π‘ππ πππ¨π£π π¨πππ ππ, πͺππͺπ π¨π ππ‘π’ππ§π
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 1
Majira ya saa nane mchana, jua limesimama angani likionesha uwamba wake kwa wale watembea kwa miguu na wakaaji ambao hawakua wamejikinga na mwamvuli. Jua lilichachamaa kweli kweli halikuchagua wa kupiga kila aliesimama mbele yake lilimshushia joto, wapo waliomlalamikia malaika kitengo cha jua kwamba apunguze joto ila katu hakuna hata mmoja aliethubutu kuomba mvua, iweje uombe mvua wakati huna uhakika na biashara yako ya siku π.
Licha ya ukali wa jua, eneo la kariakoo ndani ya jiji la Dar es salaam liliendelea kuwa busy. Watu walitembea huku na kule, wafanya biashara walipaza sauti kuwaita wateja na wateja nao walikua makini kulinda simu na vitu vyao vingine vilivyopo mfukoni, wasijerudishwa mjini maana Dar es salaam nijiji ambalo huwapeleka wakazi wake darasani kila siku endapo hotokua makini na mambo ya wizi.
Katika umati huo huo wa watu kuna dada mmoja mrembo kwa sura, umbo mpaka mwendo ulisadifu yaliyomo, alitembea kwa madaha akapoteza umakini baada ya kumkwepa mbeba mizogo mmoja aliekua katika kasi ya ajabu, ukwepaji wake ulimfanya kukanyaga biashara ya watu.
“Weee demu ni mjinga sana kwanini unaharibu biashara yangu π‘” jamaa mmoja mfanyabiashara wa viatu aliekua kapanga viatu vyake pembeni mwa barabara hawa hujulikana zaidi kama machinga.
“Samahani kaka sikukusudiaπ₯Ή”
“Hujakusudia nini wewe ndo ukanyage viatu vyangu kwa mamiguu yako yenye mchanga hebu nitokee hapa mshenzi wewe” kijana alimsukuma kwa nguvu huyo mwanamke pembeni kwa namna alivyokosa balance alikua anaenda chini moja kwa moja kwasababu nguvu za kijana zilikua nyingi sana. Bahati nzuri kuna mwamba pembeni alimdaka huyo mrembo asiende chini.
“Ouuuh ahsante bro sijui ningebamiza kichwa na kufa kabisa”
“Haliwezi kutokea hilo mbele ya macho yangu, tulia hapa kwanza mdogo angu nikuoneshe kitu”
“Kwahiyo dogo stress zako za biashara ndo unataka kuzimaliza kwa mdogo angu na unataka kumuua kabisa”
“Mdogo wako hana adabu na alichokipata kimestahili kabisa kwani wewe unatakaje” huyo mfanyabiashara aliendelea kutema maneno ya shombo bila kujua ni nani aliekua anamtemea maneno hayo.
“Ngoja nikuoneshe mimi nani” huyo mwanaume alimdaka kijana kwenye shati lake na kuanza kumvuta. Kijana alijitahidi kujipapatua kuondoka mikononi mwa mwamba lakini hakuweza kuchomoka hata mara moja.
“Sasa kijana tunaondoka wote nikakuoneshe nini maana ya adabu na kuheshimu watu”
“Oyaa weee hata kama mwenzetu amekosea ila hakuna kuondoka nae”wafanya biashara wengine wakaanza kumtetea kijana.
“Mimi ni kapteni wa jeshi kitambulisho changu hiki hapa kama kuna mtu anataka kumsindikiza mwenzenu tuongozane tuelekee Lugalo” kusikia kwenda kambini jeshini hakuna mfanyabiashara hata mmoja ambae alithubutu kunyanyuka kutaka kusindikiza hiyo safari ya jeshini.
Huyo kepteni akamchukua mwamba wakatembea mpaka karibu na kituo cha polisi cha msimbazi.
“Afande mbona huyu jamaa ananichukua kwa nguvu hivi anataka akanifanye nini?” Kijana aliejichanganya aliomba msaada kwa afande flani hivi wa jeshi la polisi. Kabla ya afande hajachangia chochote kidogo walifika wanajeshi wengine wawili kitendo cha kuwaona wanajeshi hao wenye sare kamili, polisi akafyata mkia na kujifanya kama haoni vile π.
“Vijana tunaondoka nae huyu kajichanganya” kepten akamkabidhisha kijana kwa wajeda halafu yeye na mdogo ake wakafuata, wote wanne walipanda gari la jeshi na kuondoka kwa kasi eneo hilo, kijana kayatimba kwa wajedaπ.
EP 2
Ndani ya jumba moja kubwa lenye uzuri na ufahari usiopimika ambao umepambwa kuanzia getini, nyanya madhubuti juu ya fence za ulinzi.
