MJEDA USIFANYE HIVYO MI NI MDOGO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 11
Marco alicheka, nakumwambia mama ake, mama achana na kaka apo alipo anamwaza Diana tu, anahisi huelewi chochote, acha tukahalalishe tu, mimi nashauri ata ndoa mngewafungisha tu anaweza kusoma akiwa na cheti kabisa, inawezekana, make uyu kijana wako sijui kama ataweza kujiamini, hasa akifika chuo, Max alijibu siwezi kumpeleka chuo bila ndoa apo ata aongee nani sitaelewa, Advance naweza nikajikaza ila chuo usalama ni mdogo, wote walicheka…
Upande wangu nililala, na ule uchovu, nakuja kuamka, Saa 8 wenzangu wameshakula cha mchana,niliamka nikaenda kula, Anna akaniuliza kama tumeelewana na kaka ake, nilitabasamu tu nakukubali, alifurahi mwenyewe, akasema saiv atakuwa ananiita wifi, nilicheka, tukaanza kupiga story simu ya Anna ikaanza kuita alikuwa ni Max Anna akasema pokea tuone kama anajua kututofautisha, nilikubali wazo la Anna nikapokea, “haloo Anna mke wangu bado tu jamani hajaamka? Kamuangalie basi anatakiwa ale muda umeenda sana, nilijikaza kucheka nikajibu bado, akatulia kwanza, afu akaita, Diaa, nikakataa mi Anna, akajibu “naijua sauti ya mke wangu kuliko ata ya kwangu, mbona umeamka ata hujanitafuta?…
Tukaamua kumvuruga nikampa Anna simu, ajajibu , kaka jamani unaota au? Anna acha kunizingua nilikuwa naongea na Dia saivi, usinichezee akili yangu mpe simu basi wifi yako, tukasikia uko wanamcheka mama na kaka Marco, ikabidi nikate tusiendelee kumsumbua akapiga tena nikaamua kumtumia txt kwenye simu yangu, akajibu, Max sio vizuri unaongea mbele ya mama ivo ujue, “Dia mke wangu kwani mama hajui nini? Ila sawa nikifika nitatafuta sehemu tuongee, vipi lakini uko sawa saivi?..
Ndio nimeamka poa, tulielewana nikamuacha, walifika nyumbani, walipokelewa vizuri mno, hawakusema kama wanaenda kufanya nini walitoa tu taarifa wanaenda, mama na baba waliwapokea na kuwaandalia walikula ndipo wakaanza kuongea, mama alisema ukweli watoto wameshavuka mipaka wanataka kutengeneza undugu wa damu sasa, mwanzo baba alichukia kujua tayari Max kashafanya yake, ila waliongea na kukubaliana tu sasa wapokee mahali, na ndoa ipite ya kimya kimya, wasituache bila ndoa, baada ya kumaliza shule tutafanya sherehe…
Walikubaliana na kupokea mahali, walitoa na zawadi walizopeleka mama akanipigia kuuliza kama nikubali kuolewa na Max sikujua kama wameweka sauti ila nikakubali bila ata kujizungusha,Max alifurahi nilivyojibu, make waliweka kwa sauti ili wote wasikie, mama akasema niliweka sauti ili wote wasikie jibu lako kabla hatujapokea mahali yako, niliona aibu nikakata simu, Max alinitxt mke wangu asante, sema unasauti nzuri sana Dia wangu….
