BIKRA YA HOUSEGIRL ILIVYONITOA JASHO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 09
Tulipoishia
“Mi Doto, ingia WhatsApp kuna kitu nimekutumia” alisema Doto
“Ok” Ray alijibu na kuingia WhatsApp moja kwa moja, alipongia hivi aliona ametumiwa ujumbe na Doto, akaingia kwenye msururu, alichokiona kutoka kwa Doto wala hakuamini
Endelea
Huwezi amini yule msichana mdogo alikuwa amemtumia picha zake akiwa nusu uchi, nyingine alivalia ch…upi tu halafu hata hakuogopa na wembamba wake, jamaa akamtazama akatabasamu halafu akamjibu
“Acha upumbavu wewe mimi sio wa kutamanisha na hizo picha zako, natamanishwa na picha za watoto wazuri jiheshimu na mimi nitakuheshimu ok? Acha kunifananisha” alijibu kama vile ni mtu mwenye nidhamu sana.
Yaani kule binti alipokuwa, alijisikia vibaya mno maana alifikiri ni zamu yake yeye kupewa utamu lakini jamaa alikaza, na mtoto wa kike alikata tamaa kabisa kutokana na ile hali.
Ray aliamua kumblock mtoto huyo halafu akampigia Elinami “Hallo Elinami” alimuita baada ya binti kupokea simu
“Nambie kababa” alijibu
“Mh umenikera” alisema mtaalam
“Kwanini jamani?” aliuliza
“hujui? Eeh kwanini unawapa watoto wadogo namba zangu?”
“Watoto?” aliuliza binti kwa mshangao “Watoto gani?”
“We hapo si umempa namba yangu yule msichana uliyekuwa umefuatana naye, hakajielewi kananitumia picha za uchi mimi eenh?” alifoka kwa hasira huku akimtazama mzee wake aliyekuwa anakuja kutokea kule nyumbani
“Jamani jamani jamani….mi sijampa namba….kumbe ameniomba simu ili aniibie namba yako? Ok embu subiri” alisema binti
“ok” alisema Ray na kukata simu halafu akaiangalia kwa hasira na kuinuka kwenye jiwe alipokuwa ameketi.
Mzee wake alifikia pale ndipo Raymond alipompisha na kwenda kule nyumbani maana kuchunga ilikuwa sio jukumu lake. Aliketi kwenye sofa, na kuanza kuwasiliana na rafiki yake mmoja akimuuliza habari za Dar.
Mama yake Ray alitoka nje na kusimama, halafu alimuona mume wake akiwa anapambana na mbuzi jirani kidogo, ikabidi amfuate mumewe ni mumewe hata kama umri umeenda hivyo alitembea ili wakataniane kidogo.
Akiwa amemuacha Ray pale sebuleni, Nasma aliingia chumbani kwake akavua nguo zake zote, halafu akajifunga khanga tayari kwa ajili ya kwenda kuoga, alipomaliza, alichukua kisimu chake cha batani mezani na kutoka nacho akaangalia kushoto kulia, akili ikamwambia apite sebuleni akamtamanishe kijana Ray na khanga yake moja.
Alienda taratibu huku akiogopa, akafika pale sebuleni kisha akaweka simu kwenye meza iliyokuwa karibu na soketi na kumuita Ray
“Kaka Ray” alimuita kwa mapozi huku akiwa hamtazami yeye anatazama ukutani huko na kumuachia makalio nyuma ili jamaa ayaone
Ray aliinua uso, maana muda wote alikuwa anatazama simu yake, alipotazama hivi, alikutana na mtoto akiwa amefunga kakanga kake japo alikuwa mdogo lakini alikuwa ni mtoto mzuri mwenye mvuto, cheupee kutoka singida halafu alikuwa na umbo lakini alikuwa hajatanuka vizuri labda kutokana na shida
“Naaam” alisema Ray huku akimkodolea macho, binti akajigeuza kwa mapozi na kutabasamu kidogo
“Samahani, naomba unisaidie chaja yako nichaji simu yangu” alisema binti kwa hisia “Mi chaja yangu mbovu”
“Anhaa, kumbe una simu”
“Ndio ninayo”
Ray aliinuka na kunyoosha mpaka chumbani kwake kisha akachukua chaja na kutoka nayo akamkabidhi mtoto wa kike “Hii hapa” alisema na kumkabidhi, yule binti akapokea huku akibonyea kidogo kwa nidhamu
Nasma aliiweka kwenye chaji “Betri lenyewe bovu yaani hata simalizi kuoga kabla halijajaa” alisema binti
“oh unaenda kuoga?” alimuuliza
“Ndio” alisema binti yule na kwenda moja kwa moja kupita kordoni.
