Jamaa Aliua, Akafungwa Jela, Akatoka Kwa Msamaha, Tazama Alichofanya
Simulizi Ya Kweli
Julai mwaka 1991 jamaa aliyeitwa kwa jina la Gregory Green alimuua mke wake, Tonya Green ambaye alikuwa mjauzito wa miezi sita huko Michigan nchini Marekani.
Alimuua kwa kumchoma kisu mara kadhaa usoni na kifuani na baada ya hapo akapiga namba 911 na kuwaambia polisi kuhusu mauaji hayo.
Akahukumiwa kifungo kirefu tu gerezani na baada ya miaka 16 akaonekana kubadilika, alikuwa na utii, hakuwa na fujo hivyo watu mbalimbali wakaanza kumuombea kibali ili atolewe gerezani.
Marafiki, familia yake na hata mchungaji wake wote hao walimuombea mwamba atoke gerezani. Waliandika barua mbalimbali na mwaka 2008 hatimaye hilo likafanikiwa na kutolewa.
Lakini mwaka 2016 tukio jingine likatokea. Green akawamaliza watoto wake waliokuwa na miaka 4 na 5 kwa kuwawekea sumu ya hewa kwenye gari lake walipokuwa wamelala.
Hakuishia hapo, akawachukua watoto wa mke aliyekuwa amemuoa na kuwapiga risasi. Yaani baada ya mchungaji kumwamini Green, akamruhusu amuoe binti yake, sasa akaanza kuwafanyia unyama. Alipowamaliza, akammaliza na mkewe ambaye ni mtoto wa mchungaji.
Alifanya kama ilivyotokea mwaka 1991, alipomaliza kuwaua, akapiga simu polisi na kuwasubiri ili waje kumkamata.


1 Comment
This design is wicked! You certainly know how to keep a reader entertained. Between your wit and your videos, I was almost moved to start my own blog (well, almost…HaHa!) Great job. I really loved what you had to say, and more than that, how you presented it. Too cool!