CEO BIBI ATANIPIGA, TOA JAMANI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 1
“Hamida hebu nitolee utoto wako kwani wewe ndo wakwanza kuachwa, cheki macho yalivyokuvimba kwa kulia, unamlilia bwana. mwenyewe hakutaki” “Yaani wewe hujui moyo wangu unavyouma, kifua kinawaka moto natamani nikipasue. nikimwagie maji ili kipoe, nimempa mtaji wa matunda na bado kaniacha jamani yaani mimi wa kuachwa kweli, nimekosea wapi mimi
“Sasa Hamida rafiki angu wanaachwa watu waliowanunulia wapenzi wao majumba ya kifahari wengine wanawasomesha mpaka wanapata kazi na bado wanaachwa sembuse wewe uliempa Juma hizo elfu ishirini za machungwa, emu ndugu yangu acha kujiumiza bure mimi unanikwaza ujue”
“Badala unipe pole wewe ndio unaanza kunisema namna hiyo, weee sawa tu” “Bhasi bhasi kipenzi changu sikusemi tena, poleee weeeee, twende kwa mpemba tukale bagia na vikachori, amka nawewe nikuspoil kidogo mrembo wangu nilishusha sauti yangu na kumbembeleza rafiki angu Hamida aliekua analia baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kuitwa Juma.
Hamida na Juma walikua kwenye penzi shatal shata kipindi hiko Hamida anafanya biashara ya kutembeza uji, Juma alikua kijana wa mtaani asie na mbele wala nyuma, Hamida akajitahidi kumpa Juma pesa ya mtaji wa kuuza matunda, ili asiwe wa kushinda kijiweni tu angalau apate chochote kitu, baada ya juma kufanya kazi ya kuuza matunda na kupata visenti akaona Hamida wa kazi gani tena mtembeza uji. akampa jina baya la malaya mtembeza uji mwishoni akambwaga shosti angu, akiwa analia kitengo cha kumbembeleza kilikua kwangu, sema mimi mwenyewe ndio chenga kabisa, sikuona kama kuna umuhimu wa kulia lia eti kisa mapenzi yaani kwa ugumu wote huu wa maisha na bado mtu unapata ujasiri wa kulilia mapenzi niliona sio kweli, kwa upande wangu. kwa niliyoyapitia kwenye ulimwengu huo wa mapenzi hata unipige na tukio gani siumiii wala sishtuki kabisa,
Tulitoka nyumbani kwa kina Hamida na kwenda barabarani mpaka kwenye meza ya mpemba muuza bagia na vikachori, tulifika kwa mbwembwe kama zote, ukitupekua mifukoni hatukua na pesa hata nyingi, nilitoa elfu moja na kumpa mpemba, tulianza kula bagia na vikachori mimi niliamua kula vinne tu na sita nikamwachia ale Hamida, wakati wote mate yangu yalikua yanautamani mchuzi wa pweza ila sikua na pesa, kamtoko hako tu kalitufanya tufurahi wenyewe, nilimwona Hamida akitabasamu hilo ndio nilipenda tayari ilishafikia saa mbili usiku tukaamua kurudi mtaani. Hamida alienda kwao. na mimi nilikua uelekeo wa nyumbani, nilipitia dukani nikakopa mshumaa, dagaa na unga robo, muuza duka alilalamika kwamba nalikuza deni ila nilimpiga kiswahili mpaka akajaa kwenye mfumo kwani ningeshindwa kufanya hivyo bhasi usiku huo, tungelala giza, pia tungekosa chochote cha kutia kinywani, nilifika nje ya nyumba yetu tuliokua tunakaa na bibi angu, nilimkuta bibi yupo nje, nilijua kaamua kukaa nje kwasababu ya hakukua na mwanga ndani, kwa pamoja tuliingia ndani niliwasha mshumaa, nilipika haraka ili mshumaa usilshe kabla sijamaliza kupika, tukala na kwenda kulala, kitandani nilikua na mawazo mengi juu ya maisha niliyokua naishi na bibi angu, licha ya matatizo yote niliyokua napitia, nilitabasamu baada ya kukumbuka kwamba siku inayofuata nakwenda kuanza kazi, niliamini kazi hiyo ni mkombozi kwa familia, nilisali na kulala, niliamka saa kumi alfajiri niliwasha kamshumaa. kaliko baki, nilijiandaa, na kumuaga bibi kwamba naenda kazini, niliondoka nyumbani na kutembea haraka haraka, nikiombea nisikutane na vibaka wakanifanyizia kitu mbaya, nilifika kwenye banda la mama Bonge, banda hilo lilikua ni mgahawa wa chakula walikua wanapika siku. nzima ndipo ambapo nilipata kazi ili nipate ujira wa kuendesha maisha yetu, mimi na bibi angu. “Shikamooo” nilimsalimia Mama Bonge kwani
ndio muda ambao alikua kafika akiwa na binti
mmoja.
