote hajaenda peke ake huyu mjinga halafu mbona anazidi kuwa mzuri” Damian alipata wasaa mwingine wa kumtazama mkewe, lile umbo matata lenye uwezo wa kumpagawisha mwanaume yeyote alikua nalo mkewe.
Alifikicha macho ili aone vizuri alimwona mkewe akiwa na uzuri wa ajabu.
“Babaa tumekumiss eti ukuje” Mimah alijidekeza kwenye video call.
“Hebu subiri kwanza nitakupigia” Damian alijibu kwa ukali kidogo, alifananisha Mimah alivyo na mkewe alivyo alijilaumu sana alifata nini kwa Mimah.
Alituma meseji nyingi mno bado hakuweza kujibiwa, alipiga simu ndo haikupatikana, mawazo ya namna mkewe anavyoweza kuikatikia akaunganisha doti kwamba yupo mwanaume anakatikiwa hivyo aloooh ilijua kumuuma Damian mpaka machozi yalimtoka, hakwenda chumbani usiku huo alilala sebleni.
Aliendelea kubaki nyumbani bila kwenda hospitali kwa Mimah hakupokea wala kujibu jumbe za Mimah, alichokua anawaza ni mkewe Patricia. Baada ya siku tatu Patricia alirudi nyumbani.
“Heee mbona haujaenda kazini kwema kweli”
“Oooh mke wanguuuuuuuuuu uuuuuuuh π” Damian alimkumbatia mkewe huku akiwa amepiga magoti.
“Nimekumiss mke wangu naomba unisamehe sirudii tena kukufanyia vibaya” Damian aliomba sana msamaha siku hiyo.
“Sawa nimekusamehe ila kwa sharti moja”
“Mpigie Mimah mkatae mtoto wake na umwambie mmeachana kuanzia leo hii humtaki tena”
“Jamani mke wangu kwanini nimkatae yule malaika?”
“Kama hutaki kufanya hivyo kila mtu ajue hamsini zake”
“Bhasi bhasi nafanya hivyo mke wangu” Damian alimpigia simu Mimah.
“Baby uko wapi nimeruhusiwa kutoka hospitalini hebu uje huku mtoto anaumwa umwa”
“Sikia wewe mchawi mkubwa, dawa zako ulizokua umenirogea zimeisha ni hivi narudi na mke wangu, usinijue kuanzia leo”
“Heee makubwa na huyu mtoto je”
“Malaya mkubwa huyo mtoto sio wangu”
“Hebu rudia nikusikie vizuri”
“Huyo mtoto sio wangu sikutaki wewe wala yeye”
“Sawa babuu unahisi siwezi kumlea mwanangu, nisikuone pua yako kwenye maisha yangu kubwa jinga weee” Mimah nae hakua mnyonge alirudisha vita ya maneno baada ya hapo ni kublockiana na kufuta namba.
“Kwahiyo mke wangu leo si tutalala wote”
“Aah bado tukachek kwanza afya tukirudi mambo yote yataendelea vizuri walienda hospitalini walipima vipimo vyote na hakuna hata mmoja ambae alikua na maambukizi”
“Ahsante Mungu kwa kunirudisha tena kwenye familia yangu, nilipotea na kuuacha upendo wa kweli ila saivi nimerudi nakuhakikishia sitomuumiza tena huyu mwanamke ulienipatia na nikala kiapo mbele ya madhabahu yako” hayo yalikua maombi ya Damian kabla ya kulala, wangewezaje kulala bila kucheza mechi wakati ulipita mwaka na miezi minne bila kulala kitanda kimoja kila mmoja alionesha kumuhitaji mwenzake sana.
EP 20
Mechi ilichezwa kwa uzuri kabisa usiku huo, na siku ziliendelea kama mapenzi yao yameanza upya mwezi mmoja ulikatika na Patricia alikua na mimba nyingine.
“Woyoooo Mungu ametupatia uzao mwingine wa kufurahisha nafuraha sana mke wangu”
“Nna furaha pia mume wangu unahisi huyu mtoto atakua wa jinsia gani?”
“Natamani awe wa kike ili tubalance vizuri wakiume na wakike na hiyo siju unajifungua nitaruka ruka kwa furaha”
“Hahahah hebu nioneshe utakavyofanya?”
Damian alioneshq atakavyoruka ruka kwa furaha.
“Vizuri bhasi umeshaona ila wewe hautakuwepo pembeni yangu siku hiyo”
“Heeee kivipi mbona sikuelewi mke wangu”
“Yaani ni hivi kuanzia sasa mimi na wewe bhasii”
“Bhasi kivipi nimekosea wapi mke wangu”
“Kitendo cha wewe kusaliti ndoa na kwenda kuishi na mwanamke mwingine pale pale uliyafuta mazima mapenzi yangu juu yako”
“Sasa kwanini ulinirudisha tena huoni huo ni ukatili mke wangu jamani π”
“Hapana sio ukatili ukilinganisha na wewe uliyonifanyia, nakurudisha mtaani kule nilipokutoa ili ukajifunze ukipata nafasi nyingine kwenye maishq yako usiichezee”
“Jamani kumbe siku zote ulikua unaniigizia mpakq tunapata mtoto mwingine ni nini umefanya au una mwanaume mwingine”
“Sina mwanaume mwingine ila sikutaka kuchanganya damu na wakati watoto nawapenda, ndoto yangu ilikua kupata watoto wawili na sasa huyu atakua wapili sijawachanganya baba hivyo maisha yataenda kwa raha kabisa”
“Mimi siondoki hapa nakwambia, siondoki mimi”
“Hahahahahaha weee jamaa nilikua nakutamani kweli naona unataka kipondo changu ondoka mwenyewe kabla vijana wangu hawajakushughulikia, unapendwa unaonesha maringo” Kepten Pius aliingilia ugomvi, wajeda wawili waliokuja nae walimtoa nje ya geti Damian akiwa katika hali ya kulia na kujutia.
Alimpigia simu Mimah kumuomba aende kwake ila alikutana na hayo matusi ambayo hajawahi kutukanwa tangu anazaliwa. Damian alikosa kazi, alikosa msaada akarudi mtaani kuokota makopo ili kupata mlo wa siku, maisha yalipinduka kwa haraka sana.
Kufikia hapa ni mwisho wa kazi hii nzuri inayokwenda kwa jina la Nimekupa ulambe wewe umeng’ata, Damian alipewa alambe ili afaidi ila yeye akaamua kung’ata na kuacha maumivu makali ambayo yalimrudia mwenyewe.


