πππππ ππ¨ππͺπ π¬π π ππ πͺππ‘ππ¨, ππππ©π¬π’π‘ππππ‘π¬π π‘πππ¦ππ πππ π π πππ ππππ, π‘πππ‘π π¬π π‘π¬π¨π ππ π¬ππ‘ππ¨ π πͺππ‘π¬ππͺπ
EP 1
“Mke wangu!, kuna mwanamke nilimpa mimba.” Daudi alimwambia mke wake Sophia. Kabla ya kufika nyumbani usiku huo, aliamua kusema ukweli baada ya kujaribu kuuficha kwa mda sasa.
Alijua mke wake asingependa kusikia wala kupendezwa lakini aliamini ni jambo bora zaidi kufanya hivyo kwani ukweli siku zote humuweka mtu huru.
“Nilitenda kosa lakini nitamwambia asitoe mimba yangu ili nami nipate mtoto . Vipimo vinaonesha kwamba, ni mtoto wa kiume. Nimekuwa nikitamani kupata mtoto na unajua hatujaweza kupata mtoto tangu tufunge ndoa miaka kumi iliyopita. Nimevumilia vya kutosha na niliamua kujaribu nje hatimaye nimepata. Tafadhali, bado nakupenda. Nisamehe Sophia.β Dauduli alisema. Sauti yake ilisikika kwa upole na uangalifu mkubwa.
βSawa. Hakuna shida. Ninafuraha kwa ajili yako. Hongera sana!β Sophia alisema huku akimkumbatia mumewe na kutoka sebuleni kuelekea chumbani ambako alilala kwa amani.
Daudi alishangaa kwanini mkewe hakumkasirikia kuhusu ujauzito huo. Usiku huo, hakuweza kulala kando ya mke wake. Alilala kwenye kochi pale sebuleni kwa sababu alishindwa kuelewa mtazamo wa mke wake. Daudi aliogopa kwamba mke wake anaweza kumchoma kisu kama atalala naye kitanda kimoja.
βNi mwanamke wa aina gani anaweza sikia mumewe kampa mimba mwanamke mwingine na kunyamaza juu ya jambo hilo? Kwa nini hakukasirika? kwa nini hakuuliza swali lolote kuhusu msichana huyo? Kwa nini hakujibu kwa hasira? Hii inatisha sana, ni hatari sana kwangu.” Daudi alijisemea huku akiwa amejilaza kwenye sofa huku akitazama juu ya dari jeupe. Kuanzia usiku huo, Daudi aliamua kujiweka mbali na mke wake Sophia hadi ahakikishe kwamba hatomdhuru.
Sophia alimwamsha mumewe asubuhi kwa kifungua kinywa ambacho alikiandaa kwa upendo mwingi kuliko alivyokuwa akifanya siku za nyuma.
βMpenzi habari za asubuhi. Fanya haraka ule ili uende kazini.β Sophia alisema huku akimpigapiga bega mumewe.
βNa kwa nini ulilala hapa usiku? Nilikuwa nikikungojea kitandani. Nilikukumbuka sana kitandani mpenzi wangu.β Sophia alisema. Akatoka sebuleni. Alikuwa tayari amevaa nguo za kazi kwani yeye ni mwalimu.
Alipotoka, mume wake alienda chooni moja kwa moja na kumwaga chakula alichokuwa ameandaliwa.
βNinawezaje kumwambia mke wangu kwamba nilimpa mimba mwanamke mwingine na hakuwahi kusema neno la hasira au kunihoji kuhusu utambulisho wa mwanamke huyo? Na ananiamsha na kifungua kinywa kitamu. Nina sababu za kuamini kwamba maisha yangu yako hatarini.β Daudi alisema, akajiandaa na kwenda kazini. Alipofika kazini alinunua chakula kantini na kula.
Akiwa njiani kurudi, alinunua pia chakula na kukificha kwenye begi lake. Alikula kwenye gari lake kabla ya kuanza kurejea nyumbani kwake. Tayari aliamua kutokula chakula cha mkewe. Alikuwa na sababu za kuamini kwamba angemuua kwa sumu ya panya.
EP 2
βKaribu nyumbani mpenzi! Nimekusubiri kwa hamu mpenzi . Ni nini kimekuchelewesha kwa muda mrefu hivi? Lazima ulikuwa na siku yenye shughuli nyingi kazini leo. Tafadhali, nilikuchemshia maji ya kuoga. Na unapomaliza kuoga, chakula kinakungoja, Nimekuandalia supu uipendayo β Sophia alisema huku akikusanya begi la mumewe na kumsaidia kuvua suti yake.
