INATOSHA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 4
Ilipoishia..
Nilipokuja kuzinduka tayari nilikuwa narudishwa gerezani,kitu kilichonifanya nishtuke ni tumbo la uchungu ambalo lilikuwa likiniuma na kunivuta sana haswa kwa maeneo ya kitovuni ndipo palikuwa pakiniuma sana.
“Uuhh…! Uhh….! Hapa ni wapi…? Nauliza hapa ni wapi….?”
“…yani kuua uue sasa hivi unazinduka nakujifanya hujui ulichofanya…? Si ndio…?”
“…nisameheni jamani aiyaaa…! iyaaaa…! iyaaaa….! Levina mimi naozea jela uwii…!”
Songa nayo sasa…
Nakumbuka ilikuwa mida ya saa tatu za asubuh huku nikipandishwa kizimbani tena kwa mara ya pili nakusomewa mashtaka yangu juu ya mauaji niliyofanya,yule mama niliokuwa nikiishi naye alikuwepo huku akitoa machozi yaliochochea hisia zangu nakunifanya nitamani japo kumumuuliza kuhusu miradi yangu lakini ilishindikana kwani nilikuwa chini ya ulinzi mkali,nilikuwa nikitetemeka mdomo huku meno yangu yakiumana.
Hatimaye jopo la mahakimu likiongozwa na mawakili waliojitokeza angalau kunisaidia kesi yangu japo haikusaidia kitu, nakujikuta nikihukumiwa kifungo cha maisha gerezani,nilishindwa kuzuia uchungu nilionao nakujikuta nikizimia na kupoteza fahamu zangu zote.
~ BAADA YA MIEZI 2 ~
Nilikuwa tayari natumikia kifungo changu cha maisha huku nikiwa na mimba ya miezi mitano kama na nusu hivi, niliwekwa sehemu maalumu na wasichana wenzangu ambao nao walikuwa ni wafungwa wenye mimba kama nilivyo mimi.
Nilijitahidi sana kusahau mambo yote yaliyonitokea huku nikijishughulisha kwenye vijikazi vidogo vidogo vya humu ndani ya gereza, sikuhitaji kabisa kuwa na marafiki humu ndani kwani niliamini kama nitajenga upya mazoea namarafiki humu ndani basi watajua ukweli wangu toka nilipotokea hivyo aibu kubwa iliyoambatana na siri kubwa niliiweka moyoni mwangu.
Siku zilizidi kusonga mbele kwani sasa ilikuwa imefika kama miezi mitatu toka niingie hapa gerezani bila hata ya kupata taarifa yoyote kutoka nyumbani,nilizidi kuumia sana moyoni huku nikiwa sijui nini haswa cha kufanya,
Usingizi kwangu ulikuwa ni wa shida sana kwani mara nyingi usiku katika ndoto nilikuwa nikitokewa na baadhi ya matukio niliowahi kufanya hapo nyuma na hata ile ya kumpoteza mwanangu ‘Jelly katika treni kipindi kile alichopigwa risasi na Gervas kwa bahati mbaya,nikiwa bado kwenye dimbwi la mawazo ya hapa na pale huku nikizitafakari ndoto zangu ninazoota mara kwa mara,
Ghafla tumbo likanizidia nakuanza kuniuma sana huku likinikata kata nafikiri ilitokana na mimba niliokuwa nayo,sikuwa na msaada kwa muda huu kwani wenzangu karibu wote walikuwa wakijishughulisha na wengine wamejilalia mara nikashuhudia watuhumiwa wengine wanaletwa pale gerezani lakini kati ya yao alikuwepo mtu mmoja niliokuwa namfahamu..
“Oooh My God…! kafuata nini huku huyu…”
Nilianza kuingiwa na woga huku mwili ukinitetemeka nakufanya
Meno yaumane kwa woga na mshangao wa kumwangalia yule mtu huku akinifuata eneo nililopo.
“Mamaaaaaa….?”
Niliita kwa mshangao kwani aliponikaribia kwa karibu sana nilivuta hisia nakuweza kumtambua mara moja kuwa ni yule mama niliokuwa nimemwachia miradi yangu.
“Levinaaaaaaa…?”
“Vipi…? ….imekuwaje tena na wewe umeletwa huku…?” nilipigwa nabutwaa kwa nilichokiona huku nikiwa sijielewi elewi mara, “Embu tulia ukoo mpumbavu mkubwa weee…!”
Sauti ya askari wa magereza ilimuamrisha yule Mama kuwa anyamaze kwani aliponiona tu alizidi kulia nakuniacha mwili wote ukiendelea kunitetemeka nisielewe nini chakufanya,hisia kali zilinijaa akilini zikiambatana na hasira.kiukweli nilitamani nimshike yule mama kwa nguvu zote nakumnyongea mbali kwani kumuona sura yake tu kulinizidishia hasira kali na dukuduku moyoni huku nikitaka kujua chanzo cha yeye kuacha mali zangu nakuja huku kufungwa
“nani sasa atasimamia mali zangu…? na huyu mtoto nitakayemzaa atasimamia mali zipi…?”
Ni kati ya maswali niliokuwa nikijiuliza sana moyoni bila kuyapatia majibu yeyote.
Haraka haraka nilikimbia kwenye jumba la la upande mwingine kwenda kupumzikia kisha nikachukuwa shuka nakujifunika huku nikiulazimisha japo usingizi niweze kusahau kwa muda lakini bado hilo halikusaidia chochote,nilisumbuka kwa muda mrefu kidogo pale kitandani huku nikitapatapa kitandani,nikiwa bado nipo najigeuza huku na kule mara sura yangu ikakutana tena kwa mara ya pili na yule Mama akijongea huku kavalishwa jezi zetu za huku gerezani na kwa muda huu alikuwa ameshanyolewa upara mkubwa,alikuwa akiangaza huku na huku.
“We mama unakwenda wapi…? au na wewe una mimba kama sisi…?”
Aliropoka Yuni,mmoja wa wafungwa huku akimtolea macho yule Mama kwani sisi wafungwa tuliokuwa na mimba tulikuwa tumetengewa sehemu maalumu tofauti na wengine ambao hawakuwa na mimba,yule Mama hakusikia lolote akawa anazidi kusogea huku akiendelea kuangaza huku na kule mara wafungwa wenzangu kama watatu wakamvamia nakutaka kumpiga.
“Mwacheni.. Mwaaacheeeee….!”
Niliongea kwa sauti kali na ya juu nakufanya kila mtu anishangae na pia nilikuwa naogopeka ndani ya muda mfupi niliokuwa nimepelekwa pale gerezani,basi wale wafungwa wenzangu walinielewa na kumwacha huku akinifuata mpaka kwenye kitanda changu.
“..Levina…?”
“..unasemaje…?”
“…..kuwa mpole Levina nikusimulie kilichonikuta..”
Moyo wa huruma ukaanza kunitawala,kutokana na kila mmoja wetu kunitolea macho mimi na yule mama,nilichokifanya nilimshika mkono nakumtoa mpaka nje kisha.
“Haya niambie Mama kilichokusibu huko uraiani…?”
“…mwanangu Levina…? Ni stori ndefu lakini haina budi kukuelezea…”
“we niambie tu imekuwaje huko….?”
“ni kuhusiana na Gervas…!”
“Gervaaaaas….? Gervas yupi tena…?”
“…si yule aliyekuwa mumeo….!”
“Enhe…! Kafanyaje tena si alishakufa….?”
“Hapa ninavyokueleza nikuwa Gervas hajafa yupo hai na anaishi mpaka sasa..!”
“anaishi na nani tena Jammy..? Uhhh…! Uhh…!”
Nilijihisi mkojo unapenyeza ndani ya nguo yangu ya ndani huku nikijihisi kama uchungu wa kujifungua mimba kabla ya muda wake, kijasho chembamba kilianza kunitiririka kikiambatana na msisimko mwilini uliofanya mishipa ya kichwani kunitoka na kusababisha kubaki mdomo wazi kwa muda huku macho yakiendelea kunitoka yakiambatana na mchozi kwa mbaali ulioanza kunidondoka..,
“unasema kweli mama…?”
“Levina,ujue niliumia sana pale maaskari waliposhirikiana na wafanyakazi wa Gervas na Bosi,Happy kufanya maamuzi ya haraka ya wewe kuhukumiwa kifungo cha maisha bila hata kufanya mazishi…”
“Mama…! Nilistahili kufungwa kifungo hiki hiki cha maisha wala hawakukosea….?”
“lakini mbona Gervas mzima…?”
“hata kama….! Nilivyoona huko nyuma mpaka nikasema Sitaki tena,nastahili kufungwa maisha…! enhe embu nieleze ilikuwaje baada ya mimi kuhumiwa Gerezani maisha….?”
“Levina…,unakumbuka siku ulipowapiga risasi Gervas,Jammy na omari…?”
“…nakumbuka na siwezi kusahau katika maisha yangu,kwani ilikuwaje….?”
“basi Levina baada ya wewe kuwapiga risasi pale wakaanguka chini na kilichofuatia miili yao kuwaishwa hospitali ya ‘LUTAHIA ‘ moja kwa moja mpaka chumba cha wagonjwa mahtuti kwani walikuwa bado wanahema,hivyo niliwafuatilia mpaka kujua hatma ya miili yao,nilikaa peke yangu pale hospitali mpaka usiku nikijibanza huku nikitaka kujua kama kweli atapona mtu au la,mpaka ilipofika usiku sana kwenye mida ya saa sita nikashuhudia jopo la madokta wakiongozana na manesi huku wakishikilia dripu na wengine mirija ya kutolewa hewa (oxygen) wakiwa wanaburuta mgonjwa kwenye kile kibaiskeli lakini yule mgonjwa sikuweza kumtambua kama ni Gervas,Omari au Jammy kwani alikuwa mbali,pale pale ndio ukawa mwanya kwangu kuingia kwenye chumba kingine nikitaka kujua aliyebaki ni nani?
Nilipofika tu ndani ya kile chumba cha wagonjwa mahtuti nikakutana na askari mmoja akiwa na manesi huku wakimsimamia yule mgonjwa aliokuwa amebaki….”
“nani sasa Gervas…?”
“tulia sasa nikumalizie Levina mbona una haraka hivyo….?”
“na we nawee….! haya endelea,ikawaje sasa…?”
“…pale pale nikachukuwa bunduki ya yule askari kinguvu na kumuua kwanza yule askari kisha nikawafyatua wale manesi mule chumbani nikausogelea ule mwili nakwenda kuufunua nikidhania labda atakuwa ni Gervas, nikaufunua,kumbe alikuwa ni Jammy tena anaonesha hakufa vizuri kwani alikuwa akipumulia mirija,pale pale nikammalizia kwa ile bunduki kisha nikatoka nje huku nikifuata mwili wa Gervas ulipo,mwili wangu wote ulikuwa umechafuka damu,watu wengi waliniona jinsi nilivyo ikiwa ni pamoja na manesi na baadhi ya wagonjwa walinikimbia huku na kule kwa usiku ule,makelele yalitawala sana karibu eneo lote,hatimaye nikawa nimeingia wodi aliyekuwa amepumzishwa Gervas,niliwakuta maaskari takribani sita na madokta huku wakiwa hawajui kinachoendelea kwani walikuwa wakisadiana na manesi bila kupoteza muda nikalikoki lile bunduki nakuanza kupiga baadhi ya maaskari na manesi,nilifanikiwa kuwapunguza kwani maaskari wote sita walikuwa tayari nimeshawaua wakiwa ni pamoja na madokta wawili,baada ya hapo nikausogelea mwili wa Gervas nikaunyoshea ile bunduki nakuanza kufyatua huku Gervas akionesha kuniangalia kwa macho ya huruma,
“….kwa hiyo ukamfyatua….?”
“hapana Levina..?”
“shit…!!! Sa kwanini ukamwacha na wewe…? Au umesahau alivyonitendea…?”
“….nakumbuka levina na ndio maana nilikuwa na uchungu naye wa kutaka kumuua…!”
“sasa kwanini ulishindwa kumuua Mama…?”
“hapana…!! Ile nataka tu kufyatua nilishtukia napigwa sindano ya usingizi shingoni mwangu na Dada mmoja alioonesha kuwa ni nesi wa pale hivyo nikamgeuzia bunduki nakumfyatua,nilimmiminia risasi kwa hasira mpaka nguvu zikaniisha nakujikuta usingizi mzito ulioambatana na kulegea kwa viungo vyangu vya mwili, papo hapo nadhani ndipo nilipokamatika,kwani nilipozinduka nilijikuta nipo mikononi mwa polisi huku mikono yangu ikiwa na pingu nikisomewa mashtaka ya mauaji.
“…sasa imekuwaje umeletwa hapa…?”
“Levina….!! Nilisota sana katika gereza la ‘USANTU ‘ pale Mtwara na kutokana na umri wangu kuzeeka sana hivyo nikaletwa huku kuwasaidia baadhi ya wafungwa wajawazito sana sana wale wanaokaribia kujifungua…”
“…pole sana Mama kwa yaliokukuta….!”
“Ahsante Levina mwanangu…, na hivi ninavyokuambia nimeletewa taarifa kuwa mali zote anazimiliki Gervas hivyo kaa ukijua Gervas kapona nakuwa sasa anafanya kila njia kuhakikisha tumekufa huku gerezani….”
“Hamuwezi mtu hapa…”
Moyo wa kishujaa ulianza kunitawala nakuona sasa acha niwe Levina yule wa zamani.’
“Mama…? ingekuwa hii mimba ina miezi miwili au mitatu ningeshaitoa…”
Hasira zilizonitawala akilini mwangu nakunifanya niropoke maneno huku nikimwacha mdomo wazi yule Mama.
“Mama….? ama zake ama zetu…. Nitahakikisha mali zote zilizo kwa Gervas, anasimamia huyu mtoto wake huku tumboni na siyo huyo msaliti mkubwa asiyekuwa na hata chembe ya huruma…”
Siku zangu za uchungu wa mimba zilifika huku yule mama akiwa ni mtu wa karibu sana na mimi kuhakikisha najifungua salama, kwakuwa alishawahi kuwa nesi hivyo alinisaidia yeye na baadhi ya manesi nikajifungua salama namshukuru mungu nilipata mtoto mzuri wa kike,
~ BAADA YA WIKI 1 ~
Uchungu ulishapotea na sasa ilikuwa ni furaha tu juu ya mtoto niliekuwa naye, ilifika kipindi hadi nikajisahau kuwa ni mfungwa kutokana na furaha niliyokuwa nayo.. “Mama embu niambie huyu mtoto tunamwita jina gani sasa…?” “Daah.. Kwa mimi ningependelea umwite Happy…!”
“Nani…? Happy…? Umeshamsahau yule mpuuzi wa Zambia, si anaitwa Happy… hapana hilo jina silitaki…” “kweli Levina, sasa tumwite nani…?” “Lauryn…” “ndio limaanisha nini sasa…?”
“mh..! nawe Mama umezidi sana ushamba, hayo majina ya kizungu na halina mana yeyote na kifupi chake ni Lau…” Furaha ilizidi maradufu kwani tuliafikiana mtoto aitwe jina la ‘Lauryn’ nakuanzia siku hiyo mtoto akawa anajulikana jina la Lauryn au Lau. Maisha yalizidi kuwa mazuri.
“Levina…?”
“abee…”
Ilikuwa ni sauti ya yule Mama ambaye alikuwa karibu sana na mimi na kwa muda huu alikuwa ametoka na amerudi huku akihema,
“unasemaje Mama,kwanza mbona upo hivyo…?”
“Levina…? Amini usiamini nimemuona Gervas mwenyewe…”
“Gervaaaaaaaaaaas…?”
“ndio,yupo kule anaongea na maaskari tena nimemshuhudia akimpa kibahasha kidogo cha kaki askari mmoja pale…”
“sasa we Mama…? Unafikiri mimi naogopa kitu…? Hapa hanitishi chochote….!”
