π‘ππ πππ¨π£π π¨πππ ππ, πͺππͺπ π¨π ππ‘π’ππ§π
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 4
“Afande mbona hakuna mtu humu ndani”
“Acha tufanye kazi yetu kama hujamficha jambazi humu ndani bhasi utabaki salama na kinyume na hapo jiandae kukabiliana na sisi” inspector wa polisi alikua kauzu kweli kweli hakutaka Patricia kuwa kizuizi hata kidogo.
Walilazimisha na kuingia ndani walikagua kila upande wa nyumba hawakuweza kumwona Damian hata Patricia alijawa na maswali mengi kijana huyo ameelekea wapi.
Kuwa mpole na kusubiri kisha kuombea Damian asikamatwe maana akakikamatwa siri yao itajulikana kwamba walimteka na kumpa kipondo cha nguvu.
polisi walikagua na hawakufanikiwa kumpata huyo jambazi, polisi waliaga kwa mikwala mingi kisha wakaondoka zao. walivyoondoka tu akaanza kumtafuta
“Uko wapi wee binadamu au umenifia humu ndani duuh na hivi sijawahi kaa nyumba moja na maiti au atakua mwanga huyu kijanaπ₯Ή” mawazo mengi yalipita kichwani mwa Patricia na kumpa sana hofu.
Alianza zoezi la kumtafuta Damian alimtafuta ndani ya nyumba bado hakumpata akakumbuka kuna eneo moja tu hajalifikia na hata polisi pia hawakupita huko, akasogea mpaka kwenye tenki la kuhifadhia maji ya mvua huko akachungulia ndani kwa msaada wa simu akamwona Damian amejificha humo ndani bahati nzuri ni kwamba tenki halikua na maji mengi ila alikua mwingi wa kutetemeka mwili kwa baridi kali.
“Toka huko njoo nje tafadhali wameshaondoka polisi” Patricia alipaza sauti ila Damian ni kama aliendelea kumtazama tu.
“Kaka kakaaa toka bhasi” Patricia aliendelea kusema kwa nguvu ila Damian bado aliendelea kumtazama tu.
Ikabidi Patricia nae aingie kwenye tenki maana alihisi kijana huyo amepatwa na mshtuko wa gafla.
Patricia alimtikisa sana Damian ila Damian bado aliendelea kumtazama tu, akahamia kwenye kumwagia maji mengi sana.
“Nahisi baridi” Damian aliongea maneno mawili tu kisha akamkumbatia Patricia.
“Niachie bhana niachieeeeeeeee nitakusemea kwa kaka” Patricia alijitahidi kujiondoa mwilini mwa Damian ila bado Damian aliendelea kumkumbatia mpaka Patricia nae ikabidi atulie tu.
“Niko tayari tunaweza kwenda sasaπ€¨” Damian aliongea ikabidi arudie kwa mara nyingine ndipo Patricia akaweza kumsikia akili ya bibie ilikua kilomita za umbali mrefu japo halikua kumbatio rasmi ila kuna upande wa raha pia aliusikia.
“Sawa sawa tangulia nakufuata” Patricia alipendekeza ila Damian aliamua kufanya lingine akambeba Patricia ili watoke haraka haraka.
“Wewe kaka siku ya kwanza halafu unaleta kunizoea zoea unahisi mimi ni mwepesi mwepesi mjinga wewe ngoja kaka angu atakutia adabu π‘” Patricia alibadilika gafla baada ya kufika nje.
“Huogopi nyoka?”
“Unanitishia sio”
“Nilikubeba kwaajili ya usalama wako”
“Usalama wa konyo”
“Haya huyo nyoka pembeni yako kabiliana nae” Damian aliongea na kuanza kuelekea ndani. Patricia alipotazama pembeni kweli kulikua na nyoka.
“Mamaaaaaaaaaa” Patricia alipiga ukelele huku anatetemeka kwa nguvu, nyoka alivyosikia kelele akaachama ili kumdunga Patricia. Binti wawatu alikua kwenye hatari kubwa sana.
