UDANGAJI ULINIPA MUME TAJIRI
SEHEMU YA KWANZA
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Unaambiwa akuna aijue kesho ila leo tunaiyona kesho ndio pagumu mtu kujua maan ingekua rahisi kila mtu angejua kesho yake inakujaje ili aweze kabiliana nahali iyatayokuja kumtokea.. Mungu niwaajabu sana.
Niliamka mapema tu nikawa natazama nje nikiwa Ndani Yajumba langu ila kulikua nijuu yaghorofa ya nyumba yangu ilikua nzuri tu nakubwa sanaa ata siwezi kuyelezea …
Niliangalia nje hali ilivo Nakushika tumbo langu ambalo lilikua nakiumbe ndani yake.. Nikakumbuka maisha yangu yanyuma Sasa nikiwa namiaka 24..
Unajua kila mtu najua alichopitia kwenye maisha yake kiwe kizuri au kibaya pia.. Lakini ndio alichokipitia..
Nakila tunachokipitia kwenye maisha ujenga istoria sikuwai kuota kama ipo siku nitakuja kuishi maisha kama aya niliyaota tu nakuyaona kwenye tv.. Ila ndoto yangu ilikuja kutimia baada yakumpata mume wangu
Jina namficha kidogo ( ??).. Alinitoa kwenye hali ngumu sanaa yamaisha yangu Nakuyabadili pia .. Basi nami nawapa istoria yangu njice nilipitia msoto namaisha mabovu sana kwangu yalikua mabovu.. Sana nawala sikuvutika nayo.
TURUDI NYUMA KIDOGO
MIAKA 6 Nyuma kabla yakua mke wamtu nakumiliki jumba kubwa tu…
Kwamajina naitwa Lulu..
Sasa Nilikua namiaka 18 tu
Maisha yanyumbani kwetu yalikua sio mazuri sana ata baada yakumaliza kidato changu channe sikuweza kuendelea so nilikua nipo nyumbani kwetu tu
Nikasidiana na mama yangu bi shausiku Kushona shona mama alikua nakiujuzi chakushona shona akawa anawashonea watoto pale mtaani nguo zao nazile zilizotoboka..
Simnajua mzunguko wakijijini waela sio sana kama wamjini pia wazazi wangu wao walijiusisha nakilimo nanilikua mimi namdogo wangu mmoja alietwa sophia yeye alikua bado anasoma shule yamsingi darasa lasaba ndio alikua mbioni kumaliza lasaba..
Nilitamani ata siku moja nitoke nyumbani kwetu nakwenda mbali ili nitafte maisha nami nije wasaidia wazazi wangu
Siku moja nilikua nipo jikoni nipika nilimsikia mama akimkaribisha mtu kwafuraha..
“Jamani fau bint yangu umerudi uku kwetu jamani karibu bint yangu..!!”
” Ahsante mama nishakaribia.. Nilivosikia ile sauti Nikatoka jikoni haraka maan nilisikia sauti yamtu nae mjua nikatoka..
” Waooh da fau. Nilienda kumkumbatia kwafuraha kweli alikua dada yangu japo sio mzaliwa nasisi yeye alinizidi umri miaka yake 27 alikua bint wapale pale mtaan kwetu na alizoena nafamilia yetu pia alimpenda mama yangu nakumuona kama mama yake japo nae alikua nafamila yake lakini alimzoe sanaa mama yangu.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
“Da fau unazidi kupendeza jamani..!! nilimtazama kwamatamanio kwasababu alipendeza juu mpaka chini vitu alivo vaa vilikua vyagharama tu.
“Ahsnte mdogo wangu ata wewe umekua kweli Lulu umezidi kua mrembo sana.
“Mmmh ata sikuzidi wewe mimi manguo Yashamba aya kila siku nanuka moshi tu.”
Basi mama alimkaribisha ndani mimi nikarudi jikoni kuendelea kupia.. Baada yamuda nilitoka jikoni chakula changu niliivisha kilikua teari.. Nikawafata seblen nilipenda kweli kumtazama da fau.
“Eeh leo umemuona fau dada yako unafuraha kweli ayo makande yangu yameiva kweli??.. Mama aliniuliza.
” Mama bhana yameiva.. Da fau utakula makande?? au ushazoea vyakula vyamjini!”
“Ila Lulu wewe unazidi kukua namaneno yako yaudogo adi leo ujaacha tu.. Nitakula sindio chakula chakwetu mdogo wangu..
“Tenga kama kipo tayari ili Ale mwenzio.. Basi nilienda nikatenga chakula tukala.. Muda flan nilikua nimekaa kwenye kochi mama akiongea na da fau.. ila da fau alikua akinitazama kweli.. Kisha akasema.
” Mama kwani Lulu anafanya nini apa kijijini kwetu..??!!”
“Anachakufanya sasa! kamaliza tu shule yupo yupo alafu kilimo ndo ivo tena awezi akilima kidogo et kachoka nikavivu aka usikaone tu apa nakanajifunza nacherani yangu pia.”
“Aah sawa sasa mama yangu mimi kule mjini naduka langu kubwa languo unaonaje nikimchukua awe ananisaidia kuuza uza nguo uko maan mimi sikai dukani sana nakazi nyingine uwa nafanya.”