Tangu nimzae mwanangu Lau nilizidi kujiamini kwa kila kitu na ndicho kitu kilichonisaidia huku gerezani ‘UKONGA’ kwani kiukweli niliogopeka sana Levina mimi,nikiwa bado nipo na yule Mama tunaongea mara akaja askari mmoja wapo hadi eneo tulilokuwepo,
“Levina…? Unahitajika ofisini sasa hivi…!”
“sehemu gani…?”
“upande wa mapokezi tena ufanye haraka..”
Sikuwa na hali ya hofu kabisa zaidi ya kuzidi kujiamini huku nikiamini kabisa Gervas hawezi kunifanya chochote,
“Mama…? Embu nipe mtoto wangu niende naye kabisa…”
“Levina mwanangu,mimi nakuomba umuache hapa utamkuta tu mwanangu…”
Nilimuamini sana yule Mama hivyo nikaamua kumuachia mwanangu,huku nikiondoka taratibu mpaka kwenye ile ofisi,
Nilipofika tu macho yangu yalikutana uso kwa uso na Gervas akionesha mwenye afya tele tena akionekana kung’ara sana kuanzia ngozi yake mpaka mavazi,
“umefuata nini malaya mkubwa wee…?”
“Levina mpenzi….”
“Naaaaani…? Nani mpenzi wako…?”
“naomba unielewe najua kuwa ni vigumu kwa mimi nawewe kurudiana ila….”
“….ila nini? Ulivyonisaliti Gervas inatosha…, inatosha Gervas…?”
“kumbuka una damu yangu Levina,na mtoto anahitaji apate malezi bora kutoka kwako na kwangu pia…”
“leo hii unakumbuka hilo…?”
Nikamjibu na kumfyonza pale pale huku nikiinuka nakuondoka zangu kurudi kwa mwanangu nilipomuacha na Mama
“Levina pliz..!,usiondoke mpenzi,pliz Levina..!”
Sikulijali hilo zaidi ya kugeuza jicho langu la ukali huku nikimshuhudia Gervas akitokwa na machozi kwa mara ya kwanza tangu tulipoachana naye kipindi kilee.
Kiukweli nilikuwa na jazba ya hali ya juu,maaskari wote pale walikuwa wakitushangaa na wasielewe kitu gani kinaendelea kati ya mimi na Gervas,nilitoka pale na nilipofika sehemu yangu ya kupumzika sikumkuta yule Mama pale nilipokuwa nimemuacha,hofu na akili kunibadilika vilinianza huku nikichanganyikiwa nisijue Mama alipoelekea,
“eti yule Mama ninayekuwa naye karibu umemuona wapi…?”
Nilimuuliza mmoja kati ya wafungwa wenzangu naye hakujua alipoelekea,nilizidi kuchanganyikiwa huku nikielekea kumtazama japo chooni,napo nilipofika sikumkuta hivyo nikarudi tena bwenini huku nikiendelea kuchanganyikiwa mara mfungwa mwenzangu mwingine akanifuata nakuniambia kitu..
“umesema…?”
“kweli,ulivyoondoka tu kwenda ofisini,walikuja maaskari wawili wakamchukua nakwenda naye huko huko ofisini ulipokuwa”
“pamoja na mwanangu…? Au mwanangu kamwacha na nani…?”
“ameondoka huku kambeba mtoto”
Sikutaka kusikiliza tena chochote zaidi ya kukimbia huku nikirudi eneo la ofisini,nilipofika napo sikuweza kumwona,kijasho chembamba kilichoambatana na mkojo vikianza kunitoka huku nikijihisi kama nina presha tena ile ya kushuka,
“namtaka mwanangu.., namtaka mwanangu…?”
“we acha upumbavu hapa,huyo mwanako kaletwa na nani hapa mpaka umtake…? Na yuko wapi…?”
Aliongea askari mmoja wa kike aliyeoneshwa kukasirishwa na kitendo cha mimi kung’ang’ania mtoto huku simuoni,wale maaskari walinipiga vibao huku wakinivuta kuelekea ndani ya bweni, lakini kwa bahati nzuri macho yangu yaliweza kupenyeza mpaka kwenye kakorido kapale ofisini kwa maaskari nakumshuhudia Mama akiwa amembeba mwanangu ‘Lau’ huku akiwa na Gervas namaaskari kwa pamoja wakitoka nje kabisa,
“Mama unakwenda wapi mama..? mlete mwanangu?”
Nilizidi kuumia huku wakiendelea kuniburuza na kunipiga,niliumia sana lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kubaki nikirudishwa ndani huku mwili wote ukinilegea na kupoteza nguvu kabisa hapo hapo nikajihisi kizunguzungu.
**********
Nilipokuja kuzinduka nilijikuta bado nipo ndani ya bweni,nikaamka pale kitandani nilipokuwa nimelala haraka haraka nikainuka nakuelekea nje huku nikiwa na shauku ya kujua kama ni kweli mtoto wangu ‘Lau sina tena au la!
Kagiza kalikokuwa kametawala huku ubaridi mkali ulioambatana na upepo ulinifanya nirudi tena ndani huku wenzangu wakinishangaa jinsi nilivyokuwa nimechanganyikiwa,
“Lau..! Lau mwanangu….? Umekwenda wapi Lau…?”
Nilikuwa mtu wakuongea mwenyewe huku mchozi ukiendelea kunidondoka,ndipo nilipofika hadi eneo la kitanda changu na kwa safari hii niliweza kutambua kama kuna kitu nilikiacha pale,haraka haraka nikaangalia nakugundua kuwa nikikaratasi tena kilichokunjwa kunjwa ovyo huku nisielewe ule mwandiko ulivyokuwa umeandikwa,nilijitahdi kuusoma vizuri tena kwa mara ya pili,
“SAMAHANI SANA LEVINA KAMA UTAKERWA NA MIMI LAKINI IMENIBIDI KUFANYA MAAMUZI HAYO…, KWA TAARIFA TU MIMI SIYO MFUNGWA ILA NILITENGENEZWA TU ILI KUHAKIKISHA HUYU MTOTO WAKO ‘LAURYN’ ANAKUWA MIKÖNONI MWA GERVAS..,
GERVAS AMENITUMA NA HATIMAYE NIMEWEZA,HIVYO YALE YOTE NILIOKUSIMULIA HAPO NYUMA KUHUSIANA NA GERVAS NA JAMMY NI UONGO MTUPU KWANI BADO WOTE WANAISHI PAMOJA KAMA WANANDOA WANAOTAMBULIKA,
NAKUTAKIA KIFUNGO CHEMA HUKO GEREZANI,
MIMI NI MAMA ULIYENIACHIA MTOTO WAKO…”
Niliumia sana baada ya kusoma kile kikaratasi huku nikizidi kuchanganyikiwa nisijue nini cha kufanya,
“….Yani Mama ndio wakunifanyia mimi hivi…? Mama…? Ama kweli nimeamini rafiki yako ndio adui yako, na umuaminiaye ndiye akugeukae..! ama zangu ama zao na niwe hai ama nimekufa nitahakikisha mtoto wangu Lau anarudi mikononi mwangu kwa njia yeyote ile hata ya kumwaga damu,miye ndio Levina yule unayemfahamu…”
Nilijisemea kimoyomoyo huku akili yote nikiiamishia ni jinsi gani mwanangu anarudi tena mikononi mwangu.
~ BAADA YA WIKI TATU ~
Bado nilikuwa katika majonzi mazito huku nikiwachukia zaidi wale maaskari waliokuwa wakinipiga mara ile ya mwisho nilipompoteza mwanangu Lau kwenda kwa Gervas, nikaanza mipango taratibu huku nikiangalia njia zote zakuweza kupambana na Gervas pamoja na Mama na huyo Jammy wao, kila muda nilikuwa sibanduki maeneo ya ofisi za maaskari huku nikijiamini kwa asilimia mia kuwatoka wale nitakuwa kama nimelamba dume kwani ndio utakuwa mwanzo wa mimi kutoroka.
Nilifanikiwa kujua kila kitu ikiwa ni pamoja na wafungwa wote wanapoachiwa huru kwa msamaha wa Rais huwa majina yao na rekodi yao kwa ujumla huwa zinafutwa kwa kupigiwa mistari majina yao.
Nakumbuka siku moja niliamua kutokulala kabisa huku usiku wote nikiutumia katika kuhakikisha natoroka,wafungwa wenzangu karibia wote walikuwa wamepitiwa na usingizi,kila muda nilikuwa mtu wakutoka nje huku kisingizio kikubwa ikiwa nikuelekea chooni.
“safari hi iwe na isiwe lazima nitoroke tu, mie ndio Levina”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijivika moyo wa kijasiri nakuhakikisha kwanza breki ya kwanza naelekea katika mitambo nakuzima umeme eneo lote la gerezani,nilinyatia huku nikijiziba ziba katika kijigiza huku nikijiamini kuwa nitafanikiwa,hatua mbili tatu kabla sijafika sehemu ya mitambo nilikutana na askari lakini kwa bahati nzuri hakuweza kuniona hivyo ilikuwa kama mwanya,nilivuta kipande kidogo cha chuma kilichoonekana chini kwangu nakumuwahi kumziba mdomo kisha nikampiga na kile chuma maeneo ya utosini mwake kwa nguvu na hasira na hatimaye nikamuua,nilimlaza pale chini kisha kilichofuata niliichukuwa bunduki yake nakuingia mpaka chumba cha mitambo kisha nikazima ‘main swtich’ (umeme mkubwa unapotokea ),
Kisha kilichofuata nigiza lililofanya wafungwa wote wapige kelele gereza zima huku na kule,giza kali lililokuwepo limetanda pale ilikuwa jibu tosha kwa mimi kuongoza mpaka lango la kutokea huku kila askari niliyekutana naye nilikuwa nikimfyatua tu,nilijihisi kama umati wa wafungwa wenzangu unanifuata huku risasi zikiendelea kurindima humu ndani.
Hatimaye nilifanikiwa kutoka mpaka nje ambapo kulikuwa hamna giza lolote,nilijibanza kupitia magari ya pale gerezani yaliokuwa yamepaki nje, nikiwa bado nasikilizia ni jinsi gani nitaendelea na safari yangu mara umeme ukawa umewashwa mule ndani gerezani,hofu ikaanza kunitanda ,huku nikiwa nimeshatoka nje ya gereza nikishuhudia mapolisi kama wanne wakitoka nje ya hili gereza huku wakiambizana,
“kapitia huku,we pita huku siye tunapita upande wa huku…”
Nilijihisi kama mkojo unataka kunitoka kwani nilikuwa nimejificha uvunguni mwa gari,wale askari walizunguka huku na kule lakini mwishowe niliwasikia wakipanda gari ambayo nilikuwa nimejificha uvunguni mwake,nilitamani nichoropoke lakini isingekuwa rahisi kwani askari kama wawili walikuwa wamebaki eneo like lile la pale magereza,gari ilianza kuwashwa,hatimaye uzalendo ukanishinda nakuamua kutoka pale uvunguni mwa gari,
“kamata huyo,kamata afande..!
Kama kawaida Levina mimi ujasiri niliokuwa nao ndio ulinisaidia kuchoropoka mbele ya wale maaskari kwani na ndani ya sekunde chache tu nilikuwa nimeshajificha tena kwa mara ya pili huku nikiwasikilizia wale maaskari kama kweli watakuwa wameniona nilipojificha..
“…Mkuu limepita kwa huku…”
“Sasa wewe nenda upande wa huku nami wa huku sawa….?”
Zilikuwa ni sauti za wale maaskari wakiambizana njia ya kunitafuta,nikiwa bado nipo maeneo ya pale pale mara nikahisi kama naguswa na kitu mabegani mwangu,akili yote ikaanza kunihama na ujasiri kunipungua huku nisielewe nini cha kufanya kwa muda ule,nilitamani sana nigeuke ili nimjue ni mtu gani mara tena nikaskia sauti za wale maaskari wakiongea,
“Mkuu nimerikamata hili hapa…!”
Pale pale nikaendelea kupata hisia tofauti nakugeuka nyuma haraka huku nikianza kutetemeka nakuona sasa mwisho wangu utakuwa umefika na kama nitarudishwa tena gerezani itakuwa nikifungo cha kunyongwa na wala si cha maisha tena nilipogeuka tu,
“….Uuuhfff….”
Kumbe ulikuwa ni uoga wangu tu kwani hakuwa mtu yeyote bali ukuta niliokuwa nimeuegemea ulinipa hisia tofauti, fasta fasta nikatoa macho yangu nakuangaza ili nijue ni mtu gani aliyekamatwa na wale maaskari ile naangalia upande wa pili namuona ni mfungwa mwenzangu ‘Yuni’ ambaye naye alikuwa ametoroka na kwa muda huu alikuwa yupo mikononi mwa wale askari waliokuwa wakinitafuta na kiukweli walikuwa wanahasira sana kwani walimvamia yule ‘Yuni’ bila kujali alikuwa anamimba au la!
“Maskini Levina mimi, nimenusurika pale….?”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiondokea eneo lile taratibu nikinyatanyata huku nakule huku nikijificha kwenye magari moja baada ya jingine, kwa muda huu sikuwa natetemeka tena kwani nilijikuta woga wote umenitoka japokuwa nilikuwa sijatoka lile eneo la magerezani na tena bado nilikuwa ndani ya zile sare za magereza lakini kwa sasa nilishaanza kulivuka bila kukutana na mtu yeyote wala kitu chochote mara,
“…we mama unakwenda wapi utakufa wewe…?”
Ilikuwa ni sauti ya dereva taksi mmoja ambaye kidogo anigonge nilivyokuwa navuka barabara kwa uoga na kwa muda huu alisimamisha gari yake nakuniongelesha,
“…Achana na mimi endelea na safari yako…”
“Wamama wengine bwana mnamatatizo kweli, haya nenda ukafungwe huko….?”
Japokuwa nilimjibu vibaya yule dereva lakini alipoongea suala la kurudi gerezani moyo wangu ukaniripuka ghafla,
“we dereva…?”
“si umeniambia niachane na we Mama…? Sasa unachoniitia nini tena”
Hasira kali zilimshika yule dereva akawasha gari kwa kasi huku akitaka kuondoka,
“….Dereva..!, Dereva..!, simama pliz….?”
Akalisimamisha gari lake na hapohapo sikutaka kupoteza muda nikaufungua mlango wa ile teksi nakuingia palepale,
“Nipeleke kurasini…?”
“Samahani sana siwezi kubeba mfungwa mie…?”
Alijibu kwa nyodo huku akikataa kuondoka na mimi katukatu, tukiwa bado tunajibizana pale pale nikageuza kichwa changu nakuaangalia upande wa nje macho yangu yakakutana na rundo la maaskari wakiwa wanakaribia eneo ambalo nipo pale,
“…..Dereva pliz washa gari twende, nitakamatwa mimi…?”
