UDANGAJI ULINIPA MUME TAJIRI
SEHEMU YA 16
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Mpaka kigiza lewis ndio ananiachia tukaenda kuoga sasa tukashuka kupata chakula chausiku.. Lulu jiandae week ijayo tunaenda kwenu.. Aliniambia lewis wangu tukiwa mezani tukipata chakula..
Nilifurahi kweli.. Natamani ata umuoe leo jamani kachangamsha nyumba. Be tabu alichangia nae..
“Ndio maan naitaji nimuoe haraka maan naona shetani ayupo mbali.. Ata sikuelewa alimaanisha nini kusema shetani ayupo mbali.
Kumbe bhana da fau alikuja kwenda nyumbani kwetu kuniharibia kabla sijafika.
“Ndio mama yani lulu kaja kunigeuka akaanza tabia mbaya nakutembea nawanaume zawatu tu uko mjini imetapakaa sifa mbaya sanaa kwake adi naona aibu mimi niliompeleka.
Aliwajaza wazazi wangu uwongo mtupu.. Jamani bint yangu kapatwa nanini Lakini mbona alikua mtoto mwenye adabu tu jamani!!!..
“Yani mama kakutana namagroup uko yaajabu alafu sasa kajipeleka kwamume wamtu kujiweka kabisa kwake yani Lulu amekua natabia mbayaaa… Da fau alizidi kunipakaa masinzi nyie..
“Nilisema lakini asiende mahali ila mkaforce ona sasa nint yangu anapotelea kubaya.
“Baba mimi nilimlea kama mdogo wangu ila makundi sasa akunisikia akawa jeuri tu..
“Lakini mbona tunaongeaga nae napesa anatuma dada ata anaga tabia mbaya kiasi icho.. Sophia mdogo wangu aliongea.”
“Nyamaza sophi mdogo wangu we bado mdogo sanaa ujui maisha soma kwanza nausije muiga dada yako.. Da fau eti anampa mdogo wangu ushauri alivo maliza umbea wake akaondoka zake.
Mama alibaki akinisikitikia tu bint yake jamani nimeharibika bila kujua uyo mleta taarifa ndio kaniharibu.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Mimi Nampenzi wangu lewis tulijifungasha siku iyo mazawadi kama yote nilimbebea mama yangu kila kitu nguo viatu baba yangu pia nikamchukulia nguo adi mdogo wangu sophia nilifanya shopping yamaan vyakula mafuta dumu kubwa mchele sukari yani gari ilijaa full kwenye buti so poa.
Safari iliwadia mimi nampenzi wangu tukaanza kwenda kwetu… Ilituchukua masaa sita kufika so tulifika usiku tukiwa tumechoka kweli kweli.. Tulishuka uku lewis akishangaa kwetu palivo apakua pabaya sanaa sema kidogo apajaendelea.
” Mamaaa!!! nilimuita kwafurahaaa.. Kweli maan niliwamiss eti.. Akatoka mdogo wangu soph akawa kasimama anasema
“Niwewe da Lulu..!!! ndio nimimi.. Jamani umependeza dada yangu kama mzungu nikivalia tu gauni refu lenye vimikanda vyembamba mabegani ili kuachia mwili wangu upumue sema lilikua zuri tu uku nikiwa nimevaa viatu vyangu virefu kichwani nimesuka nywele yangu yabei mbayaa.
Basi mdogo wangu akanikumbatia uku akilia kabisa.. Da fau kaja apa kamjaza mama nababa maneno aliniambia taratibu mama nae akatoka ndani.. Akaniona ile namfata nimkumbitie mama yangu aliniwasha kofi mjarabu adi lewis akasogea karibu yangu nakunikumbatia.
” Mama sasa mbona unampiga dada bhana kisa umbea wa da fau..!!!! sophia aliongea kunitetea”
” Funga domo lako unajua nini wewe… Mama shkamo.. Lewis alimsalimu mama wala akuitikia alafu akasema shikamo mwenyewe mxyuuuu!!!.. Alisonya.
Nikisikia baba akisema jamani nasikia sauti yabint yangu Lulu nini..ndio baba da lulu kaja soph alimjibu.. Aya njooni ndani wanangu tukaingia uku mama kavuta domo.