Chapter 12
Walimaliza mambo ya mahari wakapanga tarehe ya ndoa, walikaa nyumbani siku tatu, ndipo wakaanza safari ya kurudi nyumbani, siku io nilikuwa na furaha mno, mpaka Anna akajua leo nimeamka vizuri,nilienda na Anna sokoni, nikaingia mwenyewe kupika, nilijipinda haswaa, kitu kikatoka kila mtu anakisifia, nilitoa nyama kidogo zile anazopenda Max, nikaziweka kwenye kahotpot, nikaenda kumfichia chumbani kwake, kumbe Anna kaniona, nilivyorudi tu , akanidaka nakuona wifi, umeamua kumfichia nyama mme wako, nilijikuta naona aibu tu apo ilikuwa bado kama lisaa limoja tu wafike, nilikuwa na heka heka, nilikimbia kuoga, nikaanza kuvaa kila nguo naona hainikai, Anna aliingia, akaanza kucheka tu, akaniomba anichagulie, make anauhakika nitamaliza begi zima na bado sitapata nguo, alinichagulia kigauni chekundu, kilinikaa mno, akaniandaa nilipendeza mno, miguu tulivyoenda sokoni nilipita nikasafisha kabisa, nikapaka na rangi, yani nilikuwa smart mpaka mwenyewe, nikawa najitamani, Anna alinisifia, ila akanishauli nisivae kwanza hio gauni, huenda kukawa na mtoko ndo niivae, saiv nifunge tu khanga na kishart, nilikubali japo kwa shingo upande…
Chumbani nako nilipapanga haswaaa, muda hakukukawia, wakawa wamefika,nilikuwa na ham yakumuona Max wanguπ«£, ila aibu nikabaki namchunguria tu wanavyoingia, aliangaza hakuniona, wakaanza kumcheka, nikaona katoa begi aingie nalo ndani roho ikanisunta, dada wakazi akaomba amsaidie akakataa, ikabidi tu nijitokeze, alivyoniona alisimama, nilifika nikavuta begi kwa aibu, afu ata bila salamu nikaenda kwa mama kwanza kumsalimia, Marco akawa anacheka yani uyu shemeji yangu kwakucheka ni kiboko…
Aliniambia shem usithubutu kunisalimia, uko ulikotoa hilo begi hali sio shwari wahi tu kabla hajapasuka, niligeuka nimtizame, akawa kaingia ndani, ilibidi nimfate, nikakuta yuko anazunguka tu chumbani na hasira, nilimkumbatia kwa nyuma, nakuanza kumuuliza za safari, “saivi ndo umeniona sasa, amna Max jamani, nilitaka nipate chance yakuja chumbani kwako, Max alinikata jicho, nikamkaribisha maji ya kuoga, akaniuliza ” tunaenda wote? Nilicheka nikamwambia hapana mimi naenda kukuandalia chakula, tukiwa bado tunaongea mama alipiga simu kwa Max, ikabidi apokee “Max tunanjaa sisi naomba msubili ata usiku aisee, “mama mbona mnatuwazia sana? Anakuja alikuwa ananijulia hali tu…
Nilivyosikia ivyo nikaona aibu, nikatoka nimefika jikoni nikamtumia txt Max, acheki nyama nimemfichia, alifurahi, akala kwanza ndo akaenda kuoga kaja mezani pia akala, Anna si akatoa siri, nikabaki naona aibu tu, baada ya kula ilibidi wapumzike,Max aliomba niende anamaongezi na mimi, ilibidi niende, kufika akanambia tulale amechoka leo ilikuwa zamu yake kudrive, Max we lala mimi nikacheki movie, alinizuia ikabidi nikubali, alinikumbatia tukalala, Marco kaamka akawa anatafuta pc, yakwake imezingua, akaja mpaka chumbani kwa Max bila hodi, alivyofungua tu akatuona, sema tulikuwa na nguo, alitoka mbio, kakutana na mama ake, akampamia mama akamuuliza na wewe vipi tena?, alikuna kichwa na kujibu, niliingia kwa kaka bila hodi…
