MJEDA USIFANYE HIVYO MI NI MDOGO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 16
Mmh Max nikapata kibarua tena cha kumbembeleza, alinishika akaniambia “Dia mke wangu, usije ukaibiwa uko kisa unaona sikujari, mke wangu majukumu tu lakini mwenzio sina ata jeuri yakukuacha, usije ukawaz ujinga basi, nilicheka nikamwambia sasa mme wangu na hili tumbo kweli nani atanipenda?
“Dia usinipange, mimba sio sababu kina Martin wapo wengi tu, mwanzo nilihisi ukiwa na mimba nitapunguza wasiwasi ila toka Martin alete mahari, nimekuwa naishi kwa hofu hujui tu, make sijui wangapi na wewe wanakumendea uko, ila kuwa na mke mzuri jau basi tu, nilicheka make alikuwa anaongea kwa masikitiko, Max mme wangu sio rahisi mke wa mjeda kuibiwa kila mtu anamuogopa mpaka imefika hatua saivi naogopa kusema kama ni mke wa mjeda na taja tu jina lako cheo kinanizibia ridhiki , Max alinikata jicho akakausha nikajua yameisha, kesho yake chuo akasema anatupeleka yeye mwenyewe kimbembe katoka kavaa magwanda, nikajua kabisa uyu anataka kujitambulisha, kusikia ukiwa pisi ya mjeda unaogopeka apa nimeyakanyaga, Anna akaniuliza oya vipi leo nikamwambia tulia wifi nitakupa mkanda badae acha nijaribu kusave kwanza, nilimsogelea kumshawishi avae kawaida akajitia hajanisikia…
Kibaya zaidi tulikuwa na pepa, ilibidi tuwahi tu chuo, alitufikisha tulivyofika tukashuka na yeye akashuka, akaniita, nikajua naenda kutakiwa mtihani mwema tu, nilivyosogea tu nikapigwa bonge la kiss,ndo akasepa apo ni mbele za watu,nilimfata Anna nikiwa nacheka, ikabidi nimsimulie, alicheka akasema ” wifi kazi unayo kaka anaonekana kabisa anawivu mno, ndo maana anakonda huenda anamashaka,tulicheka tukaingia kwenye pepa apo tayari maneno yashasambaa, mara nimekuja kuwatambia, maneno yakawa tofauti tofauti ata sikujisumbua kujibu, nikawa kawaida kabisa,wakati tunatoka tunakuta gari inatusubiri, Martin alimuaga Anna kisha akamsogeza kwa Max, Anna alivyomuona kaka ake na gwanda tena akashindwa kuvumilia akaanza tu kucheka, Max akawa anajitizama kuna nini haoni tatizo, mpaka tunaondoka haelewi tunachekea nini, tumefika nyumbani apo tayari miezi imeshasogea, kumbe mwenzangu uchungu ukaanza na makadrio walisema mwezi ujao, bahati nzuri mama alikuwa anatuletea matunda akakuta tunapambana kumwingiza kwenye gari, tulimkimbiza hosptal, Martin alitoa maelekezo apelekwe kwenye hospital yake, tulifata maelekezo akapelekwa alikuwa analia ikapelekea na mimi kupata hofu nikazimia, nimekupa kupata fahamu, mwenzangu kashajifungua, nilifurahi nikaenda kuona katoto karikuwa kakike karembo kenyewe, nilisahau kama alikuwa analia alikatazwa asinisimulie uchungu aniache kwanza na mimi nishushe, akawa kanidanganya na mimi nikajua ni rahisi tu, nikawajipa moyo, nikawa nimetoka nikawaacha Max na Martin, na mama, Max akaanzisha niombeeni tu kwa huu uoga wa Dia wangu sijui siku io itakuwaje, make aya tu uchungu kaumwa mwingine yeye kazimia…
Chapter 17 na 18
Martin alimtoa hofu, akamwambia asijali siku ikifika nitapata tu ujasiri, maisha yakaendelea, Rameck akapata taarifa Anna kajifungua, akatamani kuja kuona mtoto, alijikaza akaja mpaka kwa mama mkwe, na mimi ilibidi nirudishwe kwa mama mkwe kwa uangalizi…
Kagonga dada kaenda kufungua kwakuwa hamjui alivyomuaona na gwanda tu akamuachia akaingia,kafika sebleni,wote tukainuka kwanza mama hakutaka maelezo akamtimua akawa analeta ubishi, Anna alikuwa kalala aliamka akaja kuona nini, na alikuwa kaniga mtoto uzazi umemkubali na penzi ndo kwanza linazidi kunoga,Rameck alivyomuona Anna kwanza akadata, aliganda kumshangaa mpaka Anna akamuuliza umefata nini hapa? Rameck akataka kumkumbatia nilikuwa na glass mkononi nikamtwaga nayo kabla hajamfikia Anna, bahati nzuri Max akawa kafika, alimtandika ngumi mpaka mwenyewe akakimbia…
