πππππ ππ¨ππͺπ π¬π π ππ πͺππ‘ππ¨, ππππ©π¬π’π‘ππππ‘π¬π π‘πππ¦ππ πππ π π πππ ππππ, π‘πππ‘π π¬π π‘π¬π¨π ππ π¬ππ‘ππ¨ π πͺππ‘π¬ππͺπ
EP 3 – 4
“Wewe ndiye una mimba ya mme wangu?” Sophia aliuliza. Juliet alikuwa akitoka kwenye gari huku Daudi akiwa amesimama moja kwa moja nyuma yake. Mimba yake imekuwa kubwa. vitu vyake vilikuwa kwenye buti la gari, lakini hata kabla hajaanza kuingia ndani ya nyumba hiyo, tayari Sophia alikuwa tayari kuwakaribisha.
βNdiyo! Mimi ndiye. Unashangaa?β Juliet aliuliza huku akiwa amekunja uso kwa nguvu. Aliwa tayari kwa mapambano. Alidhani Sophia angemzuia asiingie ndani ya nyumba, Aliwaza Sophia ataumia moyoni baada ya kujua kuwa yeye amekuwa mchepuko kwa mme wake. Lakini alishtuka mambo yalipokuwa tofauti.
“Hapana! Kwa nini nishangae? , sina hasira na sijashtuka. Kwa kweli, ninashukuru kwamba wewe ndiye. Badala ya mume wangu kumpa mimba kahaba, ni bora ampe mimba rafiki yangu mkubwa. Yaani nimekufahamu tangu utotoni na tumekuwa marafiki. shetani unayemjua ni bora kuliko malaika usiyemjua. Nitakushukuru milele kwa kubeba mtoto wa mume wangu. Nimeona amefurahishwa na ujauzito wako. Niko hapa ili kukusaidia kwa njia yoyote niwezavyo katika muda wako wa miezi tisa utakayobeba Mimba. Juliet, unakaribishwa sana nyumbani kwetu.β Sophia alitamka huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
Mshtuko kwa Daudi uliongezeka. Alijiuliza mke wake aligeuka kuwa mwanamke wa aina gani katika siku chache zilizopita baada ya kujua kuhusu ujauzito huo.
βNi mwanamke wa aina gani anagundua kuwa mumewe alimpa ujauzito rafiki yake kisha kumkaribisha yeye na huyo mjamzito kwa mikono miwili? Huyu ni mwanamke wa aina gani?β Daudi alijiuliza. Ilikuwa kana kwamba hakuwahi kumjua mke wake, hata hivyo, walikuwa wameoana kwa miaka kumi lakini Sophia alimshutua sana.
“Hebu tuingize vitu vyako ndani.” Sophia alisema huku akianza kufungua gari na kuchukua mizigo wa Juliet na kuiingiza ndani ya nyumba. Kwa aibu, Daudi aliungana naye kuhamisha mizigo hiyo. Juliet hakubeba chochote aliingia tu ndani na kuketi moja kwa moja sebuleni. Ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni.
Daudi alipoleta begi la mwisho alipokelewa kwa shangwe na vicheko vilivyojaa sebuleni. Alijiuliza nini kinaendelea. Akasogea karibu na eneo la kulia chakula na kuona meza na viti vimewekwa kwa ajili ya tafrija ndogo. Alijiuliza nini kinaendelea kwani hakuomualika mtu yeyote aje kwa sherehe yoyote.
βNi nini kinaendelea hapa?β Daudi alimuuliza mkewe aliyekuwa akitoka jikoni na sufuria kubwa la walia. Aliweka wali kwenye meza ya kulia chakula na kisha akapakua kwa sshani ndogondogo na kuanza kuwagawia wageni.