Mama alimtizama, kisha akamwambia, ndo ukome, yani Max kama hawajatiana mimba awa sijui Mungu atusaidie tu naziona dalili za kuitwa bibi na ujana huu π,Marco alicheka akamwambia mama ake mama kwa ujana gani ulionao, apo sio tu kuitwa bibi, ujiandae kulea mkamwana atakuwa shule π, mama alimtimua Marco, akaendelea na yake, uku anawaza kuitwa bibi uku bado hajazeeka…
Chapter 13
Upande wetu uku nilikuja kushtuka ni usiku tayari,nilimtoroka Max nikarudi chumbani kwangu, amekuja kushtuka, akaja chumbani kwangu, nilisahau kufunga hivyo ikawa rahisi kwake kuingia, alikuta nimelala, akaunga na yeye, nilishtuka make sikuwa nimesinzia, nilimuuliza kulikoni, akajibu leo hataki kulala mwenyewe kanimiss sana, nilikosa cha kujibu nikatulia tu, ilikuwa kulala lakini akaibua mengine,alinipa na ubuyu wa ndoa, na tarehe waliyopanga, mimi sikuwa na pingamizi…
Tulimaliza tukaoga na kulala apo tuko hoi, saa ngapi tusichelewe kuamka, mama na Marco wakawa wanajua nipo chumbani kwa Max, hivyo hakuna alieenda ata kugonga, tumeamka saa tatu asubuhi watu wote wako seblen, tukawaza Max atapitaje apo, na anahitajika kazini saivi, simu imepigwa, alijikaza akatoka watu wote wakashangaa, katokea chumbani kwangu, mimi sasa nikabaki ni aibu tu kutoka nashindwa…
Nilikaa nikatoka mchana watu hawapo sebleni, siku hazigandi nikaanza maandalizi ya ndoa, siku hio hio, tumetoka tu kanisani kufunga ndoa, matokeo yakatoka, apo tulikuwa hotelini, niliogopa ata kuangalia, ilibidi, Max aniangalizie uku ananituliza, Mungu alikuwa upande wangu nilifaulu, Max alisema leo ni siku nzuri sana, alinipa zawadi ya kufaulu, akaomba nijitahidi nikasome, “saivi wewe ni jukumu langu, ujue kabisa mmeo napambana uku ili usome, sasa kalete utani..
Nilikumbatia nakumahidi nitafanya vizuri, alifurahi nyumbani pia walicheki matokeo mimi na Anna wote tulifaulu, mama mkwe wangu akawa anaomba tu Mungu nisiwe na mimba, alimpigia simu Max kumsisitiza amwagie nje,Max alicheka akasema mama usijali niko makini,mimi natumia dawa za kuzuia nisimpe mimba, hivyo kuwa na amani, apo mama akatulia, na mimi nilikuwa na hofu nikapata amani, nakuachia yote, rasmi nikaanza kuishi na Max nyumbani kwake, alikuwa likizo likizo ikaisha akaanza kuwa bize adi nikawa nachukia, simu kwa siku anaweza kukupigia mara moja tu, au asikupigie mtakutana usiku akirudi,nikinuna ananiletea vizawadi kesi imeisha, nilikuwa na panic mno, natamani anichatishe kama mwanzo, leo alinikela nikamtumia sms umenikwaza leo, hakujibu jioni karudi na chocolate, nikamuuliza Max hutaki kujua umenikwaza nini? Akajibu najua ni kaujinga tu ndio maana sijauliza, nilichukia…
Chapter 14
