CEO BIBI ATANIPIGA, TOA JAMANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 6
Daktari alinipima vipimo pale, kisha alimgeukia Kendrick na kumjibu.
“Vipimo vinaonesha ni mshtuko tu hakuna tatizo lingine mwilini mwake, tumechukua vipimo vyote muhimu na hakuna shida kabisa tuliyoigundua, tutampa dawa za kutuliza maumivu na unaweza kwenda nae mgonjwa wako ila mpaka ulipe bili ya matibabu na vipimo, bili ni hii hapa” Daktari alimkabidhi karatasi ya bili Kendrick aliitazama kidogo na kuiweka pembeni, mimi nilitupa macho na kuangalia, bill ilikua milioni moja, nilishtuka zilikua pesa nyingi sana ambazo uswahilini kwetu ilikua mara chache sana kuzisikia zikitajwa niliogopa sana.
“Daktari malipo ni cash au naweza chanja na kulipia
“Yes ofcourse unaweza kufanya hivyo Nesi aliekua na mashine ya benki alimkabidhi Kendrick nae alitoa wallet na kuifungua alichukua kadi yake ya benki na kuchanja alithibitisha malipo.
Daktari alimwandikia nesi dawa za kutuliza maumivu ambazo alirudi nazo baada ya dakika chache tuliruhusiwa kuondoka, nilikua na nguvu za kutembea mwenyewe kwa kujitegemea ila Kendrick aliomba kiti cha wagonjwa aliniweka hapo akaanza kuniendesha taratibu mambo kama hayo nimewahi ona kwa wenzetu tu huko india au korea nikiwa kwenye mabanda ya video uswahilini kwetu, eti leo nayaona mambo hayo live bila chenga tena nafanyiwa Magrita mimi, nilijikuta natabasamu mwenyewe, mapenzi yalinifika pazuri.
Aliniendesha mpaka eneo la maegesho ya magari alinibeba na kuniingiza ndani ya gari. “Pole sana kipenzi changu najua nimekuendesha haraka haraka ila sasa tunaenda kwangu” Kendrick aliniambia huku akinifunga mkanda vizuri ndani ya gari lake kalii. “Hapana nahitaji kwenda nyumbani kwetu, bibi angu atakua na hofu kubwa kuhusu mimi, siwezi lala nje na nyumbani sijazoea kufanya hivyo
“Ooh sawa babe, twende huko kwa bibi utanionesha njia” aliniambia na kuwasha gari yaani CEO kendrick alikua anajali kupitiliza yaani vile anavyoongea kwa upole, unapoongea wewe anasubiri umalize ndipo na yeye aongee Ilikua amaizing sana, tulienda mpaka nyumbani kwetu.
Nilijisikia vibaya baada ya kufika na kumkuta bibi angu hakua ameingia ndani muda wote alikua ananisubiri nje nije, nilijikuta nashindwa kujizuia nilimkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu sana, kwa pamoja tulitokwa na machozi, alinieleza alivyokua na hofu juu yangu nami nilimtuliza kwamba ndio nimekuja sasa.
Nilimwomba CEO kendrick nikanunue mshumaa ili tuwe na mwanga ndani kwetu hivyo yeye anisubiri hapo.
CEO kendrick alikataa kubaki pale na kunambia kwamba atanisindikiza huko niendako, nikweli tuliondoka wote maduka ya karibu yalikua yamefungwa kwani tayari ilikua saa tano usiku, tulienda mbele zaidi, CEO Kendrick alinipa pesa na kunambia ninunue kitaa cha solar kuliko kununua mshumaa unaoisha kila siku, nilimshukuru tukaelekea banda la chips tulinunua chips sahani tatu, alinunua na kuku mzima, na soda. Hivyo vilikua kwaajili yetu watatu yaani mimi, bibi na CEO Kendrick tulitembea uswahilini kwa kufurahiana na kushikana mikono wakati tunarudi, tuliruka mitalo na madimbwi ya maji machafu pasipo CEO Kendrick kulalamila wala nini, tulipita kwenye kichochoro kimoja mbele tuliona watu watatu wakiwa na mapanga, tulipotazama nyuma tulipotoka kulikua na wengine wanne nao walikua na mapanga yao, kuwatazama vizuri wahuni hao hakuna hata mmoja niliemfahamu kwa maana walitokea mtaa mwingine, hivyo Ingekua vigumu kuongea nao watuachie ili tupite
“Sikieni nyie vipwantu, mnapita kwenye utawala huu hapa wa machizi mox angusheni ushuru chini, na msaule nguo zenu sisi tuishi navyo harakaa kubabake” kibaka mmoja aliongea huku akiuparaza upanga wake ukutani walianza kutusogelea zaidi ili kutuvua nguo na kuondoka na kila kitu tulichonacho.
