πππππ ππ¨ππͺπ π¬π π ππ πͺππ‘ππ¨, ππππ©π¬π’π‘ππππ‘π¬π π‘πππ¦ππ πππ π π πππ ππππ, π‘πππ‘π π¬π π‘π¬π¨π ππ π¬ππ‘ππ¨ π πͺππ‘π¬ππͺπ
EP 6
βTafadhali, usiende. Rudi ndani. Ninaahidi kuzungumza na mke wangu. Nitazungumza naye akirudi.β Daudi alisema kwa sauti ya juu kama mtu aliyevurugwa.
βUtamwambia nini? Utamwambia acha kunyamaza na kukasirika kwa kuwa ulinipa ujauzito? Nijibu! utamwambia anipige kofi, a au anifukuze? Au utamsambiaje ! hayo yote uliyakiwa kuyafanya kabla ya mimi kuja huku kama ulitama amani ndani ya nyumba hii. Juliet alimuuliza Daudi maswali mengi kwa sauti ya juu.
βTulia Juliet. nipe hadi leo jioni nishughulikie suala hili. Rudi ndani ukapate ukapumzike. Sote tulikuwa na usikumbaya! Nitalishughulikia hili. Nipe muda nijue cha kufanya. Tafadhali mpenzi!β Daudi aliomba.
Akaanza kumgusa Juliet kwa mahaba naye akamgusa kimahaba. kwa upole, alimrudisha sebuleni. Muda si mrefu wakaangukia mto mmoja laini pale sebuleni wakavua nguo na kufanya mapenzi.
Alipomaliza tu, Daudi alijiandaa kwenda kazini. Juliet alilala kwenye sofa na hakuamka hadi mida ya jioni Sophia aliporudi kutoka kazini.
βJuliet, habari? Lazima uwe dhaifu sana kwa sababu ya hali yako. Umekula?” Sophia alimuuliza Juliet. juliet alikuwa akijaribu kujifanya kama mtu ambaye bado alikuwa amelala lakini kiukweli alikuwa anamuogopa Sophia.
βNdio nimekula wali.β Juliet alidanganya. Hakuna wali ndani ya nyumba na Sophia alijua anadanganya. Alikuwa akijaribu tu kukwepa kuchukua chochote kutoka kwa Sophia.
βAngalia hapa, nimekununulia aiskrimu, juisi na Apple. Kula apple kwanza kisha mimina na juisi hii, fuatisha ice cream. Sijawahi kuwa mjamzito lakini nimesikia wajawazito wanapenda kula βvitu vitamu vitamu.β Sophia alisema huku akicheka. muda wote alipokuwa akiongea, Juliet alikuwa akitetemeka. Alichukua kifurushi kutoka kwa Sophia na kukiweka karibu yake kwa nguvu.
“Kwa nini unaniogopa?” Sophia aliuliza.
βNiambie Sophia. Unafanya nini? Unadhani sijui kuwa unnataka kunitilia sumu mimi na mtoto wangu aliye tumboni? Wewe mchawi tasa! mbona huna hasira kuwa nililala na mumeo? Ni mwanamke wa aina gani hufanya sherehe ya kukaribisha mimba ya mke wa nje ndani ya nyumba yake? .Najua mpango wako.
Unataka kunitilia sumu mimi na mtoto wangu ambaye hajazaliwa. Chukua vitu vyako kula mwenyewe. β Juliet alisema.
“Mpenzi wangu, hakuna haja ya kupiga kelele. Tulia na ufurahie maisha yako sawa. Umebarikiwa kuwa mjamzito. Watu wengi wameomba kwa miaka mingi kupata mtoto huyu ambaye Mungu alikupa kwenye sinia ya dhahabu. Unapaswa kuwa na furaha na kubeba mtoto kwa amani.” Sophia alisema. hakujibu moja kwa moja tuhuma alizozitoa Juliet.
Juliet aliamua kuanzisha ugomviye l ili kuona Sophia atafanya nini. Aliinua mkono wake wa kulia na kumshushia kofi zito Sophia ili tu kumchokoza Lakini Sophia alikataa kulipiza kisasi. kofi lilimuuma sana lakini alificha maumivu.