Bustani ya maua mazuri vipepeo wakiruka huku na kule huku hewa safi ya ubarizi ikipunga kwa utulivu ndani ya jumba hilo kwenye chumba kimoja wapo alisikika mwanaume akilia kwa uchungu kutokana na yale mateso ya mwili aliyokua anayapitia.
“Hivi unaitwa nani mbona unalia kama demuπ” kepten alimuuliza kijana muuza viatu kariakoo.
“Naitwa Damian, kamanda mmenitesa sana naomba mnisamehe jamani sirudii tena mimiπ”
“Hahaha kipindi unamsukuma dada angu hukuliona hilo lazima nikunyooshe ili heshima yako ikue”
“Kaka msamehe naona adhabu uliyompatia ni kubwa sana, utamuua kijana wawatu bure” Patricia aliamua kumuombea msamaha Damian hakutaka kuendelea kumwona kijana anapitia mateso zaidi wakati kosa alilolifanya ni kumsukuma tu tena hakua ameanguka kabisa.
“Ila wanawake kwa huruma haya bhana kwakua umetaka mimi nipo tayari kumuachia huyu ila asijaribu kujichanganya kupita kwenye anga zangu tena sindio dogo” kepten Pius aliendelea kumchimba biti Damian.
“Nimekuelewa bro nimeelewa mimi sirudii tena haki ya mungu nimekoma mimi nimekoma sana” Damian alionesha kujutia kosa alilofanya hiyo ongea yake sasa ukimuangalia mbona unacheka, ukiweka huruma pembeniπ.
“Vijana mchukueni mpeleke kwake na afunge mdomo wake asiseme popote”
“Bro naomba nimpeleke mimi” Patricia aliamua kuingilia kati hakutaka Damiani aridishwe na wajeda maana huenda wangeenda kumtupa hata porini huko na Patricia hakutaka kubaki na hatia kubwa moyoni mwake.
“Tuondoke” Patricia alimshika bega Damian baada ya kufunguliwa kamba katika hali ya kukokotana wakatoka mpaka nje hali ya Damian bado haikua nzuri.
Alimsaidia kumwingiza ndani ya gari na kuanza kuondoka.
“Naomba unisamehe kwa yaliyokukuta kaka angu” Patricia alifungua mazungumzo huku akimfunga mkanda vizuri Damian.
“Nisamehe mimi kwakua ndo nimezingua, nilipaswa kufanya vingine tofauti na nilivyofanya mimi naomba unipeleke nyumbani kwangu nikapige hata mitishamba nitarudi barabarani”
“Hautaenda kwako, tunaenda wote nyumbani kwangu, kuna kitu nataka tukafanye”
“Madam laki……….”
“Nimeshasema hapa tunaenda kwangu au unataka nikurudishe ndani ubaki hapa”
“Bhasi bhasi twende tu huko kwako” Damian alikubali haraka haraka bila kujua ni kitu gani, Patricia alitaka wakafanye, akilini alikua na maswali lukuki ambayo hayakua na majibu ya haraka. Moyoni alikua na hofu kubwa juu ya hiyo safari alichotamani zaidi ni kheri wangemalizana kila mtu apite upande wake lakini haikuwezekana.
EP 3
Ndani ya gari ukimya ulitawala kila mmoja alikua ana mawazo yake yaliyounganishwa na hiko kitu ambacho walitakiwa kwenda kukifanya nyumbani kwa Patricia.
Safari yao ilikwenda kuishia Mbezi beach, moja ya mtaa wenye nyumba nyingi za kishua kwa kutumia rimoti iliyokua mkononi mwake. Patricia alifungua geti na gari iliingia mpaka eneo maalumu lenye maegesho ya magari, jumla ya magari yote yaliyokua hapo ni magari matatu. Na yote yalivutia kwa mwonekano wa nje hata bei ya kununulia hayo magari ilionekana imechangamka kidogo.
“Karibu ndani jisikie kuwa huru sana naishi mwenyewe hapa” Patricia aliendelea na ukaribisho wakati ambao Damian aliendelea kuchunguza uzuri wa jumba hilo la kifahari.
“Ahsante sana kuishi peke ako hapa huogopi?” Damian alitoa swali ambalo lilikua na mtego ndani yake kupitia hilo swali alitaka kujua kama Patricia ameolewa au laaa na kama kaolewa bhasi aone ni namna gani atachomoka kwenye mtego wa kufumaniwa na mwenye mali yake.
“Kwa ukubwa huu niogope nini sasa, wakati wa likizo huwa anakuja mdogo angu wa mwisho pia huwa natembelewa na marafiki kingine nimezoea tu kuwa mwenyewe sihitaji hata mfanyakazi maana kazi karibia zote naziweza”
“Ooh sawa hongera kweli wewe ni mwanamke na nusu”
“Hahahaπ ahsante karibu ndani sasa” Patricia na Damian waliingia mpaka seblen mahali ambapo kulikua na vingi vya kuvutia.