EP 5
“Mamaaaaaaaaaaaaaaa” Patricia akaanza kukimbia huku anaruka ruka juu, yule nyoka aliendelea kumfuata kwa kasi Patricia alipomfikia Damian alimrukia huku akiendelea kuogopa, bibie alibembea mwili wa mwamba.
Nyoka alimn’gata mguuni Damian bahati nzuri mguuni palikua na bandeji ngumu ambayo iliwekwa kwaajili ya vidonda ikamsaidia Damian kuepuka meno ya nyoka mwenye sumu kali.
Nyoka alivyoona hajafanikiwa akapita zake hivi. Patricia hakutaka kushuka kabisa aliendelea kubebwa na Damian mpaka ndani.
“Ni salama sasa unaweza kushuka tu”
“Sawa kwani unadhani naogopa bhasi unaniona mimi dhaifu eeehπ”
“Hapana wewe ni imara sana tena unaweza kuruka vibaya mno π”
“Naona unanizoea wewe kaka”
“Sitamani hilo litokeee, naenda nyumbani kwangu saivi”
“Kwanini na usiku wote huu?”
“Kwaajili yako nikiendelea kukaa hapa polisi wakirudi kwa mara ya pili watajua kwamba mliniteka sababu mlichonifanyia na kaka ako ule ni utekaji sio ukamataji na cha pili ninapoishi nisipoonekana wezi wataniibia kila kitu”.
“Duuuh sasa si ubaki tu usiku umeenda sana jambo la hatari linaweza kutokea huko njiani”
“Hatari na shida tumeumbiwa wanaume kwahiyo nitakabiliana nazo tu”
“Heeeee muoneni huyu anahisi nitam’bembeleza nendaa tu babu, muda wa kum’bembeleza mtu mi sina π” dakika hizo hizo Patricia ameshabadilika yaani ni mtu wa kubadilika badilika hovyo ukitazama matendo yake mbona utacheka π.
Damian hakumjibu badala yake akaondoka zake kurejea mtaani alipokua anaishi kwa kutumia usafiri wa daladala, aliunganisha tatu mpaka inafika saa kumi na moja alfajiri ndo anaingia nyumbani kwake, aliwakuta wezi wakipambana kuvunja kufuli na nje, akawafurusha na hiyo ikawa pona pona yake. Akafungua mlango na kuingia ndani. Alivuta kikapu chini ya kitanda hapo kulikua na majani flani akayaponda ponda kwa kutumia kinu, kisha akachemsha na mizizi mingine, dawa ilikua chungu sana mdomoni, aliinywa yote, mwili ulilowana jasho chapachapa hata feni ndogo iliyopo ndani ya chumba haikuweza kumsaidia akapitiwa na usingizi aliamka majira ya saa nne asubuhi.
“Simu yangu” alikumbuka kwamba hakua na simu na kumbukumbu zake zilivyomkaa vizuri kichwani alikumbuka simu aliangusha wakati anavutwa na wajeda waliomchukua siku iliyopita hiyo akajua tayari ni hasara.
Akajiandaa chap chap hakua amepona vizuri ila mji haukumpa nafasi ya kuendelea kujionea huruma.
Alikwea usafiri wa daladala mpaka mahali ambapo huwa anapanga viatu vyake alikuta sehemu yake imebebwa na mfanyabiashara mwingine.
“Cossie niaje vipi mzigo wangu umeweka stoo au vipi?” Damian alimuuliza jamaa ambae alimwacha siku iliyopita wakati anachukuliwa na wale wajeda.