“Ah Ah! Mume wangu mpendwa. usiniambie unataka kumleta mama mtoto wako nyumbani kimya kimya. Haifanywi hivyo na sivyo tulivyolelewa. Katika utamaduni wetu. Unapoleta mke mpya nyumbani, lazima uwajulishe majirani zako na lazima upige tusherehekee. Ndiyo maana niliwaalika marafiki zetu na watu wanaotutakia heri na hata washiriki wa kanisa letu kusherehekea ujio wa mke mwenzagu β Sophia alisema huku akiendelea kula wali.
βDaudi, mkeo yuko sahihi. huwezi tu kuleta mwanamke wa pili nyumbani bila kuwafahamisha marafiki na familia yako. Tumekuja kufurahi pamoja nawe. Hongera sana mtu wangu. Hivi karibuni utakuwa baba.” Joff alisema huku akimsogelea na kumkumbatia Daudi na kumpigapiga mgongoni.
Daudi alinyoosha mikono juu huku asijue nini chakufanya. Hakuitikia vyema kumbatio la Joff. Juliet alikuwa ametoka sebuleni na kuungana na Dauadi pale alipokuwa amesimama. wote wawili walikuwa wameduwaa na kuchanganyikiwa . Daudi aliona aibu na pia Juliet.
βTafadhali mabibi na mabwana, Naomba mnisikilize tafadhali?β Sophia alisema
βNyinyi nyote ni marafiki zangu na baadhi yenu ni marafiki wa mme wangu. Mnakaribishwa kwenye sherehe hii ndogo na asante kwa kuitikia mwaliko wangu. mkutano huu mdogo na asante kwa kuheshimu mwaliko wangu .
Wote mnajua mimi na mume wangu tumekuwa tukihangaika kupata watoto tangu tufunge ndoa miaka kumi iliyopita, lakini hatujafanikiwa. Sijaweza kupata mimba hata baada ya kuhangaika kwa kila namna .
βNimetembelea zahanati nyingi na hata kwenda kuwaona waganga wa tiba asilia lakini hakuna kilichofanya kazi hadi sasa. Jambo la kushukuru, rafiki yangu Juliet sasa ana mimba ya mume wangu. Tatizo letu la kukosa watoto limetatuliwa. Ninataka hasa kumshukuru Juliet kwa kupata mimba na kukubali kuwa mke wa mme wangu. Na pia namshukuru kwa kukubali kuja kuishi nasi. Nitakuwa mwenye shukrani kwake milele.
Kwa mume wangu kipenzi, ninashukuru kwa dhati uvumilivu wako miaka yote iliyopita. Sikulaumu kwa chochote na sina hasira kwamba ulimpa rafiki yangu mimba. Uwe na uhakika wa upendo wangu. Mtoto huyu akizaliwa, nitamlea kama wangu.
kila mtu anafurahi familia yetu kuongezeka” Sophia alisema na kila mtu akampigia makofi . Alirudi na kuendelea kula wali
Daudi alijiona mjinga sana. Hakuwahi kujua mke wake Sophia aliandaa sherehe ya kushtukiza ambayo kwa makadirio yake ilikuwa ni kumtia aibu mbele ya marafiki na majirani zake. kabla ya sherehe, hakuna mtu aliyejua kwamba alimpata mwanamke mwingine mimba, lakini baada ya hapo, ikawa habari ya mji kwamba alimpa mimba rafiki wa mke wake.
Aliona aibu kiasi kwamba hakuweza kuinua miguu yake pale alipokuwa amesimama. Aliona aibu, Juliet pia alikuwa na aibu. Hakuelewa ni kwanini Sophia anafanya sherehe ya kumkaribisha Julliet
Muda mfupi, Sophia aliosha sahani mbili, akawahudumia chakula Daudi na Juliet. Aliongeza vipande viwili vikubwa vya nyama na chupa mbili za juice. kwa mara ya kwanza baada ya siku nyingi, Daudi alikula chakula cha mke wake. Alikula kwa sababu kilipakuliwa kutoka sufuria lilelile walilokuwa wakipakuliwa wengine kwenye . Hata hivyo, yeye na Juliet bado walikula kwa hofu.
