MJEDA USIFANYE HIVYO MI NI MDOGO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
Mwenzenu leo nilikuwa na furaha mno, nimemaliza mtihani wangu wa kidato cha 4, naenda Dar kwao rafiki yangu, kuna namna nilikuwa naona kama hakukuchi, ni rafiki yangu wa toka utotoni, tumesoma wote mpaka darasa la saba, familia yao ikahamia Dar, hivyo nina miaka 4 hatujaonana, na familia zetu zilielewana kupitia sisi, tulisababisha wazazi pia wakawa marafiki mno, kwetu nimezaliwa peke yangu, ila rafiki yangu kwao wako watatu kaka zake wawili na yeye,kulikucha nilienda na baba akanikatia ticket ya jioni…
Mda ulifika niliwaaga wazazi wangu nikapanda basi kutoka Singida kwenda Dar, nilikuwa na simu ndogo niliwasiliana na rafiki yangu Anna na wazazi wake, walijiandaa kunipokea kwa shauku mno, masaa yalikimbia hatimae Diana nikafika Dar kwa mara ya kwanza, nilifurahi mno, Anna, mama ake na kaka ake mmoja walikuja kunipokea, tulikuwa na vibe mno, ila uyu kaka mtu akawa kauchuna tu, nikakumbuka kipindi tuko shule ya msingi alikuwa na vibe, zawadi kama zote sasa kulikoni hii miaka kama 5 tu make yeye alienda jeshi tukiwa darasa la 6, tena siku anaondoka nakumbuka nilimlilia mno, make alikuwa anatujari mno, sasa leo hacheki yuko kama mtegua mabom kalikanyaga bom sasa…
Nilimminya Anna nakumpa ishara kwani dereva wetu ni bubu, akacheka kwa sauti nakujibu “ Diana we acha tu rafiki yangu, siku izi tunapelekwa mwendo wa kijeshi mpaka ndani, apa tulipo familia nzima inamuonea huruma wifi atakae kosea kuolewa nae sijui ataishije maskin kwa hii hali😕, Anna aliongea kwa huzuni,niliamua kujibu, Usijali Best uyu mbona mlain tu hakuna mkate mgumu mbele ya chai, tena nakwambia atakuwa mpole huyo hamtaamini, mimi naamini kaka akipata chombo kikajaa kwenye moyo, aah atapoa mbona ngoja atukazie tu sisi kiboko yake itapatikana tu…
Nilivyosema ivyo ghafla tu, jamaa akafunga break kali, apo ametoka barabarani atuelewi kulikoni tumetolewa barabarani afu kafunga break, aligeuka na kututizama…
Chapter 2
Mama alimwambia, “Max kulikoni ghafla unafunga break na hii njia vip?, Kaka Max, Alijibu na sauti nzito mno, “mama sipendi kelele, nataka nipack niwaache waoongee kwanza wakimaliza wataniita nikakae pale, wote tulishangaa, mama akamwambia “ebu toa mambo yako yakijeshi tupeleke nyumbani, wanangu sio mabubu, wasiongee ili wanuke midomo ama wewe inakumalizia nini? Max ukoje siku izi? Ebu usituharibie siku mapema kabisa asubuhi ya baraka hii, alivyoona mama anaongea sana hakujibu chochote aliondoa gari, akairudisha barabarani…
Tukaendelea na safari, apa nilianza kama kumuogopa ivi, tumefika nyumbani,nikakuta bonge la mjengo, na maandalizi ya kunipokea yalikuwa makubwa mpaka nikashangaa, nilikaribishwa vizuri nikapewa chumba changu peke yangu, nilioga tukala, nikaambiwa nipumzike afu nikiamka tutatoka, “Max naomba kesho utusaidie kijana wangu, utawapeleka binti zangu kutembea nina chama jioni sitoweza kuambatana nao, kaka Max alikubali…
Nililala nimekuja kuamka saa 6 mchana, kulikuwa na dada wa kazi alikuwa anaandaa,chakula cha mchana, na mimi napenda kupika kuliko kazi zote,niliomba nimsaidie, alisita ila Anna akamwambia awe na amani mimi na kupika ni dam dam, fundi wa jiko nilipika msosi kwanza ata kabla haujafika mezani harufu tu ikawa inawasumbua, Anna aliniganda jikoni, anaijua shoo yangu, ndie nilikuwa nampa kuonja, ata wakati tuko shule ya msingi, nilikuwa napika yeye kazi yake ni kuonja na kunipa mrejesho, chumvi ikoje, harufu na radha…