“Ni heri ukamatwe kuliko niongozane na wewe, wafungwa kama nyinyi ni kesi tu…”
Yule dereva aligoma katu katu na mpaka akaamua kulizima kabisa gari lake huku akiwatizama wale maaskari waliokuwa bado kidogo wafike eneo tulilopo, nikajivaa sura ya Levina yule wazamani nikaona kama nitaendelea kumbembeleza huyu dereva atanifanya nikanyongwe gerezani,nilichokifanya nikamsukuma upande aliopo mpaka akatoka na mlango akadondoka nje kabisa kisha kabla hajainuka pale chini nikaliwasha gari nakuanza safari,lakini huyu dereva alionesha kuwa mbishi sana kwani aliingia kupitia mlango wa pili hivyo nikaliendesha gari kwa kasi huku nikiliyumbisha huku na kule japo adondoke lakini alinishika ‘mstering’ hapo hapo nikagundua kuwa hapo kitu cha kufanya nikuwasha kile kidude cha moto wanachotumia kuwasha sigara kwenye gari nikakiwasha nakukichomoa huku nikiendelea kuendesha gari kwa kutumia mkono mmoja wa kulia na mwingine nikiutumia kumchoma yule dereva shingoni na usoni mwake,alinipiga vibao na mangumi lakini sikujali zaidi yakuendelea kuliyumbisha gari mpaka mwenyewe akasalimu amri baada ya mimi kufunga breki ya kushtukiza akagonga kioo cha mbele nakuzimia papo hapo, ikanibidi kupunguza mwendo lakini ile namshangaa yule dereva alivyozimia mara king’ora cha polisi nikakisikia kikiashiria kinanifukuzia, hapohapo bila kupoteza muda nikafungua mlango kisha nikamsukumiza yule dereva aliyekuwa amezimia na kilichofuata nikutoka kwa kasi ya ajabu huku nikiitafuta barabara ya ‘Pugu’ kwa usiku ule wa mida kama ya saa 5 na nusu usiku huku nikielekea barabara ya ‘Chanika’,spidi ilikuwa kali kwani niliendesha mpaka spidi 160 lakini bado gari la polisi lilikuwa nyuma yangu likinifukuzia, ndani ya dakika kama kumi na tano nilikuwa njia panda ya ‘Kajiungeni’ huku nikiendelea na safari ya kuwakimbia mapolisi waliokuwa wakinifukuza kwa nyuma,
“Oooh.., my God…!, Why…!Why…! Why…! Why…?”
Ile gari niliokuwa nayo ilikuwa imeshaanza kuishiwa nguvu na kwa muda huu ilikuwa imepungua sana spidi kwani ilikuwa inashindwa kupanda hata kamwinuko kadogo,ma kwa muda huu ilipungua kabisa spidi mpaka ikafika spidi 40 na haikuzidi zaidi ya hapo kila nilipoizidisha hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kusimamisha lile gari kisha nikaingia uvunguni mwa ile gari nakujificha ili kama liwalo na liwe,
Haikufika muda sana kwani ndani ya dakika kama mbili tatu nilisikia sauti za watu wakiongea wenyewe kwa wenyewe,
“ritakuwa rimekimbiria wapi sasa….?”
Hapo hapo halmashauri yangu ya kichwa ikanituma moja kwa moja kuwa itakuwa ni wale maaskari tu,niliendelea kujibanza pale uvunguni mwa gari huku sala zangu zote nikizielekezea kuwa waondoke eneo lile nililopo.
Mara nikaanza kuhisi majimaji yananidondokea mwilini,hivyo nikachukuwa mkono wangu nakugusa kisha nikanusa ili nijue nikitu gani,
“Mungu wangu…!”
Yalikuwa ni mafuta yalioonesha kuvuja sana kutoka kwenye lile gari nililokuwamo tena ya petroli na kwa muda huu yalikuwa yakivuja kwa kasi huku yakiniloanisha nguo zangu (sare za magereza) nilitamani nichoropoke lakini haikuwezekana,wale mapolisi nao hawakutaka kuondoka haraka pale hivyo wakaniweka katika wakati mgumu.
Mara nikahisi kama kipisi cha sigara kimeangushwa na polisi mmoja wapo,pale pale moto kwa mbaali ukaanza kunifuata,nikajibiringisha upande wa pili fasta kabla moto hujanilipukia na kwa bahati nzuri nikawashuhudia kwa mbaali wale mapolisi wakiondoka pale na kuelekea kwenye gari lao kwa ajili ya kuondoka,walipoingia tu kabla hawajaondoka nikaliwahi gari lao nakudandia kwa nyuma, mara moto ukalipuka katika lile gari nililoliacha hivyo ikawafanya wale askari washuke kwenye gari lao nakurudi tena maeneo ya lile gari lilipolipuka,
“Bora rife…, ripumbavu kabisa…”
Nilisikia sauti ya askari mmoja akishukuru kuwa ni bora nimekufa kwenye ule moto ulioripuka pale,
“Afe nani…? mtakufa nyie…!!!!!”
Nilijisemea kimoyomoyo
Huku nikiingia ndani ya gari lao kiulaini bila wao kujua kisha nikaliwasha gari lao fasta nakuligeuza huku nikiwafuata pale walipo,nadhani hawakujua kama ni mimi hivyo niliongeza spidi kali pale pale nikawapitia baadhi ya mapolisi nakusonga mbele huku nikijiamini kwa asilimia mia kuwa hawaniwezi na hataniweza mtu yeyote,
“….na bado Gervas, Jammy na huyo Mama aliyenichukuliwa mwanangu Lauryn, ole wao niwakute huko…?”
Njia nzima nilikuwa mtu wakuongea mwenyewe huku nikiendesha gari lile kwa kasi,nililipita lile eneo la magereza kwa kasi ya ajabu bila wao kulitambua kama ni gari lao,hivyo ndani ya kama nusu saa nilikuwa raundi abauti ya pale ‘Kamata’ (k/köo) huku nikiitafuta ‘Kurasini’ nilipokuwa nikiishi mimi na Gervas.
Kadri nilivyokuwa napakaribia ndivyo mapigo yangu ya moyo yalikuwa yakinienda kasi hivyo nilipokaribia kufika tu nikalitelekeza gari barabarani kisha nikachukuwa bastola iliyokuwepo ndani ya lile gari nakutembea kwa mguu mpaka maeneo alipokuwa akiishi Gervas.
Giza kali lililokuwa limetanda halikunitisha hata kidogo eneo lile hivyo ndani ya kama dakika kumi nilikuwa nje ya geti la nyumbani kwa Gervas.
Nilipiga hodi taaratibu huku nikiamini tu lazima mlinzi atafungua,
“….wewe ni nani na unataka nini usiku huu…?”
“naitwa Mamamia Mango, pliz nifungulie…?”
Yule mlinzi akawa na moyo wakunifungulia.
“…unataka nini usiku wote huu…? Na unatokea wapi….?”
“Nakaa mtaa wa pili huko, ona Mume wangu amenipiga kweli na amenifukuza,hivyo nimekuja kwa mjomba wangu Gervas kupata hifadhi….”
“sikiliza binti, Bosi Gervas huwa hapendi kuamshwa wala kugongewa anapolala hivyo kama utaweza kuvumilia kwani sasa ni saa tisa kasoro hivyo jipumzishe hapa pembeni ‘then’ kesho asubuhi atakupokea vizuri tu…”
Nilihisi kama yule mlinzi anamachale kwani angeniachia mwanya kidogo tu ningeharibu kila kitu,hivyo nilichokifanya sikukata tamaa zaidi ya kuendelea kumbeleza amuamshe Gervas anifungulie,
“…nimesema siwezi kumuamsha bosi wangu sawa…? Na ukiendelea kunilazimisha na mimi nitakupiga kama huyo Mumeo, nikufukuzilie mbali mpumbavu mkumbwa wee….!”
Niliona sasa yule mlinzi anataka kama kunizoea hapohapo mkono wangu ukapapasa mpaka mifukoni mwangu nakuchomoa ile bastola na kilichofuata nikumnyooshea,
“haya twende ukamuamshe huyo bosi wako fala wee…”
Akawa bado mbishi japo alikuwa amenyoosha mikono juu kujisalimisha huku akielekea mlango wakuingilia nyumba kubwa ya Gervas,nikamuwahi kwa mgongoni nakumfyatua risasi mbili za fasta akawa amekufa na kilichofuatia nikuuburuza mwili wake mpaka kwenye kibanda chake,na hapo nikaanza kulitafuta dirisha analolala Gervas.
Madirisha yote yalikuwa yale ya vioo tena ya ‘kuslide’ hivyo ikawa rahisi kujipenyeza ndani ya dirisha mojawapo huku nikiamini ni lakina Gervas,kulikuwa ni giza sana hivyo nikaingia hivyo hivyo kisha breki ya kwanza ni kuangaza kitandani huku mkononi mwangu nikishikilia ile bastola kikamilifu,nilipofika kitandani tu,
“Sshh…! nyamaza kimyaa,ole wako upige kelele…? Mwanangu yupo wapi…?”
Hakuwa Gervas wala Jammy bali alikuwa ni yule Mama aliyemtorosha mwanangu na kwa muda huu alikuwa mikononi mwangu.
“yupo kalala na Gervas chumba cha pili…”
Alipomalizia tu kusema hivyo hapo hapo nikamfyatua yule Mama kimyakimya akafa na kilichofuata nikuenda chumba cha Gervas, nilipofika kila nikijaribu kufungua mlango wake ilishindakana kwani kulikuwa kumelokiwa hivyo halmashauri yangu yakibhwa ikafanyakazi fasta nakugundua kuwa nipitie dirishani kama nilivyofanya kwenye chumba hiki,ndani ya dakika kama mbili nilikuwa nimeshaslide dirisha la Gervas kimyakimya nakuingia kiulaini bila ya wao kujua,nilipoingia tu nikawasha taa sambamba na bastola yangu nikawanyoshea.
“Levina…? Umefuata nini hapa…?”
Nilihisi kama wananipotezea muda wangu tu,nikaikoki vizuri bastola yangu ile nataka kuwafyatua tu mara sauti ya mwanangu ‘Lauryn’ nikaanza kuisikia analia hivyo mwili wote ukanisisimuka nakuachia ile bastola ikinidondoka huku nikimfuata kwenye kakitanda chake cha kulalia huku nikiwaacha Gervas na Jammy wakiendelea kunishangaa, nilipomfikia karibu tu nguvu ziliniishia nakujikuta nikidondoka kwenye kitanda alicholala Gervas na Jammy hapo hapo kwikwi ikanishika na macho yakageuka huku mishipa ya shingoni ikinitoka ikiambatana na mapovu pembeni ya mdomo wangu ikiashiria kama sio kifafa basi itakuwa ni dalili kupooza mwili wangu.
Nilipokuja kuzinduka tayari nilijikuta nipo kwenye kibaiskeli cha kubebea wagonjwa sebuleni kwa Gervas huku macho yakinitoka kwani kwa muda huu nilikuwa mtu niliyepooza, uwezo wa kuona nilikuwa nao lakini sikuweza kutambua kitu chochote ikiwa hata na sababu ya mimi kuwa hapa,kifupi sikuwa na fahamu yeyote lakini kilichokuwa kinanishangaza ikifika muda wa kula kuna dada mmoja ndio alikuwa akinilisha chakula na ninapokitema au kutapika naambulia kupigwa vibao na makonzi, nilikuwa si Levina yule aliyekuwa mtukutu kutokana na kupooza kwangu.
***********************************
::: Levina mikononi mwa Gervas na Jamila upya huku Levina akiwa amepooza na haelewi chochote kinachoendelea. Kweli mapenzi yanaumiza sana ten asana. Je unavyodhani Jammy na Gervas wataweza kweli kumlea Levina tena akiwa katika hali ya kupooza..
Sehemu Ya 5
~ BAADA YA MIEZI 3 ~
Bado nilikuwa sijielewi elewi na kati ya vitu ninavyoweza kuanza kama kukumbuka ni sura ya kijana na mke wake napo nilikuwa siwatambui ni kina nani, pia walikuwa wakiishi na mtoto mdogo aliyeonesha kuwa anatambaa, alikuwa ni mtoto mzuri sana wa kike, kila muda alikuwa miguuni mwangu akinichezea chezea japo sikuwa na hata nguvu yeyote,na ilipofika kipindi cha kuogeshwa au kulishwa alikuwa akilia kwa sauti ya juu sana nakunifanya mchozi uendelee kunidondoka bila kuweza kuufuta.
Mateso kwangu yaliendelea kama kawaida, kunakipindi nilikuwa nalala na njaa bila ya kupata chochote huku nikiambulia kupigwa makofi, na hata sikuwa na kitanda zaidi ya kumalizia usingizi wangu pale pale kwenye kibaiskeli nilichokalia, ilifika kipindi hadi nakaa siku mbili mpaka tatu na kinyesi changu mwenyewe bila kubadilishiwa nguo au hata kusafishwa,kifupi nilikuwa tayari Levina mchafu tena yule mchafu haswa kuanzia juu mpaka chini, nilibabuka sana miguu na magonjwa ya ngozi yalinijaa karibu mwili mzima,nilikuwa mtu wa kung’ong’wa na ma inzi.
Ilifika kipindi nikawa nalazwa nje ya nyumba (uwani) bila kuwa na msimamizi yeyote na kila inapofika jioni ama usiku mateso kwangu huwa ndio kama yanaanza.
~ BAADA YA MWAKA NA NUSU~
Mateso niliyopata kipindi cha mwaka mzima karibia na nusu kilinifanya nipungue sana nikawa kama mtu aliyeathirika na gonjwa hatari tena kama la ukimwi, nguvu za kutembea bado sikuwanazo lakini uwezo wakuwatambua watu nilikuwa ninao, kuongea na kumsikia mtu kwa mbaali niliweza.
Na hata ilipokuwa ikifika jioni kila siku huwa nawaona watu wawili mwanamke na mwanaume wakiingia na gari mpaka ndani ya geti kisha wanashuka nakuingia ndani japo kuwatambua nikawa siwajui ni kina nani kwani ndio hao hao waliokuwa wakinitesa huku wakiongea maneno nisiyoyajua.
Yule mtoto alikuwa amekuwa na ikafika kipindi nikawa namshuhudia akinifuata nakukaa pembeni yangu japo hilo swala hawakupenda hata kidogo wazazi, upendo niliokuwa nimeanza kujijengea kwa yule mtoto ilinifanya nianze kuongea,
“Jammy Jammy…, Happy Happy…, Gervas..?”
Nilijikuta naachama mdomo wangu nakuanza kumwita yule mtoto majina mchanganyiko huku nikimwacha akinishangaa mpaka mfanyakazi wa ndani alipokuja kumtoa kinguvu pembeni yangu huku akiniacha kwa kunipiga makofi na mateke,
“…ukome,tena ukome kumfuata fuata huyo chizi…”
Hisia kali nilizokuwanazo zilinifanya niweze kumsikia kwa mbaali japokuwa sikuwa naelewa anamaanisha nini,
“kelly…? Haya baba yako Gervas huyoo amerudi twende nje tukampokee…!”
Bado waliniweka kwenye fumbo tena kubwa kwani sauti nazisikia wanavyoongea japo kwa mbali lakini maana na kumbukumbu sina kabisa hivyo nikabaki nikijiuliza tena kwa sauti ya kimyakimya,
“Kelly…?,Gervas ndio wakina nani tena…?
Nilibaki nikijiuliza bila ya kupata majibu yeyote na hata ya kuelewa kitu chochote.
“…Lakini, jina la Gervas kama nalikumbukaa…? Kwani hapa ni wapi…?”
Nilijikuta nikiendelea kujiuliza maswali mengi bila ya kujua na kwa muda huu nilijaribu kusimama mwenyewe bila ya mtu yeyote kuniona lakini tatizo likawa ni katika kutembea.
Nilianzisha kamtindo tena kipindi ambacho nyumba inakuwa haina mtu niko peke yangu nilikuwa mtu wa kujikokota na kibaiskeli changu huku nikijaribu kufungua vyumba vingine bila ya mafanikio yeyote, nilijaribu chumba kimojawapo mpaka nikahisi kama kuna kitu nimekidondosha then nikafanikiwa nakuingia chumbani, nilijikongoja mpaka kitandani ambapo chumba kilikuwa nikizuri kilicholembwa na picha kubwa ukutani zikionesha mwanamke na mwanaume siku ya ndoa yao,niliangalia bila ya kuwajua ni kinanani,nikaendelea kusachi mule chumbani huku na kule mpaka nikakutana na picha mchanganyiko,
“..My God..! Mamaaaa….”