Hili suala kidogo lilimtatiza Ray, kwa sababu binti alikuwa amekuja kumtamanisha, wakati wazazi wake wakiwa hawapo, alihisi tu lakini alitabasamu huku akimdharau maana alikuwa anajua fika hawezi toka na katoto kama kale tena kadogo kachafu kachafu, hahaaa ilikuwa ni shida kabisa.
Aliona majanga lakini alikumbuka ana mwanamke ambaye anampenda sana, akachukua simu akitaka ampigie simu yake ikaingia ujumbe kutoka kwa Elinami “Nimeshamalizana naye shenzi yule” alisema Elinami kwenye meseji
Ray hakuijibu ile message badala yake aliishika simu akawa anafikiria kwamba alitaka aandike nini akasahau “Duuh hivi nilitaka nifanye nini na hii simu lakini?” aliwaza huku akiwa ameishika simu anashangaa shangaa, mara akakumbuka “Ahaaa, nilitaka nimpigie Rose jamani maana amenisusa sana huyu mwanamke” aliongea peke yake huku akitafuta namba ya Rose akaipiga
Simu ya Rose iliita hadi mwisho bila kupokelewa, akapiga tena na tena na tena, wala hakujua kwamba Rose amepatwa na nini, ndipo akaamua kumuandikia message “We endelea kunichunia, kuna wenzako wanahangaika kunisumbua halafu nikishawatongoza unaanza kusema wanaume wote ni mbwa” alituma kwa hasira na kuweka simu pembeni akajilaza kabisa usingizini pale pale kwenye sofa
Baada ya Nasma kuoga vizuri, alienda chumbani kwake, akavua khanga yake na kujingalia mwilini, kisha akatabasamu kidogo, ndipo alipoona avae nguo yake ile ya pili aliyokuwa akivaa muda ambao sio wa kazi, alipomaliza kuvaa, alijipaka mafuta usoni na kujifuta nywele alizokuwa amesuka mistari mikubwa mitatu halafu halafu alipomaliza alijitazama kwenye kakioo kake kadogo kalikopasuka pasuka akajivisha hereni
Gauni alilokuwa amevaa lilikuwa gauni la piki, gauni fulani hivi lililomshika, lilikuwa gauni la aina fulani hivi linavutika kama big G, ya kata mikono, akajiangalia huku kichwa chake kikimuambia kwamba atoke mpaka sebuleni akachukue ile simu yake.
Alifika sebuleni, akakuta bado Ray amesinzia pale kwenye sofa, akamtazama lakini jamaa hakumuona, binti aliimba wimbo lakini Ray bado hata hakushtuka usingizini. Ndipo Nasma alipochukua simu yake, hata ilikuwa haijajaa, akachomoa na chaja kwenye soketi halafu akasogea mpaka pale alipokuwa amejilaza Ray
Nia yake ilikuwa ni Ray amuone ndo aridhike kwamba ameonekana na mtu aliyemuambia akaoge.
