MLENDA WA PORINI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA KWANZA
MWANZO: Mwaka 2002, ijumaa ya pili ya mwezi wa tisa, ndani ya jiji Dar_es_salaam, mida ya saa nne za asubuhi, maeneo ya Malamba mwisho, mbele kabisa ya mtaa wa, kwa mpemba, nyumba za mwisho kabisa, kabla ujauacha mji.
Tunasimama kwenye eneo kubwa, lililozungushiwa uzio, ndani yake, kukiwa na nyumba saba, nzuri na za kisasa, za wapangaji, nyumba moja kubwa yenye vyumba nane, kila moja ikiwani chumba, sebule na choo.
Pia nyumba sita za kujitegemea, kila moja ikiwa na vyumba viwili, sebule na choo ndani, na zote zilikuwa na wapangaji, wenye kipato tofauti tofauti, kama ambavyo paliweza kujieleza.
Achana na watoto, walio onekana wakicheza nje, asa wakati huu wa likizo fupi, watoto wote walikuwepo hapo nyumbani, nao walionakana wakiwa katika mwonekano tofauti wa kimavazi ata nuru ya ngozi yao.
Ilikuwa hivyo ata kwa wamama, ambao walikuwa tofauti kwa mwonekano wao, ukilinganisha wale wa nyumba kubwa, ambao walionekana kuwa wa kipato cha chini, huku wamama nyumba zilizo jitenga wakionekana wakiwa na mavadhi ya gharama.
Pia kingine ni magari na pikipiki zilizopo pale nje, japo ilionyesha baadhi zilikuwa zimetoka, lakini palionekana kuwa, wakazi wa nyumba izi, walikuwa na kipato kizuri, hatujuwi kuhusu kodi ya pango, ya nyumba hizi, pengine ni kama zilivyo jitenga.
Maana ata yale magari yaliyo onekana, yalikuwa yamesimama kwenye zile nyumba zilizo jengwa kwa kujitegemea, huku pikipiki mbili zikionekana kwenye hii nyumba kubwa, ambayo ilikuwa na wapangaji nane.
Lakini basi, wakati huo huo, tunaona gari aina ya Mercedes Benz S 430, chuma yamaana kwa wakati huo, 4.3L V8, la mwaka 2001, rangi nyeusi, gari jipya kabisa, kwa wakati huo, ungezunguka jiji na pengine ungekutana nalo moja, ambalo ndio ili.
Linaingia ndani ya geti lile na kwenda kusimama, mbele ya nyumba ile kubwa, ya wapangaji ambao, tunaweza kusema niwakipato cha chini, watu wote wanalitazama lile gari kwa umakini na mshangao.
Milango mitatu ya gari inafunguliwa, wakwanza kushuka toka kwenye gari, mlango wa abiria wa nyuma, alikuwa kijana wa mvulana mdogo, wa miaka kama saba hivi, mwenye mchanganyiko wa uchotara wa mbali sana wakiarabu.
Alievalia kanzu nyeupe, nzuri, yenye dalizi ya nyuzi za rangi ya dhahabu, kofia nzuri aina ya baraghashia, nayo nyeupe, yenye daridhi ya nyuzi zenye rangi ya dhahabu, chini akivalia sendo, zenye rangi ya kaki, unyayo mweusi wenye fito nyeupe,.
Wamama wote wa nyumba zilizo jitenga, wanasogelea gari, wakati anashuka mschana mmoja, mswahili, asie changanya rangi ata kidogo, toka mlango wa mbele wa abilia.
Huyu alikuwa amevalia gauni ndefu, mpaka chini, huku kichwani akifunuka nywele kwa ijab, na kuanza kusalimiana na wale wakina mama, ambao walikuwa wameungana, na wale wa nyumba hii kubwa.
Naaaaam!, wamwisho kushuka toka kwenye gari, na baada ya gari kuzimwa, alikuwa ni dereva wagari ili, huyu ni mwanadada, mwenye hasiri ya uchotara wa mswahili na mwarabu, mwenye umri wa mkadilio wa miaka ishirini na saba au ishirini na nane.