Baada wa watu wote kutawanyika, Daudi na Juliet wwalijilaza sebuleni wakiwa na godoro jipya alilonunua siku si nyingi. Lakini Sophia alikuja na kuwaamsha.
βNimewaachia nyinyi chumba cha kulala. Nimeandaa chumba cha wageni. Kuanzia sasa nitakaa hapo. tafadhali Juliet, usikatae hii. Sina hasira hata hivyo. Ninataka tu uwe na amani na mume wangu, na pia mtoto. Ninyi wawili mnapaswa kwenda chumbani mkalale kwa raha.β Sophia alisema huku akienda zake.
wakati huo, Daudi na Juliet walitazamana kwa hofu zaidi machoni mwao.
“Ni mwanamke wa aina gani anayeacha kitanda chake cha ndoa kwa mwanamke wa nje ya ndoa ambaye ana mimba ya mme wake?” Juliet alimuuliza Daudi.
βSijui anamaanisha nini. Lakini, silali katika nyumba hii. Sasa naogopa sana. nina hakika yuko kwenye uovu. Tafadhali nifuate sasa hivi.β Daudi alisema. Walitoka nje na kulala ndani ya gari.
NYIEEEEE π π π
EP 5
“Sasa tunaweza kuingia ndani. Mke wangu ameenda kazini. Unajua yeye ni mwalimu; huenda kazini saa kumi na mbili asubuhi ili asichelewe shuleni. Tuingie ndani ili nijiandae na kwenda ofisini.β DaudiΒ alimwambia Juliet huku wakiamka kutoka kwenye gari walilokuwa wamelala usiku uliopita.
Hawakulala vizuri hata kidogo na Juliet hakuwa na furaha. Tayari alianza kufikiria kurudi nyumbani kwake baada ya hofu ya kuishi na Sophia kuongezeka .
βMaisha ya aina hii si mazuri kwa mwanamke mjamzito. Sidhani kama nitaendelea kuishi hivi. Niangalie tu nimelala kwenye gari. Siyo vizuri hasa ukiangalia hali yangu niliyonayo.Nina chumba changu mwenyewe kwanini niteseke kulala kwenye gari?. Sidhani kama nitaingia nyumbani kwako tena.β juliet alisema huku machozi yakimtoka.
Alikuwa na wasiwasi na hofu juu ya maisha yake kwa sababu ya jinsi mke wa Daudi alivyofurahia ujauzito wake.
βTafadhali, Juliet usiondoke!. Niko pamoja nawe kwa kila namna. Nimechukua jukumu la kuhakikisha mtoto wetu anazaliwa salama n bila kujali kitakachotokea.Iwe mvua liwe jua nitakuwa na wewe mpenzi wangu. Please usiindoke” Daudi alisema.
“Unasema!? Je, mkeo akituua?.
Mbona hajajibu kwa hasira tangu aliposikia kuwa ulinipa ujauzito? mtazamo wake unaonyesha kwamba anapanga mauaji makubwa juu yetu na sipo tayari kupoteza maisha nyumbani kwako. Juliet alisema.
Aliingia ndani ya nyumba na kuanza kufunga virago vyake ili aondoke lakini Daudi alimfuata na kuanza kumsihi asiende.
βTafadhali, si lazima ufanye hivi. tafadhali usiende. Mke wangu hawezi kukudhuru, nina uhakika na hilo.β Daudi aliomba kwa upole
βUnayaongea haya kutoka moyoni mwako? Je, Humuogopi?, ona jinsi alivyotudhalilisha jana mbele ya watui. Nina hakika kuwa nawe unaogopa. Tafadhali usiniambie kwamba hawezi kufanya lolote.β Juliet alisema. Alianza kuburuza begi lake nje ya nyumba lakini Daudi alisimama mlangoni na kukataa kumruhusu kuondoka.
INAENDELEA