“Daaah nisamehe kaka nilimwachia Kabenga, nilipigiwa simu ya haraka kwamba mtoto wangu kaishiwa damu na kalazwa hospitalini hivyo ikabidi niwahi kuondoka nenda ukamuulize yeye pia pole kwa matatizo”
“Ahsante ndugu yangu nilikabiliana nalo kiume na kwakweli yameisha, ngoja nipambane na mtaa kivingine bila kuingilia maisha ya watu wengine”
“Huo ndo uamuzi sahihi kaka karibu tena kitaa”
“Ahsante sana ndugu yangu ngoja kwanza nimfuate Kabenga nione kuhusu mzigo wangu maana huo ndo nautegemea hapa mjini”
“Poa poa fanya hivyo kaka” wawili hao waliagana na Damian kuelekea upande mwingine kwaajili ya kuzungumza na huyo Kabenga.
“Mkali Kabenga, oya Kabenga babaaaaa, mtaalamu mwenyewe wa kariakoo, umenyooka kama ruler mtaalamu π” Damian aliingizia utani wa haraka haraka.
“Nini babu mbona tunasumbuana sumbuana muda wa biashara huuπ‘” Kabenga alionesha kuchukizwa na Damian.
“Samahani sana kaka sema nini kuna mzigo wangu ulinihifadhia jana”
“Mzigo gani wee jamaaa umechanganyikiwa au”
“Mwanangu nimeshavulugwa mimi sitaki vita nyingine”
“Vita ulete kwa msingi gani pita hivi sina mzigo wako mimi” maneno ya Kabenga yalizuia ugomvi mwingine hapo hapo kati duuuh ngoja tuone ni kipi kitafuatia.
EP 6
Twende kwanza upande mwingine wa jiji, kwenye moja ya jengo kubwa jijini, ndani kabisa huko, floor namba sita inapatikana ofisi ya za kampuni ya ADO ADO MAGARI, ni kampuni inayojihusisha na ununuzi na uagizaji wa magari nje na kuyaleta Tanzania, floor nzima ilikodishwa na kampuni hiyo, kwenye moja ya ofisi, walionekana wanawake wawili mmoja alikua mbele ya kioo cha kompyuta akionesha umahili wake wa kubonyeza keyboard na mwingine alichapa usingizi kama yupo juu ya godoro dodoma.
Mlango ulifunguliwa na aliingia mbaba mmoja kitendo cha kuingia mbaba huyo kilimfanya yule aliemacho kuonesha userious kwenye kile alichokua anakifanya pia hakujisumbua kumuamsha mwenzake aliekua amelala.
“Patricia mbona unalala ofisini una shida gani leo?” Mwanaume huyo ambae alifanya kazi kama HR kwenye hiyo kampuni alimtandika swali Patricia.
“Duuuh samahani boss leo mwili wangu haujisikii vizuri kidogo”
“Aah kwakua sio kawaida yako kulala lala hovyo ofisini, bhasi kwa leo unaweza rudi nyumbani na ukajiangalizia afya yako vizuri maana kuna maisha baada ya hizi kazi” maneno ya HR yalimfanya yule aliekua pembeni kukaribia kupasuka moyoni kwa hasira kwani alitamani ajionee namna Patricia atakavyokua anagombezwa lakini haikutokea hivyo.
“Sawa boss nashukuru sana kwa kujali Mungu akubariki sana”
“Ahsante Mungu akuponye pia” HR alivyotoka nje.
“Salma ngoja nikapumzike kesho bhasi undugu wangu”
“Sawa ila kazi zako wala sifanyi mimi”
“Hilo usijali nitakamilisha mwenyewe” Patricia alibeba vitu vyake, akaingia kwenye lift na kushuka mpaka ground floor kwaajili ya kuondoka.
“Unaelekea wapi mrembo na muda wa kazi huu” sauti ilisikika nyuma ya Patricia na alipogeuka alimwona Doctor Ndunguru.