Wacha tu ni mwelezee, japo kiduchu, kwamaana ikipita hivi hivi, nitakuwa sijamtendea haki, hakika aitoshi kusema ni mrembo, kwa jinsi alivyo alivyo vaa, kuanzia gauni rake refu, rangi ya kama ya kaki hivi, lenye mauwa ya dalidhi, lililofanana na ijab yake.
Pia alitunduka mikufu na herein, na pete za dhahabu harisi, huku maungo yake, yakilifanya gauni lake lilaumiwe, kwa kushindwa kuifadhi, vyema mitundo ya maungo yake, kama hips makalio ya wastan na matiti yake yaliyo jaa vyema kifuania.
Niseme tu, kuwa huyu mwanamke ni mzuri aswa, tena mzuri kuliko uzuri wenyewe, kama nikiendelea kueleza kuhusu macho pua midomo, na vitu vingine, tuta maliza eps nzima, kumwelezea mwanadada huyu.
“karibu dada, naona umetutembelea ghafla” alisema mmoja kati, ya wale wanawake, waliotoka kwenye nyumba zilizojitenga, akimkabilisha mwanamke huyu, ambae ndie mmilikiwa wa nyumba hizi, za wapangaji.
“wala siyo ghafla, nimekuja kutembelea mama Ratiff, nilisha mpigia simu” alisema yule mwanamke mzuri na mrembo, ambae sasa tunaisikia sauti yake kuwa ni tamu kuliko.
Kila mmoja anaonekana kushangaa, maana awakujuwa kuwa, wawili awa wanafahamiana, asa utofauti wao wakipato, pia licha ya yote, hakuwa na utaratibu wa kutembelea hapa mara kwa mara.
SEHEMU YA PILI
“yupo ndani mwake, karibu” alisema yule mama, ambae anaonekana ndie msemaji, au mwongeaji mkuu, kuliko wapangaji wengine, na ndie ambae ni msimamizi wa wapangaji wengine.
Mwanadada chotara, na watu aliokuja nao, wanaingia ndani ya nyumba kubwa, huku wakiwaacha midomo wazi wamama wengine, wakitazamana kwa macho ya mshangao, ni kama wanajiuliza imekuwaje leo.*******
Naaaaam!, dakika chache baade, mwanadada mrembo, anaingia kwenye moja kati ya vyumba vile, akiwa ameongozana na yule mvulana na yule mwanamke mswahili, lakini kabla ajagonga.
Mlango unafunguliwa, anaonekana mwanamke mmoja mswahili, ambae akuwa na mchanganyiko wowote wa hasiri, zaidi ya kuwa mswahili, ambae anawatazama wageni wake, na kuachia tabasamu laini lenye kila mwonekano wa urafiki.
Huku chini yake kuwa na mtoto wa kiume, mwenye umri wa miaka mitatu, au minne, ni wazi ndie aliekuwa anafunguliwa mlango, aende akacheze, “dada asalam aleykum, anasalimia mwanamke huyu, ambae ndie mama Abdullratiff.
“waleykum salam, dada habari za toka jana” alisalimia mwanadada chotara, “salama tu, karibu ndani, sikutegemea kama utafika mida hii” alisema yule mwanamke, ambae nivyema kama, nikimwelezea japo kidogo.
“asante sana, yani nimetoka kuswali, nikasema nisiende nyumbani, nije nikuone kama nilivyo kuambia” alisema mwanamke chotara, “karibu dada yangu, karibu ndani” alisema yule mwanamke mswahili, kwasauti yenye ukarimu.
Ambae kiukweli, licha ya kuvaa nguo za kawaida sana, baibui jeusi na ijab, lakini ungesema amevaa baibui la mdogo wake, kwajinsi lilivyo mkaa vyema, kiasi cha kwamba usingejari kuhusu uchakavu wake.
