Isaya Yunge Avunja Rekodi na Kuweka Heshima Kubwa huko Kenya
ANGALIZO: Hakuna ukweli au uthibitisho wowote rasmi kuhusu hii Taarifa, maana Isaya Yunge hajawahi kutaja kiasi chochote cha mahari hadharani na suala hilo limebaki kuwa siri ya kifamilia. Kwahiyo, tambua kwamba unakwenda kusoma Taarifa ambayo imetoka kwenye Mitandao ya kijamii.
Chanzo: VOICE OF JUBA
Mwanamume wa Kitanzania alipa Shilingi bilioni 7 za Kenya (Bilioni 140 Tsh), helikopta mbili na basi ili kumuoa binti wa Rais
Mfanyabiashara wa Kitanzania, Isaya Yunge, aliyemuoa Charlene Ruto—binti wa Rais wa Kenya William Ruto—anasema alilipa mahari ya Shilingi bilioni 7, ikiwemo helikopta mbili na basi la abiria (nganya).
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kenya, Yunge pia alidai kuwa alimnunulia Charlene pete ya dhahabu yenye thamani ya dola za Marekani 433,000.