Mimi niliogopa lakini hofu yangu kubwa ilikua kwa CEO Kendrick niliona kwamba lolote baya litakalomkuta CEO Kendrick bhasi nitakua nahusika kwa kila kitu, tulikua kwenye wakati mgumu sana.
Chapter 7
“Hey wakuu nawapeni pesa, niambieni mnataka kiasi gani ili mtuachie hapa tuondoke hapa salama CEO Kendrick aliingilia kati.
“Hahahahaha weee kitanta sikia, tunataka kila kitu mlichonacho hapo” kijana mwingine alidakia.
“Oyaaa Duma, Pizzo na Skeleton wasauleni hao naona wanatuletea taarabu hapa” amri moja ilitolewa ili tuvuliwe nguo na kunyanganywa kila kitu. Katika hali ambayo sikuitarajia CEO Kendrick alichomoa bastola kiunoni na kuwanyooshea vibaka, hakuna hata mmoja ambae alipata ujasiri wa kutoroka, kila mmoja aliogopa kupigwa risasi ya kichwa kwani CEO Kendrick aliwatishia hivyo, aliwaambia walale chini wote, kulikua na maji machafu yanakatiza kwenye uchochoro huo, hilo hakulijali CEO Kendrick aliyakomesha kweli mavibaka yalilala huku yakigalagala kwenye maji machafu, mimi hoi kwa kucheka nilishindwa kujizuia kucheka kwakweli maana kitendo kilikua kinachekesha baada ya adhabu hiyo aliwaruhusu waondoke, na sisi tulienda nyumbani kwetu, tuliwasha kile kitaa cha Solar, bibi angu alifurahi sana akisema. anaona kama tuna umeme nyumbani kwetu, kweli maisha yetu yalikua hoi bin taabani, bibi alimshukuru sana CEO Kendrick kwa wema. wake huo wa kutununulia kisolar.
“Wazazi wako wamekulea vyema sana mjukuu wangu, natamani niwaone ili niwapongeze kwa malezi hayo mazuri” bibi angu alimwambia CEO Kendrick juu ya shauku yake.
“Hilo usijali kabisa bibi angu siku sio nyingi utaweza kuonana nao na kutimiza ukitakacho, japo kwa sasa wao makazi yao ni huko Marekani, hapa Tanzania nimebaki mimi tu nikisimamia mali na kampuni yao” CEO Kendrick alimjibu bibi waliendelea na stori zao za hapa na pale, mimi kwangu niliona raha na furaha kuwatazama watu hao wawili wakizungumza namna hiyo.
Nilijua kwamba CEO Kendrick ni mcheshi sana, swali ambalo niliamua kuliweka kiporo kwamba siku moja nitamuuliza ni iweje siku ambayo tulikutana kwa mara ya kwanza alikua kauzu na hakuonesha kucheka hata mara moja. Tuliongea hapo ilipofika saa saba usiku, CEO Kendrick aliniambia kwamba ataniombea ruhusa kwa mama Bonge hivyo nisijisumbue kwenda kazini, nitulie mpaka nipone kabisa, nami nilimkubalia kwani nilijua mama bonge mbele ya CEO Kendrick hachomoi, tulisali na bibi angu na kulala zetu, nilichelewa kuamka na muda. nilioshtuka usingizini nilisikia sauti kubwa mfano wa gari ila sauti hiyo ilikua nzito zaidi.
“Magrita magritaaa, wanataka kubomoa nyumba, wanabomoa nyuma yetu jamaniiiiiiii” bibi aliniamsha kwa nguvu huku akilia, nilishangazwa na jambo hilo, nilitoka nje kushuhudia mwenyewe, kweli nililiona greda(kijiko) nje ya nyumba yetu.
