“UNACHEZA NA WATOTO WA WAKUBWA” – POLISI ALALA CELO USIKU MZIMA, BAADA YA KUMKAMATA MTOTO WA MBUNGE KWA KUVUNJA SHERIA ZA BARABARANI
Katika Kaunti ya Nakuru, afisa wa trafiki aliripotiwa kujipata katika hali ngumu baada ya kumsimamisha kijana aliyekuwa akiendesha gari ovyo na kutofuata sheria za trafiki.
Afisa huyo alikuwa katika kazi ya kawaida alipoona gari hilo likitembea kwa njia ya kutiliwa shaka na kuamua kulisimamisha kwa ukaguzi. Inaarifiwa kuwa afisa huyo hakujua kuwa kijana huyo ni mtoto wa mwanasiasa mkuu nchini.
Baada ya kumsimamisha, askari huyo anadaiwa kumwamuru dereva atoke nje ya gari na kisha kumwagiza aende kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Alipofika kituoni, inasemekana afisa huyo alichukua funguo za gari na kumfunga pingu kijana huyo na kumweka kwenye selo.
Hata hivyo, ndani ya dakika chache, mkuu huyo wa kituo cha polisi anadaiwa kupigiwa simu na viongozi wakuu wakiamuru mtuhumiwa huyo aachiliwe mara moja.
Baada ya kijana huyo kuachiliwa, alidai funguo za gari lake. Kwa bahati mbaya, afisa huyo hakuwapata, kwani walikuwa wamepotezwa. Hali hii inaripotiwa kusababisha mvutano zaidi, na mambo yakaongezeka haraka. Baadaye afisa huyo alijipata matatani na kufungiwa katika seli kwa usiku huo.
Hata hivyo wakenya wengi wamekashifu tukio hilo wakisema kwamba sheria zinafaa kutumika kwa usawa kwa kila mtu bila kujali hali au mali.
Walisema kuwa hakuna mtu anayepaswa kutendewa tofauti linapokuja suala la kuvunja sheria za trafiki, na haki inapaswa kudumishwa kila wakati katika mfumo wa haki.