Nilijikuta natoa sauti kubwa na ya ukali baada ya kuona picha mchanganyiko zikiwaonesha bibi na bwana siku ya harusi yao,
Kumbukumbu zikaanza kunirudia taratibu nakukumbuka,
“..Gervas..! Gervas.., Kelly…! Kelly…!”
Nikawa nayatamka hayo majina huku nikijitahidi kujua atakuwa ni nani kwenye ile picha.
“Namtaka mwanangu…, namtaka mwanangu…, mwanangu… mwanangu…!”
Nikawa kama kichaa si kichaa huku nikitoka nje na kile kibaiskeli cha wagonjwa tena kwa sauti ya juu sana mpaka nilipokutana na yule mdada wa humu ndani,
“…Unakwenda wapi nyang’au wee…? Nani kakwambia utoke nje…?”
Maskini Levina mimi niliambulia kupigwa vibao na mateke kutoka kwa yule Dada wa kazi. Niliumia sana lakini haikuwa na jinsi zaidi ya kuvumilia kupigwa huku machozi na hasira vikinipanda zaidi.
“..kwanini huyu dada ananitesa hivi kila siku, nimemfanyaje lakini…?”
Nilibaki nikiusemea moyo huku kwikwi ikinipanda.
~ BAADA YA MWAKA MMOJA ~
Fahamu yote ikawa imeshanirudia ikiwa ni pamoja nakuwatambua vizuri Gervas na mkewe Jammy, muda wote nilijifanya bubu japokuwa yule dada wa kazi aliwabishia sana wakina Gervas nakuwaambia kuwa mimi naongea, kwa upande wa mavazi bado sikuwa na nguo nzuri,uwezo wakutembea nilikuwa nao lakini sikutaka wajue zaidi yakujifanya bado nang’ang’ania kukalia kile kibaiskeli, yule mtoto niliweza kumtambua nakumjua kuwa ni wakwangu tena anaitwa kelly nasiyo lauryn, alinizoea sana lakini nikawa mtu wa kuangalia ni jinsi gani nitatoroka na yule mtoto wangu.
Kila siku yule mfanyakazi anapotoka tu unakuwa mwanya kwangu wakupekuwa kila kitu cha Gervas,
Sikufanikiwa kupata pesa zaidi ya kuambulia shilingi elfu ishirini tu pamoja na hati za nyumba,gari na pasport zao za kusafiria, nilitoka nje nakumchukuwa mwanangu kisha tukatoka naye nje kabisa nakukodi teksi nakutokomea kusikojulikana.
Maisha ya mimi na mwanangu hayakuwa mazuri ndani ya wiki moja toka nitoroke kwa Gervas, kwani sikuwa na eneo maalumu la kulala zaidi ya kujibanza vichochoroni huku Tandale na kila ilipofika muda wa asubuhi na mapema kazi kubwa ilikuwa ni kwenda na mwanangu mpaka magomeni usalama tena pale kwenye ‘ki prefti’ na kazi iliyokuwepo nikumvalisha mwanangu nguo chafuchafu nakumwacha akiomba omba kwenye magari yanapokuwa foleni pale, ilifika kipindi hadi tukawa tunapata shilingi elfu kumi na tano mpaka ishirini kwa siku,nakumbuka siku moja nikiwa nimeshamwandaa mwanangu tayari kwa kuingia barabarani mara nikamwona kama anaongea na mtu huku akinyooshea kidole eneo nililopo, nami sikusita kuwaangalia,
“My God..!, nimekwisha, nimekwisha Levina mimi, si Gervas yule…?”
Nilibaki nikitetemeka huku nikimwangalia akiwa ndani ya gari akiongea kitu na mwanangu huku akinitolea macho kwa hasira pale kwenye foleni ya magari,
Hatimaye magari yakaruhusiwa kwenda lakini cha kushangaza gari la Gervas halikwenda,likasababisha msongamano wa magari pale,lilisimama palepale kisha Gervas akashuka akamshika mtoto huku akinifuata na mimi eneo nililopo.
Niliingiwa na moyo wa kishujaa na sikutaka kumuonesha kuwa nina uoga wowote, pale pale nikainuka na kumfuata kwania ya kukutana naye na nilipomkaribia karibu,
“Gervas nipe mwanangu…?”
“Levina hivi unaakili wewe…? Kwanini umetoroka nyumbani..? Na kwanini unamtesa huyu mtoto asiyekuwa hata na lepe la shida…?”
“Embu nipe mtoto uko…?”
Nilimpokonya Gervas mtoto nakumuacha mdomo wazi huku akinishangaa kwani nilikuwa nimechenji nakuwa Levina tofauti tena yule wa kipindi kile.
Nilimchukuwa kinguvu nakutokomea naye kusikojulikana huku nikimwacha Gervas akitiwa hatiani na trafiki wa usalama.
“Levinaaa…! Levinaaa…?”
Niligeuka kwa jicho la dharau huku nikimwachia fyonyo kali,
“nani arudi…? Mpumbavu mkubwa weee..? Twende mwanangu achana naye..”
Kiukweli Gervas alikuwa ameniharibia siku kwani kwa siku hiyo sikupata chochote zaidi ya kurudi uswahilini kwetu Tandale kupumzika.
*********
Tangu Gervas aliponichefua sikuwa tena na hamu yakurudi kuendelea na biashara ya kuomba omba barabarani na mwanangu.
Nilijiepusha mbali kabisa na Gervas pamoja na Jammy,na kwa muda huu mwanangu alikuwa na umri kama miaka 4 hivyo alikuwa anatambua kipi kibaya na kipi kizuri, mradi niliokuwa nimeuanzisha ni kufungua genge dogo la kuuza angalau vijinyanya ili angalau niweze kujipatia riziki mimi na mwanangu Lauryn.
Nakumbuka siku moja nikiwa katika mizunguko yangu ya kwenda soko kubwa kwa ajili ya kujinunulia mahitaji ya jumla ya kuuza,nikakutana uso kwa uso na Jammy ambaye alionesha na yeye yupo katika hali si ya kawaida kwani alikuwa amechoka, bora yangu hata na mie,
“Levina…?”
Aliniita kinafki,nikamwangalia kwa jicho la dharau kisha,
“…unanitakia nini we mwanamke…? Umeshaniharibia maisha yangu inatosha…”
“hapana Levina, pliz nakuomba kwanza acha hasir….”
“niache nini..? embu achana na mie…”
Muonekano wake tu ulinifanya nijisikie kichefuchefu na hata hamu ya kuongea naye sikutaka kabisa.
“haya sema unasemaje…?”
Nikatulia nimsikilize anachotaka anachokisema.
“Levina, mie ndio chanzo cha yote Levina, naomba kwanza nisamehe…?”
“nikusamehe kwa lipi tena Jammy…?”
“Levina, Gervas ameniacha na yote hayo ni kwasababu yako Levina….”
“hivi wewe Jammy..?,unanifanya sina akili enh? Kwa taarifa yako tu, sidanganyiki…?”
“Levina nielewe, tangu tulipofunga ndoa na Gervas nyumba imekuwa haina amani kabisa.., amini Gervas bado anakupenda Levina…”
“ananipenda…? Na wewe je uliyefunga naye ndoa atakupeleka wapi…?”
“mimi hanitaki tena…!”
“kisa…?”
“Levina mie mgumba, na ndicho kitu kilicholeta matatizo mimi na Gervas mpaka unaniona hapa sokoni, naskia Gervas anakusaka kwa hali na mali ili mradi arudiane na wewe mlee mtoto wenu…”
“pole sana Jammy, nimekusamehe kwa yote yaliyokukuta”
Nilijikuta naingiwa na ile roho yangu ya huruma.
“kwahiyo Jammy unaishi wapi sasa hivi…?”
“sina eneo maalumu, kwani nilirudia ile biashara yangu ya zamani yakujiuza mwili na kwasasa naishi mabibo jeshini,ila ikifika jiona naenda kujiuza mwili pale manzese..na wewe unaishi wapi Levina…?”
“Tandale kwa mtogole,kama vipi twende ukapajue,naishi na mwanangu Lauryn tu…!”
“usijali Levina,siku nyingine nitakuja,ila leo nina buzi nalifukuzia pande za mikocheni nikitoka hapa…”
“sawa bwana,ngoja mie ninakunue vitu vya gengeni kwangu kisha nijiondokee…”
Tulimalizana na Jammy pale kwani alinikumbusha mbali sana haswa mema mengi aliyonifanyia kipindi anaishi na marehemu mama yangu japokuwa mabaya machache aliyenitenda.
Ile tunaachana naye tu mara,
“Levina…!, kwa ajili yako wacha nighairi huko ninapoenda,nipo pamoja nawe hadi kwako leo…!”
“twende Jammy nimefurahi sana, bado nakupenda sana rafiki yangu…”
Tuliondoka naye mpaka nyumbani kwangu.
*********
Tulipofika tu nilienda mpaka nyumba ya jirani nilipokuwa nimemuacha mwanangu Lauryn na baada ya hapo tukaelekea kwangu mpaka ndani.
“karibu Jammy jiskie upo nyumbani rafiki yangu wa zamani..”
“ahsante Levina, Levina ujue rafiki ni rafiki tu siku zote, na rafiki lazima awe na mema na mabaya na ndio maana hata anapokosea husamehewa na kuendelea na urafiki…”
Ni kweli kabisa Jammy…”
Niliingia mpaka chumbani kubadilisha nguo,kisha nikachukuwa kanga na kopo la kuogea tayari kwa kwenda chooni kuoga.
“Jammy wacha nikajimwagie maji kidogo si unajua tena kwetu uswahilini chooni ndipo bafuni…?”
Nilimwambia kiutani kisha nikaenda kuoga huku nikimwacha pale sebuleni na mwanangu,ndani ya muda mfupi nilimaliza kuoga na niliporudi ile naingia sebuleni sikuwakuta zaidi yakukutana na karatasi iliyoandikwa na kuachwa mezani.
“LEVINA…,
NAJUA NI VIGUMU KUAMINI LAKINI ITAKUBIDI UAMINI KWANI MTOTO ULIYEKUWA UNAISHI NAYE SI WAKWAKO BALI NI WAKWANGU NA MUME WANGU GERVAS,NA HAITWI LAURYN BALI ANAITWA KELLY.
MIMI SIYO MGUMBA NA HAITATOKEA,
YALE YOTE NILIYOKWAMBIA NIUONGO MTUPU ILI NIMPATE MWANANGU KELLY NA MTOTO WAKO LAURYN YUPO KWENYE KITUO CHA KULELEA YATIMA ‘TAIFA LETU ORPHANS CENTRE’ PALE KIGOGO,FANYA UKAMCHUKUE .
NI MIMI,
MKE WA GERVAS,
JAMMY A.K.A MAMA KELLY.
*********
Nilishtuka pale chini nilipokuwa nimelala,
“Lauryn…? Lauryn mwanangu…!”
Nilimwita mwanangu na kumfanya anishangae, kwani ni muda mrefu sijawahi kulala mchana nakumbuka nilipomaliza tu kupika chakula tukala na mwanangu kisha nikajilalia zangu,nilipokuja kushtuka kumbe yale yote yaliyonitokea na Jammy mpaka nikamleta huku nyumbani Tandale ninapoishi ilikuwa ni ndoto tena nindoto kama zile zilizokuwa zinanitokea hapo kipindi cha nyuma.
“mh Levina mie kwa kuota ndoto mbaya…?”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mwanangu kwa jicho na mdomo wa tabasamu kuonesha kuwa nampenda sana tu.
“Mama…?”
“unasemaje mwanangu…!”
“lini tutaenda kwa baba…?”
Tangu nimeishi na huyu mwanangu hajawahi kunitamkia neno kama hilo hivyo aliufanya mwili wangu usisimke sana nakunifanya nikitetemeka ni jinsi gani nitamjibu.
“Lau mwanangu…! Baba yako sasa hivi kasafiri, akirudi tu kutoka safari tutaenda sawa mwanangu…?”
“sawa mama…!”
“haya nenda kacheze na wenzako mie naenda gengeni eenh..!”
Alinielewa hivyo nikarudi gengeni kwangu ambapo huwa kuna mtu ananishkia ninapokuwa sipo.
~ BAADA YA MWAKA ~
Bado niliendelea kumdanganya mwanangu asiweze kukutana na Baba yake kwani niliamini kufanya hivyo kutaleta utata mkubwa baina yangu Jammy pamoja na Gervas mwenyewe.
Mtaji wangu ulizidi kukua siku hadi siku kwani ilifika kipindi mpaka nikajiandikisha kwenye vikoba vya kinamama (upatu) na nikawa natumia majina mengi ili nijipatie hela ya kutosha kukidhi mahitaji yangu,kiukweli ndani ya mwezi nilikuwa ninauwezo wakuingiza hadi laki 4 na nusu,ilifika muda nikahama pale nilipokuwa naishi nakupata nyumba kubwa yenye vumba vitatu na hata lile genge niliokuwanalo nikalibinafsisha nakufungua duka kubwa la bidhaa za nafaka tena la jumla na rejareja, kiukweli sijisifii ila nikweli kabisa nilikuwa na mkono wa biashara, mpaka nikafanikiwa kununua nyumba ya kuishi.
Mwanangu nilimwanzisha chekechea tena ile ya kiingereza tupu.
Habari kuhusiana na Gervas wala Jammy zilifutika kabisa akilini mwangu, jina nililotambulika zaidi maeneo haya niliokuwa naishi ni Salma au Mamaa Sammy.
Ndani ya miaka miwili na zaidi tayari nilikuwa namiliki mashine mbili za kusaga nafaka na kisima cha maji ambapo nilikuwa nikiuza maji kwa bei ya jumla na reja reja pale nyumbani kwangu hivyo nikajipatia fedha nyingi tu.
~ BAADA YA MIEZI 6 ~
Niliendelea na miradi yangu kwa muda mrefu mpaka nikafanikiwa kumiliki gari aina ya Toyota ‘Noah.
Nilijizoesha mazoea ya kwenda beach na mwanangu Lauryn ambapo nilikuwa nahakikisha mwanangu anaenjoy vyakutosha, siku moja tukiwa tunatoka maeneo ya beach mara nikashangaa macho yangu yanakutana na sura kama naifahamu, niliingia ndani ya gari nakuliwasha tayari kwa kuondoka lakini kabla sijaondoka pale yule mtu alinisimamisha kwa kutumia ishara ya mkono mmoja kwani kiukweli yule mtu alikuwa ni mlemavu wa miguu,
“Jesus…! Kumbe ni Gervas,hapa kafuata nini…? Nakwanini yupo vile..?”
Maskini yule ni Gervas, na hakunitambua vizuri kama anayemsimamisha ni Levina mimi kwani nilikuwa nimevalia miwani mikubwa meusi,nilichokifanya,
“mwanangu Lauryn…? Unamuona yule mtu…?”
“ndio mama…”
“yule ni baba yako na kila ninapomuona huwa namchukia sana tu, alitutelekeza Lauryn…”
Ilinibidi tu nimweke wazi mwanangu Lauryn kwani hili dukuduku ningekaa nalo muda mrefu hivyo nilichokifanya nikutoka spidi huku nikimlenga kwania ya kumgonga, nilitoka spidi ya ajabu huku nikimfuata,
nilipomfikia karibu ile nimeanza kumgonga tu sauti kali ikatoka ndani ya gari yangu,
“Mamaaa…! Mamaaaa…! Mamaaaa usimuue babaaa….!”
Ilikuwa ni sauti ya mwanangu Lauryn kwa sura yake yenye huzuni na machozi yaliokuwa yameanza kumtoka yalinisababishia kupiga breki ya ghafla kisha nikashuka kumwangalia kama kweli nitakuwa nimeshamgonga au la..!, maskini Gervas wa watu alikuwa akitapatapa pale chini huku magongo yake ya chuma yakiwa nyang’anyang’a, umati wa watu ulianza kutanda pale nilichokifanya,
“Lauryn mwanangu.., fungua huu mlango wa nyuma haraka…!”