“Kaka Ray” aliita lakini Ray alijigeuza tu kwa utamu wa usingizi “we kaka…..kaka” alimuita kwa nguvu
“Mmmmh” jamani aliitika bila kupanua mdomo halafu akamtazama binti, binti alitabasamu
“Jamani umesinzia hapa?” aliuliza
“Daaah, kweli usingizi mtamu, vipi mbona umeniamsha?” alimuuliza
“Ninashukuru kwa chaja yako jamani?” alisema na kumkabidhi
“Imeshajaa?” jamaa aliuliza huku ufahamu wa usingizi ukienda ukimuisha kidogo
“Ndio tayari”
“Ok” alipokea simu na kushuka kwenye sofa, “Ngoja nikalale ndani” alisema jamaa na kuinuka, akaanza kutembea
Binti alimuwahi chapu na kukaa mbele yake, akawa anatembea kulekea nje huku akijitikisa kidogo, hakika jamaa aliona umbo la yule mtoto maana aliumbika japo alikuwa bado hajakaa vizuri, ila alionekana kuwa na umbo…..nguo aliyokuwa amevaa yenyewe ilimshika na ilikuwa inavutika na kumchora vilivyo
“Samahani Naa” Ray alisema na Naa aligeuka na kumtazama akijua tayari lengo lake limetimia
“Wewe una miaka mingapi?” alimuuliza
“Kumi na nane kasoro siku chache tu” alimuambia
“Umezaliwa tarehe ngapi mwezi wa ngapi?” aliuliza huku mkono akishikilia kitasa chake anataka aingie ndani
“Tarehe 29, mwezi wa 3” alisema binti
“Ok, poa” Alisema jamaa na kufikiria halafu akashtuka “Tarehe 29? Mwezi wa 3? Aliuliza mshikaji kwa mshangao
“Ndio kaka” alisema binti “Mbona umeshtuka?” alimuuliza
“Hamna, ila umependeza ulivyooga na kuvaa vizuri” alisema Ray
Binti alitabasmu kwa furaha na kuinama kwa aibu “Jamani asante kaka?” alisema
Ray aliingia ndani akaendela kulala na binti akaenda jikoni kumalizia mapishi……………..
SEHEMU YA 10
Baadaye mida ya saa saba mchana, Raymond alishtulia na kelele za TV, zikichanganyika na za wazee wake walizokuwa wanapiga sebuleni. Huku kelele za vyombo zikisikika, kwani mambo ya msosi yalikuwa yanawekwa vizuri jikoni, halafu aliinuka kitandani na kuketi, akaishika simu yake kwa makini na kuitazama,
Ray alishtuliwa sana na message kibao zilizokuwa ametumiwa na watu wengi sana, akazifungua “Hallow, pole sana Ray, Oh vipi mzee ndo maana umekimbia au? Oi mbona kimenuka? Mh aisee hawa wanawake ni hatari”
Hizo zilikuwa baadhi ya jumbe alizokuwa ametumiwa na marafiki zake, na wafanyakazi wenzake, hapo aliogopa na kumpigia mmoja wao simu
“Vipi mzee Karimu? Alimsalimia
“Bomba nipange boss” alisema kijana huyo
“Dah mishe zinaenda?” aliuliza kikuda ili apate ukweli kuambiwa ni kipi kilichokuwa kimetokea
“Yap boss, naona umekimbia mji” alisema kijana huyo
“Hamna kawaida, halafu mzee mi sielewi nakutana na message za watu kibao ambazo, zinanishangaza kidogo, mi sielewi kuna nini mbona watu wananipa pole wakati sijafiwa mimi?” aliuliza kwa mshangao
“Ina maana hujui kilichotokea?” aliuliza karimu
“Nisingekuuliza bobu, embu nipe yaliyojiri”
“Hahaaa….mzee unazingua….rose mnawasiliana?” alimuuliza
“Namcheki nashangaa hapokei simu yangu tangu nilipoongea naye jana halafu amenifokea balaa”
“Ok sawa, ngoja dakika moja, ingia WhatsApp” alisema karimu na kukata simu
“Mh” Ray alibaki ameduwaa hakuelewa tatizo linaanzia wapi kwani yeye alikuwa haelewi kilichokuwa kinamaanishwa. Aliingia WhatsApp, na karimu muda huo huo alimtumia link ikafuatiwa na ujumbe “Fungua hiyo babu” alimwambia, ikabidi jamaa afungue.
Aliifungua ikaanza kufunguka.