Mimi nikalopoka kwanguvu.. Kweli da fau??! … Eeh kweli ila mpaka mama apa akuruhusu..
“Kiukweli nilitamani sana kubadili maeneo mazingira Pia natoka nimezaliwa adi nimekua nakusoma sikuwai kutoka pale kwetu nilimiss kweli kutoka nyumbani nikafatafte maisha..
Wenda on day ningetoboa nakuja kua msaada mkubwa kwetu.. Jamani akuna asiependa maisha mazuri ayupo dunia hii tusidanyanyane..
Mama alikaa Kimy kwamuda akifikiri “akasema niwazo zuri ila ngoja baba yake mzee Lucas arudi kutoka shamba nitaongea nae akikubali basi utaondoka nae..
Apo nikawa naomba mungu baba akubali tu mimi niende zangu mjini.. Da fau aliaga pale akatoa pesa niliona nyekundu mbili yani elfu 20.. Mama akapokea nakushukuru.
Da fau aliondoka ila jicho lote kwangu Mmh! mpaka nikawa nasema mbona natazamwa ivo au naonekana mshamba sanaa nini!! .. Ombi langu lilikua baba aje mama amwambie nae akubali.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Basi bwana Usiku baba alivokuja niliitaji kujua mama atavo mwambia nae atakubali pia!!… Sasa bhan nikaenda kuwasikiliza mlangoni..
“Wewe unamuaminije! uyo fau mtu anakaa mbali naapa bint yangu akipata shida uko alipo ana ata ndugu?? Usisikie mjini mkajua maisha nisafi napo nitagumu pia.”
” Aah!! nikaona uyu mzee nae anazengua sasa jamani siakubali tu mimi niende zangu mjini uko japo kwetu apakua kijijini sana ila alipokua anakaa da fau kulikua namwendo sana nakulisifika nikuzuri kumeendelea majengo mazuri mzunguko pia wabiashara ulikua mzuri.
“Mume wangu mpe mtoto chance amekaa apa kijijini miaka yote ajawai kutoka adi Leo kamaliza shule fau pia nibint waapa apa naumchukulia Lulu kama mdogo wake eti.. Awezi fanya jambo baya.”
“Sawa mruhusu aende ila uyo fau wako mwambie awe makini nabint yangu.”
Nilivosikia baba kakubali nikasema yesiiiii!!!!… Nilikimbia chumbani kwangu nikaanza kupanga nguo zangu ucku ule ule kwenye chaka chaka langu uku nukiona masaa mbona yanaenda slow sana asubuh akufiki jamani.. Nilijipangia nguo vizuri tu sikutaka kusubiri mama aje aniambie uku mie nishasikia jibu nindio.
Asubuh mama alinifata nakuniambia baba yako kakubali nijiandae..
“Nikasema sawa. Muda wasatano ivi asubuh da fau alikuja nyumbani kwetu jamani nguo zake nzuri nzuri tu zilinifanya nikavutika kuondoka nae muonekano wake pia mzuri
Uku mimi sikua namambo mengi sket yangu nablauzi yangu uku yeye kavalia msurual uwo uliomshika barabara nywele nzuri imekaa kichwani ikatulia jamani kama niduka analo sio kwakua smart ivo.
Alisalimiana na mama yangu uku akiwa kashika kimkoba chake nacmu yake kubwa tu sijui ndio smarty phone zinaitwa! mimi nipo nachaka chaka langu la shangazi kaja nikiwa nipo tayari kwasafari ..
Fau kamtazame Lulu kama mdogo wako kama ndugu yako atapokosea mkanye pia muonyeshe njia sahii nailio jema kwake pia..
Alafu nawewe Lulu ukawe msikivu usimsumbue dada yako fau sawa! nilikubali uku da fau alisema mama usijali.. Lulu nimdogo wangu nitamlea kama mdogo wangu atapata shida.”
“Mimi nilitamani kumuona baba yangu ila aliwai kwenye mashamba yake mapema basi tuliaga pale uku mdogo wangu sophia akilia akwenda shule ilikua wekend alilia kweli nisimuache nikimpa matumini..
Nitarudi asome kwabidii sababu alikua ndio yupo darasa lasaba namuda sio mrefu angeamiliza .. Alinikumbatia pale tukaagana. safari ikaanza yakwenda mjini moja.
Jamani naenda mjini mie…. Like uwezavyo ujue lulu baada yakufika mjini itakuaje!!! duka lipo kweli….!!!!….
Itaendelea…
SEHEMU YA PILI
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Tukiwa tupo ndani yagari da fau alikua aishi kunitazama jamani alafu anasema. “Lulu ujue we nimrembo sanaa ila matunzo tu mdogo wangu..
“Nikamjibu kweli da fau?? ndio kweli yani usijali upo namimi Da fau wako nitakufanya ung’ae upendeze we ngoja.
” Basi nami navopenda urembo sasa!!! nikawa nafurahi. Safari ilizidi kusonga nailichukua muda kufika kama masaa sita nazaidi so tulifika usiku ushaingia.
“Jamani jamani nyie nyie watu kweli umaridadi uficha umaskini..
