ππππ πππ π π£π¨π‘ππ
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 66
TULIPOISHIA..
“Wee Jofu ivi unaelewa anachozughumza uyu mkeo, maana anaongea vitu ambavyo havipo kabisa maana nasikia Mara Canada Mara sijui kulipwa na MUNGU, kwakweli Mdogo wangu kapona ila nahisi akili zake bado hazipo sawa.!”
Kwanza nilimshangaa Sana Shemeji yangu kwa kuniona Mimi Mjinga na mpuuzi nadhani hajui nani kaniponya, ila kabla Jofu hajamjibu chochote Shemeji nikamkatisha kwa kusema..!!
ENDELEA NAYO
Nilimshangaa sana Shemeji yangu ananiona Mimi Mjinga sina akili, kabla Jofu hajajibu nikamwambia Dada kuwa inatosha nilicho ongea kimeeleweka uzuri hakuna mtoto hapo. Ndipo Dada akasema huku akionyesha wasiwasi kidogo;
“Kwaiyo Mdogo wangu Koga Ndio unaondoka kwenda Canada kweli..!??”
“Ndio ivyo Dada, acha niende nikamtumikie Mungu maana bila yeye ningekuwa maiti..!”
“Sawa, lakini mbona imekuwa ghafla sana Mdogo wangu, Mimi nashukuru umepona nilitaka tule bata kwa uzima uliopata ivyo nilitegemea utasubiri Mama arudi tufurahi Pamoja ndio uende huko Canada sasa Mdogo Wangu. Pia Mimi nimesha kusamehe kabisa naomba husiondoke ili ikiwezekana tufungue ukurasa Mpya wa maisha yetu, sababu ata Baba tayari kafariki kwaiyo nilidhani wewe unaenda kumsimamia Mama kuzipangilia zile Mali kule kijijini..Koga husiende Canada Mdogo wangu nakuomba.!!”
Alipomaliza kuongea nilimuangalia sana Dada yangu maana nilimuona mpaka sasa hajui Mimi ninani, na ndipo nikamjibu;
“Dada Mimi nilisha kufa sawa ndio maana wote mliukimbia mwili wangu, akabaki binadamu mmoja tu Mwenye roho ya ajabu ambaye ni Jofu, lakini yote ayo nimesha wasamehe kwa dhati kabisa kama Mimi alivyo nisamehe Baba yangu Yesu Christo, sasa ujio Wangu huu au kuzaliwa kwangu huku mala ya pili ni special kwa ajili ya kazi moja tu hapa duniani ambayo nikuakikisha wewe na familia yangu yote mnaenda mbinguni na iyo kazi ndio ajira yangu kwa sasa. Kwaiyo ukurasa unaotaka wewe nifungue Mimi tayari nimeshaufungua ukurasa Mpya tena wa HOLY BIBLE (Biblia takatifu) kwaheri Dada yangu naomba kesho mnisindikize airport hapa naomba tu process za Passport zikamilike vizuri ili kesho niondoke zangu, ila katika jina la Yesu itawezekana..!!
“Mmh! Sawa Mdogo wangu naona umeamua Mimi sina neno zaidi..!!”
Basi ilipofika jioni wahudumu walikuja mpaka tunapoishi tukafanya maombi kwenye kile chumba kisha wakatuambia kuwa taratibu zote za Passport zimekamilika kwaiyo safari ipo tayari, kwaiyo kama tupo tayari basi tujiandae kwa safari yakwenda alipofikia Pastor. Basi nikamfuata yule mbwa wetu Nasri aliyeokoa maisha yangu nikafumba macho huku nimemshika kichwani nikamuombea maombi ya kumtakia maisha mema na uzima tele, baada ya hapo alichukuliwa na Dada nakuondoka naye kuelekea kwake.
Tukapanga panga nguo nakuweka vizuri chumba chetu na jioni iyo iyo tukaondoka mpaka New Africa Hotel ambapo ndio alikuwa amefikia Pastor Stefansson, alifurahi sana kutuona alikuwa akinitazama kwa shauku kisha akasema;
“I don’t know why people they don’t realize the name Jesus, the only healing name.!!”
(Sijui kwanini watu hawalitambui jina la Yesu, jina pekee linalo ponya.!!”