Achana na ilo baibui, huyu dada mzuri, mwenye umri wa miaka kama ishirini na tatu, au ishirini na nne, yani licha ya kuonekana ametokea katika maisha ya chini, na kukosa kujipamba kwa wanja na poda na rangi ya midomo, lakini amejaliwa sura nzuri na umbo la kuvutia.
Naaaaam!, dada chotara wakiarabu, anaingia ndani ya chumba kile, ambacho wanafikia sebuleni, sebule ambayo tunaweza kusema ni ya kawaida, kwajinsi ilivyoonekana.
Kwanza aikuwa na meza wala kiti au kochi, chini palitandikwa mkeka ambao siyo mpya sana, wala siyo chakavu, ila palikuwa na mito minne, kama ile ya kulalia kitandani.
Upende wa kulia wa chumba, palipangwa ndoo za maji na vyombo vya chakula, ndani ya mabeseni, na vifaa vingine, lakini upande wa mbele yao, upande ambao kuna mlango wa kuingilia chumbani, kulikuwa na tendi ya TV na iliyobeba Tv ya chogo juu yake, chini yake kukiwa na redio cassett.
Yaaaap!, mara baada ya baada ya kusalimia, kijana mdogo wa kiume, anamshika mkono mvulana mdogo, kwa upendo mkubwa, kama vile mdogo wake, wanatoka nje kwa pamoja, wakiongozana na dada mswahili.
Naaaaam!, sasa ndani ya nyumba ile, wamebakia dada chotara wakiarabu, na mwanadada mswahili, wote ni wazuri, japo huyu chotara, anaonekana kuwa mzuri zaidi.
Wakiwa wamekaa kwenye mkeka ambao, kwa adhi ya mwadada huyu chotara, usingweza kuamini, kama amekubari kukaa pale mkekani, wanawasindikiza kwa macho wanao toka nje, mpaka wanapo funga mlango.
Hapo mwanadada chotara, anainamisha kichwa chini, na huku uso wake umepoa, kama mshatikiwa mbele ya hakimu, anasubiri kusomewa mashtaka, au anataka kuanza kujitetea.
“dada mimi nimekuja kama nilivyo kuambia, ninamaongezi na wewe” alisema mwanamke chotara, ambae achana na uziri alionao, ila pia, alibahatika kuwa na fedha nyingi akiwa mschana mdogo.
“sawa dada nakusikiliza” anasema mschana mswahili, kwa sauti iliyopoa, huku akiwaza kuhusu maongezi aya, ni kuhusu nini, maana licha ya kumfahamu mwanamke huyu, kwa muda mrefu, na msaada ambao amewai kumpa mara mbili, lakini awakuwai kuwa na ukaribu wa kufanya maongezi.
“kwanza natanguliza samahani dada yangu” alisema yule mwanamke chotara, kwa sauti tulivu, yenye nidhamu na heshima ya hali ya juu, kiasi cha kuzidi kumshangaza mwanamke Swahili.
“bila samahani dada” alisema mwanamke mswahili, kwakuona nidhamu ya mwanamke huyu, ambae pia ni mama mwenye nyumba yao imezidi, na siyo stahili yake.
“dada nimekuja, ninaombi kubwa sana kwako” alisema dada mrembo wa kichotara, kwa sauti ile ile yenye upole na unyenyekevu wa hali ya juu, ungesema anae stahili kunyenyekea ni yule mswahili.
Inazidi kumshtua zaidi, mwanamke mswahili, ambae ndie mama Ratiff, ambae kichwani mwake anajiuliza maswali mengo, na kujipa majibu mwenyewe, “au anataka nikawe dada wakazi nyumbani kwake” aliwaza mama Ratiff.
Lakini kabla ajajiuliza swali la pili, akamsikia mwana dada chotara akiongea tena, “ombi langu aliusiani na chochote nilicho kufanyia, wala aliusiani, chochote nilicho nacho, naomba usinielewe vibaya” alisema tena mwanadada chotara, kwa sauti ya unyenyekevu.