Aliufungua kisha kilichofuata nikumbeba Gervas hivyo hivyo nakumpakiza ndani ya gari langu na breki ya kwanza nimpaka nyumbani kwangu mikocheni.
Ndani ya dakika kama arobaini nilikuwa tayari nipo nyumbani kwangu, bado hali ya Gervas ilizidi kuwa mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu mdomoni na puani mwake, nilichokifanya nikumpigia simu dokta wangu aje hapa nyumbani kwa ajili kumpatia huduma ya kwanza,niliogopa kama ningempeleka hospitali ya serikali ingekuwa kesi nyingne kwani mimi ndiye niliyemgonga hivyo wasingeweza kumtibia mpaka kibali toka polisi (PF3).
Baada ya kama nusu saa bado dokta niliyempigia simu alikuwa hajafika hapa kwangu, Gervas alikuwa kishapoteza fahamu na nilichokifanya,
“Aaah..! liwalo na liwe…!” nikambeba nakumpeleka kwenye gari nakumpakiza tena nakuelekea hospitali binafsi zozote ili apate kutibiwa.
~ DAVIES MODERN DISPENSARY ~
Ndio hospitali niliyofanikiwa kumpeleka kwa usiku huu kwani ilikuwa kama saa moja usiku na nilipomfikisha tu alipokelewa na manesi mbali mbali pale kisha akatundikwa dripu na mashine yakutolea hewa, muda wote mwanangu Lauryn alikuwa akitokwa na machozi lakini mimi nilikuwa kama nimepigwa ganzi kwani sikuogopa kitu sijui kwakuwa nilikuwa nikimchukia Gervas.
Madokta na manesi walihangaika kuhakikisha Gervas anapona, walimtibia majeraha yake yote niliyokuwa nimemgonga.ikiwa ni nakumpiga x- ray sehemu ya mgongoni.
Ilichukuwa kama masaa 4 pale hospitali na kwa muda huu ilikuwa imeshatimia saa 5 za usiku nikiwa bado nipo pembeni mwa kitanda cha Gervas pale hospitali mara nikamsikia Gervas akikohoa kisha akafumbua macho hapohapo yakagongana na macho yangu,nilianza kusisimka mwili wote nikamwinamia nakumpa busu shavuni mwake nakumuöngelesha,
“Gervas, bado nakupenda nanitazidi kukupenda daima…”
Nilijikuta naropoka hayo maneno kwa nguvu nakufanya mwanangu na manesi wanishangae pale,sikuridhika nikambusu tena kwa mara ya pili huku Gervas akiniangalia kwa jicho la tabasamu,
“Mama…? Unampenda kweli baba…?”
Ni sauti ya mwanangu aliyekuwa pembeni yangu na aliniona nikimbusu Gervas shavuni wakati nilishawahi kumtamkia kuwa namchukia Gervas sana.
“Lau…, huyu ni baba yako inanibidi na mimi nimpende ili tuishi naye si ndio mwanangu…?”
“ndio mama…”
Tukatoka nje na mwanangu huku nikimpisha dokta amtibie Gervas,ndani ya muda mfupi dokta alitoka nakuniita.
“Hali yake inaendelea vizuri hivyo ile dripu ni ya pili na ikiisha nafikiri itakuwa ni kesho asubuhi mtaondoka naye,ila mumeo kapata matatizo ya ndani kwa ndani haswa maeneo ya mgongoni, unaona hii x- ray inavyoonesha, hapa karibia na uti wa mgongo ndio palipoumia sana,lakini usijari kuna dawa za kuchua na za kumeza tutakupatia hiyo kesho asubuhi.
~ KESHO YAKE MCHANA ~
Kwa upande wa mwanangu Lau alikuwa kishapitiwa na usingizi lakini mimi nilijikaza mpaka nihakikishe Gervas anapewa ruhusa nakutoka naye pale.
Ile dripu iliisha nikalipia kila kitu ikiwa ni pamoja na madawa kisha nikamchukuwa Gervas na mwanangu nakwenda nao mpaka nyumbani.
“Dad..? Dad.., i love you..!, I love you dad…”
Njia nzima ilikuwa ni sauti ya mwanangu ikimwongelesha Gervas nakunifanya nisisimke njia nzima huku machozi ya furaha yakinitoka.
Haikuchukuwa muda mrefu sana tukawa tumeshafika,hivyo nikafungua kibaiskeli cha wagonjwa nilichokuwa nimepewa kwa muda kisha nikampakia Gervas nakumwendesha mpaka ndani na breki ya kwanza ilikuwa ni sebuleni nikamwacha na mwanangu Lauryn na zoezi lililofuatia nikwenda mpaka jikoni fasta nakumtengenezea uji ili japo apate nguvu sikuwa naishi namfanyakazi wa ndani zaidi ya mimi na mwanangu Lau, na nilikuwa natumia jiko la gesi hivyo haikuchukuwa muda nikawa nimeshamaliza kutengeneza uji wa ulezi hivyo nikawa naupoza kwenye bakuli huku naelekea sebuleni haraka haraka,nilipofika nilimkuta bado yupo na Lau wanapiga stori kabisa hivyo nikaanza kumnywesha uji Gervas,
“Lau mwanangu nikutume,embu nenda jikoni kaniletee tambaa la kufutia hapa chini uji umemwagika kidoogo inzi watajaa hapa”
Niliendelea kumnywesha huku mwanangu akijiendea jikoni nilipomtuma haikuchukuwa muda nikasikia kama kuna kitu kimelipuka huko jikoni halafu kimya kikatanda,
“Lau…? Lau…? wee Lauryn…?”
Kimyaa, sikusikia sauti yoyote nikamwacha Gervas pale nakukimbia hadi jikoni na nilipofika tu nilikutana moshi mzito sana kuashiria kuna kitu kimelipuka. Nilijihisi moyo kushtuka,akili kukosa nguvu na hata mwili wangu kunilegea. Nilikaa kama dakika moja nzima nikiwa katika hali ya bumbwazi. Hapo hapo nikugundua kuwa nilisahau kulizima vizuri lile jiko la gesi na ndio litakuwa limeleta matatizo,hivyo mwanangu Lau nikamkuta kadondoka chini huku anahema juu juu kuashiria kaivuta ile hewa nzito ya moshi sana,
“Gervas…? Gervas mwanetu anakufa huku nisaidie, Yesu wangu..!Yesu wangu…!, msaada jamani…?”
Mara nikashangaa Gervas anatembea tena kwa haraka haraka huku anakaribia eneo nilipo,
bado nilikuwa na marue rue,kizunguzungu si kizunguzungu kwani kila nikimwona Gervas namuona kama amesimama mara kama amekaa kwenye kibaiskeli cha wagonjwa,nafikiri sikumwona vizuri kutokana na huu moshi uliokuwa umetanda hapa jikoni,nilichokifanya
Nilimbeba mwanangu nakutoka naye mpaka nje huku nikimwacha Gervas akinifuata kwa nyuma na nilipofika nje nikagundua kuwa kumbe bado alikuwa kwenye kibaiskeli cha kubebea wagonjwa,
“Levina…? Levina…..”
Aliniita Gervas kuonesha anahitaji msaada ili aongozane na mwanangu mpaka hospitali japokuwa hajiwezi hata kutembea, lakini nilichokifanya nilimuingiza Lauryn kwanza kwenye gari kisha nikamfuata Gervas pale nje,
“Gervas hali ya mtoto ni mbaya kama unavyoiona, mie wacha nikimbie kwanza hospitali narudi baadaye nivumilie kwa hilo….”
Sikuwa na jinsi nilimwacha Gervas pale ndani na baada ya hapo nikamfuata mtu anayenisaidia kuuza maji pale nje kwangu,
“we Baraka,ndani kuna mgonjwa yupo kwenye kibaiskeli cha wagonjwa,hakikisha hatoki humu ndani mie wacha nimkimbize huyu Lau hospitalini….”
“vipi kwani kafanyaje….”
“nikirudi nitakwambia wacha niende kwanza huko…..”
Niliwasha gari langu nakutoka spidi breki ya kwanza ilikuwa ni hospitali ile ile niliyompeleka Gervas.
Alipokelewa nakuwekewa oxygen ili kidogo apate pumzi kidogo.
Ndani ya nusu saa mwanangu akawa mzima tu wa afya lakini tatizo kubwa alilegea sana hivyo hakuwa na nguvu zozote, alitibiwa pale kisha nikampakiza kwenye gari nakurudi naye mpaka nyumbani.
Gervas alikuwa anashauku kubwa ya kumuona mwanae na tulipoingia tu alimkimbilia nakumwangalia,
“levina umeambiwaje huko hospitali…?”
“nimepewa dawa hizi hapa na ule moshi aliokuwa ameuvuta ndio umemletea kupoteza kwakè fahamu…”
Kwa hiyo kazi yangu kubwa ikawa nikuwahudumia Gervas na mwanangu Lau kwa muda moja, niliishi nao vizuri sana kwani huduma zote za kwenda msalani nilikuwa nikimsaidia mimi mwenyewe na hata kumuogesha na kumvalisha nguo Gervas ilikuwa ni jukumu langu.
Ndani ya mwezi mwanangu Lau akawa amepona na anaendelea na shule kama kawaida, nilikaa na Gervas katika kipindi chote hicho kwanza bila kumgusia chochote kilichomfanya akawa vile lakini siku moja uzalendo ukanishinda ikabidi nimuulize,
“embu niambie ukweli Gervas imekuwaje mpaka ukawa na matatizo haya ya miguu…?”
Aliinama chini kama dakika moja halafu,
“Levina….?
“abe…”
“ni stori ndefu sana Levina ila kwakuwa tuko pamoja itabidi nikwambie….”
“we niambie tu…!”
“Jammy ndio aliyepoteza muelekeo wa maisha yangu yote mpaka sasa…”
“Eenh ilikuwaje tena…?”
“ujue tulipendana naye sana baada ya kufunga ndoa, alinijali kama mume wake namie nilimjali,ilifika kipindi nilikuwa huru zaidi kwake kwa yote lakini alichokuja kunifanyia sitasahau..”
“alikufanyaje kwani…?”
“yani ninavyokwambia Jammy anatembea na bosi wangu na wamefanya kila njia kuhakikisha sina pakwenda,nilirogwa Gervas mimi…, nilirogwa Levina…!”
Maskini ile stori aliyonisimulia Gervas ilinifanya nisisimke na mchozi kuanza kunidondoka.
“Eenhe ikawaje Gervas…?”
“walinichomea moto vyeti vyangu vyote vya kazi na waliniitia wahuni nakunipiga piga na magongo nakunisababishia kuwa mlemavu mpaka sasa,maisha yangu yakawa nikuomba omba mtaani nakulala kwenye vibanda au beach kama ulivyonikuta nazurura kule…”
Gervas akiwa bado anaendelea kunisimulia mara nikasikia hodi inapigwa nje,mwanzoni nilijua labda atakuwa ni mwanangu ametoka shule lakini hodi ilipigwa tofauti na ninavyosikiaga kila siku,
“nakuja kukufungulia…”
Nilipofika tu nje nilishangaa kukutana na kundi la maaskari kama watano wakiwa na silaha kila mmoja huku wakiongozwa na mdada aliyevalia miwani kubwa meusi,alipovua miwani,
“Jammy…? Jammy umefuata nini kwangu…?”
Kabla hajanijibu chochote.
“polisi, mtuhumiwa mwenyewe huyo hapo kwenye hicho kibaiskeli cha wagonjwa mchukuweni twende…”
Maskini walimchukuwa Gervas,alikuwa mbishi wakampiga vibao nakumburuza huku wakitoka naye nje kwenye gari lao walipolipaki,
“Gervas…, Gervas…, Jammy nimekukosea nini jamani…? Gervas kakukosea nini…?”
“embu nyamaza huko…?”
Aliongea jammy kwa ukali huku akiondoka kwa mwendo wa makogo nakuniacha nikipiga makelele kwa kulia huku kwikwi ikinibana.
::: Unavyodhani kwanini Jammy ana hasira na Gervas..?? Kwanini anamfanyia yote hayo??
::: Inamaana Levina atawaacha waishi pamoja?? Nini hatma ya Levina katika simulizi hii kali na ya kusisimua, kusikitisha na hata kukutoa machozi??
Sehemu Ya 6
Niliendelea kulia huku nikitoka nje kwa kutoamini kwamba kweli Gervas ametoka mikononi mwangu kweliau la…!
Umati mkubwa wa watu waliokuwa wanachota maji hapa nje kwangu na wengine majirani walijaa kushuhudia ni kitu gani kimetokea hapa,niliendelea kulia tena kwa sauti ya juu huku wakimpakiza Gervas kwenye gari lao nakuondoka naye, niliendelea kuumia zaidi pale Gervas aliponyanyua mikono yake nakuniaga kwa kupitia dirisha la lile gari huku Jammy akiwa pembeni yake akioneshwa kufurahishwa na alichokitenda.
“…mi ndio Levina a.k.a mamaa Sammy, nitahakikisha Gervas anarudi kwenye himaya yangu…”
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikirudishia geti nakurudi ndani,
“mama…! Mama….”
Ilikuwa ni sauti ya mwanangu akirudi toka shuleni na kwa muda huu alishuhudia umati wa watu ukisambaratika kutokea hapa nyumbani kwangu,
“….eti mama kuna ninì hapa leo mbona watu wamejaa hivi…?”
“…wala hamna kitu mwanangu twende ndani…”
“Baba yangu anaendeleaje…?”
Nilijikuta nasisimka huku nikipatwa kigugumizi cha ghafla nishindwe nitamjibu vipi,
“twende yupo ndani”
Niliongozana naye mpaka ndani na tulipofika tu ilinibidi nimwambie ukweli japokuwa alilia sana nakutaka nimpeleke alipokuwa baba yake.
¤¤¤¤¤¤¤¤¤
Siku hiyohiyo muda wa usiku kama saa moja moja nilimchukuwa mwanangu japo alikuwa akilia sana nikawasha gari langu na safari yakuelekea kwa Jammy kumtafuta Gervas ikaanza japo nyumbani kwao nilikuwa napakumbuka kidogo toka kipindi kile nimetoroka na mwanangu akiwa mdogo, nilijitahidi kukumbuka mtaa mpaka nikafikia ile nyumba nakusimamisha gari kisha nikamwambia mwanangu anisubiri ndani ya gari nakuelekea getini moja kwa moja,
“…samahani mlinzi hapa ndio kwa Gervas…?”
“Gervas..? Gervas yupi tena…?”
“kuna kaka mmoja anaitwa Gervas anaishi na mke wake anaitwa Jammy, nimewakuta…?”
“…aanhaa unamzungumzia bosi Jamila…?”
“huyo huyo..!”
“sasa yule ameshahama hapa muda mrefu na hii nyumba alishaiuza muda kidogo…”
“kwahiyo sasa hivi anaishi wapi…?”
Yule mlinzi akainuka nakuanza kunielekeza,
“unaona njia hii…? Nyooka nayo moja kwa moja mpaka inapokata kona then hesabu nyumba mbili kutokea hiyo kona kuna nyumba kubwa inafensi yapinki ndio hapohapo..”
“ahsante,nimekupata wacha niende…”
Niliingia kwenye gari nakwenda mpaka nilipoelekezwa tulipofika nje tu nilisikia makelele ya kama mtu anapigwa tena akitoa sauti kubwa tu na yakiume moja kwa moja halmashauri yangu yakichwa ikanituma kuwa atakuwa ni mume wangu Gervas bado wanamuonea na kumtesa huko ndani,
“maskini Gervas mh…?”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mwanangu ambaye tayari alikuwa amelala.