“Eneo limeuzwa kwa mtu mwingine, mnatakiwa kutoa vyombo vyenu ndani ya dakika thelathini mkishindwa kufanya hivyo tunavunja nyumba na kuhusu mavyombo yenu mtajua wenyewe Mwanaume aliekabidhiwa kusimamia nyumba yetu kuvunjwa aliongea maneno hayo ambayo yaliniumiza sana moyo wangu.
Nilipotazama vizuri nilimwona mwenyekiti wa mtaa nilimfuata na kumwomba azuie zoezi hilo la ubomoaji wa nyumba kwani hatukua na sehemu nyingine ya kwenda.
Mwenyekiti alinikataa na kusema hana msaada mwingine zaidi ya kuniletea vijana wa kunisaidia kutoa vyombo nje. Nilijisikia vibaya sana, nilimtazama bibi yangu namna alivyokua analia kwa uchungu nilijiona ni mtu nisie na msaada. nilisogea mlangoni na kuwaambia hivi.
“Mkitaka kubomoa nyumba ni kheri mniue ndani ya nyumba hii kuliko kuhamisha vitu” niliongea maneno hayo na kujifungia ndani ili wakibomoa nyumba ni bora ibomoke juu ya kichwa changu na nife kuliko kuipoteza nyumba hiyo.
Chapter 8
Bibi aligonga mlango kuniita ili nitoke nje lakini mimi sikutaka kufungua kabisa mlango, nilikua nalia sana, nikiwa tayari kwa chochote, wenye kijiko waliamua kusitisha zoezi hilo kwanza na kumpigia mnunuzi wa kiwanja ili afike mahali hapo kwani walihofia kujiingiza kwenye mauaji yangu na badae ikawa shida kwao. Ndani ya muda mfupi gari nyingine iliingia alishuka mwanaume mmoja ambae ni mnunuzi wa hiyo nyumba.
“Enhee mnashindwa nini kubomoa hii nyumba mpaka muda huu yule mwanaume alianza kufoka, kuisikia sauti yake ilibidi nitoke nje kuonana nae uso kwa macho ni mwanaume ninae mchukia kuliko binadamu wote duniani, kama kuna dhambi umitakayonipeleka motoni bhasi ni kumchukia huyo mwanaume.
“Peter mwanangu kumbe wewe ndie unaetaka hii nyumba Ibomolewe ili mama ako nikalale nje, kama mimi ndie nilikuleta kwenye hii dunia Peter nakulaani kwa jina la Mungu Bibi alianza kutoa maneno ya laana kwenda kwa baba mdogo, huyo Peter ni baba yangu mdogo yaani mdogo ake baba kabisa kabisa ila hakutupenda wala kututhamini, alikua na chuki mbaya sana juu yetu ndio sababu ya yeye kununua hilo eneo ili sisi tukose pa kuishi na kwenda kulandalanda mtaani.
“Heeee muoneni huyu, hivi huyu bibi chizi nini yaani mimi inikute laana ya mchawi, vitabu vyenyewe vya dini vinasema usimwache mwanamke mchawi akaishi yaani wewe kuishi ni makosa unatakiwa ufe wewe mchawi mkubwa, hebu burnoeni nyumba haraka hakuna kumsikiliza mtu kama atataka kufia ndani ajipeleke huko ndani tutamsaidia kufa halafu sisi ndio wenye nchi tunajua haya mambo tunamalizana vipi” Babs mdogo Peter aliongea kwa majigambo sana.
Nilipotaka kuingia ndani, bibi alinishika miguu na kunizuia, Kijiko kilisogea na kuanza kuangusha nyumba yetu na vitu vikiwa ndani, mimi na bibi tulilia sana, majirani walituonea huruma ila hakuna ambae alisogea kutusaidia, wema wawatu una mipaka, wapo waliochekea kimoyo moyo, maisha yamejaa siri nyingi, mara alifika CEO Kendrick, alikuja kwa dhumuni la kunikagua mgonjwa anakutana na huo msala wa kubomolewa nyumba, alimhoji mwenyekiti wa mtaa juu ya jambo hilo, mwenyekiti alidai kwamba mnunuzi ana haki ya kubomoa nyumba wakati wowote atakao, baba mdogo alimvulumishia matusi ya nguoni na kumtisha CEO Kendrick, kijana hakuongea sana alituchukua, mimi na bibi na kwenda wote mpaka nyumbani kwake kwani hatukua na mahali pengine pa kuelekea.