“aina aja ya kusema hivyo dada, we ongea tu, mimi nakusiliza, kama nauwezo na ombi lako, nitakusaidia bila kusita” alisema mama Abdullratiff, akimsihi mama mwenye nyumba wake, ili asionyeshe hali kama ile, mbele yake.
Hapo dada mwarabu akashusha pumzi nzito, huku ameinamisha kichwani, kisha anaongea kwa sauti tulivu, “naomba ombi langu, lisiwe zito kwako” alisema mwanadada chotara.
Hapo hofu ikaongezeka kwa mama Ratiff, na kuanza kuingiwa na wasiwasi, akihisi pengine, mama mwenye nyumba wake, anataka kumwomba figo, au kitu kikubwa cha kugharimu uhai wake.
Mama Ratiff anakumbuka siku ambayo, alimwambia mwanamke huyu, kuwa atamsaidia chochote ambacho anakiitaji toka kwake, ikiwa atakuwa na uwezo nacho.
Kabla mama Ratiff ajauliza chochote, akamsikia mama mwenye nyumba anaongea, “dada yangu, naomba niwe mke wako wa pili, kwamaana mumeo ndie mwanaume pekee, anaefaa kuwa mume wangu” alisema mwanameke mwarabu.
SEHEMU YA TATU
Ili mshtua sana, mama mama Ratiff, inamfanya amtazame mwanamke huyu chotara, ili kubaini kama anaongea ukweli au anamtania, maana siyo tu, kwamba ni mgeni kwa mwanamke huyu.
Ila anafahamu adi chimbuko la familia yake, ambayo ni watu wenye fedha nyingi na maisha ya hali ya juu, asingeweza kulingana na iki anacho kiongea, maana mume wake ni mtu wa kipato cha chini, anaeishi kwa kutegemea kazi ya gereji.
Mama Abdullratiff anamwona mschana huyu, mwenye kila sifa ya kupendwa au kutamaniwa na mwanaume yoyote, tena wale wenye fedha, akiwa ameinamanamisha kichwa chini, kwa nidhamu na tahadhima.
Mama Ratiff anajiuliza maswali kadhaa, swali la kwanza likiwa ni kitugani ambacho, mwanadada huyu, amekipenda kwa mume wake, kwamaana ya utofauti walio nao, na adhi ya chini aliyonayo mume wake.
Pili kama kweli anampenda, ameanza kumpenda toka lini, inamaana walisha tongozana, na wakakubariana ilo, na kama walisha fanya hivyo, inamaana walisha wai kuzini wawili awa.
Nakama walisha kubariana na kufikia hatua ya kuzini, nawezekanaje iwe kwa muda mfupi, namna hii, kwamaana ni niwili tu, toka aje kukutana nao na kuwasamehe kodi ya miezi sita.
“au nipo ndotoni?” alijiuliza mama Abdullratiff swali ilo la mwisho, lakini akaamua kutafuta jibu, la moja kati ya maswali yake, “samahani dada, naomba kuuliza” alisema mama Ratiff.
“niulize tu dada, nitakujibu kwa busara, kama utakavyo” alisema mschana wa kichotara, ambae ndie mama mwenye nyumba ile, kwa sauti ambayo ilijaa unyenyekevu, wa hali ya juu, ungesema kitwana mbele ya mtwana.
“hicho unachosema ni kweli, na kama kweli, ulisha kubaliana na baba Ratiff?” aliuliza mama Abdullratiff, huku anamtazama mschana chotara, ambae tumeona amekuja na dada mswahili, na mtoto wakiume, nae ni chotara kama yeye.
“hapana sijaongea nae, naomba wewe uniombee kwake, aniowe mke wapili” alisema mschana mwarabu, kwa sauti ile ile yenye unyenyekevu, huku ameinamisha kichwa chake, kwa utulivu mkubwa.