Ilikuwa ni video ya mtandaoni, alipoifungua tu hivi, ilipiga kelele “Assh oooh baby….baby” alishtuka na kukata chapu ili isisikike sauti nje wajue anaangalia video ya ngono, aliinuka kidogo na kuvuta mkono akataka achukue earphones lakini alipotazama akaona bora apunguze sauti maana alikuwa kiukweli anatetemeka na wasiwasi alikuwa ameshapata
Alipunguza sauti na kuanza kuitazama ile, video, hakuamini macho yake, kwani alimuona live mpenzi wake, Rose akidinywa na boss wake, tena juu ya meza. Ray alichanganyikiwa
“Whaaat? Aliinuka na kuketi vizurii halafu akaichukua na kuitazama vizuri “Ina maana Rose…aana…aanago..ngwa na…nana” aliongea peke yake kama mwehu, alisikia moyo umekuwa wa ubaridi, akaogopa kabisa yaani akaona kama vile anaota
Ilibidi aikate ile video na kumpigia simu karimu, huku kijasho kikimtoka kwa sababu hakuamini kwamba imekuwaje hiyo kitu “Mh Karimu” alimuita mwenzake baada tu ya kupokea simu
“Daaah, umeshuhudia hilo tukio?” alimuuliza
“Daaaah…..” machozi yalianza kumtoka maana alikuwa ni mwanamke wake wa malengo lakini ndo hivi alikuwa ameshaanza kuharibu
“Pole sana mwamba, hawa ndo wanawake tulioumbiwa ok?” alisema karimu
“Ina maana ndo maana amenikaushia mazima? Aisee kweli usimuamini mtu”
“Hamna, tulia tu atakutafuta mwenyewe”
“Ok powa kaka baadaye basi” alisema Ray
“Poa”
Alipokata simu alitulia akiangalia sehemu moja kwa sababu ya mawazo, halafu akainuka na kutazama nje, akawasha taa, akazima, halafu akaketi kitandani na kutoa pattern kwenye simu, akaandika namba ya Rose na kutaka kumpigia lakini alisita kidogo
“Ngoja nimuandikie tu SMS” alijifikiria na kuingia upande wa message akaanza kumuandikia
“KUMBE WEWE NI MALAYA ROSE NILIKUWA NAKUHESHIMU SANA” aliandika lakini akasita kuisend, akatulia kwanza kwa muda huku akiitazama ile message akafuta na kuandika nyingine “KWANINI UMEAMUA KUNIKAUSHIA ROSE?” aliangaliaaaa lakini akaogopa kusend, roho ilimuuma akaamua kuacha kabisa kumtumia ujumbe, akainuka na kutoka nje, akaingia hadi bafuni akafungulia maji na kunawa uso, kisha akatoka nje ya bafu na kwenda hadi sebuleni huku simu bado akiwa ameiacha kitandani.
Roho ilizidi kumuuma pale sebuleni akawa hana raha, Mara akaingia binti na chakula akaweka mezani na kutaka kutoka lakini mzee Mfinanga akamuita “We Nasma”
“Abee babu” alikuwa anapendelea kumuita Babu kutokana umri wa mzee huyo
“mh leo msafi sana, hongera sana ndo inatakiwa iwe hivyoo” alisema mzee.
“sawa ahsante babu” alisema binti na kumrushia jicho Ray, la shukrani halafu akatoka nje kwenda kuleta vitu vingine vya kula
Mzee alimgeukia Ray “Hivi Raymond” alimuita
“Naam mzee” aliitika kwa nidhamu
“Hata nyama hatuli na umekuja kweli?” alimuuliza
“Aaaagh, sasa muda huu buchani kuna nyama?” aliuliza
“Ndio zitakuwepo, ila tunataka kitimoto mimi na mama yako” alisema mzee
“Ok, sawa, ntaenda kuleta ngoja nile kwanza” alisema Ray
“Ok”
Akiwa anazidi kukaa pale na wazazi, alikumbuka kwamba ufunguo wa geto lake kule Dar alimuachia Rose, yaani alipata mawazo akajua kwa aibu ile angeweza amuibie vitu kabisa. Hapo ndipo alipoinuka chap na kwenda chumbani kwake kwa ajili ya kuweza kushughulikia suala hilo
Alichukua simu na kumpigia Karimu “Oyaaa” alisema baada ya Karimu
“Nambie” Karimu aliongea
“Daaah, unanisaidiaje?”