Aliongea Pastor huku tukipeana mikono akaniambia;
“Groly to God”
(Utukufu kwa Mungu)
Nami nikamjibu huku nikivunja goti kuonyesha heshima kwa uyu Pastor;
“Amen”
Tukiwa hapo Hotelini tulikula Chakula kizuri kabisa, tuliongea mengi sana na jopo zima la wahudumu wa Pastor Stefansson. Muda wakulala ulupofika Mimi sikulala na Jofu kutokana nakuwa sio mume wangu ivyo nililala na wanawake wenzangu. Tukalala hapo na asubuhi ya saa moja tulichukuliwa na gari mahalumu la hapa hotelini mpaka airport, ambapo kwa mara ya kwanza nilipanda ndege mahalumu nikiwa na kundi zima la Pastor Pamoja na Jofu wangu. Ndege iyo iliyotumwa na serikali ya Kenya, ili Pastor akafanye huduma kwenye nchi yao.
Tulifika Kenya na huduma ikaanza, tulifanya maombi mfululizo kama siku tatu tu watu walifunguliwa vilema walitembea wapagani mamia kwa mamia walimpa yesu maisha kwakweli ilikuwa ni utukufu kwa Mungu.
Baada ya huduma iyo nzuri ya hapo Kenya atimaye safari ikaanza kuelekea Uganda, maana Pastor Stefansson alisema ngoja afanye maombezi East Africa yote kuliko kufanya Tanzania tu na Kenya.
Basi kwakuwa tulifanya huduma kubwa sana nchini Uganda huku Mimi nikiwa busy kuwasadia wagonjwa wa aina zote ata awe kajinyea Mimi sijali kabisa, maana naijua hali niliyokuwanayo Mimi hapo awali. Sasa waganda wakawa wananishangaa nakuniona Mimi ni msichana wa ajabu sana wasijue nilikuwaje;
“Wow! this is a wonderful woman!”
(Aisee! Uyu ni mwanamke wa ajabu sana)
Nilimsiki mtu mmoja aliyekuwa karibu yangu akiongea, baada ya Mimi kumshikilia mmoja ya mgonjwa aliyekuwa anaumwa moto wa Mungu, nadhani kilichomfanya uyu mganda kunishangaa nikutokana na ugonjwa uo ulivyo mmbaya na hatari sana yani bora uugue Ukimwi na magonjwa mangine mangine unaweza kuishi maisha ya kawaida kabisa lakini sio kwa huu ugonjwa ni hatari sana.!!
Basi baada yakumaliza kufanya maombezi katika jiji la Kampala nchini Uganda, atimaye ndege mahalumu kabisa toka nchini Canada ilifika Entebbe International Airport nakutusubiri hapo. Tulifika uwanja wa ndege mapema alfajiri nikaiona ndege kubwa yenye maandishi ubavuni mwake yanayo someka
AIR CANADIAN WORSHIPβοΈ
Tukatazama usoni Jofu alafu kila mmoja akauvuta mdomo wake pembeni nakutengeneza tabasamu changa. Zikafanyika taratibu kadhaa hapo kisha tukaingia ndani ya ndege iyo kubwa sana tayari kwa safari ya kuelekea ulaya au America ya kasikazini.
Lakini huwezi amini maana ghafla nili…!!!
EP 67
Tulipopaa tu angani nikamwambia Jofu;
βJofu Nasikitika kukwambia kuwa sirudi tena Tanzania au nyumbani..π’β
Kisha machozi yakaanza kunitoka, kwakuwa tulikuwa tumekaa seat moja basi Jofu akanikumbatia huku akiniambia;
“Upo sahihi kabisa Mama hakuna sababu yakurudi tena nyuma kuna nini cha maana kilicho baki kwanza zaidi ya maasi na maovu yanayofanywa kila siku twende Mama twende tukamtumikie MUNGU ili tuishi maisha ya furaha na amani.!!”
Safari ilikuwa ndefu sana na kilicho saidia ni kwamba hii ndege ilikuwa ni special kwa safari za nchi nne tu yani ikitoka Dar es salaam inaweka kituo Ethiopia, ikitoka hapo inatua Egypt (Misri) baada ya hapo inakuja Turkish alafu ndio inakuja Emirates (Dubai) ikiluka hapo ndio moja kwa moja mpaka Toronto au Ontario Canada.
Izo ndio route za hii ndege ivyo hakuna kusimama simama ovyo njiani kama daladala.