Nilimsalimu baba nae Lewis alimsalimia pia.. Baba alikua amelala tu kwenye kochi nilimketisha lewis japo makochi yetu yaadhi yachini ila ndio ivo.
“Bint yangu kwema uko!! umezidi kua mzungu adi nimekusahau bint yangu.. Baba aliongea kwakuonyesha huruma kweli..
“Ndio kwema baba vep hali yako nawewe??.. Naendelea salama tu karibuni..
” Akaribie wapi kaiba mume wamtu aitoshi kamleta adi apa nilishangaa mume wamtu tena jamani mimi..!!!
” Usishangae dada yako fau kasema kila kitu umeacha kuuza duka ukawa changu doa mtoto wewe umejiunga namagroup yaajabu adi sasa unaiba wanaume wawatu mbona sijakulea ivo mimi.. Jamani!!!???..
Nilishangaa da fu kaja nichafulia nyumbani kwaduka gani wasomaji wangu simnajua duka nililo kua nauza!!!!… mimi.. Nikaona da fau sasa kazidi kazidi tena kazidi sanaa..
“Mwanamke siupoe kwanza watu wapuzike !!!.. Baba alimwambia.. Nipoe!!! ili nigundue nini..!!! nikamwambia mama usinione apa bint yako nimekaa mbele yako nilioyapitia wenda ungenikuta marehemu kabisaaa..!!!
Mama Kusikia kauli ile yamarehemu alitoa macho ayo🙄…!!!
Kama da fau kaamua kunipakazia mimi pia sio bubu nasema bila kujali….
Ataendelea.
SEHEMU 17 – 18
Mama aliyatoa macho aswa kwakauli Yangu….!!!!🙄
Mama yani ungenipoteza wala apa ulipo niona mshukuru mungu.. Da Fau alinichukua apa akisema ananipeleka kuuza duka mama lakini wapi..!!!
Mama mimi da fau alikua akiniuza kwawanaume mama wanaume mbali mbali pesa anachukua yeye da fau anaishi maisha yaajabu sanaa sanaa ata nilijuta kuondoka apa nyumbani mama nimeteseka bint yako nimepitia madhira..
Alafu leo da fau anakuja kusema uwongo wake mnaukubali mama.. Adi nilianza kulia mama akawa mpole kama sio yeye alianza kunisema..
Uyu Mnae muona apa mbele yenu ndio mwanaume alie nisadia mimi adi leo mnaniona apa mbele yenu wala sio mume wamtu da fau kawadanganya tu..
Ili kuwajengea hofi ila yeye ndio mbaya.
” Sasa mwanangu ulishindwa kurudi nyumbani kweli..???!!! mama nilipata hela nikawa nampango wakuja ila wewe ile cku nilipo kupigia cm nilitaka nikwambie ila ulipoanza kusema mdogo wangu kafauru baba nae anaumwa nikakutumia pesa yote nilio ipata niliendelea kufanya vile uku nikiwatumia pesa mama nimepitia magumu sanaa..
Mama adi nae alianza kulia nakuniomba msamahaa mzazi akoseagi nilijua tu nihofu nahasira yamama yaliisha pia.
” Mama naitaji kumuoa bint yenu nimekuja kujitambulisha kwenu.”
“Kijana unafamilia kwani!!??.. Baba alimuuliza lewis.
” Apana baba walishafariki ila nipo naishi namlezi wangu tu.”
“Basi pole kijana wangu.. nilienda kwenye buti yagari nikatoa mizigo nilioleta sukari kimfuko mafta niliwachukulia dumu kubwa lalita 20.. Mchele mama alifurahi kweli nanguo zao wote soph mdogo wangu alifurahi kweli..!!!!..
Mama nababa walifurahi pia tulilala pale nyumbani.. Mimi nalewis palikucha nikaaga naondoka uku lewis akiacha pesa kama laki tatu cash. Mama alizidi kufurahi uyo.. Mimi nikarudi mjini nampenzi wangu kujianda mambo Yandoa.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Miezi miwili ilipita nikiwa bado nipo mjini nampenzi wangu.. Siku moja tulikua tumekaa tunaangalia tamthilia kwenye tv nilipata kichefu chefu kibaya nikakimbia kutapika.. Hali gani hii tena jamani.!!!