Tukiwa bize wananisifia, tulishangaa, kaka Max kaingia jikoni, akatutizama na kusogea mpaka tulipo, nikakumbuka kaka Max anapenda kuonja nyama jikoni, nikacheka ata kabla hajasema chochote nikaongea, usinambie kaka Max bado unakale katabia kakuomba nyama jikoni, nakudokolea, Anna alicheka akasema “leo maajabu kaka Max alikuwa kaacha kukanyaga jikoni, nikajua mwenzetu jeshini wanazuiwa adi kukanyaga jikoni, kumbe ni ubishi bwana 😃😃, Max aliganda tu anatutizama, akachukua bakuli na kunipa bila kuongea chochote, nilitabasamu nikamwambia, Kaka Max kama unataka nikupe, tabasamu kwanza, ukicheka mi nakupa bila shida…
Nikashangaa kweli katabasamu, kisha akanisogelea sikioni, ata sikuogopa wala kuwaza, akaninong’oneza tu kweli utanipa bila shida? Bila kufkiria mara mbili nikamhakikishia, alitabasamu aisee uyu kaka akitabasamu anazidi kuvutia ni bonge la HB, afu anakimwanya flan ivi cha kuvutia, unatamani uendelee kumtizama tu, ila akinuna kuna vitu vinapotea, nilimsifia, Ewaaaaa!! Kaka angu uyo, Aiisee sipati picha wadada wanavyokugombania uko nje, sio kwa uzuri huu hasa apo ukitabasamu lazima wadada wachanganyikiwe…
Kaka Max alinitizama sana, nilimpakulia nyama nikamchagulia nzuri, nikamwekea nakindizi, nikageuka kumpa nakuta kaganda kunitizama, nikajua kabisa, kadata na msosi, nikamshtua akashtuka na kuchukua msosi alitoka kama kafukuzwa, tulicheka na kuendelea kuandaa mboga za majani na matunda, sipendi kuanda matundaa, nikamwachia Anna, afu dada wa kazi akawa anaandaa chakula ili kiende mezani, tuliandaa vizuri na kupeleka, tukawakaribisha kula, wakawa wamemsahau, kaka Max, ikabidi niagizwe nikamuite, nilienda na kumgongea…
Chapter 3
Niligonga, akaitikia na ile sauti yake, nilimkaribisha chakula akasema anakuja, kweli hakukawia akaja,tulianza kula, kila mtu akawa anasifia msosi umepikwa haswaa, kaka anaefatana na Max, akasema “Diana kwenye mapishi hujawai kukosea aisee nilimiss ivi vitu aisee wewe sio wakutoka umu ndani, kuna watu huwa hawali sana ila leo naona wanaongeza tu misosi, apo wote tulicheka make aliyeongeza ni Max, “Marco kuwa na heshima wakati wa kula, Max aliamua kuongea, ila Marco alijibu tu, nimegusa penyewe Bro, sema sijamwaga mtama nishukuru tu, tukashangaa Max kamkata jicho Marco mpaka akanyamaza kimya, mama akauliza ” mbona kama kuna siri inaendelea mnatuficha, aliwatizama vijana wake wote kwa zam zam lakini hakuna aliempa ushirikiano hata mmoja…
Mimi nilishiba nikainuka nikajiandae na mtoko, kumbe nimeacha watu wananishangaa, mpaka mama akaamu kukohoa kumshtua aliekuwa ananishangaa, mi kazuri japo kadogo dogo, nikakishep chakutamanisha, nilikuja nimevaa kigauni cha solo, vitu vikawa vimejificha sasa hii mchana nimefunga khanga mambo yako 🔥, walimaliza kula kila mtu akaishia kivyake, mama akaenda na Marco chamani, mimi na Anna na dada wa kazi tulibaki, dada hakutaka kuondoka leo alisema hayuko sawa, tulimsubiri kaka Max atupeleke, aliingia akajiandaa mwamba katoka mpaka nikaganda kwanza kumtizama, alikuwa kavaa shart nililowahi kumpa mimi kama zawadi siku wanaondoka, nilimpa Anna aje kumpatia, nilishangaa