Hapo mama Abdullratiff anashusha pumzi ndefu, nikama mtu alie choshwa na jambo zito, nae anainamisha kichwa chini, anawaza uzito wa jambo ilo, ambalo kiukweli lilimuwia vigumu, japo alitoa ahadi ya kumpatia dada huyu kile atakacho itaji, endapo tu, kitakuwa ndani ya uwezo wake.
Mama Abdullratiff anainua uso wake, na kumtazama tena mwanadada chotara, ambae bado ametazama chini, “samahani kwa swali langu nitakalo kuuliza” alisema mama Abdullratiff.
“nitajikujibu kwa busara, kadiri unavyo taka” alijibu mwanamke chotara, kwa sauti yenye unyenyekevu wa hali ya juu, mama Abdullratiff anamtazama vizuri mwanadada huyu, mwenye hadhi ya VIP.
“wewe unakila kitu, na uweza kupata mwanaume yoyote unae mpenda, vipi utake kuolewa na mume wangu, tena uwe mke wa pili?” aliuliza mama Abdullratiff, huku anamtazama mwanadada chotara.
“mumeo ni wa kipekee sana kwangu, naomba tu unikubalie, na kuomba unikubalie, na uniombee kwa mume, niwe mke wapili, maana ninaitaji mume, na mume mwenyewe ndie yeye” alisema mwadada chotara, kwasauti ya kuombeleza kwa unyenyekevu.
Ata wewe ungeshangaa kwanini anafanya hivi, ingali ata mwanamke mwenzie, anamwona ni mzuri na mwenyesifa ya kuwa na mwanaume yoyote mzuri, ebu turudi miaka minne nyuma, tujuwe kilicho tokea ********
Ulikuwa mwanzoni mwa mwaka 1998, mwanzoni, ulikuwa ni usiku mkubwa sana, katika kati ya msitu mkubwa wenye kutisha, usiku wa giza nene, usiku uliokosa mbala mwezi, hapakuonekana nyota wala vimondo.
Mvua kubwa ilikuwa inanyesha, upepo unavuma kwanguvu, miale mikali ya mwanga ilikuwa inamulika kwa kushtukiza, huku ikifwatiwa na ngurumo kubwa ya mpasuko radi.
Angalau mwanga wa umeme wa radi, unao umiza macho na kuogofya, ndio ambao ulisaidia, kuweza kuona ata mita nne mbele, kwa nukta chache, kisha giza nene kurudi tena, na kuongeza upofu.
Maji ya nashuka ardhini, na kutengeneza mifereji, inayo tililisha maji kuelekea kwenye mwinamo, hali hii ya kutisha, katika usiku huu, inawafanya ata wanyama wakali watulie kwa kuogopa.
Lakini katika msitu huu wakutisha, ambao ukubwa wake, una tupofusha kuweza kuona mji unapo anzia, wala dalili ya mji au kijiji cha jirani, tunacho kiona ni kijinjia chembamba, kilicho funikwa na nyasi zilizo mea vyema, kinacho elekea ypande wa magharibi.
Naaaam!, kwa shida sana tunawaona watu watatu, wakiwa wanatembea kelekea upande wa mashariki, na tunapo angalia vizuri na kwa ukaribu, tuna weza kugundua jinsia zao, na pengine umri wao.
Kati yao, alikuwa mwanaume wa miaka, zaidi ya arobaini na nne, anae kokota baskeri, baskari ambayo ilimbeba mwanamke wa miaka kama 38, mjamzito, aliekaa kwenye kitako cha nyuma, kwa kuegemea kingo ya miti miwili, iliyofungwa vizuri.
Lakini mtu watatu, alikuwa ni mschana wa umri wa miaka kama kumi na tisa, akisaidia kusukuma baskeri tokea nyuma, na kuhakikisha usalama wa, mwanamke yule mwenye tumbo, ambalo lina ukubwa wa miezi nane au tisa kasoro.