“Heee we nae salamu salamu za nini na kazı hatujaanza, nikipata maokoto yangu ya siku ndipo unisalimie Mama Bonge alinijibu vile alivyojisikia wala sikutia neno niliwajua watu kama mama Bonge, biashara zao huendesha kwa mikopo ya vicoba au kausha damu hivyo hasira zipo sebuleni tu.
Kazi ilianza rasmi baada ya mama Bonge
kumwaga mlangoni madawa yake ya kuitia wateja, kwangu ilinishangaza kidogo kwakuwa ni mgeni ila mwenzangu mwenyeji hakuonesha kushangaa kabisa, sikutaka kujisumbua na mambo ya watu, tulianza kukanda unga ngano, tulipika chapati maandazi yaani nilisukuma mpaka mgongo uliniuma ila sikua na namna nyingine wala kulalamika kwani ningefanya hivyo ningekutana na ukali wa mama Bonge. Wateja mbalimbali walianza kuja bandani kwetu saa tatu, tuliwahudumia vizuri ilipofika saa nne
“Nyie mabinti napeleka chai kwa mafundi kule
barabara ya pili nataka nikanyukane nao vizuri ili wanilipe madeni yangu yote ya nyuma Mama Bonge alituaga tulimwitikia sawa, wakati huo mimi nilikua jikoni na mwenzangu alikua akihudumia wateja, alipoondoka mama Bonge nilimwomba mwenzangu wa kuitwa Rehema, anipokee kwenye mapishi na mimi nihudumie kidogo japo niweze kupumzika kidogo. Rehema alikubali, nikaanza kuhudumia wateja pale, mara akaingia kijana mmoja mrefu, mwili hakua mwembamba wala mnene, uso maji ya kunde, alivalia suti yake nadhifu rangi ya bluu, alipoingia bandani, harufu nzima ya banda ilibadilika, yule kijana alikua ananukia nyie tena ananukia utamu utamu tu, kwa mwonekano wake hakustahili kukanyaga kabisa bandani kwetu ila sikuelewa kwanini alifika hapo.
Nilimsalimia na kumkaribisha kwa unyenyekevu na uchangamfu, licha ya kufanya hivyo vyote hakunijibu, sikujali kilvyo kwani mimi na wanaume mashausi tunapita njia tofauti kabisa, nikaamua kusimama kwenye misingi yangu ya kazi, kijana hakumsalimia yeyote mie bandani. nikajua bhasi ni tabia yake.
Nikamuuliza anakula nini, alinijibu “chapati mbili chai ya rangi kumbe anasauti tamu ndio maana. analbania bania vile, nilienda jikoni nilichukua chapati mbili kwenye sahani na kikombe cha chai, nikarudi na kumwekea mezani. Niliendelea. na wateja wengine cha ajabu yule kijana hakuongea chochote wala hakula, baada ya dakika tano alinyanyuka na kuondoka, nilishangaa sana ila sikumuongelesha. Reherna alinlita kwa nguvu sana.
Weee Magrita emu njoo mara moja kumbe sikujitambulisha bhana, jina langu naitwa Magrita. Nilienda alipokua Rehema, nilimwona mwenye wasiwasi mwingi.