alijaisha tu miaka yote hiyo sikuvunga nikauliza,Anna akadakia Diana unashangaa ilo la juzi tu kuna zile zawadi tulimpa tukiwa darasa la nne huwezi amini amezitunza adi leo zipo, yani madada tunapendwa japo siku izi hatuchekei ila tunaimani sisi ndo vipenzi vyake, angekuwa hatuthamini asingetunza hivyo, Anna aliongea uku Max anasikia saa ngap asirudi kuvua, katoka na mshart mwingine nikanuna na kusema, kaka yani hio shart imekuharibikia naomba tu ukavae uliyokuwa umevaa mwanzo,akagoma nikasema kama hubadirishi hatuendi tukajua,lazima tu kwa anavyotupenda wadogo zake atarudi kubadilisha, ajabu akasema kama hamtaki kutoka rudini mkalale tukajua utani,lakini alitulazia mpaka inafika saa 10, ikabidi tu tukubali kwenda ivo ivo ila tulichukia sio mimi wala sio Anna ata kuongea hatukuwa tunaongea…
Aliona ice cream na mimi anajua kabisa napenda vibaya mno, alitununulia akatuletea lakini nikagoma, alinitizama sana nakuniambia niache utoto, ata sikujali nikazikataa, alijua kweli nimechukia, akaamua kugawa kwa watoto walikuwa wanapita, kisha akaenda kutusubiri kwenye gari, tulimaliza kuenjoy hao tukaenda kwenye gari aturudishe nyumbani, alivyoona tupo kimya tu, akaamua kuvunja ukimya na kuuliza, ” Dianna mme chukia? Huwa anapenda kuunganisha majina yetu apoa katuita wote Diana na Anna, tulikaa kimya hatukujibu, aligeuka kututizama, akakuta kila mtu yuko cool…
Chapter 4
Alivyoona tumemchunia, akanyamaza kimya mpaka tukafika nyumbani,apo roho inaniuma kuzikataa zile ice cream, najikaza tu nimefika tukakuta dada kashapika, tulioga tukatoka nilifunga zangu khanga, japo ndani nilivaa suruali, na kibode kulikuwa na joto hivyo sikuvaa kitu ndani, nilijiamini niko nyumbani, niliongea na mama angu akaongea na Anna kisha tukaenda kumsaidia dada wa kazi kuandaa meza ya chakula na kuleta chakula, mama na kaka Marco pia walikuwa wamesharudi, japo sisi tuliwatangulia…
Muda wa chakula ulivyofika, Max yuko chumbani mwake tukaagizwa kumjulisha msosi tayari, ila tukauchuna, mama akauliza kwani hamsikii? Tukajikuta tumejibu kwa pamoja, mama Kaka katuuzi, tuliulizwa katuuzi nini kila mtu kimya, mama aliamua kutupuuza na kumwambia kaka Marco akamfate, kaka alienda..
Akafika nakugonga, Max akajibu ingia alijua ni mimi, Alivyoingia Marco alimind akaanza kumuuliza kwa nini umekuja wewe kwani wengine hawapo? Marco alianza kwa kumcheka kwanza kisha akasema, ” Bro umewafanyaje dada zako wamekasirika wamegoma kuja kukuita kibaya zaidi mpaka kipenzi chako, kagoma ushaanza kumkela ata kabla hujaukamata moyo wake, sasa sijui unampango gani, “Marco ujue Dia anautoto sana, kosa ni mimi kuvua nguo aliyonipatia zawadi na kuvaa nyingine, na chanzo ni wao walianza kutamba kupitiliza, ” Bro sasa wanawake nao niwakwenda na biti lao kweli si utachanganyikiwa 🤔, ungewaacha waongee ndo furaha yao,mbona ni kawaida, tatizo hutaki kuonekana umempenda lakini nakushauri tu kwa usalama wako, mapenzi ni kikohozi, usijisumbue kuyaficha, huwezi kushindana nao, ukifanya kupingana nayo, nakuapia Bro tutakuja kukukuta humu unalia ama unataka kujiua, mapenzi hayana comando, yani cha kukusaidia tu, hakikisha unajisalimisha, waombe msaaa, kisha ongea nae, ngoja kaende chuo wajanja wapite nako ndo utanielewa, ” Marco acha kunitisha unafikiri ni rahisi hivyo?..