Nikamwambia Max sikupendi nakuchukia, alitabasamu akajibu, huo sasa si uongo mke wangu, ata hakuongeza neno akasepa kuoga, nilichukia, nilimkaribisha chakula uku nimenuna, alinibeba toka chumbani adi sebuleni uku ananilisha chocolate kwa mdomo, tumefika sebleni, akanipakata nakuanza kunilisha uku anakula, hakuwa anaongea kila nikitaka kuongea nawekewa chakula mdomoni…
Alihakikisha nimemaliza kisirani changu, akaomba na tamu nikampa π, nishasahau kila kitu, kesho yake alienda kwa mama mkwe akamuomba ushauri, ikiwezekana Anna aje kwangu ili anisaidie kuwa bize niache kumsumbua, mama alimshauri anifungulie biashara niwe bize Anna hatanisaidia bado nitamsumbua, walielewana, akaja kuniuliza biashara gani naweza fanya, nikaona bora ata nifanye biashara,mambo yakulingiwa nishachoka mimi, nakaa ndani kama utumbo, nilimwambia anifungulie hotel, alikubali, akajipiga piga, na mkopo juu, akanifungulia hotel japo haikuwa kubwa sana ila ilikuwa ya tofauti na ya viwango sana, tofauti na zile za mama ntilie za mtaani hii ilikuwa hotel ya kati, wapishi nilichukua wapishi haswaa na sare tukaandaa yani ilikaa kishua mno, nilianza kuwa bize, ata kumpigia simu nikawa sikumbuki…
Jioni narudi nyumbani nimechoka ata sina kelele, alifurahi mwenywe, akawa na amani ila siku sijaenda kazini kunakucha upya, muda wa kwenda shule ulifika, niliweka msimamizi, nikaenda shule, mimi na Anna tulipangiwa shule tofauti, hatukuwa na jinsi, ilibidi kukubali, nilisoma team ikaisha nikarudi kuhudumia ndoa, kulikuwa na ugumu, ikabidi likizo nisirudi kwangu ili akili ibaki kwenye kitabu, nikawa naenda ukweni, mme wangu alikuwa muelewa japo kuna muda yanamshinda anakuja, hatimae nilimaliza form 6, nikarudi kusubiri matokeo…
Tuliludi nyumbani tukafanyiwa Graduation ya pamoja mimi na Anna, lakini Anna alionekana kutokuwa sawa, nilihisi baada ya sherehe nitakaa nae chini na kumuuliza akadai anamimba, na kibaya zaidi mwenye mimba kaikataa, nilichoka nikataka kumjua, akanitajia ni rafiki yake na Max, nilikasirika, tena aliwahi kunitambulisha kidem chake kingine tu, niliumia, mno, nikajikuta nalia, nilimwambia tu Anna kuzaa sio kilema huenda sio ridhiki, tulishauriana na kuona ni vyema aje kuishi kwangu kwa muda, kabla nyumbani hawajajua…
Tuliwaza ata tukilazimisha uyo jamaa kumuoa haitasaidia kitu, ataishi kwenye ndoa ya mateso tu, tulianza kuishi wote, ila jamani siri na ndoa haijawai kuwezekana, saa ngap nisiseme kwa mme wangu, Max alikasirika, akavaa nguo usiku huo huo akamfata rafiki yake mimi ikabidi nimfate pia, kufika, wakaanzisha ugomvi, Rameck akamjibu Max, “Max inakuuma ee, uchungu wa dada umeona unavyouma? Unakumbuka wewe ulichomfanyia dada angu?, alikupenda alijitoa lakini kila siku ukawa unamwambia uko nae kimakosa unamtu wako, alijitahidi kukupenda, ila wewe ukaishia kumuumiza na ulivyomkatili alivyobeba mimba yako ukamtoa dada angu mimba unajua niliumia kiasi gani?..