“Nini tena boss?” aliuliza
“Bwana si ufunguo nilimuachia yule manzi, sasa sikia, nenda pale kazini kwake, muambie akupatie basi maana nahisi anaweza akanipiga vibaya sana” alisema Ray
“Hiiii, ngoja niende” alisema Karimu na kukata simu yake
Alipomaliza tu kukata simu ujumbe uliingia kwa Ray kutoka kwa Rose
“SAMAHANI RAY NAJUA UNAUMIA KISA MIMI LAKINI SIKUWA NA JINSI, NAOMBA UNISAMEHE KAMA ITAWEZEKANA TUENDELEE NA MAPENZI” alituma Rose message iliyomuweka Ray katika wakati mgumu wa kushindwa kuelewa amjibu nni mpenzi wake huyo waliyetoka mbali…………..
SEHEM YA 11
Alibaki akiiangalia ile message, akaitazama sana, huku akifikiria ajibu nini lakini alipofikiria vizuri alipata jibu kwamba akimkubalia waendelee basi itakuwa ni njia rahisi sana kuzilinda mali zake ambazo binti ndo ana ufunguo, alimjibu kwa nidhamu
“Sasa jamani Rose hata nikikusamehe, marafiki zangu watanionaje? Japo nakupenda sana Rose” alisema Ray
“kama unanipenda Ray usisikilize maneno ya watu, nakuahidi sitokusaliti tena” alisema mtoto wa kike
“Ok, bana mimi sina shida, ila kwanini umefanya vile maana roho inauma mpenzi?”
“Ni tamaa, alinilazimisha Ray, lakini nimeamua niachane na kazi aliyoniajiri yule mzee, kwa sababu nimedhalilika nimeamua kuhama Temeke sa hivi naishi vingunguni Ray” alisema binti ikabidi Ray ashtuke kwanza maana kama ni kazi kaacha ina maana kumpata itakuwa na ngumu vibaya zaidi ni kwamba kahama pale alipokuwa anaishi
“umehama???” alimuuliza kwa mshangao
“Ndio…mbona umeshtuka?”
“Ufunguo wangu?”
“Ninao, si ukirudi tutatembeleana jamani? Kweli Ray nakupenda sitoweza kukuacha kweli, naomba unisamehe, sikuwa na kusudi”
“Haya usijali, mimi nakuja muda sio mrefu” alisema jamaa kumtia moyo tu maana alikuwa ameshamchukia kabisa.
Ray alimtumia SMS Karimu “Demu kaniambia kwamba amehama, na kazi ameamua kuacha, sasa mtafute akupatie ufunguo mimi sina mpango naye tena, wewe jifanye ni kitu unaenda kuchukua kule ndani
Ray alipomaliza kuweka suala hilo barabara, basi aliondoka na kurudi sebuleni kwa ajili ya kuweza kujiandaa kuutafuna msosi. Walikula kisha akainuka, kichwani bado alikuwa na mawazo sana, alijua fika binti alikuwa ametembea na boss wake kwa muda mrefu, hivyo basi aliona kwamba alikuwa anadanganywa tu, alichukua maji akatoka nje akinywa, kisha akarudi na kuweza kuingia chumbani akachukua pesa na kutoka nje nje
“Baba….ngoja nikalete nyama” alisema mtaalam maana mzee wake alikuwa amemtuma kitimoto.
Alitembea kutoka getini, akapiga hatua chache, kushoto kulia ndo akaanza kujiuliza “Sasa….kwani Nasma ni muislam au mkristo? Mh na kama ni muislam itakuwaje ale kitimoto,hapana, embu ngoja” Alijisemea na kutoka simu yake mfukoni kisha akampigia baba yake
“Ee mwanangu” alisema mzee
“samahanim namuomba Nasma mara moja aje” alisema
“Wa nini? Mzee aliuliza
“Kuna vitu anisaidie”
“Sawa…..wewe Nasma?” mzee aliita ikiwa bado hata hajakata simu
“Abee babu” alisema binti
“Kaka yako, anakuita……kwani wewe Raymond uko wapi?” aliuliza
“Siko mbali na getini niko karibia na kwa mzee kakore hapa” alisema
“Ok sawa, anakuja” mzee aliongea
Ray alijibanza kwenye kivuli huku akimsubiri, lakini muda huo wote Ray alikuwa chumbani kwake anajipamba zaidi, mdomoni alijipaka lip stick yake vizuri na machoni wanja, halafu vikorombwezo vingine alijaka, akapendeza hasa
“We Nasma” mama aliita kwa hasira “Huko ndani unafanya nini, hujui kaka yako anakusubiri huko njiani?” alisema mama
“Oh, naenda mama” binti alifanya haraka haraka akajifunga mtandio kichwani kama vile hijab halafu akabna na vipini fulani hivi kisha akatoka nje ya chumba hicho akapitia mlango wa nyuma ili wazee wasimuone, alitoka akiwa amevaa kandambili lakini usoni alikuwa amependeza sana, hivyo akakimbia na kuelekea mpaka alipoambiwa Ray anamsubiri.