“Bro huwezi kuficha na ukichelewa na jinsi alivyonona saiv, nakuapia atasepa na wajanja, mama mwenyewe kashashtuka unamtizama kiaina njiani kaanza kunidadisi nimejikaza tu nisitoe siri, sasa wewe jitie unaweza kuficha, Max alishtuka mno, akaomba waende kwanza kula, walifika mezani, Max akawa anaulizia chakula cha mchana, dada wa kazi akasema kiliisha, Max alianza kula, lakini alikula kidogo sana, tofauti kabisa na mchana…
Alimaliza akainuka nakuelekea chumbani kwake, na sisi tulimaliza kila mtu akaelekea chumbani kwake, tulilala usiku ikaingia sms no ngeni, kifungua nakuta sms mimi Max save no yangu, ata kusema samahani akuna liko kusema tu save no, nilizidi kukasirika, nikapitiwa na usingizi, kulikucha nikawai kuamka na kusaidia kazi nikaandaa na vitafunwa na chai, kisha nikakaa kusubiri waje kupata chai niliwahi mno, kila mtu alivyoamka na kukuta nishapika walishangaa, dada wa kazi alinishukuru nikamwambia asijali,mama aliamka tayari nilisha msalimia nilipita kumsalimia mapema nilivyomaliza tu kupika, watu walijumuika kupata chai, nilimsalimia Max kwa shingo upande, alinitizama sana, akasema kwa sauti Dianna mjiandae kuna mahali niwapeleke…
Chapter 5
Hatukujibu chochote,ila kwa jinsi tunavyopenda kutoka, hatukuleta kisirani, Max alikunywa chai vikombe 4,mpaka Marco akaanza kulalamika ilihali na yeye kanywa vitatu, na sambusa za nyama walikula kama wapo kwenye mashindano ya kula, sisi tuliwaacha na vita yao tukaingia kujiandaa, Anna alikuja na kunipatia kigauni flan ivi, aliniandalia kama zawadi nilifurahi mno, kilikuwa chakushep kilinikaa vizuri mpaka mwenyewe nikajua kabisa nimependeza, nilitoka kila mtu akawa ananitizama mimi, mama alinisifia na kusema aisee binti yangu we ni mrembo sio haba na hio rangi yako sasa,nilitabasamu tu,nakusema chaguo la Anna halijawahi kuniangusha, Anna alikuwa na simu kubwa aliniga picha, nikanogewa na kuweka mapozi, huku nasema Mungu huwa anajua kuna kiumbe akikipa kitu fulani dunia itapata tabu,yani mimi nikipata simu yenye camera matata, mbona itajuta kumilikiwa na mimi, wote walicheka, mama akataka kuongea ila akanyamaza baada ya kusikia Max pia anaongea, naenda kukununulia saivi, aliongea hivyo ikabidi nimtizame nakuta kavaa lile shart, kapendeza mwenyewe…
Apo nikafurahi nakujibu kwa furaha, usinambie nyie nilimkimbilia nakumkumbatia kwa furaha, nikaona anashindwa ata kumeza mate nikamuachia, ila akawa kama kavurugwa hivi, akageuka na kukimbilia chumbani bila kusema chochote aliondoka kama mtu aliesahau kitu,Marco alimfata kwa nyuma, akamkuta kafumba macho huku anajipiga uso, alimzuia na kumpa maji akanywa, “umeona Bro hilo nikumbato tu, mnala umesoma, kesho anawez kukukiss kama kaka, atavaa na khanga moja umu siku moja, kisa kaka zake, kumbe ni mme na mashemeji tupo humu ndani, mshtue mapema kabla hujapata aibu ya huo mnala mbele za watu, atakuja akutambulishe mme mwenzio ubaki unalia lia hovyo, Marco aliongea kisha akatoka…
Baada ya mda, tulitoka, mimi nilikaa nyuma na Anna, tulifika maduka ya simu, akanichukulia simu, nilifurahi mno, kama kawaida kumbato nikamuongeza na busu la shavu, alifumba macho kwa hisia, akanitoa nakusema tuwahi ratiba sio rafiki, nilipanda kwenye gari uku naji snap tu na Anna, Kaka Max alitupeleka, sehemu tulizungushwa sana, ilivyofika mchana, alitupeleka sehemu kupata chakula, tumemaliza kula, akaomba akawa kapigiwa simu, akawa kama anatoka, Anna akasema kamuombe nauli turudi nyumbani,ukute anaenda zake kazini ivyo, alishawahi kuniacha mara kibao na hizo simu zake, ilibidi mimi nimkimbilie kaka Max, nikamuona kuna mahali anaelekea kwa miguu, akiwa bado anaongea na simu…