Nilipaki gari nje kidogo na ile nyumba huku nikijishauri jinsi ya kuingia na nikiangalia saa yangu ilikuwa inaniambia saa 4 kasoro,mara nikashuhudia geti linafunguliwa kisha gari jeusi likatoka,niliangalia vizuri jibu nikalipata kuwa ni Jammy,hivyo nikaliwasha gari langu nikaanza kulifukuzia kwa nyuma taaratibu mpaka linapoelekea, ilikuwa ni njia ya kuelekea bagamoyo ambapo Jammy alikuwa akielekea,
“…leo ama zake ama zangu nitahakikisha namtoa duniani mshenzi mkubwa sana..”
Kiukweli nilijivika sura ya Levina yule wazamani huku nikiingiwa na hasira kali juu ya upumbavu alionifanyia Jammy.
~ BAADA YA MWENDO WA KAMA NUSU SAA ~
Sasa ilikuwa ni kama nyumba hazionekani kwani nakumbuka ilikuwa nimaeneo ya mbele (Bunju) ambapo Jammy alikunja kona yakuingia ndani ndani hivyo nilisimamisha gari langu nakujipachika kwenye magari yaliolazwa kisha nikazima taa zote,nikashuka nakuwafatilia taratibu huku nikimwacha mwanangu Lau akiendelea kulala ndani ya gari,mara akasimamisha gari lake kisha wakatoka wanaume kama watano hivi huku wakibebea kiroba kikubwa nakukitupa kisha wakaingia ndani ya gari nakugeuza,
Nilijificha bila wao kujua na waliponipita tu ukawa ndio mwanya wangu wakwenda pale kuangalia walichokuwa wamekitupa,
“maskini Gervas…”
Kumbe alikuwa ni Gervas amefungwa katika kile kiroba alikuwa nyang’anyang’a miguuni kwa kupigwa huku mdomoni mwake kukiwa na plasta iliyosababisha asipige kelele nikamfungua akatapika pale pale nakukohoa,nikiwa bado namshangaa Gervas pale mara mwanga mkali wa gari ukawashwa mbele yangu nakunimulika huku höni zikipigwa kwa nguvu zikiashiria kuna watu wameniona na wako ndani ya gari inayonimulika taa.
Sikuonesha kushtuka kwa hali yoyote,kwa moyo wakijasiri nikamwinu Gervas pale chini nikaanza kumburuta kuelekea upande ule uliokuwa unanimulika nilipofika karibu,
“uuhff uhfff..!”
Ilinibidi nipumue kwanza kwa nilichoshuhudia na kutokuamini kwani kiukweli lilikuwa ni gari langu mwenyewe na ndani yake mwanangu Lau alikuwa amehamka toka usingizini hivyo aliwasha taa sambamba na kupiga honi japokuwa hajui kuendesha lakini aliniogopesha sana,
“mama…? Huyö ni Baba…?”
“ndio mwanangu embu fungua mlango nimweke…”
Gervas alikuwa hajiwezi hata kuongea mwili wake ulikuwa na damu damu kuanzia kichwani hadi kwenye nguo zake zilizochanika chanika, nilimbeba nakumpakiza kisha safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.
Ndani ya kama dakika 40 nilikuwa tayari nimeshaingia nyumbanì huku mlinzi akitufungulia mpaka ndani,tulisaidiana na kumbeba Gervas mpaka ndani na kwa bahati nzuri kile kibaiskeli chake cha wagonjwa kilikuwepo ndani hivyo ikawa rahisi kumuingiza mpaka ndani.
Hasira kubwa juu ya Jammy bado zilinishika lakini nilijipa moyo kwanza apone mume wangu Gervas then atanijua mimi ni nani?
***********
Hatimaye Gervas alianza kupata unafuu kidogo kidogo kwani ni mwezi 1 tu ulikuwa umepita toka walivyomuumiza wakina Jammy, nilijitahidi kumuhudumia nakuhakikisha anaendelea kupata matibabu vizuri kupitia kwa dokta wetu anayetutibia hapa nyumbani,vitisho vya kutaka kuniua bado viliendelea kupitia simu yangu tena kutoka kwa Jammy na sijui namba yangu aliipata wapi.
Nilikuwa na mazoea kila inapofika mida ya jioni namchukuwa mwanangu pamoja na Gervas huku tukizunguka naye kwa kutumia kibaiskeli chake, nakumbuka siku moja nilipokuwa natoka nje ya geti huku namsukuma Gervas kwa bahati mbaya alidondoka nakutapatapa huku vidonda vyake vilivyoanza kupona vikawa uinatoa damu nikabaki nikipiga sana makelele kuomba msaada huku nikisisimka nakutetemeka mwili mzima huku nikishindwa nianzie wapi kumnyanyua pale chini,sikupata msaada wowote hivyo nikawa namweka Gervas peke yangu kwenye kibaiskeli chake mara nilishangaa geti kusukumwa kwa nguvu huku nikimshuhudia Jammy akiwa na watu waliovalia nguo ndefu,
Aliingia kwa dharau huku akinitolea macho,
“Levina…, Levina…?”
“hivi Jammy unanitakia nini mimi…?”
“Mchungají huyu ndio binti niliokwambia amenichukulia mume wangu tena wa ndoa”
Jammy alikuja na mtu aliyedai kuwa nimchungaji na eti alikuja kutoa mashitaka kwangu hivyo nikabaki nawasikiliza,
“binti Gervas ni mumeo wa ndoa..?”
Aliniuliza mchungaji,
“hapana mchungaji ila ni mchum…”
Kabla sijamalizia kujibu nilishangaa napigwa bonge la kibao kutoka kwa Jammy, sikumwonesha hasira yeyote ya kutaka kupigana naye na nilichokifanya,
“Jammy si umesema huyu ni mumeo wa ndoa,haya mchukueni sasa mimi simuhitaji”
“No no Levina nooooo?siwezi kwenda kuishi tena na Jammy ataniua ataniua huko anapotaka kunipeleka,jaman nionee huruma levina,
“Gervas mimi siyo mkeo wa ndoa nenda na Jammy ambaye ni halali kwako”
Nilimwacha Gervas akichukuliwa tena na Jammy huku akipakizwa ndani ya gari na kwa muda huu sikuonesha kulia sana kwani hali ile nilishaizoea hivyo nikawa kama mtu aliyepigwa ganzi.
Jammy alipomaliza kumpakiza Gervas katika gari akanifuata,
“Levina? Haya kamuage mara ya mwisho kwenye gari na kwa taarifa tu tunaenda kumuua”
“unasemaje Jammy,unasemaje?”
Alinichanganya kiakili hivyo nikakimbia hadi kwenye gari aliokuwamo Gervas pale nje,
“Gervas.., Gervas shuka, shuka watakuua hao..”
Ndani ya sekunde chache nilikuwamo mlangoni mwa ile gari lakini chakushangaza nilivutwa kwa nguvu na mchungaji mule ndani ya gari na baada ya hapo Jammy akaingia nakilichofuatiwa niku lockiwa milango na madirisha yote na baada ya hapo yule mciungaji alivua nguo zake za uchungaji huku akitoa kisu na kamba ndefu sana nakuanza kunifunga funga,
Nilipiga makelele lakini haikusaidia chochote mule ndani kwani vioo vyote vilifungwa,
Kumbe hakuwa mchungaji yule bali nikama muuaji,
“hakikisha tunamdhalilisha humuhumu ndani ya gari huyo Gervas wake anayemng’ang’ania amshuhudie”
Aliongea Jammy huku akiliwasha gari. Yule mtu alivua nguo zake sambamba na zakwangu
Huku akitaka kunibaka.
Nilianza kupiga makelele nakutapatapa huku yule mchungaji akianza kunishika shika matiti yangu kisha akaanza kutelezesha mikono yake mapajani mwangu,sikuwa na hisia zaidi ya hasira kali,kwa muda huo Gervas hakuwa na jinsi ya kunisaidia zaidi kunitolea macho,kamba alizonifunga yule mchungaji zilinibana haswa haswa mpaka nikajikuta sina tena jinsi ya kujinasua zaidi ya kumwachia yule mchungaji afanye anavyotaka kwenye mwili wangu.
Alinibaka na kuniumiza haswa na baada ya kuridhika alichukuwa vidole vyake nakunidumbukizia katika sehemu zangu za siri tena kwa nguvu,nilichoka namwili wote kunilegea huku Gervas akishindwa hata kutoa sauti,
“Adrian…? Adrian…?”
Aliita Jammy aliyekuwa anaendesha gari hapo hapo halmashauri ya kichwa ikanituma kuwa atakuwa ni yule mchungaji ndio anaitwa Adrian,
“Naam mkuu…”
Aliitika kwa sauti huku akiniachilia nakuvaa nguo zake,
“Tumeshafika nyumbani sasa hakikisha hatoki mtu humu ndani ngoja niende nikakuongezee majeshi sawa Adrian…?”
Aliamrisha Jammy huku akimsisitiza Adrian, alishuka ndani ya gari nakutuacha mimi na Gervas pamoja na huyo Adriani.
Ndani ya dakika kama kumi Jammy alikuwa akifungua mlango wa gari kwa kutumia ufunguo wake kisha nikamshuhudia akiwa na wanaume kama wawili huku mikononi mwake akiwa kashkilia bastola moja pamoja na burungutu la pesa sambamba na karatasi kubwa ilioambatana na picha kubwa mbili huku akiwapa maelezo wale watu wake,
“hii ni ramani ya mpaka hapo zambia mjini,na hizi picha ni zakwao hii ni ya bosi wa hapo mpakani mkifika na hii ni ya mke wake anaitwa Happy hakikisha mnawakabidhi hawa watu na hii bastola ni ya kujiami chukueni hii simu na bastola kwa usalama zaidi”
“sawa bosi tumekuelewa,tunakuhakikishia tutatekeleza kama ulivyotuambia…”
Wale wanaume waliingia ndani ya gari wakaliwasha na safari ya kuondoka pale ikaanza huku tukimwacha Jammy pale nyumbani kwake,
Gervas alikuwa keshalala muda nafikiri nikutokana na maumivu aliyoyapata.
Ndani ya masaa kama manne tulikuwa tumeshavuka morogoro huku tukikaribia kufika Mikumi,akili yangu ilikuwa kama imeshachanganyjiwa kwani nilikuwa kama siamini amini kama kweli narudishwa kule ambapo sikufikiria hata kidogo kama nitaonana na hawa watu yani bosi na Happy,pili nilichanganyikiwa sana kwani muda wote nilikuwa uchi huku Gervas akiwa kaniegemea mapajani mwangu kapoteza fahamu kabisa.
Baridi kali lililofanya nianze kutetemeka mwili mzima huku meno yangu yakiumana yalimaanisha kuwa tupo katika mji huu wa Iringa,mara nikasikia simu inaita mwazoni nikajua labda huenda ni simu ya wale wanaume lakini haikuwa hivyo kwani mlio wasimu ulizidi kuwa juu na ulikuwa ukitokea kwenye nguo zangu zilizokuwapo pale chini,
Mara mwanaume mmojawapo akatoka nakuichukuwa simu yangu kisha akabonyeza batani ya kupokelea akaniwekea masikioni niongee nayo.
“Mum uko wapi mama…? Baba na yeye yuko wapi…?”
Ilikuwa ni sauti ya mwanangu Lauryn akiniuliza nilipo,mwili wote ulinisisimka nakufanya mchozi uanze kunidondoka sambamba namkojo uliojipenyeya kupitia mapajani mwangu huku nikitaka kumjibu,
“Baba yako huyu hap….”
Kabla sijamjibu nilishangaa napigwa kofi huku simu ikikatwa nayule mwanaume.
Sikuwa nakumbukumbu yeyote,nilijitahidi sana kufikiria, mtoto wangu ndio alikuwa pembeni yangu huku Gervas akitetemeka meno nakunifanya niendelee kusisimka bila ya kuelewa chochote, nilitaka kuinuka haraka haraka pale kitandani,
“…no no Levina usifanye hivyo ona utajitonesha…”
Ilijuwa ni kauli ya Gervas akinisihi nisiinuke kwani kiukweli sikuwa najitambua vizuri,hapo hapo hisia zikanijia kuwa pale ni hospitalini, lakini nimefikaje fikaje hapa, kwa hapo sikuweza kujua chochote,
“mwanangu Lau, mbona unalia jamani kwani vipi…?”
“hapana mumy, ona ulivyo…! ona mumy umekuwa kama dady…”
Aliendelea kuongea mwanangu kwa uchungu na kunisababishia nijiangalie vizuri,
“oh my God…! nini tena, nini tena…! why me…! why me Levina…?”
Maskini Levina mimi nilikuwa nimekatwa mguu mmoja na sikujua chanzo ni nini,
“Gervas, Gervas embu niambie ilikuwaje mume wangu niko hivi…? Ilikuwaje Gervas…?”
“Levina kaa utulie kwanza ni stori ndefu..”
“Hapana Gervas niambie tu…”
“unakumbuka mara ya mwisho ulipokuwa unanitoa nje kwenye kibaiskeli…?”
“sikumbuki Levina kwani ilikuwaje…”
“siku ile ilikuwa kama bahati mbaya nikaanguka nakuumia sana,ulipiga makelele kwa ajili ya msaada lakini geti lilifunguliwa..”
“enh ikawaje…?”
“….wakaingia watu watatu waliovalia mavazi meusi marefu kama wachungaji”
“…nimeshakumbuka na Jammy si alikuwepo…?”
“hapana…, walikuwepo wenyewe wakakushika kwa nguvu nakuanza kukupiga kwa kutumia magongo yao pamoja na panga huku wakitaka kukuua…”
“Mungu wangu ikawaje…?”
“makelele yako yalifanya umati wa watu ukusanyike pale nyumbani na hata hivyo walikuwa wameshakuumiza sana mpaka ukapoteza fahamu na damu kukutiririka sana,tukakumbiza hapa hospitali na umezinduka hapa siku ya pili leo”
Nilianza kupiga makelele pale hospitali huku nikimwangalia mwanangu Lau kwa huruma nakugundua kumbe vile vyote vilivyonitokea vingine ilikuwa ni ndoto kama vile eti mchungaji amenibaka mara eti wananipeleka Zambia kwa bosi na Happy,
“kwanini Levina mimi nina mikosi hivi jamani…? Aaah?”
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikijilaumu kwani kiukweli nilikuwa nimekatwa mguu mmoja na sikuweza tena kutembea…
********
Nilikaa muda mrefu kidogo hospitalini. Nilikuja kuruhusiwa baada ya mwezi lakini kila siku ilikuwa inatakiwa niwe naripoti hospitalini mpaka nilipoanza kupata unafuu kidogo lakini nikawa si mtu wakuendesha gari tena ilinibidi nimtafute dereva wakutuendesha na kumlipa na nilipatiwa kibaiskeli cha wagonjwa hivyo nikawa sawa na Gervas wote walemavu, mwanangu Lau hakuwa mtu wa furaha kwani alipungua sana na kufanya afya yake kuzorota.
Nakumbuka siku moja tuliporudi kutoka hospitali na Gervas tulioga na baada ya hapo ilikuwa muda wa kulala lakini kabla ya kulala,
“Levina mke wangu…”
“niambie Gervas…”
“kunakitu kinaniumiza sana moyo…”
“kitu gani hicho Gervas…?”