Da fau Alinifikisha kwake sasa!!! kulikua uswahilini uswahili nyumba zipo jirani jirani tu sinikaingia ndani chumba kimoja Tu japo kikubwa kweli godolo lipo apo chini!!!! Lasita kwasita pana kubwa napana kweli …
Jamani kule kwetu tunashida ila kitanda atleast kilikuepo chakimtindo… alafu walikua nadresing table yao yakimtindo apo pembeni.. Yani nilishangaa da fau ukimuona utasema mtu mwenye jumba ilo tena kubwa tu lenye wafanyakazi khaaa!!!..
Alafu nilishangaa kuona wadada wawili yani kimuonekano wamekaa sijui niwaelezeeje! ila niwale wadada wamjini kidada poa yani Mikucha iyo yabandia mirefu atari… Mmh!! nijisprise siku iyo.
“Eeeeeeh! shoga yetu naona umetuletea mtoto mdogo mdogo mbichi mbichi eeeeh!! walicheka kwa kugongeana mikono..👋
“Alafu nyie jishikilieni uyu nimdogo wangu kueni naheshima.”
” Khaa! eti unamsikia fau wewe ulisemaga kwenu upo pekeako so uyu mrembo mdogo mdogo uwo udogo wako umetoka wapi!!!.. Fungeni midomo yenu. da fau akainiita
“Lulu mdogo wangu! abe da fau! .
Usiwajali awa jisikie upo huru apa kwako pia awa nirafiki zangu wazoee pia sawa mamii??.
“Sawa da fau niliitikia ila mwenzenu mie hofu ilikua njiani kwangu Niliweka limfuko langu languo da fau akanipelekea maji nje uko bafun nikaoga Nae akaoga.
Akasema sisi tunatoka mdogo wangu we utalala alafu kesho nitakupeleka mahali sawa eeh!!?..
“Mmh nikamjibu tu sawa walivaa nguo zao yeye namashoga zake izo nguo nyie sasa yani visketi navigauni vifupi vifupi vitovu nje nje yani khaa! viatu virefu kama utasema wasanii flan uko wakinarihana beyce mavazi yao… Mmh!!! wakaondoka zao.
Nakuniacha mimi kule ndani.. Nikasema Yani da fau kafika tu usiku hu ata bila kupumzika kweli??.. Niliutafta usingizi ata aukuua unakuja wote.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Palikucha asubuh namapema wakarudi da fau aliniamsha lulu jiandae nakutoa leo.. Nami nikaenda kujifanyia usafi. Nikaondoka nae uku tukiwaacha marafiki zake kule ndani.
Alinipeleka duka kubwa tu languo akawa ananipimisha nguo lakini Zilikua nguo fupi sana kwangu nilijiona nipo nusu uchi nguo mpaja wote nje jamani ndio nini ivo!! nilijaribu ata kuzishusha azishuki.
“Nawe nini acha ushamba nguo unashusha yanini!!..Apa nimjini watu ndio uvaa ivi vi..!! kwenda nafashion apa sio kijijini pakuvalia magauni yako namasket mapana kama unapokea kipa imara…!!!
“Nikamwambia Da fu lakini nifupi sanaa da fau et!! azina ufupi wowote ukizizoea utaona zakawaida sana tu.
” Lakini da fau duka ulilo sema nauza lipo wapi naanza lini pia..!!
” Nyamaza basi nawewe unanichosha Lulu Namaswali yako duka niwe nalo mimi!? utaliona muda ukifika ..!!” Alinichukulia nguo kibao zaajabu ajabu.. Naviatu pia.
Nikapelekwa saloon nywele zikaoshwa maan nilikua naywele zangu nyingi tu sema nilikua nikijisukia zangu mistali nyumbani basi nilioshwa saloon..
Nikasukwa rasta iyo iliokaa mkao kichwani uku mikia ikining’inia makalioni.. Khaa!!! nilijishangaa kwamuda kama naonekana supaster yan nywele adi kwenye makalio niliona zanifanya nisiwe huru kabisa…
Lakini nilipendeza Nilitoka mtu katika watu ofu yangu nikuto kumuelewa tu da fau basi nilivo malizwa kutengenezwa nywele Tukarudi nyumbani.
“Sasa Lulu ilo duka utaliona usiku mdogo wangu apa nimjini kila nyumba inanamba usione mimi da fau yako nang’aaa uko kwenu nikija nakuja nahela unanisifia napendeza sijui nini..
Ukaona maisha smple maisha magumu mdogo wangu kila mahali sio mjini wala kijijini watu Tunapambana eti nganga ngingii yani full kupambania maisha.
Wenzake walicheka hahahh.. Alidhani mjini maghorofa Watu tunaitaji Pesa mjini apa!!!.. Hahah.. Walicheka kweli mimi ndio nilikua kwenye harama yakujiuliza tu apa!!!.. akaniambia pumzika sawa! wao wakawa wanapiga stor zao.
“Yan kanafa kweli kwamatumizi aka alafu bado kadogo.. Yani kadogo sanaa.. Yule m,baba anavopenda dogo dogo sasa..!!!.. Akiona vyitoto vidogo anaona vinamshusha sukari.. Akikiona ichi sasa kifuani kama msubari.. Atazidi kupandisha nabipi….Hahaha walicheka😀
“Nyie pendo nalinda acheni kulopoka mnaongelea nini apa.. Iyo mada ife..!!.. Tusitake kumpa hofi mapema!!!..