Alifika pale akamkuta Ray ameegesha mkono mmoj ukutani huku akiwa anawaza mambo mengi sana kuhusiana na maisha hata hivyo suala la ile video ya ngono lilikuwa likimsumbua sana mtoto wa kiume kichwani mwake, maana alitoka mbali na Rose kiasi kwamba alijua kuwa atamuoa tu.
“Kaka, samahani nimechelewa” alisema binti akiwa anamtazama usoni, ndipo Ray alipomgeukia na kumtazama binti usoni
Unaambiwa kwa jinsi uso wa mtoto wa kike ulivyokuwa umeshaini, hata Ray mwenyewe alidata, akajikuta anamtazama tu, tatizo hapo aliona kwamba yule ni housegirl kwamba hatoweza kuishi naye hata kidogo bila kufikiria mapenzi humea popote.
“Umefika?” jamaa alisema huku akimkagua juu mpaka chini, kufika chini tu hivi alikutana na kandambili hapo ndo binti alipoharibu lakini hakuwa na viatu vingine. Jamaa alimtazama na kutikisa kichwa halafu
“ndio nimefika, samahani umeniitia nini?” aliuliza kwa nidhamu mpaka Ray akajikuta ameshapenda ile nidhamu yake na kumuuliza
“una nidhamu sana, hivi? Unanionyesha mimi pekee hii nidhamu au?” aliuliza
“hapana, ni kwa kila mtu” alisema binti huku akitabasamu
“ok, sawa nilitaka kujua kwamba wewe unakulaga nguruwe?” alimuuliza
“hapana, siwezi kula ptuu” alitema mate chini kabisa mtoto wa kike
“ohoooo, ok, ndo maana nikakuita maana sitaki uteseke pale nyumbani, sikia nilitaka nikuchukulie nyama ya ng’ombe lakini ni kwamba tu mimi siwezi kununua kitu halafu wewe usile, sikia, chukua hii pesa hapa nenda bucha la ng’ombe, nunua nyama nusu, halafu pesa itakayobaki pita pale sokoni nunua viungo vya chakula vyote, na ikibaki chenji hapo nunua viatu vya wazi vya kwako ili uvae, mimi sijapenda hizo kandambili” alisema mtaalamu akampa hela
Binti aliipokea na kubonyea kwa nidhamu “asante kaka”alisema na kugeuka anataka kuondoka.
Alikuwa amejazia sehemu za nyuma, alikuwa na umbo fulani dogo lakini lenye mvuto wa hali ya juu “Sikiliza” jamaa alimuambia ndipo binti akamgeukia na kumtazama huku midomo akiibana ikaingia ndani kidogo mashavu yakavimba
“isipotosha itakuwaje?…utanipigia simu okey?” alisema mtaalam ndipo binti akatikisa kichwa kukubaliana, Ray alitabasamu “Umekubaliana kama vile namba yangu unayo si ndio?” aliuliza
Binti alitabasamu “mh haya nipe basu” alisema huku akishika simu yake aandike namba
Ray alimtajia kisha akaanza kutembea, binti akasema “Namba yangu imeishia 26
“Ok……” alisema mtaalam.
Ray aliondoka akimuacha mtoto huyo wa kinyaturu anamshangaa kwa sababu hiyo kumjali jail hajui inatokana na nini, aliamua kuondoka.