“Vipimo vya madokta baada ya wewe kufanyiwa opereshen…”
“vimefanyaje tena…”
“Levina mi sitakuja kukuacha kamwe wewe ni wangu milele yote…”
“Gervas…? We niambie kitu gani lakini…”
“Levina..,Dokta aliniambia nifanye siri mpaka utapopata unafuu lakini nimeshindwa kujizuia Levina,siwezi Levina na siamini mpaka sasa…”
Mchozi ulianza kunitoka huku ukiteleza mashavuni mwangu na makamasi ya majimaji. Hasira kali ikinishika nakunisababishia maumivu kwa mbaali yalioanza kunitoka kupitia mapajani,nikahisi kama ganzi si ganzi,mishipa mikubwa iliyokuwa imeanza kunitoka kuanzia shingoni na mpaka machoni ilinifanya nifanye maamuzi ya ajabu kwani niliona kama Gervas ananichelewesha kuniambia hivyo nilijikuta nachukuwa mikono yangu miwili nakumbana nayo Gervas shingoni mwake kimahaba,
“Gervas niambie Gervas niambie pliz…”
“Levina niache nikwambie ukweli…”
Nilimwachia,
“haya niambie Gervas”
“Levina, UMEATHIRIKA….!”
“niiiiiini Gervas….?”
“vipimo vinaonesha hivyo na yote hiyo ilisababishwa na lile panga ulilokatwa nalo na wale watu mwezi uliopita. Inasadikiwa kuwa lilikuwa lina damu damu za mtu aliyeathirika kwa ukimwi.”
Nilinyong’onyea mwili wote na nisijue nifanye kitu gani na nilishangaa mtoto wangu akiwa mlangoni kwangu na kumbe muda wote alikuwa akutusikiliza,
“maskini mwanangu kashajua nimeathirika mimi…”
nilijisemea kimoyomoyo huku nikimwangalia mwanangu Lau kwajicho la huruma,
Kwangu ilikuwa ni wiki ya ajabu maishani mwangu kwani kuanzia hapo Gervas alikuwa kabadilika sana na kunakipindi alikuwa hataki kula hata chakula,nilijisikia vibaya sana haswa pale alipokuwa akishtuka ndotoni na kuniambia nimeathirika mara hawezi kuishi na mimi.
Nilipungua sana Levina mimi na sio kimawazo tu bali kwa ugonjwa niliokuwa nao kuna kipindi nilikuwa nakata tamaa ya kuishi kabisa kwani hata marafiki niliokuwa nao walininyanyapaa na ilifika kipindi nikawa nabadilisha wafanyakazi wa ndani na hiyo yote ni pale wanaponigundua nimeathirika walikuwa wakinitoroka.
Nakumbuka siku moja nikiwa sebuleni na mwanangu Lau huku Gervas akiwa chumbani kwake mwanangu aliniuliza,
“Mumy…! mumy….”
“unasemaje mwanangu…?”
“eti mumy na mi nimeathrika…?”
Nilinyamaza kama dakika moja bila kumjibu kisha nikavuta pumzi nakumjibu,
“hapana mwanangu,ni mimi peke yangu tu…”
“hapana mumy unanidanganya, mbona shuleni wananitenga wananiambia eti nimeambukizwa ukimwi na mama yangu…”
“hapana mwanangu waongo hao we mzima kabisa”
Nilijitahidi kumwelewesha mwanangu lakini alinielewa japo kishingo upande huku akiondoka,nikiwa bado nipo na mwanangu pale sebuleni nilishangaa Gervas akitoka na mabegi yake ya nguo,
“Levina…, Levina nashukuru kwa yote mema uliyonifanyia haina budi kukuacha sasa uendelee kuishi na mwanao…”
“hapana Gervas unakwenda wapi…?”
“levina siwezi kuishi tena na wewe siwezi, bora nikaishi popote pale duniani lakini siyo hapa”
“Gervas nilitegemea kuwa wewe ndio mtu wakaribu aliokuwa akinipa ushauri na vit..”
Kabla sijamalizia kuongea nilishuhudia Gervas akijikongoja na kibaiskeli chake huku kakumbatia mabegi yake yanguo nakutoka mpaka nje huku akiniacha nikipigwa na butwaa!
“mumy…,mwache aende mi nipo kwa ajili yako”
Maneno ya mwanangu Lau yalinifanya nisisimke mwili mzima huku mchozi ukiendelea kunitoka nisielewe chakufanya, hapo hapo mwanangu akatoka mpaka getini kumfungulia,
“bye dady…! bye…”
Mwanangu alizidi kuniliza sana na maneno yake kwani alikuwa na hasira kama za mama yake.
Ikawa haina jinsi zaidi ya kumwacha Gervas akijiondokea na kutuacha mi na mwanangu japo niliumia sana moyoni.
Ni mwezi sasa umekatika bila ya kuiona hata sura ya Gervas wala hata kuisikia sauti, mwanangu Lau alipungua sana si kwa ajili ya kumwaza baba yake tu bali ni ugonjwa uliokuwa umemtokea wa kifafa kwani alikuwa akidondoka mara kwa mara nakutoa mapovu,nilimpeleka kwenye maombi makanisa mbalimbali ili aombewe lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya.
Nakumbuka siku moja tulipokuwa tunatoka hospitali kumpeleka mwanangu ghafla nikamwona Gervas na kwa kipindi hiki hakuwa na kile kibaiskeli na magoti yake yalionesha kupauka sana ikiashiria kuwa anatambaa kwa kutumia miguu,kwa kipindi hiki alikuwa omba omba wa mtaani,dereva alisimamisha gari lakini Gervas baada ya kutuona alikimbia hivyo hatukutaka kumwita zaidi ya kumsikitikia nakuendelea na safari yetu,nilikuwa si Levina yule unayemjua kwani nilibadilika sana na muda wangu wote nilikuwa nikiutumia katika kusoma biblia na vitabu vya stori na sana sana nilikuwa napenda kusoma novel ya ‘ULINIACHA MARIA’ iliyotungwa na Andrew Carlos, niliipenda sana haswa nilipenda kujifunza mambo mbalimbali ya maisha yanayotuzunguka. Kiukweli ilikuwa ikinigusa sana maisha yangu ya kila siku.
~ BAADA YA MIEZI MIWILI ~
Kwa kípindi hiki mwanangu aliisha kabisa na sikutaka hata aendelee na shule zaidi kubaki na mimi hapa nyumbani,vipimo nilifanya kwa mara nyingine tena na ni kweli vilionesha kwa madokta kuwa nimeathirika na kwa muda wote huu nilikuwa natumia madawa ya kuongeza kuishi.
Siku moja nikiwa ndani nimetulia sebuleni kulikuwa kimya sana hivyo nilimwita sana mwanangu lakini kimya kilizidi kutanda nakufanya nianze kuingia na wasiwasi,niliingia vyumba vyote lakini niliambulia patupu!
Niliporudi sebuleni niliona kama miujiza kwani nilikutana na kikaratasi,
LEVINA,
SIKU NYINGI NILIMTAFUTA MTOTO WAKO LAKINI NILISHINDWA NA SASA NAFURAHI NIMESHAFANIKIWA,
KACHUKUE MAITI YA MWANAKO CHOONI,
Mi Jammy..”
Sikutaka kuamini amini kwani nilihisi kama mchezo nachezewa kwani ile karatasi kiukweli ilikuwa na damu damu sa swali kubwa kwa kipindi kifupi ile karatasi imefikaje fikaje pale sebuleni?
Nilitoka fasta na kuelekea huko chooni na nilipofika,
“Mamaaa.., My God..! Uuuhf….! Uuuuhf….!”
Kiukweli ilikuwa maiti ya mwanangu ipo imelalia sinki la chooni,nilitetemeka sana huku nguvu zikiniisha nilimgeuza huku na kule ili kuhakikisha kama kweli kafa au la, lakini kiukweli alikuwa ameshakufa,nililia sana pale chini huku nikimburuza lakini ile nageuka nyuma tu nakutana uso kwa uso,
“Jammy…? Kwanini umenifanyia hivi kwanini Jammy..? Mwanangu kakukosea nini Jaman…?”
Hakusikia lolote zaidi ya kunifuata panga lake huku akitaka kuniua.
Jammy hakutaka kuendelea kunisikia na matokeo yake ile ananikaribia tu akateleza mpaka chini kwani kulikuwa na marumaru sambamba na majimaji ya chooni yalimfanya Jammy kuteleza na kuliacha panga likimdondoka chini,pale pale bila kupoteza muda nililiwahi lile panga na kumkata mkono wake wa kulia kisha nikamalizia mkono mwingine,
“Levina nisamehe…! Levina utaniua..?”
“…ni bora nikuue roho yangu itaridhika, umeniharibia sana maisha yangu Jammy…”
Nilimkata kata mpaka akapoteza fahamu kwani damu nyingi zilimtoka nilipomaliza nilipiga makelele kwanguvu nikiomba msaada,yule kijana wangu anayeniuzia maji nje ndio alikuwa mtu wa kwanza kuja huku akienda kuwaita majirani kwa ajili ya msaada zaidi.
Waliuchukuwa mwili wa marehemu mwanangu Lau kisha wakamuwaisha Jammy hospitali kwa haraka ikaitishwa msiba huku nikipewa pole na majirani, siri kubwa nilikuwa nayo moyoni kuwa ninani aliyemuua mwanangu na kumjeruhi Jammy.
***********
Hatimaye siku ya mazishi ilifika,nilimlilia sana kwa mwanangu Lau na niliamini kuwa ndiye mtoto pekee niliyekuwa naye kwani sikuwa na uwezo tena wakupata mtoto licha ya kwamba nimeathirika, mchungaji aliitwa pale nyumbani kwa ajili ya kuuombea mwili wa marehemu mwanangu huku umati wa watu ukifurika,
“…umefuata nini hapa, toka sitaki kukuona Gervas sitaki tokaa…”
Wakinamama wengi waliniwahi nakunishìka huku wakiniomba nipunguze hasira kwani Gervas alikuwa amekuja kuhudhuria mazishi.
“Simtaki jamani aondoke,kwani ye ndiye chanzo cha yote..”
Nilichoropoka nakumvamia kisha kilichofuata nikumtupia Gervas vibao nakumng’ata eneo la mapajani mwake,
“Levina..? Levina unamatatizo gani mke wangu…?”
“…nani mkeo, mkeo Jammy si…”
Kabla sijamalizia kusema umati wote ukawa kimya ghafla nakunifanya nijishtukie nitulie zangu.
Misa ilianza na baada ya pale tulienda moja kwa moja hadi makaburini, hasira kali nilikuwa nayo haswa nikimwona Gervas ndipo ilinijaa,muda wa kutupia mchanga kwenye kaburi la mwanangu ulifika na nilishindwa kujizuia nakujikuta nimedondokea kaburini,walinitoa kama mara mbili,nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kwani kiukweli nilimpenda sana mwanangu Lau.
Hatimaye mwanangu walimzika kisha watu wote tukatawanyika na baadhi yakinamama walikuwa pamoja kunifariji japokuwa wengi wao waliondoka kimyakimya bila kujua chanzo cha ule msiba,Gervas sikumuona tena na ndivyo nilikuwa nikitaka.
Kesho yake mapolisi walikuja kuchukuwa maelezo kitu gani kilichopelekea kifo cha mwanangu. Uchunguzi ambao waliuchukuwa siku ya tukio haukuwa umekamilika vizuru. Wakaongezea maneno mengine kutoka kwangu. Ilinibidi niwaambie tu ukweli halisi kuwa Jammy ndiye kamuua mwanangu Lau, Nikawaelezea yote kuhusu maisha jinsi nilivyomjua Jammy na hata kunisaliti kwake.
~ BAADA YA WIKI ~
Ile hali yangu ya huruma ilianza kunijia baada yakusahau yale machungu yote ya nyuma niliamua kufuatilia hospitali nakujua hali ya Jammy,
Maskini alikuwa chini ya ulinzi mkali huku bado akipatiwa matibabu,kila aliyemuona alikuwa akimuogopa nakumtenga kiukweli alionekanika kama chizi chizi.
Nilifikiria sana maisha yangu ya nyuma jinsi alivyonisaidia wakati anaishi na mama yangu,sikutaka kulipiza ubaya wowote juu ya kunisaliti na kuolewa na Gervas wala juu ya kumuua mwanangu Lau,hivyo nilichokifanya niliwahonga polisi hela nyingi kisha mapolisi wakaifuta kesi kwa kuwa mhusika mkuu wa mtoto aliyekufa ni mimi. Niliifuta kesi kwa maandishi yangu mwenyewe polisi. Nilimchukuwa Jammy nakwenda kuishi naye nyumbani kwangu.
*********
Nilizoeana na Jammy tukawa zaidi ya marafiki kwani ule urafiki wetu wa kipindi kilee ukawa umesharudi japokuwa wote tulikuwa walemavu,kwa upande wa kwangu nilikuwa mlemavu wa miguu na Jammy alikuwa mlemavu wa mikono yote,
“Jammy nikuulize kitu..?”
“embu niambie ulipokuwa unaishi ulimwacha nan…?”
Kabla sijamalizia kumuuliza mara mlango ukagongwa ikiashiria kuna mtu anabisha hodi,
“karibu,naja kukufungulia…”
Haraka haraka nikatoka kwenda kufungua lakini mtu niliydkutana naye kumbe ni Gervas…
“umefuata nini hapa Gervas..?”
“…namtaka Jammy nimeambiwa anakaa hapa na yeye ndiye chanzo cha kifo cha mwanangu sasa leo ama zake ama zangu…”
“hivi we Gervas,kwanza ni nani aliyekudanganya kuwa Jammy anaishi hapa…?”
“Levina…? Usinione kama chizi,nina akili zangu…”
Gervas alinisukuma na kuingia ndani kinguvu moja kwa moja mpaka sebuleni huku akiita kwa nguvu,
“Jammy…?, Jammy nimesema toka mwenyewe nikuone la sivyo unajitafutia mengine….!”
Kimya kilizidi kutanda huku nikimwacha Gervas akitambaa na miguu yake huku akizunguka huku na kule akiita,na kwa muda huu Jammy alikuwa kajificha hata mi mwenyewe sikujua yupo upande upi.
“Gervas usiniue pliz…! pliz…!”
Jammy ilibidi ajitokeze na hakuweza kujisalimisha kwa kuinua mikono kwani mikono yake yote ilikatwa,
Gervas alipomuona tu Jammy na hali ile ghafla akabadilika,
“Jammy…! Jammy…”
“abee…!”
“ni we wee au naota…? Umefanyaje tena mikono…?”
Gervas alianza kutokwa na machozi hivyo kumfanya asahau alichokifuata,alinifanya na mi nisisimke sana nakuanza kuwonea huruma wote,
“Gervas…! Ni stori ndefu,ila naamini ni shetani alinitawala kwa muda mrefu nakunifanya niwachukie wewe na Levina,
Gervas kwanza nisamehe kwa yote niliyokutendea hapo nyuma ikiwa ni pamoja na mauaji niliyowahi kufanya”
“endelea…?”
“umeshanisamehe Gervas…?”
“nimesema endelea…”
“unakumbuka kipindi kile nilivyokutimua nyumbani kwangu..?”
“mmm… hhh…”
“basi kipindi kile mganga wa kienyeji ndiye aliyenishawishi zaidi nakupelekea nikufanyie vitu vya ajabu,na lengo langu kubwa lilikuwa nikuue kabisa ikashindikana ukanikimbia hivyo bado niliendelea na tabia ya ajabu ikanibidi nimuue hadi mfanyakazi wa ndani”
“nani Nosim…?
“hapana ni Mary, nilipomuua nikarudia tena kukutafuta wewe mpaka nikupate,nilitumia watu na pesa za kutosha mpaka nikafanikiwa kukuteka hapa hapa kwa Levina hadi tukakufunga kwenye kiroba..”
“Jammy, embu ishia tu hapo hapo, Gervas”
Ilinibidi nikatishe ile stori kwani Gervas alizidi kulia,
“unasemaje Levina…?”