Mmh mimi nikawa najiuliza wanampango gani namimi na da fau kasema nipumzike iyari mimi sina usingizi..!! Nini kinaendelea apa!!!.. Jamani au naenda kuchinjwa ama kuuzwa nchi zawatu uko…..!!!!…
SEHEMU YA TATU
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Da fau aliwazuia wasizidi kuongea ili wasinipe ofu.. Nilijilaza pale mpaka mida yajioni ilisogea pia…
Atimae muda ulisogea.
Usiku sasa mida yasambili ivi niliambiwa niogee nikavalishwa nguo nzuri lakini shida zilikua fupi fupi tu..
Nikapakwa makitu usoni sijui ndio make up izo basi nikasikia wale wadada rafiki zake da fau wanasema.. So beautiful jamain!!! mwaa!!💋 wakaonyesha mikono yao wakinikiss!!.. Kwambali..!!!
Cm yada fau ikaita nikasikia anasema “Hallo yes Boss lama boss Yeah yupo teari njo tu.
“Mimi mapigo yamoyo yalikua ayatulii nyie basi kama robo saa ivi tukasikia muungurumo wagari nje da fau akatoka. Muda uwo uwo akarudi kunichukua mimi .
Nikamuuliza da fau tunaenda wapi??”
“Dukani nikakuonyeshe duka langu.” Nikatoka nae adi nje nikamkuta m.baba jamani sio mkaka nim,baba kabisa Kitambi kimemning’nia kama uji uliokosa sukari alafu pia bonge.. Aka nisogeza karibu yayule baba.
” Waoo karembo sanaa.. Lile libaba nisilolijua lilisema ivo.. Fau we kiboko ujawai kukosea kwakweli mtoto bado m,bichi kabisa uyu Naona atavoenda kumishusha sukari mimi…
“Mimi ndio da fau mwenye nyota zake mjini.. Sasa Lulu mdogo wangu uyo baba atakupeleka kwenye ilo duka akuonyeshe atakurudisha asubuh sawa kipenzi!!??..
” Nikajiwazia duka gani jamani uku ili libaba lishaanza kusema mimi mbichi!! kabisa.. Kisha nikasema Da fau kwanini tusiende Wote mimi naogopa!!!”
“Usijali upo mikononi salama kabisa uyu baba anashida we nenda nae tu wala usijali kuhusu yeye namjua utafanya kazi yake alafu… asubuh atakurudisha uje upumzike.
Nikasema “kazi gani yaduka ucku jamani!!. da fu me naogopa!!!!
” Lulu ebu acha kunipotezea muda uku nimjini maduka watu uwuza adi usiku Kucha adi kunakucha wanaunganisha pia so sitaki maswali yako.. Alinishika mkono nakunipeleka ndani yagari aliniingiza akarudi zake kwalile libaba.
Muda so mrefu lile libaba likarudi ndani yagari likawasha nakuondoka pale kwadada fau.. Mimi nilikua nawoga usio nakifani..
Alafu lile baba likawa lanishika mapaja yangu maan nilivalishwa vinguo vifupi kweli so mapaja yote yalikua nje.. Niliurusha uko mkono wake nakushusha nguo ambayo ata kushuka akishuka… Sijui napelekwa wapi mimi..!!!!
Nilipelekwa nayule mbaba kwenye nyumba moja nzuri tu aliingiza gari lake ndani nikawa najiuliza duka mbona silioni apa jamani!!.. akashuka akaja nifungulia Mlango wagari nikatoka kwawoga kweli.
Akanishika mkono adi ndani mimi naogopa atari.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
” Unanipeleka wapi lakini wewe!!.. Mbona apa akuna duka!!.. embu tulia we mrembo wasi wasi wanini lakin..!! niliingizwa kwenye chumba kimoja kizuri kweli yule baba akafunga mlango.. Mbona unafunga mlango?? duka liko wapi ?? niliuliza tena
“Yani mtoto unamaswali sana wewe!! nikikuona unautoto wowote ukizoea hi mambo kwako itakua simple tu mbona…
Sikumuelewa maan yake ila kaisha niingiza adi ndani chumbani kabisa jamani.. Duka lipo wapi we mbaba..
Natumai umesoma ata kidogo kuingia uku adi uku ndani ujajua tu kinachoendelea..!!! Alafu mimi sio Baba yako niyule aliekuzaa tu tusizeeshane apa..
Kuhusu Duka!! mmh lipo uku ndani alianza kufungua tai navifungo vyashart lake akatoa shart lake akabaki kifua wazi akatoa adi nguo yachini yani surual akabaki naboxer mimi nikafumba macho nikaanza kulia 😪
“We mbaba niache Niindoke eti mimi bado mdogo niache nilijaribu kufungua mlango ata nikimbie lakini wapi niliangalia libaba limepanda ewani mtumbo uwo alafu libaba lakunizaa wenda yani linawatoto zaidi yangu!!..
“Unaenda wapi mrembo tulia apa! watoto wananyonya kwamama zao uko..!!! alinitioa pale mlangoni nakuniweka kitandani..