“Tulia hapo nilichotaka uje ufanyiwe hapa ni matibabu mazuri ya mwili wako, ukienda kienyeji enyeji hapa utatunza maumivu na vmajeraha ya ndani bure”
“Sawa ahsante kwa kujali” Damian alionesha upole na unyenyekevu wakati wote.
“Usijali ngoja niende jikoni nikakutengenezee chochote kitu wakati tunamsubiri daktari wangu aje akutibie”
“Sawa sawa madam” Patricia alienda upande mwingine wa jumba hilo na kumwacha Damian akiendelea kutazama mpira kwenye runinga hapo sebuleni.
Dakika arobaini na tano za kuhesabu Patricia alitoka akiwa na bakuli lenye supu ya moto.
“Enhee mgonjwa upate hii kwanza uupe mwili nguvu kidogo”
“Ahsante Damian alipokea hilo bakuli la supu na kuanza kunywa taratibu.
Wakawa wanazungumza mambo ya hapa na pale kidogo mlango ulifunguliwa na akaingia mwanaume mmoja mrefu amevalia shati la mikono mirefu na suruali ya kitambaa pia alikua na begi lake la kubeba.
“Nna uhakika sijachelewa nimekuja kwa wakati eeh”
“Karibu sana Doctor Ndunguru mgonjwa wetu ni huyu hapa unaweza kumtazama na kufanya matibabu yake, Damian huyu ni Doctor Ndunguru ni daktari wangu binafsi atakutazama na kukutibia vizuri” Patricia alitoa utambulisho kamili.
“Sawa karibu sana doctor” Damian alitoa tabasamu pana ila namna ambavyo daktari huyo alimtazama Damian lilikua jicho flani la nusu chuki.
Bhasi matibabu yalifanyika kwa Damian kusafishwa vidonda vyote, kupakwa dawa na vile.vilivyochimba sana vilishonwa baada ya kumaliza hayo matibabu.
Doctor Ndunguru aliomba kuzungumza na Patricia ila sehemu nyingine ambayo Damian hatoweza kusikia mazungumzo yao.
“Sikia Patricia huyu jamaa ni nani ako”
“Ni mshikaji tu nimemuokota huko nimeona nimsaidie”
“Kama mmekutana leo ndo uwe unamchekea vile”
“Kwani shida yako nini ndugu yangu”
“Shida ipo tena kubwa sana, Patricia unajua fika kwamba nakupenda tangu tukiwa shule unajua juu ya hisia zangu juu yako zimesimama wima zinahitaji nafasi kwenye moyo wako”
“Hilo nafahamu”
“Kama unafahamu unahisi nitakuruhusu huyu mhuni alale hapa bila mimi kuwepo, sijawahi hata kukuonja halafu mshamba mshamba kutoka huko akutafune bure leo tutabanana hapa hapa”
“Hauta lala hapa chukua pesa yako hii na uende nyumbani kwako, siko chini yako wala chini ya mtu yeyote yule nitajilinda mwenyewe”
“Patricia hutaki kunisikiliza kisa huyo mpuuzi wako”
“Acha kumuita huyo kijana mpuuzi, toka nyumbani kwangu”
“Unafanya makosa makubwa sana Patricia π‘”
“Babu weee kwenda mwana kwenda”
“Sawaa tutaonana nakwambia na utajutia hiki unachonifanyia”
“Nijutie nini, hebu kwenda hukoo” Patricia alihakikisha Doctor Ndunguru kaondoka kabisa ndo akafunga geti lake.
“Mbona huyu kijana nampambania sana Patricia mimi nimekuaje jamani ouuuuuuh” Patricia alishika kifua na kuachia pumzi nzito.
Aliingia ndani na kumkuta Damian amelala akajua fika usingizi umemchukua kutokana na maumivu ya kipigo na matibabu aliyofanyiwa bhasi lazima usingizi umjie bila taarifa alienda chumbani aliporudi alikua na shuka akamfunikia Damian alipotaka kwenda chumbani alisikia geti linagongwa alitoka kwenda kutazama mgongaji.
“Sisi ni askari wa jeshi la polisi tumepata taarifa kutoka kwa msamalia mwema kwamba nyumbani kwako kuna jambazi umelifuga turuhusu tuingie ndani tukague” askari mwenye cheo kikubwa zaidi ya wenzake alieleza kile kilichowaleta.
Patricia akawaza haraka haraka akajua tu kwamba Doctor Ndunguru amewaita polisi, akili yake ikaanza kuwaza anawatokaje hao polisi.
Inaendelea…