Ray alienda mpaka bucha la nguruwe, hakutaka kuchukua nyama ambayo haijapikwa, alisubiri kikawa kinapikwa halafu baadaye akarudi nyumbani akiwa na mfuko wenye nyama iliyokaangwa vizuri, pamoja na mchele kilo kama 15 hivi akaviweka ndani
Binti yeye alikuwa ameshafika amejilaza kitandani anamuwaza Ray “Mimi huyu kaka ananipenda….sasa si aseme?” alijiuliza peke yake…….
JE ITAKUWAJE?
WATAWEZANA?
UJUMBE WA LEO: UNAPOIGUSA DINI YA MTU AU IMANI YAKE, NI KWAMBA UMEGUSA SEHEMU KUBWA YA MAISHA, DINI INAWEZA KUKUSABABISHA UKAKOSA VITU VINGI, MFANO MAPENZI, KAZI, MALI, NA HATA AMANI…….
TWENDE SAWA
SEHEMU YA 12
Siku moja baadaye
Upande wa jijii Dar es Salaam, Karimu alikuwa mjini amesimama njiani anaongea na simu, hata hivyo Karimu alikuwa anamsubiri Rose ili ampatie funguo za geto la Ray. Hata hivyo alikata simu na kutembea tembea mpaka pale alipoweza kufika maeneo fulani, ndipo alipomuona Rose akiwa amesimama kajibanza kwenye kona.
Alimsogelea kwa karibu “Shem vipi?”alimsalimia
“Safi kwema?” alimuuliza
“Kwema, nimekusubiri sana ujue” alisema Karimu
“Jamani samahani sana, nilikuwa niko mbali, si unajua siku hizi naishi vingunguti?”
“Vingunguti? Tangu lini” aliuliza Karimu kama vile hajui
“Ndio, jamani mwenzako hajakuambia?” Rose aliuliza
“Hapana”
“Ok nambie Karimu” alisema na kuvuta pumzi
“Ah…mh ninaomba ufunguo kuna vitu kaniagiza niweze kwenda kuvichukua mule ndani tafadhali” alisema Karimu lakini binti alishika kiuno na kumtazama tu
“Vitu gani?” aliuliza mtoto wa kike
“Ahsh, we nipe ufunguo” alisema Karimu huku akiwa anatabasamu, lakini bado binti alikaza
“twende wote” Rose aliongea huku akiwa ameshaanza kutembea kuelekea mitaa ya getoni kwa Ray
Kwa kifupi haikuwa mbali walitembea huku wakibishana
“Ina maana Rose hauniamini kwamba amenituma au?” aliuliza
“Najua amekutuma, sawa, lakini nataka nikajue alichokutuma humo ndani maana mh, mimi simuamini sana yule mwanaume” alisema binti
“Doooh” Karimu alisema
Hata hivyo binti walifanikiwa kufika, wakasalimia majirani na kufungua mlango, binti alipomaliza kufungua mlango hivi, alichomoa ufunguo akaweza kuingia nao ndani kisha akaketi kwenye sofa
“Ingia Karimu” alisema binti, na Karimu aliingia akiwa anafikiria atamdanganya binti kwamba ametumwa nini hata hivyo alipata wazo “Niambie kwamba ni kitu gani amekutuma hapa” alisema binti kwa hasira huku akionyesha kutokuamini kabisa kinachoendelea
“Mh, ni hii sabufa, amenituma hapa…niende nayo nyumbani” alisema jamaa
“Samahani sana, kwani wewe hauna ya kwako?” aliuliza
“sina, iliharibika, sasa hii nikasikilize kabla hajarudi”
“Ok powa chukua” alisema mtoto wa kike
“Ok powa, lakini sasa shem?” aliita Karimu
“Nambie”
“Wewe umehamia vingunguti kote kule, ili nisiwe nakusumbua kuja kunipa ufunguo siku nikitaka kuirudisha, basi ungeniachia ufunguo” alisema
“Hahaaaa……Karimu nimeshaujua mpango wenu, Ray anataka aniache, jamani khaa, sasa si aseme tu?” alisema binti huku machozi kama vile yalikuwa yanamlenga lenga hivi
“Hamna shemu sio hivo”
“Najua. Ila inauma jamani sawa….kama ananiacha” alisema huku akiinama na kufuta machozi halafu akainua macho na kumtazama, “Mi ufunguo sikupi, akitaka aje kuchukua mwenyewe” alisema binti na kuinuka akatazama kule na huku
“Sasa Rose ok basi sawa nitampigia simu ntamwambia umekataa kunipa vitu vyake” alisema Karimu
“mwambie tu, ila mimi ufunguo sitakupa, mpaka aje nimpe mwenyewe ndo nione imekuwaje”
“Ok powa mi nasepa” alisema Karimu na kusogea mlangoni hata radio hakuchukua tena
“sepa tu, ila ndo hivyo mwambie akitaka ufunguo aje anitafute mimi mwenyewe…..kama ana wasiwasi na mimi basi sikupi atajua mwenyewe” alisema binti.