Yani nililia mimi likaanza kunitoa nguo.. Uku nimefumba macho nalia nafurukuta nampiga adi mateke lakini lilikua limekomaa kweli baba lile lakini wapi..!!! .. aliniachii
Akafanikiwa kunitoa nguo zangu zote. Atimae alinibakaa yani sio idhini yangu niwazi alinibaka nasikuwai kulala namwanaume maan ndio kwanza nilikua namiaka 18 tu sikuwai kushiriki mapenzi nililelewa mazingira yaheshima sana kwa age yautoto nilishavuka ila sikua naujuaji namambo yamapenzi kabisa.
Nililia maan libaba lile naumri wangu Alafu uschana wangu umetolewa nalababa kweli!!!!. Adi nilizimia baada yakulia sana Namaumivu nilioyapata mara yakwanza Nililia mimi jamani!!!!😪…
Bora ata utolewe bikra nakijana utasema afadhari nilitokewaga nakijana Ukawa nakamaringo kidogo atakama sio kwakupenda ila libaba jitu zima kabisa lakunizaa niliumia atari….!!!
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Nakuja kushutka namaumivu makali Sehemu zasiri nikwamba lilinipania ata nilipozimia au!!.. niliamaka naliona apo mbele yangu.
” Jiandae nakupeleke kwadada yako.. Mimi nalitazama tu linavofunga shart lake vifungo.. uku bado namaumivu namachungu kweli.
“Usinitazame ivo mimi sio mgawa malaika mgawa riziki.. alafu kukupeleka kwenu mimi niheshima tu maan umenipa uschana wako lakini yangekua yale yalioshindikana sinaga nayo muda.
Basi nilijinyanyua pale kitandan Kwatabu kweli akanielekeza bafuni nikaoge yani sikuongea kitu nilingia bafuni tu nikaoga.. Machozi yalikua yananitoka bafuni kama mvua uku yakisindikizwa namaji nilikua najimwagia.. Nilitoka bafuni nikavaa nguo zangu.
Akanipeleka kwa da fau.. Kwake nilingia ndani sina ata nguvu wala ham Yakuongea nae da fau.. Nilingia adi ndani nikajirusha zangu kwenye godoro nikajilia zangu yeye akabaki nayule baba nje sikujua ata wanacho ongea.
Badae alinifata akaanza kusema..
” Ooh!! Lulu mdogo wangu Pole ndio ukubwa uwo.. Najua nimefanya kitu kigumu sana kwenye maisha yako ila ndio maisha yetu usione dada yako napendeza apa niwanaume wananiweka..
Mjini naaya ndio maisha yangu jitume nawew ubadilishe maisha yakwenu.
Ona mimi naishi tu smple ila ndio nasadia kwetu nawanajua mimi uku namaduka yanguo ila sina chochote nawewe utakua ukifanya ivo ivo utazoea tu.
Kweli da fau kiboko eti nijitume??..!!!
Nikamjibu tu
“Kweli da fau wewe ndio wakunifanyie mimi ivi..!!! kama ningejua nisingekuja da fau umeniaharibia uschana wangu eti!!.. niliongea uku nalia
“Kwani mimi ndio nimeutoa uwo uschana wako!!!..Au bikra ikitoka ndio utakua mzee kisa uschana wako umetoka!!..
Alafu Uschana kitu gani bwana wee! umekua bikra maria wewe..
Watu wanathamini pesa uwo uschana wako ata ukiwa nao utakusadia nini? mjini apa? bikra zipo ata zamchongo pesa ndio kila kitu achana nauschana mambo yakale ayo..
Unakaa uko kijijini nakitega uchumi unakizungusha bure tu ukidhani kitajiinua chenyewe..!!! fursa ndo hii sasa changamka mtoto wakike..!!!
Ata sikumjibu tena niliona maisha yangu ndio Yameishaharibika nanimepoteza muelekeo kabisa au?? yani nilijikuta najikatia tamaa kabisa nikilifikiria lile libaba sasa nachoka.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Week zima ilipita sikutoka kwenda popote. Nilikua najickia vibaya vibaya tu Hali yangu aikua nzuri lakini sasa sikua nahela maan da fau atakama alipewa pesa mimi sikujua nawala sikupewa ata mia.
Akawa anaondoka nawenzake ananiacha ndani bila ata chakula njaa ilikua yaniuma kweli.
Siku iyo tena akaja akasema ” Lulu umekaa sana apa ndani ushapona sasa Leo kunamahali tutaenda wote.”
Nikasema nasikia njaa da fau.”
“Usijali utakula.. Basi alienda akaninunulia chips nasoda nikala kweli.. Akasema kaoge basi.
“Ila da fau mimi siitaji kwenda mahali!!.
Sijikii sawa kabisa sijui kitu naayo mambo eti??..
Nani alizaliwa anajua? tunajua mbele yasafari uko uko alafu mimi sitaki nabishano nawewe kaoge ujiandae tuonfoke”
“Da fau mimi sitaki kwenda mahali najisikia vibaya sana nasitaki tena kufanya kile kitendo pia”
“Utaenda tu Kitendo kwani kinakutoa uwai wako? napia usinichoshe Lulu uwa sipendi kuongea sana..!!! ushakula chpsi zangu eti ndio ugonjwa uzidi apa una namna kaoge uje apa nikupodoe naulivo karembo ivo leo utatuzidi kete.