“Wewe mbona CEO Kendrick katoka haraka amekunywa chai kweli?” Rehema aliniuliza. “Hapana mtu mwenyewe maringo mengi, nimemwekea chai, hajanywa eti kaondoka” nilijibu kwa kifupi. “Mungu wanguuuu tumeisha Rehema aliongea maneno ambayo yalinishangaza sana. “Tumeisha kivipi?” nami nilimrushia swali. Hakunijibu swali hilo bali alipiga magoti mbele ya Mama Bonge na kumwomba msamaha kwani muda huo ndio alirudi,
“Samahani mama, CEO Kendrick amekuja na hajanywa chai “Hajanywa chai?” Ndio mama msamehe Magrita alikua hajui kitu”
” Rehema alizidi kujitetea. mambo yote hayo yalikua yananishangaza sana. mpaka wakati huo. Nilipomtazama Mama Bonge alinipiga jicho kali, lilikua jicho lenye hasira nyingi zisizo na mfano. Nilijikuta natetemeka japo sikujua niseme nini au nijitetee vipi kwani sikulijua kosa langu kabisa.
Chapter 2
“Binti sikia usiniharibie biashara yangu kabisa, siku ya kwanza unaanza kazi na kutibua mambo namna hii, ili nikusamehe beba hivyo vitu mpaka ofisini kwa CEO kendrick nenda kamwombe msamaha mpaka akubali kunywa hiyo chai laa sivyo usirudi hapa na ndio utakua umepoteza kazi hivyo Mama Bonge aliniambia maneno makali sana ambayo yalitishia kabisa kibarua changu, ilibidi nikubali kwenda kumwomba msamaha CEO Kendrick.
“Sa samahani ma mama, ofisi yake ndio iko wapi?” niliuliza kwa hofu vile vile.
“Lile jengo lenye vioo nenda floor ya tano chumba namba mia mbili, muda unakimbia sana binti wahi haraka kabla hujaikosa hiyo nafasi ya kuongea nae nilichukua hotpot niliweka chapati nyingine za moto mbili, nilibeba na chupa ya chai na kikombe. Sikujua ni uhusiano gani uliopo kati ya huyo CEO Kendrick na Mama Bonge, nilikua nakwenda kumwomba msamaha mtu na kosa nililolifanya silijui, ni umaskini ndio ulionifanya kutii hayo bila ya hivyo ningesimamisha hiyo kiburi nzito niko nayo mbona wangekoma.
Nilitembea mpaka kwenye geti la kuingilia kwenye hilo jengo nilikutana na mlinzi, nilimsalimia na kumwulizia namna ya kufika Floor namba tano, akaniuliza nakwenda chumba namba ngapi nilimtajia chumba namba mia mbili.
“Unaenda kuonana na CEO Kendrick au Secretary?” Mlinzi aliniuliza. Nikamjibu ni CEO kendrick.
“Mmmmmmmmh” aliguna mpaka nilimsikia. “Mbona unaguna kaka”
“Aa aah hamna saini kwenye hilo daftari” mlinzi alionesha kupotezea hali yake ya kuguna. Bado waliendelea kunitisha na huyo CEO Kendrick, nilisaini mlinzi akanielekeza namna ya kufika floor ya tano, nilitembea mpaka sehemu nikabonyeza kitufe lifti ilifunguka, niliingia ndani yake, nilitazama vibonyezeo vingi vilivyokua kwenye ukuta, nilibonyeza namba tano na kubonyeza kingine cha kupanda juu, yote hayo nilikua nafanya kwa kubahatisha ndio ilikua mara yangu ya kwanza kuingia kwenye majengo kama hayo, tena kupanda lifti ndio nilikua sijawahi kabisa nilifanya hayo kwa kubahatisha tu, lifti ilianza kupanda juu, ule mtetemo wake ulinifanya nijishikilie kwenye kuta, lift ilihesabu ilipofika floor ya tano, Ilifunguka yenyewe nilitoka haraka isije ikajifunga na mambo yakawa mengi hapo.
Nilihesabu namba za vyumba mpaka chumba namba tano niligonga hodi kwa dakika tano sikuona majibu niliamua kunyonga kitasa na kuingia ndani. Nilipokelewa na sura ya mwanamke iliyokua inanitazama, uso wake ulikua na maswali mengi sana, bila hofu nilimfuata huyo secretary, bila karibu bila nini nilianzishiwa maswali. “Enheee nikusaidie nini dada?”
“Nimemletea CEO kendrick chai”
“Hehehehe eti nini?”secretary aliniuliza kwa kebehi kubwa.