Safari ilikuwa ndefu sana maana toka Dar mpaka Toronto kwa usafiri wa ndege inatumia masaa 16 na dakika 26. Kwaiyo kwakuwa tulitoka saa moja asubuhi ivyo Canada tunaingia kesho yake saa 4:00 asubuhi ambayo kwa masaa ya America itakuwa sijui muda gani uenda ikawa usiku.
Ayo yalikuwa ni maongezi yetu Mimi na Jofu wangu, Mimi nilianza kusinzia baada yakuluka toka Turkish wakati Jofu yeye alikuwa kavaa headphones anaendelea kusikiliza wimbo wa Fanuel Sedekia Manukato.
Nikawa namsikia akijaribu kuigizia kuuimba uo wimbo, ikabidi nimwambie;
“Jofu una sauti nzuri na yenye kuvutia, yavaa uanze kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji tukifika huko Canada.!!”
“Nashukuru kwa ushuuda wako, itabidi nifanye mazoezi sana maana uimbaji sio kazi ndogo.”
“Ni kweli, ila ukimshirikisha Mungu utaweza na itakuwa kazi lahisi sana.!”
Basi safari ikaendelea huku ma afisa wa ndege wakipita huku na huko wakijaribu kuangalia usalama wa abiria wao. Yeye Jofu alikuwa busy tu na kuigizia uo wimbo, msikie kidogo;
Verse: 1.
Umeweka wimbo, kinywani mwaangu,
Bwana uliniumba, ili nikwabuudu
Nakuabudu nakuabuduu..
******
Chorus: Γ2
Wewe uketiye juuu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato,
***
Weeweeee, wewe uketiye juu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato.
Verse: 2.
Wewe ni Niko ambaye n iko,
Milele iliyopita, na milele ijayo,
Sioni chakukulisha moyo wakooo,
Badala yakukuabudu mtakatiiiifuu.
Chorus:
Wewe uketie juu ya vyote,
Sifa izi zifike kinywani mwako,
Wimbo huu ukawe manukato.
Kama sadaka ya Aberi,
manukato.
Kama zaburi ya Daudi,
manukato.
Manukato, manukato, manukatoooh
Manukato
Aleluyaah Aleluyaah Aleluyaaaaah
Manukato
Nakuomba bwana wimbo huu, ukawee, manukato
Manukato, manukato, manukatooohh!
Manukato
Aleluyaah Aleluyaah Aleluyaaaaah
Manukato.
“Woow Jofu uyoo, akika lazima umwimbie Mungu kabisa yani.!”
Nilimwambia Jofu baada yakumaliza kuimba uo wimbo wa Fanuel Sedekia kama ulivyo, Jofu alikuwa akitabasamu tu huku akinitazama.
Mwanzo nilipenda sana hii safari ya ndege lakini tulipofika anga la juu zaidi nilianza kuogopa japokuwa sio sana maana ata nikifa sawa tu Sababu nipo na Yesu moyoni mwangu ivyo siogopi kifo, maana kufa ni lazima nakuishi ni bahati.
“Mmh! Jofu kumbe America ni mbali ujue mpaka numechoka kukaa yani.!”
Nilimwambia Jofu kisha akajibu;
“Pole Mama, subiri muhudumu akipita nimweleze ili walau utembee tembee kidogo, sababu naona system inaonyesha bado kuna miles kadhaa ndio tufike Toronto..!!”
“Kwani Jofu, unajua umbali wa toka Dar mpaka huko Toronto tuendako..?”
“Ndio najua, kwanini nisijue sasa wangu!?”
“Niambie basi na Mimi.!”
“Sawa, toka Dar Tanzania, mpaka Toronto Canada kuna umbali wa 7,967miles ambazo ni sawa na 12,821Kilometers ni palefu sana.!”
“Mmh! Ongera yako bwana”
Basi baada ya mwendo mlefu na kmya kikuu kuitawala ndege yote atimaye tuliamka wote na taarifa ya kwanza kabisa alikuwa ni salam kisha tukaambiwa tumefika nchini Canada ivyo tukae tayari tufunge vyema mikanda yetu maana ndege inaenda kutua sasa.