Tulipofika jumba lilikua ni kubwa sana, jumba la ndoto ya watu wengi, lilikua ni ghorofa moja, tulioneshwa vyumba vyetu ila bibi aligoma mimi na yeye kutenganishwa chumba alininong’oneza kwamba eti anaogopa kunyonywa damu, nilikua na matatizo lakini nilijikuta nacheka nikamwambia kwa sauti ya chini.
“Sasa nani akunyonye damu bibi angu mzee hivyo, kama damu wataanza kuninyonya mimi tulicheka kwa pamoja angalau kumwona bibi angu anacheka hilo lilinipa nguvu sana kwani nilitamani bibi angu awe sawa kuliko kingine chochote.
Mfanyakazi wa ndani aliandaa chakula cha mchana tulikula japo sio sana bado mawazo ya nyumba yalikua yanatuvuruga, ilipofika jioni. CEO Kendrick aliniomba tutoke kidogo tukazungumze mambo kadhaa, nilimwomba bibi ruhusa nae aliniruhusu bila shida yoyote, tuliingia kwenye gari alinipeleka sehemu moja hivi ya kununua na kula ice cream aliniuliza napenda radha gani ya Ice cream nilimjibu napenda Vanilla pia chocolate ni kitu napendelea, heee kwanini asiniletee Ice cream zenye ujazo wa lita tano tano, hapa vanilla hapa chocolate.
“Kweli wee CEO macho mazuri umevurugwa wewe sio bure hahaha nilimtania Ila kiukweli nilifurahi sana, nilipoonja radha ya ice cream hizo, zilikua tamu kuzidi ice cream zote nilizowahi kula mara chache zile za mia tano tano, ice cream nilizokula kwa wingi ni zile barafu za mia mia ambazo walitutengenezea kwa kutumia juice cola(super deep) si unajua tena sisi wa uswahilini muhimu utamu kidogo na ubaridi ule bhasi tunaridhika tu.
Nikiwa katika furaha hiyo Kendrick aliniuliza kwa
upole na sauti yenye utaratibu sana. “Natamani kujua kwanini wamelbomoa nyumba yenu pale na ni nani ameuza ile nyumba na kiwanja. Nataka kujua ili niweze kusaidia katika hili, sitaki mpenzi wangu unyanyasike na mimi nipo
Kendrick alitaka kujua kilichojificha ndani kabisa nami nilikua huru kumwelezea kila kitu ili ajue vizuri pa kuanzia.
Chapter 9
“Ili unielewe vizuri nitakupa historia pana ya maisha yangu ni wapi nimetokea, majina yangu kamili naitwa Magrita Justin Masika, niliwapoteza wazazi wangu nikiwa na umri wa miaka minne tu, wazazi wangu walikufa kwenye ajari ya gari ambalo liligongwa ubavuni na gari lingine kubwa.
Wazazi waliniacha mikononi mwa bibi angu, kaka angu aliekua na umri wa miaka kumi na baba mdogo angu ambae ni yule mnunuzi wa nyumba yaani ba mdogo Peter. Mali nyingi alizokua nazo baba ziliangukia mikononi mwa ba mdogo Peter, alishikilia kampuni kila kitu, baada ya miaka mitano, siku moja ba mdogo Peter alitufukuza nyumbani, mimi, bibi na Kaka angu Frank, kwa madai kwamba kamkamata bibi na uchawi hivyo hawezi kuendelea kuishi na wachawi kwenye nyumba yake. Tulipanga chumba kwa pesa ndogo tuliyokua nayo, baada ya muda tukafukuzwa kwenye kile chumba kodi Ilipokwisha na hatukua na pesa ya kulipa tena.