βMpenzi wangu utajiumiza. Kumbuka wewe ni mjamzito. Usijali, mama yangu aliniambia kuwa wanawake wajawazito huwa na usawa wa homoni ambao huwafanya wawe na mabadiliko ya hisia. Nina hakika unapitia mabadiliko ya hisia. kwa hivyo, ninaelewa kabisa kwa nini umenipiga kofi. Tulia! Kwa muda wa miezi tisa, tutabeba mtoto wetu kwa furaha. Kwa kweli, nina furaha kwamba una mimba ya mume wangu.β Sophia alisema huku tabasamu pana usoni mwake. Juliet hakuamini alichokiona na kukisikia. sophia alitoka eneo lile kana kwamba hakuna kilichotokea na kuingia jikoni na kuanza kupika.
Juliet alichukua simu yake haraka na kuagiza usafiri wa Uber. Jamaa wa Uber alifika chini ya dakika 10 na Juliet akachukua begi lake na kuruka ndani ya gari.
Daudi aliporudi kutoka kazini hakumuona Juliet.
βJuliet yuko wapi?β Daudi alimuuliza mkewe Sophia.
“Nilimwacha hapa nilipoenda jikoni kupika.” Sophia alisema kwa sauti ya wasiwasi. Daudi alitoka nje ya nyumba kwa kasi na Sophia akamfuata.
“Twende tukamtafute pamoja.” sophia alisema huku akimkimbiza mumewe.
βRudi nyumbani!, nimesema rudi!β Daudi alipiga kelele kwa hasira mithili ya mbogo aliyejeruhiwa akimtafuta Julliet…
EP 7
Juliet alishuka kutoka kwa usafiri wa Uber na kuelekea kwenye barabara inayoelekea nyumbani kwake. Barabara iliyoelekea nyumbani kwake ni mbovu , gari haliwezi kupita kupita.
Piikipiki pekee ndizo zilizokuwa zikipiaa barabarani hapi kwa vile ulikuwa msimu wa mvua na kulikuwa na maji tope jing ndiyo maana Uber haikuweza kumpeleka mpaka nyumbani.
Juliet alivuka barabara na kugeuka kuelekea mtaani kwake. Alikuwa akiburuta begi lake kwa tabu sana. Alikuwa amechoka na kulemewa na yote yaliyotokea ndani ya siku mbili zilizopita. Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni, jua lilikuwa likizama na giza lilikuwa limeanza kutanda kidogo.
Pikipiki ilionekakuinakuja nyuma yake, ilisimama na mwendesha boda akaanza kuzungumza naye kama malaika aliyetumwa kutoka juu kumsaidia begi lake.
β Habari za jioni, ningependa kukusaidia kukusafirishia hadi nyumbani kwako. Ni bure; Nakuahidi hutalazimika kulipia chochote. Naona una mimba na si vizuri kutembea peke yako na begi zito kutokana na hali yako.β Mwendesha boda alisema kwa sauti ya uchangamfu ambayo ilikuwa ngumu kupingwa na Julieth.
“Usijali! Ninakushukuru sana lakini nyumbani kwanhu sio mbali sana. Nitatembea tu. karibu niko nyumbani. Asante sana.” Juliet alisema. Ndani ya akili yake, alijua anahitaji msaada, alikuwa amechoka na mtoto tumboni alikuwa akimpiga teke tangu aliposhuka kwenye Uber. Lakini aliogopa kupanda boda tu ambayo dereva wake hakumjua.
βNasisitiza nataka kukusaidia. Tafadhali niruhusu nikupeleke nyumbani. Mke wangu pia ni mjamzito na ninaelewa jinsi jambo hili linavyoweza kuwa gumu kwako.β Yule mwendesha boda alisema huku akishuka kutoka kwenye boda na kumkimbiza Juliet ambaye aliendelea kwenda mbele bila kujali.
βTafadhali, ngoja nikusaidie. Usiogope.β mwendesha bodaalisema, aliinyakua begi lake kwa nyuma. Aliliburuta mpaka ilipokuwa boda yake.