Karimu aliishiwa pozi, akatoka huku akijicheka na kutoa simu mfukoni akaandika message kwa Jamaa
“DAAAH TRICK YETU IMEGONGA MWAMBA, AMESHTUKA AISEEE….AMEKATAA KUNIKABIDHI UFUNGUO AKIDAI KWAMBA UNA NIA YA KUMUACHA” alimtumia Ray
***
Kwa kawaida Ray alikuwa anachelewa sana kuamka, hivyo, ikiwa ni mida ya saa tano asubuhi ndipo alipojishusha kitandani na kuishika simu yake akakutana na message ya Karimu ila akaipuuzia na kuinuka akachukua mswaki halafu akaenda mpaka nje ya chumba.
Alipifika nje ya chumba alipata wazo la kurudi chumbani aweze kuchukua taulo, akaoge kabisa bafuni, alichukua taulo, sabuni ya kuogea kisha akatoka akipiga mswaki na kuzama bafuni, alimaliza kusawaki akaweka mswaki kwenye kadirisha kadogo ka bafuni, kisha akavua bukta na boxer zote akaziweka kwenye misumari nyuma ya mlango.
Hata hivyo alijisogeza pembeni mwa bomba la mvua akaanza kuoga taratiiibu huku akikumbuka tukio la nyuma. Alimkumbuka Rose jinsi alivyokuwa akiinjoy naye, akakumbuka ahadi nyingi ambazo pia alikuwa ameahidiana naye ahadi kama vile alikuwa an ampango wa kuoana na binti, lakin vivyo hivyo alikuwa amekula naye raha nyingi sana jijini Dar wakati yeye akiwa anafanya kazi ya kuuza katika duka la nguo la baba mmoja hivi.
“ahahaa” alitabasamu Ray alivyokumbuka kwamba kumbe binti alikuwa ana-date na boss wake kichwani alikumbuka mambo mengi ya maisha yake na Rose
Kumbe upande wa pili Naa alikuwa ameshaweka chakula jikoni, ilikuwa ni mseto amebandika, halafu akatoa kuni moto ukawa unawaka kwa mbalii, ndipo akatoka jikoni na kwenda mpaka chumbani kwake, kisha akalishika gauni akalivua na kubaki na chupi.
Alipomaliza kufanya hivyo, alichukua khanga na kujifungia kifuani mpaka mapajani halafu akatoka na kuingia katika chumba ambacho ndani kiligawanywa mara mbili, yaani kulikuwa na choo pamoja na bafu, vyote vikiwa na milango tofauti.
Alishika kitasa cha bafu akakizungusha bila kujua kuna mtu maana maji yalikuwa hayamiminiki, alipofungua hivi, alisikia sauti “WEWEEE. KUNA MTU” yaani mpaka sentensi ile inaisha, ni kwamba mlango ushafunguliwa, binti hakuamini macho yake, alimuona live jamaa akiwa uchi, kabisa, amejipaka sabuni mwili mzima na maji alikuwa amefunga.
Jicho lisivyokuwa na nidhamu lilitangulia kuona ile sehemu kuu, ilikuwa imeinuka kidogo. Alibaki mdomo wazi, na kugeuza uso haraka akatoka akikimbia, huku akitetemeka na kuilaumu nafsi yake.
Aliogopa akaingia chumbani na kujilaza kitandani “Heee kumbe ameshaamka jamani khaa” aliwaza mtoto wa kike huku akiifungua kanga yake akalala chali na kuanza kuwazia kile alichokiona…………
INAENDELEA…………