“Aah wewe snitch wakiume upo hapa tena nikajua utakua polisi unawapikia chakula cha mchana maana sio kwa ule umbea uliovaa dela uliofanya jana usiku”
“Niko hapa kwa mambo mawili moja kumalizia malipo ya lile gari langu la ndoto ambalo miaka na miaka nimekua nakwambia nitalimiliki na jambo lingine nipo hapa kukuomba msamaha, nimekaa usiku mzima nikitafakari juu ya mambo yaliyotokea nikajiona ni mkosaji sana mama angu naomba unisamehe sana”
“Unaona unavyolipata gari la ndoto yako na uache kuharibu ndoto za watu wengine sasa yule kijana amekufanya kosa gani mpaka umzushie kwa mapolisi kwamba ni jambazi”
“Najua nimezingua na ikitokea nikakutana na yule kijana nitapiga magoti kumuomba msamaha, mimi sina roho mbaya hiyo”
“Kama ni hivyo bhasi jambo jema maana ulijua kunishangaza sasa nikuache naenda nyumbani”
“Sijaona gari lako leo naweza kukupatia lift tu wala usijali”
“Weee baba kwa kunifuatilia hujambo haya bhana gari lipo kwa fundi nimelipeleka leo asubuhi”
“Ukimpenda mtu lazima umfuatilie na sio kwa ubaya ni vile tu umeamua kumjali na kumthamini bhasi”
“Ausio sawa bhana ila tukubaliane jambo usinipeleke kwangu nipitishe kwa fundi wangu halafu kila mtu atapita njia yake”
“Sawa tu hakuna shida” kwa pamoja waliongozana mpaka eneo la maegesho.
Doctor Ndunguru alimfungulia mlango Patricia kwa madaha alimpa treatment zote kama malkia ndani ya kasri lake.
Walienda mpaka eneo moja hivi lenye maduka mengi mengi.
“Sikia Malkia mrembo najua umechoka sana ila naomba jambo moja tu, twende madukani pale ukafanye shopping iwe ya laki,millioni hata millioni ishirini, mimi nitalipia sababu furaha yako ndo kipaumbele changu”
“Haina haja Doctor Ndunguru”
“Nooh ni muhimu kama kweli umenisamehe tafadhali sana naomba ukubali ombi langu.
“Ouuuuuh bhasi sawa nachukua vitu viwili then tunaondoka”
“Hilo halina.shida kwa pamoja walitoka na kuanza kutembea pamoja kabla hawajaufikia mlango wa duka moja lililokua mbele yako.
Kwa uwazi kabisa waliwaona walinzi wawili mmoja huku na mwingine huku wamembeba Damian wanamtoa nje ya duka hilo kwa nguvu. Patricia alihamaki kitendo hiko ila Doctor Ndunguru akajazia maneno kabisa.
“Si nilikwambia huyu jamaa ni mwizi enheee siku arobaini zimefika haraka hahahaha wezi wanakwaza sana” Doctor Ndunguru aliendelea kucheka ila kwa upande wa Patricia alizidi kushangazwa na namna Damian anavyovutwa kwa nguvu sana.
EP 7
“Muacheni muacheni mbona mnamvuta hivyo amefanya nini”
“Amekuja kuleta vurugu dukani kwetu, boss ametuagiza tumtoe ndo tunafanya wajibu wetu”
“Mimi siondoki mpaka boss wenu anipe mzigo wangu nyie ni wezi”
“Tumeiba nini na unaushahidi gani, toka hapa kabla hatujakuitia mwizi”
“Patricia Patricia tuondoke achana nae huyo jamaa ameshaanza kuchanganyikiwa” Doctor Ndunguru aliingilia kati na kuanza kumvuta Patricia ili waondoke.
“Hebu na wewe niachie huko kama vipi pita hivi huoni mtu yupo kwenye matatizo halafu wewe unaanza kuleta mambo yako ya kuvutana wee mwehu nini”
Maneno ya Patricia yalikua makali sana, ukali ambao hakuwahi uona kabisa katika kipindi chote ambacho alijuana na Patricia alijua fika kabisa ndani ya Patricia kuna kitu kimebadilika, hali hiyo ilimpa unyonge sana.