Sikua nachakufanya sina ela ata ningeondoka kwenda kwetu.. Ila nikifikiria ukatili huu!!… nachoka.
Walinipodoa aswa nakunivisha nguo zao zanusu uchi.. Kwangu ninusu uchi maan vifupi kweli kweli.
Da fau nawenzie Walinipeleka sehemu ambayo ndio uwa wanafanya kazi zao zakuuza miili yao mimi sasa ata kusogea sisogei wao wanafanya kazi yakila ataepita wananisogeza ili nionekane.
Tulikaa kweli pale bila kupata awo mabwana wao.. Ila ghafla ilipita gari moja ikawasha taa da fau akanisogeza tena Ili mwanga unimilike nionekane..!!!
Akashuka kaka mmoja alikua smart kweli suti kali alafu nikijana.
Tu japo nae mkubwa kwangu ila bado alikua kijana.
Nimempenda uyo!! alinyosha mkono kwangu. Nikasmea jamani we kaka awa ujawaona!!!..
Niliongea kwauzuni uku nikiwanyoshea vidole wale marafiki wa da fau walikua warembo mbona alafu wao wakubwa wakubwa “Funga uwo mdomo wako da fau akanistopisha kuongea.
Basi nikaingizwa kwenye gari nikaondoka nayule kaka.. Nilitamani nipate hela yanauli nirudi tu kwetu.
Nikaondoka nayule kaka.
Uku akili yangu nikiwaza nivumilie maumivu yaleo tu then nipate nauli nirudi kwetu… Siwezi vumilia kabisa tena aya mambo yaajabu…..!!!! Lulu atapata nauli arudi kwao au itakuaje!!!!..
Fau atamruhusu Kirahisi ivo!!! uku ndio kwanza mtoto anaita nanyota inawaka..!!! like
SEHEMU YA NNE
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Niliondoka nayule kaka Uku nikiwaza tu nikitumika apa usiku waleo kesho napitia nguo zangu narudi nyumbani kwetu…
Tukiwa Ndani yagari alikua kimy kweli akiendesha gari lake kimy kimy akua ata ananishika mapaja yangu kama ilivokua kwayule baba..
Alinifikisha kwenye nyumba nayo ilikua yawageni akachukua chumba kizuri tu tuakingia sikua naudhoefu naayo mambo lakini nilijikaza tu kama niuschana wangu niliutunza toka nasoma nije nipate mume bora..
Mama alikua akiniambia mume anapenda akute mke wake ajatumika Lakini aikua ivo kwangu Kwasasa..!!!
Kaka yule niliingia nae chumbani kulikua nakochi pale ndani nikakaa..
“Unaitwa nani!!
Ndio swali aliniuliza naitwa.. Lulu nilimjibu uku namtazama kiwizi wizi alipo anza kutoa nguo zake nilianza kupata mashaka nikasema leo tena nabwaka naalivo kua mrefu uku six pack imejaa apo kifuani eeh mungu alafu kijana uyu sindio ataniuwa!!!..
Alitoa nguo zake akabaki naboxer mimi macho yangu yalikua pembeni tu.. kumbe alikua anangia bafuni kuoga Nikapumua kidogo milijua napandishwa kwanguvu. Alitoka bafuni akapanda kitandani.. Alafu akema ukimaliza kutazama upande uje kitandani.. Nilishangaa nyie mbona ata sibakwi!!.
“We fau kila siku unampa uyo ndugu yako madeal sisi utuoni kabisa!!?? au kisa kenyewe nikazuri kazuri.. “
Marafiki zake Da fau walimuuliza moja aliitwa pendo mwingine Linda.
“Nini nanyie amna soko tena Lulu bado mdogo anaita idara zote.. Nandio ananiletea pesa nyingi nyigi.. Sasa nyie tafuteni wazee wenzenu.
Wao walinijadili uko nyuma nawenzao walionekana awapendi mimi nikichukuliwa uku da fau akinikingia kifua.
Kwakua ilikua nikazi mara yapili sasa alafu kaka yule alikua sio mkorofi nilitoa nguo zangu mwenyewe.. Nakwenda kuoga nikapanda kitandani..
Atimae nilishiriki mapenzi nayule kaka.. Nakweli japo sikua naupeo mkubwa ila yule kaka alinivutia kidogo kwasiku ile.
Nililala adi asubuh palikucha akanipa laki ela ambayo sikuwai kuishika jamani kwangu ndio ilikua mara yakwanza kushika laki ivo niliona ela nyingi naninyigi kuzipata haraka.
” Lulu unacmu?? Mmh nilishangaa yule kaka ananiuliza kama nacm.
Nikamjibu sina cm mimi..
“Ooh Naimani tutaonana tena!!”
“Sijui wenda ikawa siku yangu yamwisho kuonana nawewe.. Nilimjibu ivo nakuondoka nikirudi kwa da fau.
Niwaza tu Nikachukue nguo zangu niondoke niende kwetu maan nauli nishapata sina haja yakuishi tena pale sitaki yake maisha kabisa.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Ile nafika tu kwa da fau akaniambia pole umepewa shilingi ngapi!!!.. nikamtazama Tu.