Mi naona cha msingi hapa nikusameheana na pili kuangalia tunaishi vipi, napenda kama wote tukaishi kwa amani bila kuwa na malumbano yeyote”
Nilishangaa kwa mara nyingine tena Gervas akimfuata Jammy nakumkumbatia kisha bada ya pale Gervas alinifuata na mi nakunikumbatia,
“Levina…? Nakupenda na Jammy nawapenda sana”
“hata sisi Gervas tunakupenda…!”
::: Ni kweli upendo umerudi kwa wote watatu, Gervas, Jammy na Levina?? Itakuwaje hapo.. Nini hatma ya Levina na Gervas.
Sehemu Ya 7
Maisha yaliendelea kupendeza zaidi kwani kwa sasa tulikuwa tukiishi kama wanandugu tena wale wa damu na siyo wachumba tena,niliishi mi Gervas na Jammy huku mfanyakazi wa ndani alitusaidia kwa kupika chakula,hata inapofka muda wa kulala huwa kila mmoja anachumba chake,
Nakumbuka siku moja ambayo ilikuwa ni sikukuu tulitengeneza chakula kizuri nakuwaalika marafiki,hivyo tulisherekea vizuri kwa kunywa nakucheza muziki na hata ilipofika muda wakulala kila mmoja alilala kwake,kwa upande wangu nilikuwa nimelewa sana kiasi chakuamua niwahi kulala,lakini mkojo ndio tatizo kubwa nilikuwa nalo hivyo kila baada ya muda nilikuwa ni mtu wa kwenda chooni kukojoa na kwa kipindi hiki nikasahau njia ya kuingia chumbani kwangu nakujikuta nikiingia chumba cha Gervas bila kujua,na nilipoingia nilijisogeza mpaka kwenye kitanda chake kwakuwa taa ilikuwa imezimwa Gervas hakuweza kunigundua kiurahisi kwanza alikuwa kapitiwa na usingizi, hapo hapo
Nilianza kumpapasa kuanzia shingoni mwake huku nikishuka mpaka kifuani mwake hakika nilivimisi vitu vingi kwa Gervas,nilijihisi kama pombe yote imeniisha kwani niliendelea kumshika shika Gervas bila ya yeye kushtuka,mpaka nikafanikiwa kumvua nguo,hivyo nikaanza kumchezea viungo vyake vingine vya mwili akashtuka,
“nani…? Toka hapa toka…?”
Gervas alikuwa ameshtuka nakuanza kupiga kelele hapo hapo nikamyamazisha,
“ssshhh…! nyamaza Gervas usiku sasa hivi…”
Alinielewa nakulegea huku akionesha kukubaliana na mimi kwa kitendo nilichokuwa nakifanya kwake,
Nilivua nguo zake zote kisha nikazivua na za kwangu nakuendelea na yetu. Nilifurahia sana siku hiyo. Nilikumbuka maisha ya nyuma kati yangu na Gervas, Nilikumbuka mapenzi yake ya nyuma. Hakika ilikuwa ni siku iliyojirudia katika maisha yangu.
****************
Asubuhi na mapema mfanyakazi wa ndani alikujaa mpaka chumbani kwangu kuniamsha.
“Dada.., chai tayari,nenda ukanywe sebuleni,wenzako wakina Gervas wanakusubiri…”
Nilishusha pumzi nakutoka kitandani. Nikachukuwa mswaki wangu nakuingia bafuni baada ya hapo nikachukua gongo langu la kutembelea nakuacha kibaiskeli changu huku nikiongoza moja kwa moja mpaka sebuleni, aibu kubwa ilinishika pale nilipowakuta Jammy akiwa na Gervas wanakunywa chai,
“Levina…,yani bado ulikuwa umelala tu mpaka sa hivi…?”
“…ujue jana nililewa sana hata nilivyopatapata usingizi sikujitambua kwani jana sherehe iliishaje…”
“tuliwasindikiza wageni wote mpaka nje,kisha tukanywa sana kila mtu akaenda kumalizia kunywa chumbani kwake….”
Nilitoka pale nakwenda kuoga,kisha baada ya hapo nikajiandaa vizuri huku nikijisogeza sebuleni kunywa chai,
tulikunywa chai lakini kila nikimwangalia Gervas aibu kubwa inanishika nabaki naguna huku nakuangalia chini.
~ BAADA YA MIEZI 4 ~
Mazoea ya kuishi kama ndugu yalituteka sana,hakuna hata siku moja tuliogombana wala kufanyiana kitu chochote cha ajabu,
Siku moja nikiwa njiani ndani ya gari nikielekea mabibo nilikuwa mimi,Gervas,na Jammy pamoja na dereva, siku hiyo kulikuwa na foleni sana ikatubidi kutumia njia ya mkato ya kupitia Ubungo ili tuweze kutokea Mabibo mara gari yetu kwa bahati mbaya ikakutana uso ka uso na lori aina ya fuso kitendo hicho kilifanya upande mmoja wa dereva uharibike vibaya,
“Gervas…,Gervas…? Jammy…, Jammy…?”
Maskini dereva alikuwa ameshapoteza maisha huku Jammy akiwa hajielewi wala kujitambua ikanibidi niombe msaada fasta nakuwakimbiza hospitali na Tax lakini kabla hatujafika hospitali,
“Jammy…! Jammy…, Jammy amka Jammy…?”
Nililia kwa uchungu sana huku nikiwa siamini kama nimempoteza Jammy kwani kiukweli alikuwa hata hapumui,na tulipofika tu hospitali walimpeleka moja kwa moja mpaka monchwari yeye na dereva na kisha Gervas wakampeleka chumba cha wagonjwa mahtuti ‘ICU’ kwani na yeye alikuwa hajitambui kabisa,
Nililia sana huku nikiomba mungu japo Gervas apone kuliko kuwapoteza wote,nilisisimka sana,nakutetemeka nikijiuma uma huku nisielewewe chakufanya nakutamani hata ingekuwa ni ndoto tu,
“Dada unaitwa nani…?”
Aliniuliza nesi mmoja aliyekuja huku akionesha kuwa kuna habari amezileta,
“naitwa Levina.., vipi hali ya mgonjwa wangu huko…?”
“mbona unaharaka hivyo…?”
“yeah…,ndio mimi,vipi anaendeleaje…?”
“Tumejitahidi kwa kila uwezo na tunasikitika kukwambia kuwa Gervas ameumia sana upande wa kwenye mbavu zake ila chakusikitisha ni kwamba tumemkata mkono mmoja hivyo…”
“ooh my god…! Gervas wangu au..?”
“Ndio huyo huyo pole sana dada yangu…”
Nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa nikaongoza moja kwa moja mpaka chumba alichokuwepo Gervas na nilipoingia tu nilikutana na jopo la madokta huku Gervas akiwa kawekewa
Dripu na mirija ya kupumulia,nilijihisi nina mikosi tena mikubwa mno maishani mwangu Levina mimi.
Niliganda pale hospitali huku nikisubiri japo Gervas aweze kutoa hata macho nami nipate kuondoka kwani nilikuwa bado sijiamini amini kama kweli Gervas yupo hai tena.
“…dokta lakini si atapona tu…?”
“yeah..,usijali mgonjwa wako atapata nafuu tu..”
Madokta walinipa moyo sana hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyumbani nakujua taratibu ya mazishi ya dereva na Jammy itakuwaje.
Ndani ya kama siku mbili tulikuwa tumeshamzika Jammy na dereva taksi. Watu hawakuwa wengi sana,nilipewa pole na majirani waliokuwa wakinifahamu huku wengi wao wakinipa rambi rambi zao.
Maskini Gervas hakuwepo kabisa kwenye msiba kwani alikuwa hospitali akiugua,siku hiyo hiyo baada tu ya msiba sikutaka kabisaa kupoteza muda ikanibidi kwenda kumuangalia nakujua taratibu zinakwendaje huko hospitali,
Nilikodisha teksi mpaka hospitali ya ‘Hindu Mandali’ pale posta ambapo ndipo alipokuwa amelazwa Gervas na nilipofika tu niliongoza moja kwa moja mpaka kwenye wodi niliyoelekezwa nakumkuta,lakini kwa sasa hali yake kidogo ilikuwa tofauti na siyo kama mwanzo nilivyomuacha kwani hata ile mirija yakupumulia ilikuwa haipo tena hivyo alikuwa akibadilishiwa dripu tu,
“Gervas…?”
“ndio Levina umekuja? Kuniona…?”
“ndio nipo hapa kwa ajili yako nakukujulia hali pia…”
“na Jammy ndio hataki kuja kuniona kabisa…?”
Nilisisimka ghafla nakuanza kutetemeka huku meno yakiumana na vidole kushikamana kwani kiukweli Gervas hakuwa anajua lolote kuhusiana na kitu kilichotokea na kwa yeye kumbukumbu zilikuwa bado hazijamrudia vizuri juu ya tukio lililomtokea.
Ikanibidi nimdanganye japo aridhike.
“Jammy yupo na amekumis sana…”
“mbona hujaja naye sasa…?”
“nilimwacha akikuandalia mtori hivyo baada ya kama lisaa atakuwepo hapa kukuletea…”
“nitashukuru sana,kumbe kweli bado mnanipenda..?”
“ndio tunakupenda nakukujali sana Gervas…”
Nilimdanganya nakumlazimisha japo ale chakula nilichomletea cha viazi vya kusagwa pamoja na juisi, akanywa na kisha baada ya hapo nikamwacha apumzike huku nikimsisitizia kuwa Jammy atamletea chakula kingine.
~ BAADA YA SIKU TANO ~
Gervas aliendelea kuweka chuki zaidi kwa Jammy ambapo alijua bado yupo nyumbani na hataki kuja kumjulia hali, ilikuwa ni kazi ngumu kwangu kumwambia kama kweli Jammy kafariki kwenye ile ajali kwani ningemletea Gervas matatizo makubwa sana ikizingatia bado Gervas anaumwa nakumbukumbu hazijamrudia vizuri.
Nakumbuka niliongea vizuri nadokta aliyekuwa anamtibia Gervas na akaniahidi kesho yake asubuhi nije kumchuka Gervas nakufanya malipo yote aliyokaa pamoja na gharama za operesheni ya mkono aliokatwa.
Hivyo ilipofika kesho yake nilikuwa nahamu kweli nirudi kuishi na Gervas nyumbani kwangu hivyo nikafanya kujiandaa fasta nakuongoza mpaka hospitali na nilipofika nilifika mpaka pale kwenye kitanda alichokuwa kalazwa Gervas napo sikumkuta,kijasho chembamba kikaanza kunitiririka huku nikijipa moyo huenda wamempeleka kujisaidia hivyo nikakaa kwenye kitanda chake nikimsubiri,nilikaa kama dakika kumi sikuona chochote zaidi yakushuhudia mgonjwa mwingine akiletwa nakulazwa kwenye kitanda akichokuwa kalazwa Gervas huku nikinyanyuka pale nakuwapisha,
Hapo hapo akili yangu ikanituma niongoze mpaka ofisi ya dokta kumwangalia napo nilipofika sikumkuta Gervas.
“Dokta…? Gervas yuko wapi…? Gervas wangu yuko wapi..?”
Nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na sikutaka kumwelewa kabisa dokta.
“ameshakuja kuchukuliwa…”
“na nani sasa…? Na nani…?”
Nilijikuta nikilivuta koti ka dokta kwa nguvu zote huku nikiwa na machungu yakutokujua Gervas amepelekwa wapi,
“…calm down mama..!,calm down…!”
Nilimwachia koti lake nakumtaka aniambie ukweli Gervas yuko wapi.
“walikuja wanaume wawili na Mmama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jamila au Jammy nakumpa pole sana mgonjwa nakumuomba msamaha kwa kutofika tangu alipokuwa kalazwa, huyo Gervas alionesha kuwafahamu hao watu kwani alikuwa akicheka nao na pia yeye mwenyewe Gervas ndiye aliyeamua kuwa wamlipie gharama za pale kisha wakaondoka naye…”
“…n o o o o o o o o o Dokta Jammy alishafariki…!,wamekudanganya hao…!”
Nilitoka haraka haraka uku nikitembea kwa gongo langu moja kuelekea kwenye taksi nakuongoza kwanza mpaka nyumbani kwangu huenda wamempeleka nyumbani kwangu na nilipofika mpaka ndani sikumkuta mtu yeyote hivyo nikatoka tena mpaka getini na nilipofika getini tu,
“mamaaaa uwiiih….!”
“Gervas…? Gervas…?”
Gervas alikuwa kabadilika rangi ya mwili wake kabisa mithili ya mtu aliyenyeshwa sumu,alikuwa kalala pale nje ya geti,
Ile nataka tu kumshka ili nimnyanyue,
“hapo hapo…! usiinuke,uko chini ya ulinzi kuanzia sasa…”
Sikuweza kugeuka nyuma ili nimjue ni nani aliyeniweka chini ya ulinzi na nilitazama mbele ambapo macho yangu yalikutana moja kwa moja na gari lenye namba ‘PT 3005’
hapo hapo akili yangu ikanituma ni gari ya polisi hivyo nikainua mikono juu kuashiria nimesalimu amri japokuwa sikujua kosa langu haswa.
Watu waliokuwa wamevalia mavazi ya kipolisi takribani sita huku wakiwa wameshika silaha za moto mikononi mwao walinisogelea karibu wakitaka kunikamata.
“ Levinaaaaaa… Levina usikubali wakukamatee haoooooo…!!!”
Ilikuwa ni sauti ya Gervas akinisihi huku sauti yake ikionesha kukwaruza kwaruza. Nilibaki nikitoa macho yangu kuwatizama ambapo askari mmojawapo alimgeukia Gervas na kukoki bunduki yake kisha kuanza kummiminia risasi Gervas. Niliumia moyo sana kumshuhudia Gervas wangu akiteketezwa kwa risasi mpaka kufa. Damu nyingi zilimtoka maeneo ya usoni na kifuani. Wale watu hawakuwa na huruma hata kidogo ndio kwanza wakaendelea na safari ya kunifuata eneo nilipo.
Nilitumia macho yangu kuangaza huku na kule nakuona upenyo.Nikajibiringisha kurudi nyuma ya geti nakubamiza geti. Kilichofuata niulianza kusikia milio ya risasi mfululizo ikipigwa eneo la geti, Mungu ndiye pekee aliyeniokoa kwani risasi nyingi. Nilikuwa nikizishuhudia zikipenya masikioni mwangu. Haraka haraka huku nikihema kwa juu juu nikajikongoja na magongo yangu ya kutembelea, Nikazunguka nyumba kwani niliamini nikiingia ndani watafungua geti na wakinipata wataniteketeza. Ndani ya muda mchache nilikuwa tayari nimezunguka ndani ya nyumba na tayari akili ilinituma kuupanda uzio nakutokea upande wan je. Sikuweza! Sikuweza kwakuwa nilikuwa sina uwezo kwani miguu yangu haikuwepo. Nilikuwa ni mlemavu. Nikakimbilia mpaka katika banda la mbwa . Haraka haraka nikawafu ngulia mbwa kisha nikaingia katika banda la mbwa. Nikajificha!
Kilichoendelea nilisikia milio ya risasi uku mwa wakionesha kufoka,niliamini wale majambazi wanamalizia hasira kwa mbwa wangu. Nikabaki nikijikikunyata mwenyewe kwa woga. Nikiwa bado nimezubaa peke yangu bandani. Mara,
“ Huyu hapa mpumbavu, huyu uku bandani tumepata!”
Maskini jambazi mmoja wapo alikuwa yupo mbele ya macho yangu, mbele ya banda langu la mbwa nilipojificha. Akarusha bunduki yake pembeni kisha akaanza kulifungua banda kwa lengo la kunitoa..
::: Inamaana Levina amekamatika?? Je atasalimika hapo?? Na ni kina nani hao waliofanya mauaji ya Gervas??
:::: Mwisho wa INATOSHA. Season 2 inakuja
MWISHO