Muda ambao aliona huenda angetengeneza wakati mzuri wa kufurahia mapenzi yao na Patricia ila kuna kidudu mtu ameingilia kati. Ikabidi kupunguza hasira Doctor Ndunguru aondoke zake.
“Acha kugombana tuondoke tukazungumze kwanza hawa watakuumiza” nguvu ya maneno ya Patricia yalimfanya Damian akubali kuondoka ila alirusha maneno pia.
“Nguvu ya mwanaume huwa hailiwi bure kama sio leo bhasi ipo siku nitakuja wewe mzee nitakurudia nakwambia nitakujaaaaaaaaaaπ₯²” Damian aliongea maneno ambayo yalikua na uchungu mwingi kwa upande mwingine.
Walitoka kwa pamoja mpaka eneo flani kwaajili ya kupata chakula na kufanya mazungumzo kidogo japo Damian hakuonesha kuwa comfortable na hilplo eneo kutokana na namna alivyokua amevaa pia akili yake ilikua inawaza mkwamo wa maisha aliokua anaupitia.
“Nieleze ni nini kimetokea mpaka kufikia pale”
“Daaah wewe acha tu haya maisha ni kitu cha kijinga sana. Na yakiamua kukuendea vibaya hakuna sehemu utayakumbatia kuyazuia ili yasiendelee kuharibika, jana mlivyonichukus pale ule mzigo wote uliokua chini pale nilimwachia jamaa angu anaitwa Cossy kwa bahati mbaya akapata tatizo la kuuguliwa na mtoto wake, mzigo wangu akamwachia jamaa anaitwa Kabenga, yule mchizi nikamfata akaanza kuleta mambo yake ya kijinga kama hajui kuhusu mzigo wangu, nilivyozidi kumzingua ndo akanambia kauuza kwa yule mzee pale. Tena kwa bei nyepesi sana rafiki angu, nikamvuta mpaka hapa, nilivyoanza kudai vitu vyangu ndo huyu mzee kanitoa nje kama mwizi, hawa binadamu waajabu kweli rafiki angu”
“Duuuh pole sana, najua jana ndo sababu ya kila kitu kwenye maisha yako, mambo yameharibika kwa kasi sana ila usijal kila kitu kitakua vizuri tu, hebu nieleze huo mzigo wako ni bei gani unaghalimu”
“Ni mzigo wa laki nne” Damian aliongea na kurudisha macho yake chini.
Bei ya mzigo ilimshtua Patricia na kuona kwamba kumbe Damian alikua anaishi kwenye umaskini tena ule wa kipato cha chini sana.
“Usijisikie vibaya nitakupa hiyo pesa ya mzigo ila naomba uniahidi jambo moja hapaa”
“Hautakuja kugombana na hawa watu utafanya maisha yako katika hali ya usalama kabisa, promise”
“Ahsante sana dada angu nakuahidi nitafanya hivyo”
“Poa tule bhasi halafu mambo mengine yatafuatia”
Harufu ya chakula iliendelea kusumbua pua za Damian kutokana na njaa aliyokuwa nayo, hakuongea kitu alifakamia chakula chote mpaka kikaisha.
“Ahsante kwa chakula nitakulipa siku moja fedha yako”
“Kwani mimi nimekwambia unilipe mbona una matatizo sana wewe mtu”
“Bhasi bhasi nimeacha”
“Hapo vizuri uwe kijana mzuri sawa”
“Sawa dada mkubwa”
“Unajua kuna kitu nataka kujua kuhusu wewe, hasa hasa kuhusu maisha yako umaweza share na mimi kama hutojali”
“Hakikisha una kitambaa cha kuzuia machozi maana hadithi yangu imebeba maumivu” Damian alikaa sawa kuelezea kile ambacho alitaka kuanza nacho juu ya historia ya maisha yake.
Inaendelea…..