” Lulu nakuuliza umelipwa shingapi!!..
nikamjibu ela alionipa naitaji kurudi kwetu so nitafanya kama nauli naitaji kurudi nyumbani apa nimerudi kupack tu nguo zangu…!!!”
“Eeeh wewe mtoto Unakichaa!! chakuchuchuma!!!..!!! mimi nikulete uku alafu kirahisi tu nikurudishe kwenu??
Labda sio mimi nakingine kama ulikua ujui apa kwangu sheria iliopo apa ukitoka kufanywa uko ela napokea mimi then nakadilia nikulipe shilingi ngapi!!… Maan apa ndio mnalala mnakula napumzi mnapumulia apa kwenye chumba changu.. Leta izo pesa apa ulizopewa..!!!
Nikasema jamani da fau mimi aya maisha siyaitaji kwakweli naitaji kurudi nyumbani..!!
Funga uwo mdomo wako Akunaga maisha maraisi dunia hii.. ulizania pesa zinaokotwa??..
Ulikua unatamani nguo nzuri ndio izo ona sasa ivi unapendeza uko softi rang yenyewe imetulia pamahala pake unatumia mafta yagharama tu unajua yamatoka wapi!!..unataka uwende kijijini unuke moshi bure tu Nakupauka!!.
Mimi adi machozi inatoka.. Marafiki zake wanacheka tu hahha eeeh!! apa ndio mjini watu nacode zao mama.. Nakwambia da fau akavuta poch yangu akatoa pesa zote nilizopewa.
“Mmh mdogo wangu uyo ulie opoa jana kiboko laki nzima..!!! umempa nini icho!!.. Wala sikumjibu nikapita kulala tu… Uku nikisema aya maisha mpaka lini eti! nilimiss kweli nyumbani Tamaa zangu zakua mrembo namaisha mazuri kama zilikua zayeyuka zenyewe.
Aliendelea kunifanyia ule mchezo wakuniuza kwawanaume wake alafu mbaya zaidi nikitumika mimi pesa anachukua yeye.. Kitu ambacho kilikua kinaniuma sanaa…
Unajitutumua uko show show pesa anabeba yeye. Nanilikua sipati ata mwanaume wakunichukua show time yani wote niliokua nawapata nimpaka morn nighit adi asubuh.. Pesa da fau anachukua jamani..!!!
Mwezi mzima ulipita nikiwa nafanya ile kazi siku moja tena tukiwa maeneo flan yale walitega wanaume nilimuona tena yule kaka..
Wasiku ile alienipa laki.. Tena akaja nakunichagua mimi.. Nami nishakua mtumwa wa da fau. Nilienda nayule kaka kama waida yake akua mtu wakuniforce nasiku iyo ilikua tofauti.
Alinipeleka pale pale pazamani.. Mimi kama kawaida yangu sitakagi mambo mengi mwili ushakua wabiashara tu huu nikaanza kutoa nguo nikijua mimi nimtumikaji tu.
Alinitazama yule kaka alafu akasema, Lulu usitoe izo nguo kwanza sina haraka nawewe ebu njo niongee nawewe kidogo! basi sikutoa nguo tena nikasogea alipo Kua amekaa Nami nikakaa pembeni yake.
“Lulu wewe nimschana mdogo sana makadilio yangu unamiaka18 labda namiezi kadhaa tu.. kwanini unafanya kazi hii ikiwa umri wako nimdogo sana!!
Ulitakiwa uwe nawazazi wako sasa ukisoma au kufanya kazi nyingine tu kutoa hii nini kilikufanya ukawa ivi!!??.
Nikamtazma tu nakujisemea uyu kaka namjibu nini mimi..!!!.. Nambona ananiuliza ivo! kama alijua sistyle kua pale kwanini alinichangua mimi!!!.. Kingine sina ukaribu nae wowote…!… ananiuliza kama nani kwangu..!!!
“Lulu wewe nakuuliza nini kimekufanya adi unafanya kazi yaivi ambayo nitofauti naumri wako!!!… Aliniuliza tena akiwa serious kweli… Namjibu nini sasa mimi jamani…!!!!…
Nilimkata jicho nikasema ngoja nimjibu kanichukua kuja kutumikisha kwake alafu naniuliza nini….!!!!
SEHEMU YA TANO
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Nilimkata jicho uku nikiitaji kumjibu…!!!
Nilimjibu tu “akuna anaeijua kesho yake ata mimi sikujua kama ningefika apa au kua nafanya hii kazi..!! sijui ushamaliza maswali yako nijiandae kwaajiri yako??..”
“Sawa siitaji kujua maisha yamtu Ila kwako nimevutika kujua.. sawa Lakini uliniambiaga jina lako mimi siku kwambia langu.. Kama autojali nikwambie jina langu mimi naitwa bravo.. Napia ulisema auna cmu!”
“Ndio ila nitaipata tu ivi karibuni.. Nilimjbu tu kiivo japo nilitamani cm kweli niongee nanyumbani niliwamiss sana. Basi yule bravo kama alivosema jina lake alitoa kibox ata sikujua chanini akanipa..
Mimi nikamuuliza chanini??.
“Cmu iyo nimekuletea!!”