Nikarudi nimepoa yule mama tabu akasema dariri zamimba izo.. Lewis alishtuka nakusema kweli aunty itakua mimba eeh!!!??.. Ndio dariri zake izo kijana wangu kampime tu upate uzibitisho..
Basi lewis alifurahi usiku kucha alali anatamani pakuche. kweli palikucha akasema nioge..
” Jamani nimapema bhna.. Acha ubishi Lulu kaoge!! nikaoga nakuvaa akutaka ata ninywe chai jamani akidai nitanywea mbele kwambele..!! tukaondoka adi hospital kunipima wakasema namimba yaweek moja alafu mpimaji niyule yule bravo alifroti mapigo Lewis alionesha furuhaa adi kwa doctor yani.
Akanirudisha nyumbani
Da fau alikuja akanipigia cm akiniitaji niende kwake moyo wangu ulitokea kumtoa moyon mwangu lakini aliongea kama mtu Anae Umwa sanaa nilipata imani maroho yahuruma niliondoka bila kumuaga lewis kabisa maan angekataa nisiendee.
Nilimkuta kakonda jamani kakondaa mwili nuru ana tena usoni.. Nilimuonea adi huruma eti.. Akasema mdogo wangu najua sikukuonesha njia ilio bora ila leo mimi kukuleta uku ndio umempata uyo lewis naomba unisamehe mungu ukupa kinachokustyle akupi unachotaka…
Nilimtega bwana yako toka nilivomuona mara yakwanza nilikuonea wivu kwanini wewe unapata wanaume wenye pesa tu kila siku!!! nilitaka nimchukue kama nilivomchukua bravo lakini alinikatalia lewis kabisa..
Ata siku ile ulivonikuta sipo nilimtega pia nikijua nitamnasa Ili nimchukue kutoka kwako lakini Pia siku iyo ilishindikana adi akanifukuza kwako mume umepata mdogo wangu… Nilikuchongea kwa wazazi wako pia ili kukuharibia naomba pia unisamehee pia..!!!
Jamani nilimuoenea huruma adi nikatoa machozi yangu yalikua mlangoni sanaa
” Da fau ngoja nikupeleke hospital ukatibiwe unaumwa eti..!!!
“Apana Lulu nimeathirika alafu nishatumia madawa adi nimechoka.. Naona mwisho wangu umefika utaniombea msamahaa kwamama yako nababa yako pia nakwetu ukija kwenda utaniombea msamaha..
“Da fau but kuathirika sio kufa eti utakua sawa..!!!
” Apana mdogo wangu kifo nakiona nimechokaaa Nishatoa mimba nyingi sanaa apa nilipo nableed bila kukoma “
Iliniuma nikamsogelea nakamwambia apana da fau Nishakusamehe kwayote sina kinyongo nawewe kabisa..Ila mimi naita tax.. Nikaenda kuita tax japo alisema ataki kwenda hospital ila nilimpeka kibishi.
Alifikishwa tu kitandani kupewa huduma.. Majibu yalikuja kama ifyatavyo….!!!!! Iliniumaa sanaa…!!!
Itaendelea
SEHEMU 19 – 20
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Kumfukisha tu da fau hospital nikaambiwa kaisha kufa ukweli niliumia sanaa😪 akuna binadam asie nahuruma ata baada yakifo chamtu wake wakaribu aijalishi mangapi tulipitia.
Nilirudi kwa Lewis nimepoa nikamwambia kila kitu nae alisikitika kweli.. Akisema atagharamikia mazishi adi kumpeleka nyumbani akazikwe kwaheshima tu kama binadam wengine nilishkuru kweli Nakumuona lewis mwema sanaa juu yangu.
Tulisafirisha maiti adi kijijini kwetu uku nikiwapa taarifa wazazi wake da fau nanikiwambia wazazi wangu pia.. Da fau alizikwa salama nakupumzishwa kwenye nyumba yake Yamilele.
Nilirudi nampenzi wangu lewis uku wakimsifia nimtu mwema sanaa kwakila mtu maan alijitolea sanaa kwenye msiba wa da fau.