Baada ya ndege kutua tulitelemka huku tukisalimiana hali ya hewa ilikuwa ni baridi sana, nikatazama mbele ya jengo kubwa nikaona maandishi Toronto Pearson International Airport. Nikamuuliza Jofu kuwa kumbe bado kufika Canada maana hapa ni Toronto, ila Jofu akcheka kisha akasema hapana hapa ni Canada na huu mji wao au Main City kama vile sisi kule Tanzania Dar, Arusha, labda na Mbeya.
Tulifika salama kabisa nchini Canada na baada ya mwezi mmoja tukiwa chini ya Pastor Stefansson ambaye kwa hapa Canada waumini wamempa jina la The Second Jesus (Yesu wa pili) jina ambalo yeye ulikataa katu katu kabisa maana anaamini kuwa Hakuna wakufanana na Yesu, hakuna wakufanana naye..!!
Basi tulifunga ndoa na siku ya kwanza kufanya mapenzi na Jofu yani toka nipone huwezi amini kabisa maana nilijishangaa kuona kuwa nimerudi kuwa bikra kabisa yani jamani kweli MUNGU mkubwa aisee…mume wangu mwenyewe ambaye ni Jofu alishangaa kabisa akabaki kaduwaa tu baada yakuona damu kibao huku nyuzi nyuzi za uke Wangu zikikatika yani inaonyesha ni bikra original kabisa tena ambaye sijawahi ata kujiosha na vidole
EP 68
Tulipata tabu sana kukutana kimwili, maana iyo siku Jofu alipoona nalia huku damu zikitoka aliogopa sana akanibebeleza nakunipa pole za mara kwa mara huku akisema;
“Asante Mungu kwa kuniletea mwanamke mpya binti sayuni, na kuanzia leo nitamwita Sayuni..!!’
Jofu alikuwa akijiongelesha mwenyewe wakati uo Mimi nimejishika sehemu zangu za siri huku nasikilizia yale maumivu wa yaliyofanywa na chuma cha Jofu wakati wakuvunja mpaka ya mlango wangu wa sita.
Siku ya pili tukarudia tena nashukuru maana maumivu yalikuwa sio makali ila yalikuja nakutoweka atimaye ukabaki utamu tu..!! Tulifurahi sana tena sana, Mimi ndio nilienjoy zaidi nakujikuta naanza kufurahia uzima nakuzidi kumpenda nakumsifu Mungu.
Tulifanya mapenzi mfululizo Sana na Mimi Sayuni ndio nilikuwa nikihitaji na kila tukifanya
Tunapomaliza kufanya tunapiga magoti nakumuomba MUNGU atusamehe, maisha yakaendelea pale Canada huku Pastor Stefansson akisafiri nchi mbalimbali pamoja na mume wangu Jofu nashukuru MUNGU maana nguvu za MUNGU zilimshukia naye akaanza kutoa mapepo nakuwaponya watu wenye magonjwa madogo madogo.
Baada ya muda mlefu kidogo nikafanikiwa kupata mtoto wakiume ambaye tulimpa jina Stefano ili awe wajina wa Pastor Stefansson, nilisahau kabisa kama nina ndugu Tanzania na wala sikutaka kulijua ilo zaidi nilimjua Mungu tu na kazi zake. Maana ata Yesu alimjibu Petri alipomwambia kuwa;
“Bwana, Mama na ndugu zako wanakutafuta wapo hapo nje!”
Yesu alimjibu kwa akisema;
“Mama na ndugu zangu ni wale wanao nisikiliza nakulishila neno langu..!!’
Kwaiyo ata Mimi kwa kupitia mstari uo sihitaji kuwatafuta Mama na ndugu zangu zaidi ya Mungu na wanafunzi wake.
Baada ya miaka mitano nilikuwa tayari nina watoto watatu yani Stefano, Leah, Na Kenan.
Baada ya muda Pastor Stefansson alianza kusumbuliwa na maladhi ya moyo, tulimuombea nakujitahidi kumpeleka mpaka London kwenye matibabu lakini madaktari wakasema kwa ni ngumu kuweza kupona maana maladhi yake yanatokana na umri wake kuwa mkubwa sana ivyo labda turudishe umri wake nyuma ili atibike.
Badi kwa bahati nzuri ilipofika tarehe 5/10 mwaka uo huo Pastor Stefansson aliitwa na MUNGU ivyo alilala usingizi mzito usingizi ambao kwetu sisi wateule ni mzuri sana wenye kuendeza na ambao kamwe huto hitaji kuamshwa ifikapo siku ya ufufuo.