“Nimesema hivi nimemletea CEO kendrick chai” niliamua kukaza sauti na kuongea kwa msisitizo zaidi.
“Yaani uchawi wenu wa kumroga CEO kuja kunywa chai kwenye banda lenu chafu ulipoisha mmeona mumletee hapa hapa ofisini sio secretary alianza kuongea mambo ambayo sikuyajua ni nini anamaanisha, nilikaa kimya nikiendelea kumtazama.
“Hey Msichana ni hivi kama CEO hajanywa chai yenu leo, bhasi ujue uchawi wenu umefeli na kuanzia leo hatokunywa chai yenu tena, atakunywa ofisini na mimi ndio nitamtengezea Secretary aliongea maneno mengi huku akichukua jagi na kuweka maji ndani yake, aliliwasha ili kuyachemsha, alifanya hivyo baada ya kugundua kwamba CEO kendrick hakunywa chai bandani kwetu, aliona huo ndio muda muafaka wa yeye kumtengenezea chai mpaka hapo niligundua kwamba CEO Kendrick hakua anakunywa chai ofisini bali ni bandani kwetu pekee, kwasababu gani alifanya hivyo hilo sikujua kabisa. Mimi nilibaki nimeduwaa tu, nguvu za kurudi kwa mama bonge na vitu vyangu sikua nayo kwani kufanya hivyo ni sawa na kujifukuzisha kazi.
“Dada angu ni dakika moja tu bhasi naomba niongee nae nilizidi kumwomba yule secretary. “Heey wewe mwanamke mchawi hunisikii au hebu toka ofisini mara moja kabla sijakuitia mlinzi akubebe bebe hapa” kusikia maneno hayo nilijua wazi hakuna kitu nitaweza kufanya kuibadili akili ya secretary ili anipe nafasi ya kuonana na CEO Kendrick Kibaya zaidi, Secretary mwenye mdomo mchafu alikua ananiita mchawi, jina ambalo sikulipenda kuitwa tangu udogoni mwangu. Nilipiga hatua za taratibu za kuondoka, kama mtu niliepoteza matumaini kabisa ya kuendelea na kazi kabisa.
Chapter 3
“Rose hebu mruhusu aingie nilisikia sauti hiyo kutokea nyuma yangu, sauti ilikua ya CEO Kendrick hivyo niligeuza kabla hata ya kuambiwa na yule Secretary niingie, wakati huo CEO Kendrick alikua kasimama mlango wa ofisini kwake akinitazama.
Rose alinipiga jicho kali sana, ila sikujali nilichotaka wakati huo ni kutimiza lengo langu la kuongea na CEO kendrick nilifungua mlango na kuingia ndani, ofisi ilikua nzuri sana kwa samani bora na za gharama zilizopo ndani, pia chumba kilikua kinanukia harufu mbili tofauti, moja niliigundua ni ile ambayo niliisikia mara ya kwanza CEO kendrick alipokuja bandani kwetu hiyo ilikua perfume yake na hiyo nyingine nilijua itakua airfres, harufu ya ofisi ilikua nzuri kweli kweli mpaka nilitamani nisitoke humo ndani ili niendelee kuburudika nayo.
Kuingia ndani ya ofisi, niliendelea kusimama kwani sikupaswa kujiamulia kukaa chini kama mwenyeji hajaniruhusu.
CEO Kendrick hakunitazama wala kushughulika na mimi ndio kwanza alikua busy kuzungumza na simu, nilisimama kwa nusu saa, miguu ilikua Imechoka ila niliendelea kujikaza, hasira niliyokua nayo ndani yangu ingepasuka mbona ofisi ingegeuka chini juu, ila sikuweza kufanya hivyo kwakua nilikua na uhitaji zaidi, dakika arobaini na tano zilipokwisha ndipo aliniambia nikae kwenye kiti. Usoni sikuonesha sura ya kukasirika bali nilikua mwingi wa tabasamu.
“Enhe niambie kuna jipya gani nina dakika kumi pekee za kukusikiliza?”