Nilishangaa mimi sikua naurafiki nae wala ukaribu nae kiasi icho nahii ilikua mara yapili tu namimi kwake kazi yangu nikimpa mwili wangu then anipe changu niondoke. Fungua uwone.. Nikafungua bhana nikakutana nacmu iyo tena kubwa izi zakisasa simarty phone .
Nilishtka ata sikua nawaza ipo siku nitaipata ata ndotoni.. Mimi uyu Lulu leo namaliki cm kubwa nyie ushamba kila mtu anao pale unapopata kitu ulichokua unakiona tu kwawatu lazima ujisuperise.
“Utakua ukitumia iyo cm kuna namba zangu pia uko kila kitu kipo laini utajua tu mdogo mdogo.. aliniambia ivo basi ilibidi nimpe kilicho nipeleka pale Nikijutuma japo sikua na express waayo mambo nilijituma tu kama wakike ili nisizubae sanaa…!!! uku nikimpa ahsante kumshkuru kwacm alionipa.
❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣❣
Kama kawaida yule kaka bravo alinipa ela tena siku iyo ilikua laki nanusu nyie mimi naijua ela nae pia alisema iyo nilaki nanusu kanunue nguo namambo yako binafsi alivaa nguo zake nakupndoka zake akiniacha pale.
Mimi macho kodo kwenye pesa jamani niliziesabu nikicheck pembeni nacm yangu.. Nikawaza namba zamama yangu ninazo kwanini nisimtafute mama yangu??.. Nikiwa pale pale kwenye kile chumba alicho chukua yule kaka bravo.
Basi nikaweka namba zamama japo cm ilinisumbua ila kizuri aikua napaswed.. Nikaweka namba zamama yangu Bila atakujua cm inasalio au lah! .. Bahati tu nilipiga cm ikaita.. hallo!! Mama!!!!.. Nilivosikia hallo yamama yagu nilimuita uku machozi yakinitoka.
Da fau alikua anipi cm kabisa kuongea nawazazi wangu akijua nitawambia kila kitu kinacho endelea.. Lulu!! mama alijua sauti yangu. Ndio mama nimimi!!.. Lulu mwanangu nimekutafta sanaa ata fau namba yake aipatikana kabisa.
Nikajua tu da fau alibadili namba ili wasimtafte kumuulizia kuhusu mimi. “Mama nimewamiss kweli.. Vep baba! na sophia mdogo wangu ajambo namasomo yake amefauru kuendelea!??..
Nilimsikia tu mama yangu kapoa natena machozi kama yalikua yanamtoka japo sikua namuona!..
“Mama kunashida kwani nambona upo kimy!!.. Lulu we acha tu mwanangu toka umeondoka apa uku tumekua nahali mbaya sanaa yamaisha..
” Hali gani mama mbona wanitisha!?..
“Baba yako anaumwa aswa nakifua chake kile sasa kimezidi Nauku baridi kali ndio kimemuamka kabisa serious kiela nilichokua nacho akiba nilimpelekea hospital ila akijatosha sasa sipati ata watu wakuleta nguo zakushona ata vilaka mwanangu..
Baba yako Karudishwa nyumbani anatakiwa dawa kilamara shambani akuna mtu anaenda muda mwingi nipo nae nikimtazama tu. sophia Mdogo wako kafauru kwenda kidato chakwanza sina pakuanzia yani sijamnunulia chochote Sina ela mwanangu ata yaakiba ndani..
Nimekutafta sana ata nikwambie ujapokea mshahara wako waduka Navep hali yako unajituma uko dukani mwanangu!!…. Usikute unazidisha uvivu nakujua kwauvivu bint yangu..!!
” Mmh niliguna tu nikijisemea duka!! uku nikiwaza sasa nilitaka nimwambie mama hali harisi nanirudi nyumbani alafu maisha ndio aya nayo yasikia.. Majanga tupu niwazi mimi ndio msaada wao kwasasa!!.. ..We Lulu kazi yaduka vep mwanangu….!!!.. Sijui namjibuje uyu mama angejua nayoyapitia mimi…!!!???…..
“Mama mimi kazi yangu yaduka in shallah mungu anajalia inaenda sawa najituma kweli kweli.. Nilijikaza tu ili kumpa mama matumaini fake sasa ningefanyeje!!!.. Uku machozi yakinishuka mdogo mdogo.. Then Nikamuuliza.. Sasa mama yangu hii namba yako inapokea pesa eeh!!.. Ndio mwanangu inapokea.
Nikasema sawa mama nakutumia pesa nunua dawa zababa nyingine nunua baadhi yavitu vyamdogo wangu.. Nikipata mshahara mwingine waduka nitakutumia pesa zingine umnunulie mdogo wangu vitu vitavokua vimebaki.
“Nitashukuru sana bint yangu mungu akusadie mwanangu uwe mtiifu wakazi iyo alio kupa dada yako fau.”
Nikajisemea kimoyo moyo mama yangu ungejua nayoyapitia!! nilitamani nirudi nyumbani ila sasa nilioyasikia kwamama mimi ndio msaada tena uliobaki sasa nikirudi sinitaenda kua mzigo!!!!!!!….
Naaibu machoni kwao!!! maan sina thamani tena kama mschana nilijiona ivo yani sometim shida utuforce tu kufanya ata tuliokua atuyataki…!!!!!!