SEHEMU YA NNE
Lakini tunapotazama vizuri kabisa, atuoni machozi, kwa mwanamke mjamzito, ila tuna weza kusikia kilio cha cha mwanamke huyo, nikilio cha uchungu, tena uchungu wa kujifungua.
Lakini licha ya iki wanacho kipitia, wanawake awa, waliovalia mavazi meusi maarufu kama baibui, awa kukuluhusu vichwa vyao kuwa wazi, walifunika nywele zao kwa hijab.
“tumbo linazidi kuuma, nashindwa kuzuwia jamani” analalamika mwanamke mjamzito, juu ya baskari, “jikaze mke wangu, tufike hospital” alisema mwanaume, ambae kama siyo mvua, tungeweza kuona machozi ya wazi,
Safari inaendelea, mvua inanyesha, awawezi kuona mbele, kutokana na giza nene, inatosha tu kujuwa wanapokanyaga, vinasikika vishindo vyao wanapo kanyaga ardhi yenye maji, hakuna kingine kinacho sikika, zaidi ya sauti ya kuugulia maumivu ya mwanamke mjamzito.
“jikaze mama, tutafika” alisema mwanamke mdogo, aliekuwa anasukuma baskeri, kwa sauti ambayo, aikuficha kilio chake, hakika ilikuwa kumbu kumbu ngumu sana katika maisha ya mschana huyu, ambae pengine na yeye anatarajia kuwa mama, katika siku za mbele.
Usiku mnene, hapakusikika sauti ya mnyama yoyote, zaidi ya matonye ya mvua, yaliyotuwa kwenye matawi ya miti, na nyasi mbichi, ikipambishwa na zile ngurumo za radi, zilizopeana nafasi ndogo.
Naaaaam!, safari inazidi kuwa ngumu, kwao, wanatembea kwa ugumu, kila mmoja moyoni mwake amekata tamaa, awakuwa na uwezi wa kumsaidia mama huyu kujifungua, ukiachilia taaruma ya ukunga, ambayo hawakuwa nayo, hali ya hewa, aikuwa raafiki.
Achana na hayo yote, kuna kitu kingine, ambacho kilikuwa kinazidi kuwatoa machozi, siyo mama mwenye ujauzito, ambae alipofikilia ilo, alizidi kupatwa na uchungu, wala siyo baba alie kokota baskeri, au binti yao alie kuwa anasukuma baskeri.
Hii ilikuwa ni sababu ya kiasi chochote cha fedha, wakati wanaanza safari ile, kiasi ambacho, pengine kingesaidia, kwa huduma za kujifungua na matibabu, au chakula kwa wauguzaji, ambao ni baba na binti yake.
Aikuwa ni uzembe, wala hapa kuwa na mtu wa kumlahumu, sababu miezi ya kwanza na wapili, kwa wakulima uwa ni kipindi kigumu sana, kuanzia fedha mpaka chakula, kwamaana ni wakati wa kufukia na kupapalia mazao, ambayo yangeanza kuliwa mwezi wa tatu.
Watatu hao wanaendelea na safari, kila mmoja anawaza juu ya jambo ilo, angalau wangekuwa na fedha kidogo ya kuanzia, kwamaana wao wawili wangevumulia, japo awakujuwa watakaa kwa muda gani.
Na mbaya zaidi, mjini awakuwa na ndugu, ambae, angewasaidia japo chakura, maana awakuwa wanafikilia sehemu ya kula, kutokana maana wange lala ata kwenye viambaza vya majengo ya hospital.
Naaaaaam!, watatu awa, wanazidi kuvunjika mioyo yao, na kupunguza matumaini, wanapo fika njia ya mwarabu, kwenye maungio ya kijinjia iki, na barabara pana, ya kwenda kwenye mashamba ya mwarabu.
Shamba la mwarabu, ni sehemu maarufu kwa wakati huo, maana nisehemu ambayo, ilikuwa inatoa ajira kwa watu wengi sana, wa umri mbali mbali, ambao walikuwa wanafanya kazi kwenye mashamba makubwa ya mwarabu huyo.