“Naomba unisamehe kwa ubaya niliotenda ulipokuja bandani kwetu, naomba unisamehe sana, nitajitahidi wakati mwingine kuwa bora zaidi” niliongea kwa unyenyekevu mwingi. “Ubaya gani umeutenda?” CEO Kendrick alinipiga swali gumu sana kuliko mitihani yote ya hesabu niliyowahi kuifanya huko nyuma, swali lilikua gumu nilikuna kichwa ila sikupata majibu nikweli niliomba msamaha lakini sikujua kabisa kosa langu nini.
“Aaah aaaaaah ni vile tu sikukupokea vizuri” “Aaah nini wewe, sikia ulinipokea vizuri ila hukuninawisha maji mikono, muda wangu wa kukaa pale ulipoisha nikaondoka, wewe ni mgeni zingatia hilo kwa kesho”
“Sawa nitazingatia hilo, Kwahiyo umenisamehe eeeh” nilimuuliza swali hilo japo nilijilaumu kwanini nimeuliza ni kama vile liliniponyoka tu.
“Yameisha, muda wa kukusikiliza umeisha unaweza kwenda sasa”
“Mungu wangu” nilihamaki kwani muda uliisha na CEO hajanywa chai.
“Jamani CEO naomba unywe angalau kidogo tu chai nimekuletea hii, nakuomba niko chini ya miguu yako”
“Sorry sina muda mwingine unaweza kwenda tu” CEO Kendrick aliongea na kuweka kituo hapo. wakati najiuliza uliza niondoke au vipi niliona CEO kendrick alifungua kompyuta yake na kuanza kuongea mambo mengi nilijua yupo kwenye kikao muhimu cha kikazi, sikutia neno nilishukuru kwa kukutanisha mikono ili nisimsumbue na kikao chake, nilibeba chupa na hotpot langu nilitoka nje, sikutaka kumwongelesha Rose secretary hata aliponiita, sikugeuka niliendelea na mwendo wangu, kichwani nilikua napanga uongo wa kumdanganya Mama Bonge. Nikaupata kwamba nitamwambia amenisamehe halafu amekunywa chai, si hakukua na mashahidi hivyo niliamini kwenye uongo wangu, hapo nilikua na amani kidogo nilipofika kwa mlinzi getini nilimwomba chombo nilimpa chai na zile chapati, mlinzi alinishukuru sana, nilitembea mpaka lilipokua banda la Mama Bonge. Kitendo cha mama bonge kuniona tu alikuja na kunikumbatia akiwa mwingi wa furaha, sikujua ni kipi kimetokea ila alinifurahia sana, nilijionea maajabu mimi mwenzenu.
Chapter 4
“Ahsante sana binti yangu, yaani wewe kwenda kwa CEO Kendrick kumpelekea chai imesababisha kanisamehe deni la millioni moja alilokua ananidai, tena kakusifia kwa huduma nzuri sana” Mama Bonge aliongea huku akinishuru ndipo nilijua sasa umuhimu wa CEO Kendrick kwenye hiyo biashara ya mama bonge kumbe alikua akimkopesha pesa za kuendeshea banda, hivyo kitendo ambacho nilikifanya cha kumkasirisha CEO kendrick ilimaanisha kwamba nilikua namgombanisha mama Bonge na CEO kitendo ambacho kingemletea shida sana Mama Bonge kufikia kudaiwa pesa anayodaiwa, kwakua boss wangu alikua na furaha bhasi na mimi nilipatwa na furaha na kumshukuru Mungu kuisha kwa huo msala, tuliingia kwenye mapishi ya chakula cha mchana kwakua mama Bonge alikua kafurahi sana, siku hiyo tuliruhusiwa kula wali nyama.
Kitendo ambacho mama Bonge hajawahi kukifanya hata mara moja kwa wafanyakazi wake kwani mara zote alikua mtu wa kuwalisha ukoko maharage wafanyakazi au ugali mboga za majani.