Mzee mmoja ambae aliwahi fanya kazi na babu mzaa baba miaka ya zamani, alifahamiana vizuri na bibi angu hivyo akaamua kutusaidia kwa kutupatia kisehemu tujenge kajumba ka kukaa, watu walijichangisha na kutujengea kile chumba na sebule ndio tukaanza kuishi pale miaka miwili mbeleni, kaka Frank alianza kufuatilia mali zetu kwa ba mdogo Peter kilichotokea alimroga ninavyozungumza hapa kaka Frank ni chizi yupo majararani huko anaokota maakoopoooo aaaaaaaaaah nilishindwa kuendelea kuongea, hisia za majonzi zilinikamata baada ya kukumbuka magumu tuliyopitia kwenye maisha na wakati huo kaka angu sikujua alikua anakula nini wala analala wapi. Kendrick alinituliza kwa kunibembeleza, nilipotulia aliniomba nimsimulie siku nyingine ili nisiumie zaidi lakini nilimkatalia na kumwambia nimalize ili nisilie siku nyingine atakapotaka nimsimulie. Nilijikaza na kuendelea.
“Baada ya kumpoteza kaka, bibi alinizuia kwenda kudai tena zile mali hivyo niliachana nazo kwa kuhofia kufikwa na magumu kama ya kaka Frank. Miaka ikasogea yule mzee alietupa kiwanja tujenge na kuishi alifariki mwaka jana, watoto wake wakaanza kutusumbua wanataka kiwanja chao na mwisho ndio wameuza kwa baba mdogo peter kwakua ana kisasi na sisi na hatupendi kabisa ndio maana kaamua kupanunua pale ili tukose sehemu ya kuishi, yule baba mdogo Peter ni mnyama sio binadamu kabisa nilimalizia story yangu kwa kulalama, niliamini kwamba aliyotutendea baba mdogo Peter hatukustahili kutendewa hivyo hata mara moja.
“Nitakusaidia kwa nguvu zangu zote kuhakikisha mali zenu zinarudi mikononi mwenu zote ila niruhusu jambo moja tu” “Jambo gani hilo nikuruhusu?” Nilimuuliza huku nikimtazama kwa makini.
“Niruhusu nikuoe, niruhusu uwe mke wangu wa ndoa ili niliweke hili jambo katika level ya kufamilia zaidi ili nishughulike na huyo baba ako mdogo akipanda na mimi nipande, akishuka na mimi nishuke nae mpaka tupate huo ushindi” “Unanihakikishia kwamba ushindi utapatikana?” “Ndio tutashinda katika hili niamini mimi” Kendrick aliniaminisha huku akinitazama aliongea kwa msisitizo wote.
‘Nitakujibu ila nami nina maswali yangu tena ni muhimu sana, ukinijibu kwa usahihi nami nitakujibu majibu unayoyataka” niliweka kipengele mezani. “Kwanini unataka kunioa wakati una mpenzi wako Rose yule secretary. Swali la pili kwanini siku ya kwanza kukutana ulikua kauzu sana tofauti na ulivyo sasa?” Niliweka maswali yangu kabambe mezani.
“Hee kooh kooooh Kendrick alijikoolesha nikajua hiyo mbinu ya kiume anataka kuanza kunipanga III nijae kwenye mfumo wake, sekunde zilipita hakuongea bali alidokoa ice cream yangu, aiiiiiih nilichota ice cream na kumpaka usoni, kwani oce cream si yangu kwanini anidokolee, nilijinunisha kidogo, nilipokumbuka kuna maswali nilimuuliza nilirudi kwenye hali ya kawaida na kumweleza anijibu maswali yangu, apunguze janja janja.
Chapter 10
“Nisikilize kwa umakini na unielewe nitaanzia hapa, kwenye maisha yangu huko nyuma nilimpoteza mwanamke ambae nilimpenda sana, yule mwanamke alitokea kwenye familia ambayo tulikua tunaukaribu nayo, kwa maana familia yetu na familia yao. Tangu tukiwa na miaka saba, wazazi wetu walituambia kwamba tutaoana na sisi tulijua hilo tukiwa wakubwa tutaona, tulipomaliza darasa la saba wakati wa ile likizo ndogo kabla ya kujiunga na kidato cha kwanza, yule mchumba angu akiwa na familia yake walifariki kwenye ajari ya meli, wote hakuna hata mmoja ambae alipona, kifo chake kilinisononesha sana kuanzia pale nikajiapiza sitoweka ukaribu na mwanamke yeyote yule duniani, niliamua kufanya hivyo kama kuuthamini upendo wake aliowahi nionesha huko nyuma.