Alipokelewa mbinguni na Baba yetu…na akaketi mkono wakuume wa YESU.
Basi nafasi yake ikachululiwa na mume wangu Jofu, na akawa anafanya ziara kila maahali ulimwenguni huku akiongozwa na roho mtakatifu. Tulisubi roho mtakatifu atuongoze au atuonyesha ndipo tuelekee huko Tanzania, kwa kifupi Mimi na mume wangu Jofu tulikuwa tumeiva sana tena kwenye lugha ya kiingereza achilia mbali watoto wengi ambao wao walikuwa hawawezi wala hawajui kabisa kiswahili.
Tulipata taarifa kuwa Mama yangu ni mgonjwa sana..na Mimi sikutaka kabisa ndugu zangu wafe bila kuona nguvu na uwezo wa MUNGU alionifanyia. Basi nikafunga safari ya ghafla Mimi pamoja na familia nzima Kama ilivyokuwa enzi za Pastor Stefansson tukafika mpaka Dar es salama kwa bahati nzuri kumbe Mama alikuwa yupo Hospital ya Agakhan kalazwa anasumbuliwa na kisukari, miguu, pamoja na macho, sawa umri ulikuwa umeenda lakini ikumbukwe kuwa kwa MUNGU hakuna Bibi wala Babu..tukaenda pale pale hospital tukamfanyia maombi akasimama mwenyewe nakutembea mpaka ilipokuwa imepaki gari..!!
Madaktari na wagonjwa wangine walishangaa Sana na wao wakahitaji kufanyiwa maombi lakini tuligoma maana sio vyema pale ni hospital na ni maahali sahihi labda pangekuwa kwa mganga hapo sawa.
Kwa tukio ilo tulipofika tu nyumbani Dada na Shemeji pamoja na mtoto wa Dada Shinje wote wakapiga magoti nakumpa Yesu maisha yao baada ya siku kadhaa ndugu zangu na rafiki zao wote wakampa Yesu maisha yao.
Jambo la Ajabu nikwamba Munah rafiki yake Jofu alikuwa nchini India akimuuguza Baba yake aliyekuwa akisumbuliwa na moyo, Basi Jofu akampigia Simu rafiki yake Munah nakumwambia kuwa ampe Simu Baba yake ili amfanyie maombi maana hakuna umbali katika maombi, Munah alifoka nakudai kuwa Jofu analeta utani kwenye maisha au uhai wa Baba yake. Lakini kwa hekima mume wangu Jofu alimsihi sana nakumwambia akubari aone uwezo na nguvu za Mungu kuwa sio za kawaida kawaida kabisa.
Baada ya hapo Munah alikibali akapiga Simu kisha akampa Baba yake ili afanyiwe maombi.
Kweli Jofu alifanya ivyo.. Dakika chache tu Munah akapiga Simu akidai Baba yake kasimama nakuzitoa mashine zote za oxygen kwakweli ilikuwa ni furaha ilioje Baba yake Munah aliporudi toka India akatoa godauni lake moja liliopo maeneo ya Tabata ili liwe kanisa kisha na yeye akawa mkristo pamoja na familia yake yote..!!
Ikumbukwe ni waarabu….!!
EP 69
Taarifa za Baba yake Munah kuacha uisilamu nakuwa mkristo (Mrokole) zilifika Pakistan ambako ndiko chimbuko la ukoo wake, kwaiyo misugiano na migongano ilianza baina yao huku bahadhi ya wafanyakazi wake toka huko Pakistan na India wakiacha kazi nakuondoka zao kurudi kwao wakidai uyu Mzee kawa kafiri.
Siku ya jumamosi alikuja Mjomba wake na Munah toka huko Pakistan akiwa kaongozana na vijana wake wakazi, hakufikia kwa ndugu yake ila alifikia hotelini.