Kwa maana wanakumbuka ya kuwa, toka hapo njia panda, mpaka kufika mjini, kuna mwendo wa masaa zaidi ya manne, kwa mwendo wa baskeri, sasa itakuwaje, kwa mwendo wa miguu, katika mvua na wanakokota baskeri, yenye mama mjamzito.
Ni saa la nne sasa, toka watoke kijijini Mbendu, mida ya saa tano za usiku, mara baada ya mke wake, anae fahamika kwa jina la, mama Zuu, kifupi cha jina la binti yake Zuleiya.
Sasa ni saa la tatu, toka mvua ianze kuwanyeshea njiani, kuanzia mida ya saa sita, lakini bado, mvua aikuonyesha dalili ya kuisha, zaidi ya kuongezeka, mara dufu, sambamba na upepo mkali, ambao ungefananisha na mtu liepo kwenye gari lawazi.
Kweli ilikuwa, ni kumbu kumbu ngumu sana, kwa Zuleiya, kumbu kumbu ambazo, akujuwa mwisho wake, ndio mwanzo wa maisha yake mapya, yenye furaha na amani.
Naaaaaam!, watatu awa, wanaendelea kutembea kimya kimya, mvua inaendela kuwashukia, mama anaendelea kulalamika maumivu, mioyo ya baba Zuu inaumia sana, wanaposikia kile kilio cha mama Zuu.
Kuna wakati baba Zuu, alitamani kama angejaribu kumwachia mkunga wakienyeji, pale kijijini, ili afanye kazi yake, lakini akikumbuka miaka kumi na tisa iliyopita, mke wake mama Zuu, alivyo nusurika nakifo, wakati anajifungua Zuu, kijijini kwao, kwa kutumia mzalishaji wa hasiri.
Lakini sasa, upendo na kujari kwake, usalama wa mke wake, kuna mfanya aanze kujuta, kwa iki anacho kiona, kinaenda kutokea kwa mke wake, mbele ya binti yake Zuleiya.
SEHEMU YA TANO
“mmmmmh!, baba Zuu nishushe, nimeshindwa nishishushe” alisema mama Zuu, kwa sauti iliyojaa uchungu wa maumivu, “mama vumilia tufike…” alisema Zuleiya, kwa sauti ya kwa sauti iliyoambatana na kilio.
Lakini mama yake anamkatisha, “nasema nishusheni, mmmmmh” sasa ulikuwa mguno wa kujikamua, kwamaana ya alikuwa anasukuma kujifungua, “mke wangu siyo haa mke wangu” alisema baba Zuu, kwa sauti ya kikata tamaa.
Mama Zuu, akujibu kitu, zaidi ilisikika akikamua kwa kusukuma, “baba mshushe” alisema Zuu kwa sauti ya juu, yenye msisitizo, huku anazuwia baskeri, na baba yake anasimama.
Zuleiya anashikilia baskari, wakati baba yake mama, ambae alikuwa anaendelea kugugumia kwa uchungu, mvua bado inanyesha, ardhi imeshiba maji, na sasa inayamwaga kuelekea kondeni.
Lete kanga tutandike chini, anasema baba Zuu, huku anasogea pembeni barabara, akiwa amembeba mke wake, ambae bado alikuwa anazidi kulalamika kwa uchungu wa kujifungua.
Zuu ambae akufikilia mazingira yale, yeye aliofia usalama wa maisha ya mama yake, maana siyo yeye Zuu, wala baba, ambae alikuwa na uwezo wa kumzalisha mama yake, kamaana hiyo, ilikuwa hatari kwa mama na mtoto, ambae ni mdogo wake.
Anachukuwa mfuko, kwenye kitako cha baskeri, ambao mama yake aliufanya kama kikalio, na kufungua ndani, akatoa kitenge, na kumsogelea baba yake ambae bado, alikuwa amesimama, huku amembeba mke wake.