Siku zikaenda kumbe Rameck kashampenda Anna bila kujua, kisasi kikamponza, akaanza kuteseka anasumbua anamtaka mtoto wake, ilibidi baada ya miezi miwili wafunge ndoa Martin na Anna, siku ya ndoa yao, Rameck hakujua chochote, kaja kujua tukiwa ukumbuni ndoa imeshapita, alichanganyikiwa, akaja ukumbuni kufanya vurugu ila hakufanikiwa ulinzi ulikuwa mkubwa mno, mimi sasa uchungu ukaanza tena muda wangu wa zawadi, uchungu ukachachamaa nilikuwa siko sawa ila nikaogopa kusema wasijekuniambia nibaki, nikawa naumwa najikaza, nasimama na kaaa, mama alikuja kwenye harusi ya Anna, akawa anaona situlii, akamshtuwa mama mkwe, lakini tayari walikuwa wameshachelewa mimi uchungu umeshakolea, nilijikuta nashindwa kujikaza nikataka kupiga kelele, mama mkwe alikuwa kashashtukia kibaya zaidi ni mbele za watu alifanya jambo umeme ukawa umezima nikatolewa kimya kimya, mpaka hosptal, Max alishangaa, nimefika tu kitandani chupa ishapasuka ilipasukia kwenye gari, nimewekwa tu ivi kitandani, mtoto akawa kashatoa kichwa, nyie nilikuwa nimevaa wigi sijui ata nililitoa saa ngapi na ile minyoosho ya ndani nikawa nimeifumua, mpaka nimemaliza kumtoa mtoto, kichwani sifai nywere kama kichaa, Max na mama wanaingia hawana mbavu, mimi ata nguvu ya kucheka sina…
Max alinipiga picha ety kumbukumbu, akawa kamtumia mama ake na baba ake, mzee alikuwa nje kikazi hivyo hakuwa karudi bado, mama mkwe alijikuta anacheka,akaambiwa nimemletea mme, sherehe iliisha watu wakaishia hosptal, nilivyomuona Anna nilianza kumlaumu kwa nini hakuniambia ukweli, Anna akajitetea nakusema walimzuia, ilibidi mama mzazi ashike mtoto, usiku huo huo mama mkwe akanisuka za mkono angalau nikae sawa, Max alinipongeza, sijambana mtoto alikuwa na hofu kwa uoga wangu, nilimfinya, akili imkae kwanza…
Tuliagwa kesho yake Rameck kaja tena tena anaomba msamaha, tulimwambia hio ni chombo ya mtu tayari asepe, alisema atapambana alivyofatilia kujua Anna kaolewa na nani alichoka, make jamaa ni anamaokoto na ujeda wake awezi kupambana nae tena kwa hio nafasi yake ndio kabisa pale hatoboi…
Alijikuta anajuta tu nakuumia, Max alikuwa bize na mtoto kuliko mimi mpaka nikaanza kuona wivu…
Chapter 19 na 20
Nililalamika lakini haikusaidia, nikaamua kusubili tu mtoto nae achuje tuone,Anna alipelekwa kusoma nje na mme wake nikabaki naendelea peke yangu, mtoto akawa anabaki na bibi,nikawa natoka chuo napita nyumbani, hatimae nikahutimu, ikabidi tufanye na sisi sherehe ya ndoa, tulijipanga haswaa, na baba mkwe akawa pia nae karudi, Anna na mmewe walikuja nikacheki mwenzangu tayari anakibendi kingine, nikikumbuka reba namuonea huruma tu…
Sheree iliisha tulipata zawadi sio poa jamani hatukutegemea, nilipewa na Shem mme wa Anna, ile hosptal kubwa, ya ghorofa 10, aisee nikasaini kisheria kabisa sasa ni mali yangu, na uzuri nimesomea afya, mme wangu alipewa kampuni ya magari, wao walikuwa wanahama nchi, bado pesa aisee, tukalipwa kwenda nje kula honeymoon, shem akamwambia Max ili aone kaitendea haki zawadi aliyompa ahakikishe natoka honemooy nikiwa dabo, ilibidi tu tucheke, aisee, honeymoon tulienda zetu Marekani, baba mtoto nilimuacha kwa bibi yake Singida, na hivi hawana mtoto mwingine mwanangu alijua kudekezwa uko akawa kama yai…
Upande wa Rameck na dada ake walikosa cha kufanya wakaamua kukubali matokeo kila mtu akatafuta wakuziba, upande wetu mme wangu aliamua kutimiza ahadi yake kwa shemeji yake, alihakikisha siku haipiti, ata sikuchelewa ngoma ikaitika, sikuwa nataka nililalamika kanidanganya kaweka kizuizi kumbe hamna nikawa najiachia😭, alinishawishi na kunimbembeleza mpaka nikalainika nyie kuwa mwanamke sometimes ni utoto 🙃…
Nilianza tena kulea mimba uku naenda kazini, uchumi ulikubali tukawa watu flani hivi, wazazi wangu niliwaleta Dar, nikaomba nikae nao waligoma ila badae walikubali, wakaweka mpangaji, huku nikawajengea nyumba nyingine hawakutaka kukaa kwangu, ila nikaona sio mbaya muhimu wako karibu yangu, itakuwa rahisi ata kukaa na wajukuu kuliko mbali, siku hazichelewi reba nikahitajika tena, nikashusha mwingine wakike, Anna pia akaleta dume, tukawa tunapeana shift tu, saivi nina watoto watatu wakiume wawili na wakike mmoja, shemaji tangu Marco alienda zake kuoa mzungu amezaa nae mtoto mmoja, asanteni sana kwa kuwa na mimi mtunzi wenu wa Simulizi za Baby smile, ubarikiwe sana kwa support yako Mungu akuzidishie pale ulipotoa kipenzi karibu tena.
THE END.


1 Comment
mnazidi kunifurahisha2