Tulifanya kazi pale ilipoingia usiku wa saa mbili, kuna chakula kidogo kilibaki, mama bonge alitugawia tuondoke nacho, siku hiyo ilikua ya maajabu sana mpaka Rehema alinitania kwamba nimekuja na upepo wa kumbadilisha mama Bonge maana sio kwa matendo hayo ya kimalaika mimi niliishia kucheka tu, kila mmoja alienda nyumbani kwao baada ya kupewa elfu saba saba za ujira wetu, mimi nilirudi kwa bibi angu kipenzi niliupasha ule wali maharage, tulikula kwa furaha kwetu sisi wali kilikua ni kitu cha thamani sana, kwani bibi angu alienilea baada ya wazazi wangu kufariki hakuwahi shika pesa nyingi ili kuninunulia chakula hiko. Tulienda kulala mapema sana. Saa kumi kama kawaida tuliingia kazini, tulipika maandazi na chapati ilipofika saa tatu kama kawaida wateja walianza kuja lakini kasoro, CEO mtanashati Kendrick. Mama Bonge aliniita na kunambia.
“CEO Kendrick kasema umpelekee chai ofisini kwake kwani leo hawezi kuja nilikubali japo sikupenda kukutana na yule Secretary Rose kwani nilimjua kwa kuwa na roho ya korosho zilizoungua. Nilibeba vitu kwenye mfuko, nilipofika getini, mlinzi alinikumbuka hivyo alinichangamkia sana, akaenda mbali na kuniomba chai, nikamwambia nikitoka kwa CEO Kendrick kama itabaki bhasi nitampa, mlinzi alidai ataombea chai ibaki, bhasi mimi nilicheka na kuelekea kwenye lifti nilipofungua mlango wa ofisi namba mia mbili kama kawaida nilikutana na jicho baya la Rose, sikujisumbua hata kumsalimia kwani nilijua hatoitikia moja kwa moja nilienda ofisini kwa CEO Kendrick. Harufu nzuri ya kuvutia ilikuwepo kama kawaida ila kiliongezeka kitu kipya ambacho kilinikaribisha ofisini nacho ni tabasamu la CEO Kendrick mpaka nilishangaa na kujisemea kumbe huwa anatabasamu.
“Karibu sana Magrita” nilishangaa CEO kendrick ananijua jina langu nilijitahidi kuficha mshtuko wangu na kujibu ahsante.
“Niliweka hotpot mezani na kulifungua, nilimimina chai kwenye kikombe na kumkaribisha aah samahani nimesahau maji ya kunawa sijui naweza kuyapata hapa” niliongea hivyo kwani nilijua bila maji CEO Kendrick asingekunywa chai, jicho langu lilikua kwenye chupa kubwa ya maji mezani na lingine nilikua nampiga CEO kiwizi wizi kusikilizia atasemaje.
“Mmh hayo ni maji yangu ya kunywa, siwezi kuyanawa sasa sijui tunafanyaje” CEO Kendrick aliweka ugumu wa mambo.
“Ooh sawa si kuna toilet bhasi naomba ukanawe uko ili unywe chai itazidi kupoa hapa nilisogeza wazo lingine.
“Maji yamekatika hayatoki kabisa huko ndani” “Duuuuuuuh” niliguna
“Usiwaze lakini ngoja nikupe wazo Magrita naona akili yako imekwama kabisa, nitanawa mate yako”
“Heeee” nilishangazwa na maneno ya CEO Kendrick, kwamba anataka kunawa mate yangu, nikajua utani si akasimama bhana alinifuata mimi nilikua narudi nyuma, mwisho wangu ukawa ukuta alinishika shavuni nilishindwa kumzuia kabisa kwani nilihofia kumkwaza, nilifumba macho yangu kwani alikua ananitazama sana nami nilishikwa na aibu, si akanipiga denda la moto moto, lips zake zilikua na utamu sijui kaweka nini nilikaza kidogo mwisho nikajikuta nampa ushirikiano.
Chapter 5
Tulidendeka kwa dakika tano ndipo aliniachia sasa, nilishindwa kumtazama macho yangu yalikua chini.
“Unaweza kukaa sasa nimekwisha nawa mikono yangu ni misafi” aliongea CEO kendrick huku akiendelea kutabasamu, aliingia kwenye chumba kingine nilijua ndipo kilipo choo alitoka akiwa na maji maji mikononi alianza kula chapati na kunywa chai zile alizisifia sana kwamba chapati ni laini na tamu kupitiliza ndio maana miaka na miaka amekua akila kwa mama bonge, mimi nilikua natamani amalize haraka ili niondoke zangu kwani aibu ilikua kali sana kwangu niliona naukosa ule uhuru wangu kabisa. Baada ya kumaliza kunywa chai, alinambia.