Nilishugurikia mambo yangu yandoa baada yaweek kupita Baada yakifo cha da fu nikaandaa kila kitu kuhusu ndoa yangu. Nilifunga ndoa nalewis wangu nyumbani kwetu bonge lasherehee nilitishaa mtaani kuolewa nabwana mwenye uwezo wake kipesa watu walikula nakusaza.
Sherehe yangu tena ikarudi mjini sasa uko ndio ilikua balaa wafanyakazi wake Lewis alikodi ukumbi mkubwa sanaa uku marafiki zake wakinipa zawadi nyingi nakunisifia nilivo mrembo. Akika nilibahatika sana kumpata Lewis wangu.
Mwaka mmoja badae
Nilishajifungua mtoto wakiume namume wangu alimpa jina Alvin.
Mke wangu sasa naona unazidi kunivutia kila siku zinavozidi kwenda.. Lewis aliongea.”
” Ata wewe mume wangu uniishi hamu kabisa.. nilimjibu mume wangu lewis tukiwa tumemuweka mtoto wetu katikati uku sisis tukiwa pembeni yake.
“Sasa nataka tujenge nyumbani bonge Lajumba..
“Waooh kweli Nilifurahi kusikia ivo.”
“Yeah nishaanda kila kitu nilitaka tu nikusuperise.. Basi nilipita pembeni nakwenda kumkumbatia mume wangu.
Alifanya kama alivo ahidi Nilijengewa ghorofa lamtindo tu Tukama pale pazamani nakuamia ghorofani uku tukipangisha pale pazamani.
Kwetu pia nilijingewa nyumba kubwa nanzuri baba namama yangu walinisifia sanaa nakumwaga baraka nyingi kwamume wangu uku mdogo wangu soph akipata anacho kitaka uku akisoma kwabidi..!!!
Nlimfungulia mama yangu duka kubwa lakuuza nguo pia mama yangu alikua fundi chereani basi alijumlishia uko uko kushona nakuuza nguo uku nikimuwekea Mfanyakazi mmoja wakumpa kampani pale dukani kwetu kukawa atuna shida ndogo ndogo baba yangu alipata tiba akawa sawa sikuzote maisha mabovu pia uleta maradhi yasio itajika katika maisha.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
MIAKA MIWILI TENA ILIPITA
Nilimpenda mume wangu sanaa uku akikataa mimi nisifanye kazi mpaka mtoto akue jamani nikiongea naambiwa kitu gani unakosa apa au unataka kufubaa tu uko nje..
“Lewis mume wangu Jamani kwani kufanya kazi nikufubaa!!.. Nimesema kazi akuna.. Mwenzenu tena nikapata kichefu chefu kila wakati uku namtoto mdogo ivi mwenye mwaka nanusu inaweza kutokea kupata mimba yiyari unanyonyesha jamani..!!!!..
Basi nilikuja kupima nikaambiwa namimba tena yamwezi uku mtoto akiwa namwaka nausu tu..!!!! Lewis alifurahi nakusema alikua mpweke ila mimi nimempa faraja yakumletea watoto.
Mwisho wakumbuku Kumbu yangu naistoria Yangu niliowapa.. alitokea mume wangu Lewis akanikumbatia kwanyuma pale nilipokua nikikumbuka maisha yangu yanyuma.. Najua unakumbuka ulipotoka..!! acha mawazo mpe mtoto wangu watomboni uko ili apumue kidogo.. Alinitania nakunipiga busu mubasharahaa.. Prince kaishaenda shule.. Ndio muda tu dada wakazi kampeleka..
MWISHO WASIMULIZI YANGU PIA
Ujumbe naushauri maisha ayaitaji hasira naujuaji wala kiburi naubinafs nafitina pambana kivyako kufikia malengo yako ila njia yakuoambana iwe bora tu isiwe kama yangu…
Kila mtu mungu umpa kwawakati wake tumepitia mengi magumu ila inatokea cku tunapata amani yamoyo roho mbaya nachuki azistyle.. Mungu ukupa unacho stayle sio unacho taka..!!!!!
Bye bye ahsnten wote nawapenda
MWISHO