Nikawa na mfuata nyuma nyuma bila ata kuongea, tulitembea umbali mrefu mpaka nikajuta kusubiri, nakuja kutahamaki, naona magwanda inamana tuko kambi ya jeshi, nilivyojua tu ivo nikamuita kaka Max kwa sauti ili akate simu aniondoe haraka, aligeuka kwa mshangao, mda huo kuna wajeda kama 10 pia walifika nakuanza kuhoji, nilianza kutetemeka ila nikajipa moyo kaka Max yupo,saa ngap asianze kunipa adhabu yeye mwenyewe, nilijiliza lakini haikusaidia kitu…
Nilirukishwa kichura chura mpaka nikazimia, nakuja kupata fahamu niko nyumbani na pembeni familia nzima ipo,uku kaka Max ndo yuko karibu yangu zaidi, nilivyoamka, akaanza kunijulia hali, ata sikumjibu, niliuchuna, nikawasalimia wengine tu yeye nikamuacha, alielewa nina hasira nae, alinichum kwenye paji la uso nikafuta, kililetwa chakula Anna akaanza kunilisha akanipa pole nakusema, ata yeye ilishamkuta, na kaka Max hakumhurumia alimpa adhabu ya kufagia uwanja mzima wa jeshi, bila kupimzika, alivyoshindwa akaambiwa kudeki uwanja na maji, nilichoka na kujua kumbe uyu Bro anaroho mbaya sana, nilikaa vizuri ila nikawa simuongeleshi kabisa kaka Max, na hata kutoka nae nilikataa kabisa, kuliko nitoke nae bora nilale ndani mwezi mzima, hii kitu ikawa inamuumiza, akawa anatafuta namna animbembeleze…
Lakini sikuwa nampa mda kabisa, zilipita wiki mbili nimemkazia, leo mama aliniomba niende na kaka Max, nikamsaidie kununua vitu vya ndani kwake, Anna alikuwa anaumwa,nilijitetea kwa mama, lakini mama alinimbembeleza, na kuomba nisimchukue kaka Max ni kazi yake, hakuwa na jinsi, niliamua kukubali tu kishingo upande, tulienda kuzunguka nikawa namchagulia uku sitaki story namuonesha tu kisha kimya…
Tulimaliza kuhemea saa 12 jioni, tulirudi mpaka kwake, alikuwa kashusha mjengo mkubwa, afu rangi ya nyumba nzuri ilikuwa imetulia mno, tuliingia ndani, vitu navyo vilikuwa vimeshafika, Max aliomba nipike tule ndo twende nyumbani, nilikubali, make njaa ilinikamia sio poa, nilipika, Kaka Max wakati tunakula alimpigia mama akaomba nilale kesho atanirudisha kachoka muda umeenda sana, nilishtuka mama akakubali, niliamua kuongea kaka Max kama umechoka niitie ata uber niende, alinitizama kisha akasema “siwezi iamini uber, kingine apa ni kwako sizani kama kuna shida wewe kuwa hapa, sikutilia maanani alichokisema, nilimpuuza tu, alianza kuniomba samahani kwa mara ya kwanza, “Dia naomba unisamee basi naumia unavyonichunia…
Sikuwa na ujanja pale uliponifata haruhusiwi yeyote kufika na kibaya zaidi kuna mkuu wangu wa kazi alikuona nikashindwa kukutetea ingekuwa ni sehemu ya kambini lakini sio eneo hilo ningekutetea lakini pale hapakuwa salama kwa wewe kufika, sikujibu kitu niliinuka tu nikaingia chumba alichonielekeza, nikavua nikaingia kuoga, wakati natoka, nilikuwa na kitaulo kifupi sana, kumbe Max nae alikuwa anakuja chumbani, alivyoniona vile, nilipata wenge pia aibu, nikajikuta natapatapa namna yakujificha, nikiwa nahangaika kutafuta cha kujifunika nikajikuta nateleza…
Nilivyoteleza tu Kaka Max akanidaka na kitaulo nacho kikasnguka nikabaki wazi kabisa, Kaka pia alikuwa kifua wazi na kipensi tu…
Inaendelea….🔥