Haukupita muda mrefu Juliet akakubali na kupiga hatua kadhaa kurudi nyuma kisha akapanda boda. Mwendesha boda aliweka begi lake mbele ya pikipiki na wakaanza safari.
juliet alitarajia safari fupi ya kwenda nyumbani kwake, ingekuwa kama dakika tano tu kwani hapakuwa mbali na pale alipopandia Lakini safari ikawa ndefu kuliko ilivyotarajiwa. Alitaka kumuuliza mwendesha boa kwa nini hakuwa akisimama, lakini hakupata maneno. Alitaka kupiga kelele lakini sauti haikutoka. Alitaka kumpiga kofi mgongoni mwendesha boda kumwambia asipite nyumbani kwake lakini, mikono yake ilihisi kama imefungwa kwenye mwili wake kwani hakuweza kuinua. Mwendesha boda aliendesha hadi msituni mbali na mji.
Wanaume wengine wanne ambao tayari walikuwa wakimsubiri ndani ya msitu mnene waliungana naye na kumfunga Juliet na kumketisha chini kama mtumwa.
π€π€π€π€π€π€
Wametumwaaaa….????
EP 8
“Niko wapi? Kwa nini umenileta hapa?β Juliet aliwauliza wale wanaume baada ya kufanikiwa kupata fahamu zake na kufumbua macho. . Ilionekana kama mtu alimroga vikali.
βKaa kimya! Tumekuteka nyara.β Mwendesha boda aliyemchukua Juliet kutoka barabarani dakika chache zilizopita alisema. Sauti yake ilikuwa kali sana tofauti na ilivyosikika kwa upole alipojitolea kumpeleka nyumbani. Juliet alitazama huku na huko na kuona wanaume waliokuwa wamesimama kando yake wote walikuwa na bunduki.
Mmoja wao alikuwa na jeraha lililotoa damu . Juliet aliogopa sana.
βTafadhali, niachilie. Niache niende. Nina mimba. Je, huna huruma? Kwa nini unamteka nyara mwanamke mjamzito? niache niende, nakuomba.β Juliet aliomba. Lakini wanaume hao watatu walicheka kwa sauti kana kwamba wanataka kumdhihaki kwa kuomba aachiliwe.
“Mpenzi wangu! Pumzika tu. Huendi popote. Uko katika eneo la hatari! Sasa tunampigia simu mumeo atuletee pesa. Asipokuja, tutakuua na kunyofoa viungo vyako vya mwili kwa ajili ya kuuza.β Mwendesha boda alisema.
Yule mtu mwingine akachomoa jambia yake na kuanza kugusa sehemu zenye ncha kali kana kwamba tayari anataka kuanza kumchinja Juliet.
Wakati huo huo, Daudi alifika nyumbani kwa Juliet na hakufanikiwa kumkuta . Alianza kujiuliza wapi ameenda? . Mlango ulikuwa bado umefungwa. Daudi alikuwa na ufunguo wa ziada wa Juliet ambao aliutumia kufungua mlango lakini kila mahali palikuwa wazi bila kuwa na dalili yoyote ya kuwepo kwa Juliet.
Daudi akatoka nje ya eneo hilo, akachukua simu yake na kumpigia simu huku mapigo ya moyo wake yakimuenda kasi mithili ya mwanamke anayedaiwa hela ya mchezo.
“Mumeo anapiga simu nilitaka nimpigie mda huu!Una bahati sana, una mwanaume anayejali ambaye anajua unapokuwa hatarini.” Mwendesha boda alisema kwa sauti ya juu. Muda sasa ni 8:30 usiku na giza lilikuwa limetanda kila mahali. watekaji nyara walikuwa na taa yenye mwanga mkali sana iliyotundikwa juu ya mti kando yao.
βHabari mpenzi! Uko wapi? Nimetoka tu kwenye nyumba yako na hauonekanu. Umeenda wapi?” Daudi aliongea akwa simu akitarajia kusikia sauti ya Juliet.
βSikiliza rafiki yangu!β Sauti kali ilisikika. Mimi ndiye yule mwendesha boda aliyemteka nyara Juliet.
βHuyu si Juliet. Huyu ni mimi. Usijisumbue kuhusu jina langu, lakini nimemteka nyara Juliet wako na sasa tuko mbali sana kwenye kichaka kinene. Sasa, sikiliza kwa makini sana na ufanye kama ninavyokuelekeza laa sivyo hutomuona tena.