Daudi alienda kuoga, hukuakioga, aliendelea kuwaza jinsi atakavyomwambia mkewe kuwa hawezi kula chakula chake. Hilo lilikuwa jambo lisilowezekana kwa sababu alikuwa akimngoja kwenye meza ya kulia chakula. Kulikuwa na kazi kidogo angeweza kufanya ili kukwepa chakula cha mkewe.
Akilini mwake aliamini kabisa kuwa chakula hicho kilikuwa na sumu.
βMbona ananipenda sana baada ya kumwambia kuwa nimempa mimba mwanamke mwingine? Hii ni ya kutiliwa shaka sana na sio vile nilivyotarajia. Nitatafuta sababu lakini siwezi kuthubutu kula chakula chake. . Sitaki kufa mapema na Δ·izemambe namna hii.β Daudi alijisemea
Alipotoka bafuni, alichukua simu yake mezani na kutoka nje ya nyumba kwa kasi.
βNimeombwa nirudi kazini . Nitarudi hivi punde. Kuna dharura hospitalini na lazima niende kuishughulikia.” Daudi alisema.
Daudi ni daktari, kwa hiyo mke wake lazima aelewe kwamba dharura kama hii hutokea mara kwa mara.
Daudi hakurudi nyumbani usiku huo. Asubuhi alirejea nyumbani akionekana kuchoka. Alilala kwenye gari lake usiku huo.
βHabari za asubuhi mpenzi. Unakaribishwa. Lazima uwe umechoka sana na unahitaji kupumzika.” Sophia alisema huku akimfungulia mlango mumewe. Ilikuwa Jumamosi, hivyo alikuwa nyumbani. Daudi alienda kitandani moja kwa moja na kulala.
Jioni, Sosphia alimuandalia mumewe sahani nyingine ya supu ile ile lakini alianza kuigiza tena, akijaribu kutoka kwa haraka nje ya nyumba lakini Sophia alifunga mlango.
“Nimegundua kuwa hauko katika hali yako ya kawaida tangu juzi. Shida ni nini?” Sophia aliuliza
βHakuna tatizo!, niko vizuri. Ninakabiliwa na majukumu kazini. Nahitaji muda wa kuweka mambo sawa.β Daudi alidanganya.
“Acha!, Unanidanganya. Wewe ni mshauri daktari! una uzoefu wa miaka kumi na tano. Hakuna shinikizo kazini ambalo linaweza kukufanya ukatae chakula cha mke wako. Au unafikiri sikujua ulimwaga chakula nilichokuhudumia juzi? Umekuwa ukikwepa chakula changu kwa makusudi. Unafikiri nitakuwekea sumu? Au, ni kuhusu msichana uliyempa mimba? Mpenzi wangu! Sina shida hata kidogk kuhusu hilo. Nimefurahia kabisa juu yake. Nina furaha sasa tutakuwa na mtoto. Kwa kweli natamani na itapendeza kama utamleta aanze kuishi hapa nyumbani. Itafurahisha sana!β Sophia alisema.
Daudu alishtushwa zaidi na pendekezo la mke wake. Alitarajia angekasirika na kuondoka nyumbani na hatimaye kumpa nafasi ya kumuoa msichana aliyempa ujauzito, Lakini majibu ya Sophia kwa jambo zima yalimshangaza.
Aliogopa zaidi ..!
“Labda anataka kutuua wote pamoja na mtoto ambaye hajazaliwa.” Daudi alisema moyoni.
βMpenzi! Umesikia nilichosema?β Sophia aliuliza huku akimrudisha mumewe kwenye ukweli.
βNdiyo nimekusikia. Nitalifikiria.β Daudi alisema. Siku iliyofuata, alimtaarifu Juliet kwamba aje kuishi nyumbani kwake.
βMkeo amehama? Sitaki kushare mme na mtu yeyote.β Juliet aliuliza.
βCha kushangaza ni kwamba, mke wangu amekubali sisi sote tuishi pamoja. kiukweli mapenzi aliyonionyesha tangu nilipomwambia habari hii, yamenishangaza. Sijala chakula chake tangu siku hiyo. Sitaki kufa kwa sumu ya panya. Tafadhali, nisikilize, Kuwa mwangalifu sana unapohamia nyumbani kwangu, usile chochote atakachokupatia, vumilia mpaka nipate nyumba nyingine kwa ajili yetu.” Daudi alisema.
Siku iliyofuata, Juliet alihamia nyumbani kwa Daudi….
JE ILIKUWAJE?….
INAENDELEA