“tandika haraka, mtoto ameanza kutoka” alisema baba yake Zuu, kwa sauti yenye hofu, na taharuki, akionekana ameshaanza kuchanganyikiwa, ili nalo lilizidi kumtisha Zuu, ambae anatandika haraka kile kitenge, na baba yake anamlaza mama Zuu.
Sasa mama Zuu amelala juu ya kitenge, kilichotandikwa kwenye nyasi ndefu, chini maji ya mvua yaliendelea kutililika, huku mvua njingine ikiendelea kunyesha,.
“baba, utaweza kweli?” anauliza Zuleiya, kwasauti yenye uoga na wasi wasi mwingi, sambamba na kilio cha chini, baba Zuu anatikisa kichwa kushoto na kulia, uso wake ukionyesha wazi kukata tamaa.
Lakini basi, wakati wanajiuliza watafanya nini, huku mama Zuleiya, akiwa anaendelea kujikamua, kwaajili ya kupokea mtoto, mara wakaona mwanaga wagari, ukija upande wao, kutokea upande wa shambani kwa mwarabu.
Wote wawili wanajikuta wanatabasamu, japo awakujuwa wanatabasamu kwaajili gani, maana ukiachilia, tabia ya mwarabu, kutopenda kutoa msaada mara kwa mara, asa kwa watu wenye hasiri ya watu weusi.
Ila pia, tayari mama Zuu, alikuwa ameshaanza kujifungua, na kwasasa lift aikuwa na umuhimu, zaidi ya kumsadia kufanikiwa kujifungua mama Zuu, ambae sasa alikuwa anaendelea kujikamua, kwaajili ya kujifungua.
Gari linapofika usawa wao, linasimama, wanashuka dereva, na wanawake wawili, wote walikuwa wamevaa vizuri, japo walivaa kama wao, yani magauni marefu, na kuziba nywele zao kwa ijab.
Lakini awakumzidi mschana mmoja, ambae ni chotara wakiarabu na kiafrika, ambae alikuwa amvaa nguo nzuri zaidi, zilizompendeza, ungeweza kuona kuptia kichwani na miguu, maana walivaa makoti ya mvua.
“jamani mbona mnatazama baada ya kumsaidia kujifungua” aliuliza yule mschana wakiarabu, ambae kwa mkadilio wa umri ni miaka kama 24 au 25, huku anavua koti lake la mvua.
“Shikeni ili zuwieni kwajuu” alisema mschana chotara, huku anampa lile koti baba Zuu, ambae anashika upande mmoja na dereva anashika upande wapili, wanatengeneza paa la kukinga mvua.
“lakini Shaddy, sasa ni saa tisa, na gari linaondoka saa kumi nambili kamili, tunaweza kuchelewa” alisema mwanaume walie kuwa nae, ambae alikuwa ndie dereva wa lile gari aina land rover mia na kumi.
“unazungumzia elfu kumi na mbili mbele ya ilo tulilo nalo?” aliuliza kwa ukali yule mschana chotara, na kabla dereva anajibu, tayari mschana yule alisha mgeukia, yule mwanamke mwingine, walieshuka wote kwenye gari.
“ebu chukuwa kapeti la gari hapo nyuma, pamoja na nguo hapo kwenye siti yangu” alisema mschana yule ambae ni Shaddy, yule mwanamke anakimbilia kwenye gari.
“mama usiwe na wasi wasi, mimi ni doctor, nipo chuo cha madoctor muhimbili Dar_es_salaam, hivyo utajifungua salama” alisema mschana huyu, ambae tuliweza kuiona sura yake mzuri, kupitia mwanga wagari wakati anashuka toka kwenye gari.
Kauri hii, aikumpa matumini mgonjwa peke yake, ata wakina Zuleiya na baba yake pia, iliwapa matumaini makubwa, ya mama Zuu kuwa salama, “aya mama sukuma kwanguvu” alisikika Shadya.
INAENDELEA