Na siku ya jumapili tukiwa ibadani Mimi nilikuwa pamoja na mume wangu Jofu tukisubiri tupewe nafasi ili tuwaage maana kesho ndio tulitakiwa kurudi Canada Sasa sijui ni kitu gani maana Jofu aliwaambia watoto wetu waende nje kuleta zawadi zilizokuwa ndani ya gari la Baba yake Munah kweli Stefano alienda na wadogo zake wote wawili Kenany na Leah wakaenda nakuleta briefcase ya ajabu..!! Kila mmoja alishangaa maana iyo Briefcase hatuitambui kabisa kisha watoto wetu wakaenda tena nje ambako ata sikujua walifuata nini huko nje. Tukiwa tunasubiri kuona labda kuna mgeni wamempokea iyo briefcase, na sasa wamerudi kuchukua izo zawadi. Lakini hali alikuwa tofauti kabisa, maana aliingia kijana mmoja akiwa kavalia kanzu na skafu aliyoizungusha shingoni mwake mpaka mdomoni akasema;
“ALAHU AKBAR..!!”
Kisha nikamshuudia akitoa remote nakubonyeza Twiiiiiiiiiiiiiiihh..!!!
Mara ghafla ulitokea mlipuko mkubwa sanaπ₯π₯π₯.BUUUUUUUUUUUUUUUUHHHπ₯π₯π₯π₯ na kanisa lote likashika moto wakati moto unaendelea kuwaka huku ukiwa umeenea kila maahali hapo mara nikamuona mume wangu Jofu akiwa na mabawa akanishika mkono na Mimi niligundua nina mabawa pia..!!πΌπΌ kisha tukaanza kupaa kwenda juu mbinguni na watu wangine nao ivyo ivyo..!!
Baadhi ya wenzetu walibaki wakilia nakusaga meno maana moto uliwachoma vibaya sana pale kanisani tulipaa watu wachache sana nasikitika Dada yangu na Shemeji walibaki wakilia nakusaga meno wasijue nani atawakoa toka kwenye lile dimbwi la au ziwa la moto.
Tulifika mbinguni tukamuona Pastor Stefansson akiwa pamoja na Yule mtume wa Yesu Stefanie aliyeuwawa kwa kupigwa mawe mwaka 106 AD. Tukasogea na kupokelewa huku watu wote wakiimba nakusujudu. Wakiwa na mavazi meupe na malefu yakupendeza sura zao zinawaka nakung’ara kama jua. Sote tulikuwa sawa hakuna mlefu wala mfupi mweupe wala mweusi, mnene wala mwembamba, mzuri wa sura wala mmbaya, kionhozi wala hasiye kiongozi, mkubwa wala Mdogo, tajiri wala maskini, msomi wala hasiye msomi. Hakika MUNGU ni wa ajabu sana maana hakujulikana mwanaume wala mwanamke, hakika sote ni sawa. Hapo ndio nikaamini kweli binadamu tunaishi kwa kubaguana sana.
Nikaomba nitazame kidogo duniani, ndipo malaika mmoja akanipeleka sehemu mahalumu kabisa yakutazamia duniani. Aisee nilipotazama duniani kwanza nilikutana na halufu kali na mbaya ya uozo wa binadamu na maovu yao, nikajikaza nikaendelea kutazama. Nilijikuta nalia Sana nilitamani nirudi kuwachukua watoto wangu ili wasiingie kwenye mtengo na matamanio ya muovu ibilisi shetani, lakini Yule malaila akasema haiwezekani kabisa maana imeandikwa kuwa KILA MMOJA ATABEBA MSARABA WAKE MWENYEWE.
Nilipoendelea kulia nakumsihi uyu malaika anipe nafasi iyo niwafuate watoto wangu, alikataa kabisa kisha akafunga na ile sehemu kisha akaniacha Mimi nalia yeye akaondoka zake. Punde kidogo nikamuona Pastor Stefansson akiwa Pamoja na Ester pomoja na wateule wangine,waliponifikia Pastor Stefansson akasema;
“UMECHELEWA HAUWEZI KUZUIA, MAANA IMEANDIKWA KUWA NI LAZIMA KILA MWANADAMU APITIE MAJARIBU NA AYASHINDE YEYE MWENYEWE KWA KUJIKANA NAKUBEBA MSARABA WAKE MWENYEWE NA AMFUATE YESU KRISTO. KWAIYO WEWE SAFARI YAKO IMEISHA HAPO NA KITABU CHAKO TAYARI KIFUNGWA MAMBO YA DUNIANI AYAKUHUSU TENA.”
___M….W….I….S…H…O___
“Shukrani za dhati kwa rafiki zangu niliokuwanao Pamoja mwanzo wa hadithi yetu mpaka leo tumefika tamati, tusameheane kwa makosa madogo madogo ya kibinadamu.