“Nimemaliza chai, mikono ni michafu nataka ninawe ili niendelee na kazi zangu”
“Kunawa tena jamani” niliuliza kwani nilijua kinachotaka kutokea alitaka kunibusu tena, nikajisemea moyoni muone na macho yake yale, nikweli CEO kendrick alikua na macho mazuri yaani macho flani mtu anakuangalia huchoki kuangaliwa nae. Nikajua ananitania si akafuta mikono yake kwa tishu wakati nakusanya vyombo vyangu ili niondoke alinipeleka ukutani, nikaubana mdomo wangu ili asinibusu tena, si akanipapasa kwenye mbavu, hapo yaani hapo ndipo mashetani yangu yalipolalia ule mguso tu, niliachia mdomo mwenyewe, nikampa ushirikiano dakika chache, nikabeba vyombo vyangu bila hata kuaga nikaanza safari ya kuondoka zangu.
Nilifungua mlango na kutoka nje. “Enheee wee bibi kidude kwanini umekaa muda mrefu kwa mpenzi wangu ulikua unafanya nae nini au unaongea nae nini?” Rose aliniuliza kwa Jazba huku akitoka kwenye kiti chake na kunifuata nilipokua nimesimama. Kitendo cha kuniambia kwamba ni mpenzi wake nilishtuka kidogo na kujiuliza maswali kama ni mpenzi wake kwanini CEO Kendrick anibusu namna ile na mpenzi wake yupo nje, wakati nawaza hayo.
“Weee ni kiziwi au si nakuongelesha we mpuuzi” Rose aliendelea kunitolea maneno yake machafu alienda mbali zaidi alinishika tisheti yangu na kunikunja, hapo niliona dharau zimezidi sasa.
“Weee dem nitakuvuruga vuruga mpaka uchanganyikiwe, mimi sio wakisasa kama wewe, mimi ni wa kienyeji niachie mjinga wewe niliongea kimtaani kabisa nikweli Magrita mimi nilikulia mtaani yaani kule uswahilini kabisa, mambo ya kupigana yalikua damuni ila hapo. sikutaka kuyazua kwenye ofisi za watu, nilichofanya ni kumwondoa mikono yake kwenye tisheti yangu halafu bila kuongea wala nini, nilianza kuondoka, nyuma bila kujua Rose alikua kwenye kilele cha hasira alichukua stepla mashine ile kubwa ya kubania karatasi alinipiga nayo kichwani, nilikwenda chini mzima mzima na kuzimia.
Kishindo changu cha kuanguka kilimfanya CEO Kendrick kutoka nje, kutazama kunani. “Kuna nini hapa Rose, umemfanya nini mwenzako?” CEO Kendrick aliongea huku akiniwahi.
“Sijamfanya kitu mimi jamani aaaaah aaah” Rose alijitetea huku akijifanya analia kinafki. CEO Kendrick alinibeba mikononi mwake na kunitoa nje, nyuma Rose alikwenda kwenye kompyuta na kufuta ushahidi wote wa kunipiga akijiweka salama kama nitakufa bhasi kusiwe na ushahidi wa kumfunga.
CEO Kendrick alinipeleka hospitali, madaktari walinipokea na kunipa matibabu, nilizinduka usiku sana, nilitazama pembeni nilijiona nipo kwenye mazingira ya hospitalini pembeni yangu alikuwepo CEO Kendrick.
“Oooh kumbe umeamka, lala hapa” CEO kendrick aliniweka kichwa kwenye miguu yake, kisha alipiga simu kuwaita madaktari.
“Nisamehe kwa kushindwa kukulinda mpaka unaumia namna hii, nikuahidi nitakulinda maisha yangu yote haitatokea siku hata moja mtu akaugusa hata unywele wa kichwa chako. Nakupenda sana Magrita wangu” CEO kendrick alijimimina maneno mengi ya kimahaba, nilikua na maswali mengi ya kumuuliza juu ya maneno yake hayo kabla sijafungua kinywa kuongea alinipiga busu la moto moto ila CEO kwa kupenda mabusu jamani mmmh, aliniachia haraka haraka baada ya daktari kuingia wodini.
INAENDELEA