Upande wangu kusikia ayo nilihisi kizunguzungu ana akanidaka tulisikiliza bila Max kujua kama tupo hilo eneo…
Chapter 15
“Rameck ivi unajitambua kweli, kwanza labda nikusaidie tu, mimi dada ako sijawai kumpa mimba, mimi nilichoma kizuizi ili nisimpe mimba, na kingine toka alivyonilewesha ili nilale nae, sikuwahi kumpenda na nilimwambia ukweli mimi tayari nina Dianna tu kwenye moyo wangu, aniache, lakini hakuwa muelewa aliendelea na mitego yake, uku anawanaume wengine, alivyobeba mimba nilimchana mimba sio yangu, alienda kutoa kwa hiyari yake, na kumuoa mimi sikumwahidi,Rameck hakuelewa alijibu tu, uyo mdogo wako na mimi hanihusu hivyo tumemalizana, alivyoumia wakwangu acha na wakwako aumie, aisee tuliondoka kimya kimya, niliona kabisa Anna anavyoumia…
Tulirudi nikaamua kulala nae, Max alirudi akanikosa alinipigia simu nikamwambia niko chumbani kwa Anna hayuko sawa nahofia kumuacha peke yake,alielewa kulikucha, asubuhi nikaenda na Anna kazini nikajitahidi kumweka bize,alijikaza siku hazikukawia mama mkwe alijua alilia sana, nakumlaum Anna, Max aliingilia kati na kumtetea mdogo wake, nakudai yeye ndo chanzo, alimsimulia mama ake bila kuficha, mama akaelewa japo kwa tabu sana…
Tuliamua kulea mimba, mda wa chuo ulipofika tulienda chuo kimoja, Anna alinawili mno na ile mimba yake ilimkubali, akaanza kinenepa alikuwa kembamba, akapata shep moja matata, uso ukanawili, Rameck akawa anamkejeri, ikabidi avunje line tusajili nyingine kumbrock tuliona haitoshi, akiwa na tumbo lake saa ngapi, mtoto wa kishua asimpende na mimba yake, alikuwa anatusumbua, apo na mimi sijielewi kumbe tayari na mimi nimeshajazwa, jamaa kashatoa kizuizi chake…
Nimekuja kushtuka naona tumbo linaongezeka, mwanzo nikahisi huenda kitambi tu, ila kikawa kinazidi, kwenda kupima mimba miezi 5, mama mkwe alipewa taarifa akasema naona mmeamua sasa umu ndani ni mwaka wa kulea wajukuu, wasomi mkasome, tulicheka tu, Max alikuwa bize mno nikimuuliza anasema anapambana sana kwa ajili yangu, majukumu ni mengi inabidi apambane mno, sikuwa na ujanja zaidi ya kukubali tu, make maendeleo nilikuwa nayaona, alikuwa anafungua biashara anapambana nje na kazi yake…
Uku mtoto wa kishua akawa analia ashajua Anna katelekezwa, alipambana tukashauriana tumpe sharti la kwenda nyumbni kutoa mahari kama kweli anampenda Anna, kweli wifi yangu akampa jibu Martin, tukajua ndo basi atakimbia hamna mwanaume atakubali kupeleka mahali kwa mjamzito tena mwenye mimba sio yake, lakini ikawa tofauti kabisa…
Martin alimwambia Anna kesho atoe taarifa mahari inapelekwa, hatukuamini tukapuuza tu, tukiwa zetu bize kesho yake nyumbani, tukapigiwa simu nyumbani kuna ugeni, kwanza tukatazamana, mama akagomba kwa nini hatukutoa taarifa tunawatia aibu, ilibidi nijiongeze, nikamwambia mama anipe idadi ya wageni tuchukue chakula hotelini kwangu, mama akanipa maelekezo, tukapitia chakula ,Max akaja kutupeleka, bwana kama utani Martin akatoa mahali tena ml 10, hatukuamini, mimi nimetolea ml5, na bikra yangu,nyie π, Anna hakuamini alifurahi, wageni waliondoka…
Penzi likaibuka, tukapata wakutudekeza tukiwa chuo make ghaidi yangu haiko romantic kabisa, iko bze tu π,Martin alikuwa anahakikisha usalama wetu chuo, afu nyumbani akapewa Max jukum, ilibidi kwanza nicheke, Max akauliza kwa nini nacheka, nikajibu yani mimi tu huwa unasahau kama nakuhitaji, aya tumeongezeka ndo utaweza kweli?, ” tatizo mnautoto, nikajibu umeona nilijua tu hii kazi baba huiwezi wewe, kudekeza muachie Martin tu, saa ngap Max asinune….
Inaendelea….π₯