βUtaniletea milioni 25 kabla ili nimuachilie Juliet wako, ukishindwa kufanya hivyo ndani ya siku 14 tutamuua, tutamchinja yeye na mtoto aliye tumboni na kuuza viungo vyao vya mwili. , hupaswi kuwambia polisi kuhusu hili kwa kufanya hivyo mambo yatazidi kuwa mabaya .
Kumbuka, milioni 25, siku 14 na usije na polisi” Mtekaji alionya.
Daudi alihangaika sana, aliogopa na kufadhaika. Hakukumbuka ni lini alilia katika maisha yake . Machozi yalitiririka kama maji yanayotoka kwenye bomba.
Daudu alikuwa amesikia stori za kutisha za watu kutekwa nyara na kuuawa mtaani lakini hakujua zingemjia yeye au mpendwa wake yeyote.
Alikimbia hadi barabarani ambako aliegesha gari lake na kuanza kurudi nyumbani kwa mwendo wa kasi kiasi kwamba gari hilo lilikaribia kugonga mti mkubwa uliokuwa kando ya barabara.
Aliendesha gari ndani ya nyumba yake na kuenda kupumzikao .
Alipiga kelele kwa sauti kubwakama mbwa aliyejeruhiwa.
Akaruka ndani ya nyumba mithili ya simba mwenye fujo aliyejiandaa kumrukia Sophia mke wake maana anaamini kabisa alipanga na kuwalipa vijana waliomteka Juliet. Sasa, Sophia yuko katika shida kubwa na kuna moto mkali mbele yake…
EP 9 & 10
βUlichokifanya ni sawa eeh!? Hatimaye umefanikisha mpango wako! Sasa una furaha, sawa?” Daudi alimuuliza mkewe Sophia mara akaingia sebuleni na kumuona akiangalia luninga.
βUnazungumzia nini? Tatizo ni nini mpenzi wangu?β sophia aliuliza kwa sauti yake ya kawaida ya upole.
βOh! Usijifanye kana kwamba hujui ninachozungumza. Wewe mchawi mwovu, tasa.β Daudi alimwambia Sophia. Maneno hayo yalivunja moyo na roho yake lakini bado alidumisha utulivu wake.
βTatizo ni nini mpenzi? Je, ni kuhusu Juliet? nilikuambia sina hasira kwamba ulimpa mimba. Nini kimetokea? Kuna tatizo gani?” Sophia aliuliza. Bado alikuwa mtulivu sana na mwenye kushangaa .
βFunga mdomo wako uliooza kabla sijakufanya kitu kibaya!. Ulipanga na genge lako la wahuni kumteka nyara Juliet sivyo? ndio maana umekaa kimya. Aliniambia unapanga mabaya juu yake , leo imejidhihirisha. Sasa, umewaita wahuni wako kumteka nyara bila kufikiria kuhusu hali yake. Unataka afe ili mimi nibaki bila mtoto maishani mwangu?. Wewe ni mwovu sana na nitakuonyesha kuwa mimi ni nan” Daudi alisema.
βSikufanya chochote. Mimi sina hatia! Ninampenda Juliet kwa dhati na siwezi kamwe kufikiria kumuumiza.β Sophia alisema kwa utulivu. Kwa mara ya kwanza tangu sakata la ujauzito lianze, alilia machozi ya kama mtoto mdogo. Lilikuwa ni jambo moja kubwa sana kwake kuitwa mteka Nyara.
“Nyamaza! Na usijaribu hata kunichanganya na machozi yako ya kuigiza kwa sababu utalipa uhalifu huu uliofanya. Ninawapigia simu polisi ili uweze kuwaeleza jinsi ulivyomteka Juliet. Utaozea jela.” Daudi alisema kwa sauti ya juu sana. Alichukua simu yake na kupiga namba ya dharura ya polisi, ndani ya dakika chache likafika gari la polisi aina ya Hilux na Sophia akakamatwa na kupelekwa kituoni.
Safari ya kuelekea kituo cha polisi ilikuwa ngumu kwani gari aina ya Hilux lilikuwa likitembea kwa kasi sana. Sophia alilazimishwa kukaa kwenye benchi nyuma ya gari. Polisi wawili walimlinda wakiwa na bunduki zilizojaa risasi. Mume wake, aliwafuata akiwa kwa gari lake mwenyewe.