Niliamini kwamba moyo wa binadamu uliumbwa kumpenda mtu mmoja tu na mimi nilimpenda yeye bhasi. Kifo chake kilinifanya kuwa mtu wa kujitenga sana, nilikua mbali na wanawake, nikawa mbali na wanaume pla, nikawa mkimya na mtu mwenye hasira sana, akili nikaiwekeza kwenye kazi. Wazazi wangu wamewahi nitafutia wanawake zaidi ya mara tatu ila niliwakataa wote kwakua sikuhisi msisimko ndani yangu, hata yule Rose aliwekwa na wazazi wangu ili kunipa ukaribu lakini imeshindikana kumpenda.
Cha ajabu siku niliyokuja mgahawani kwa mama bonge na kukuona nilihisi kitu kipya ndani ya moyo wangu, nilijikuta nakutazama kila nilipojitahidi kuacha ila niliendelea, nilipenda huduma yako, hukuninawisha nikaondoka nikajua utaambiwa uniletee tu, yote ilikua sababu ya kutaka kukuona, moyo wangu umefufuka tena, miaka ambayo ulilala imeisha nimependa tena, nimependa kwa kasi nimekupenda sana Magrita nakuomba unipe nafasi ndani ya moyo wako nawe uishi ndani ya huu moyo wangu” Kendrick alikamilisha maneno yake huku akipiga piga kifua chake upande wa kushoto ulipo moyo
“Mmmmh na Rose je atakaa wapi sasa?”
nilichokoza lingine.
“Jamani Magrita mama angu si nimekuambia
kwamba Rose hajawahi kuwa mchumba angu na
hatokua mchumba angu milele”
“mmmmh wee nidanganye tu nione mimi kama
bibi ako”
“Kaone kwanza kazuri kama nini, hata ukinuna bado uzuri wako upo” Kendrick alinisifia nilijikuta nacheka tu.
“Turudi nyumbani bibi atakua anatusubiri sana” Tulirudi kwenye gari na kupitia duka moja la simu, alininunulia macho matatu, sikuamini kama na mimi namiliki simu ya gharama namna ile, nilimkumbatia na kumshukuru kwa zawadi hiyo, alinitoa hofu na kunambia kwamba mambo mazuri yapo njiani yanakuja, niwe mtulivu ninyonye maisha pamoja na yeye, tuliingia kwenye gari na safari ilikua kurudi nyumbani, nilikuta bibi angu amelala, sikutaka kumuarnsha kumsumbua, nilioga nikiwa natazama Tik Tok niliona ujumbe kutoka kwa Kendrick, eti nikampashie maji kwani bomba la maji ya moto limeharibika. Nilimcheka kwa kumwambia iweje mwanaume aoge maji ya moto, aliniambia eti akioga maji ya baridi ataumwa ngiri, nilimwona wakishua anadeka sana, nilitoka kimya kimya chumbani kwa bibi nilichukua jagi na kupanda nalo chumbani kwa Kendrick kutanguliza mguu mbele alinivuta mkono wangu alinigeuza kiuno na kunibambia, kumbe alikua ameshaoga kunisumbua tu.
“Sikia nilikumiss sana yaani hizi dakika chache tu nimeona kama mwaka nikaona nitumie kaujanja ka kukuita huku ili uje nikukumbatie weeh” Kendrick alininong’oneza sikioni, alikua na sifa sijui alijuaje kama sauti yake inanidatisha hasa akiniongelea sikioni ndio kabisa alikua ananimaliza, alianza kunitomasa mwilini, kwakua sikucheza mechi ya kikubwa muda mrefu nilijikuta naweweseka zaidi, tulijikuta kitandani, nikiwa mwingi wa kutamani shughuli pevu, rungu la Kemdrick lilipopenya maungoni mwangu ndani ya dakika moja lilivyotoa wazungu lilisinyaa, nilijitahidi kulichezea linyanyuke lakini wapi. Kendrick alionesha kufadhaika sana kwa kitendo hiko, nilimwambia tukaoge, tulienda bafuni nilimshika shika na kumwagia maji ya baridi lakini wapi, babu hakusimama.
Nilimtakia usiku mwema na kwenda chumbani kwa bibi kulala, japo nilikua na hasira nilitamani shughuli pevu kama nilizozea uswahilini halafu yeye alishindwa kunifikisha popote kwenye safari yangu.
INAENDELEA