Punde si punde, wakawa wamefika kituo cha polisi na Sophia alikuwa amefungwa pingu kama mwizi.
Aliburuzwa hadi kituoni na kupelekwa kwenye chumba cha mahojiano ambako alihojiwa na afisa wa polisi aliyeonekana mkatili kweli.
Daudi aliitwa kwenye chumba cha mahojiano.
“Ulimteka nyara mpenzi wa mumeo?” Askari polisi aliuliza. Sauti yake ilikuwa ya kichefuchefu na isiyopendeza. Alikuwa akiandika baadhi ya pointi wakati akizungumza na Sophia.
“Hapana! Sikumteka nyara mtu yeyote.” Sophia akajibu. Hakuwa akilia na alikataa kuonyesha dalili yoyote ya kuzorota kihisia. Sauti yake ilikuwa thabiti.
“Mwongo wewe! Afisa usimsikilize. Alimteka Juliet.” Daudi alisema. Alikuwa akipiga kelele.
“Nyamaza bwana Daudi. Mimi ndo afisa wa polisi wala sio wewe.” Yule polisi alisema.
“Ulifanya nini ndani ya saa 72 zilizopita? Ulikwenda wapi na ulishiriki shughuli gani?” Askari polisi alimuuliza Sophia.
“Mimi ni mwalimu. Nilikwenda kazini siku ya Ijumaa, nikaandaa tafrija kwa ajili ya mume wangu na mpenzi wake siku ya Jumamosi. Hayo tu ndo nakumbuka.” Sophia alisema.
Afisa wa polisi alishangaa aliposikia kuwa Sophia aliandaa tafrija ya mumewe na mpenzi wake.
“Kwa nini ufanye tafrija kwa mwanamke anayejaribu kuchukua mume wako ?” Aliulizwa Sophia.
“Ilikuwa kwa nia njema na si kitu kingine chochote pia, ni mjamzito, kwa hiyo ilikuwa ni njia ya kumkaribisha yeye na mtoto nyumbani kwetu kwani ndivyo mume wangu anataka.” Sophia alijibu.
“Nipe simu yako.” Afisa wa polisi alimwambia Sophia. akaichukua simu yake, akapekua namba zilizopigwa kana kwamba anataka kujua kama amewapigia watekaji. Lakini hakupata kosa lolote na akamrudishia simu.
“Unaamini kwa dhati kwamba mkeo alimteka mpenzi wako?” Askari polisi alimuuliza Daudi.
“Ndiyo. alikuwa amepanga kila kitu huku akijifanya kuwa mzuri na mwenye furaha.” Daudi alisema kwa sauti ya juu.
“Bwana Daudi , hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kuwa mkeo alimteka nyara mpenzi wako. Nilichoona ni ushahidi tu kwamba alikuwa mwema kwake. Huku ni kupoteza muda tunamwachilia mke wako bila mashtaka. Tutaanza kazi ya kutafuta na kuokoa mara moja ili kumwokoa mpenzi wako. Mpeleke mkeo nyumbani.” Afisa wa polisi alisema huku akisimama na kuwatoa Daudo na Sophia nje ya chumba cha mahojiano kabla hawajaondoka, Daudi aliandikisha maelezo ya jinsi watekaji nyara walivyodai milioni 24. Waliendesha gari hadi nyumbani kimya kimya bila kusemeshana.
Walipofika nyumbani Daudi aliidondosha simu yake kwenye chini kwa hasira kisha akaingia chooni kujilaza.
Sophia alichukua simu na kutafuta namba ya simu ya mtekaji. Aliona simu ya mwisho iliyopigwa na Daudi kabla ya kupiga polisi ilikuwa ni namba ya Juliet. Anayo kwenye simu yake kwa sababu yeye na Juliet ni marafiki.
sophia alitoka na kupiga namba ya Juliet kwa simu yake na watekaji wakapokea.
“Halo! mimi ni Sophia. Mimi ni dada yake Juliet. Usimdhuru dada yangu, nakuja kukupa hiyo milioni 24 ” Sophia alisema na kukata simu bila kuwaruhusu watekaji kuitikia.
Muda ulikuwa tayari 10:30 jioni na kila mahali kulikuwa na giza. Sophia aliingia ndani, akaoga na kulala. Kesho ni siku ya vita…..
INAENDELEA


