𝗠𝗨𝗪𝗔𝗦𝗛𝗢
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
EP 28
Nilisubiri nikiwa nawaza tatizo nini la mwanamke huyo, halafu akaanza kuongea tena
“Halloo……hallo” Alisema
“Nakusikia” Nilijibu
“Ndio, kama nilivyojitambulisha, naitwa mama Mshirakandi natokea katavi”
“Nimeelewa”
“Sasa, kuna habari zako nimesikia”
“Habari gani” Niliongea kwa mshtuko sana maana sikujiamini
“Haha sio habari mbaya, kwa kifupi nisikupotezee muda, kuna mtu kanipa habari kwamba wewe ni msichana mdogo mwenye kufanya biashara katika mkoa wa Rukwa na upo vizuri sana katika suala zima la mapishi, hivyo basi, mimi kama mmiliki wa Softhearted Hotel iliyoko mkoani Katavi nimeona nikuombe angalau uje ufanye kazi katika Hotel yangu maana unasifiwa na watu sana” aliniambia nikaguna
“mh”
“Ndio, mshahara ni mzuri nitakulipa laki sita” alisema maneno yaliyonishtua nikachanganyikiwa na kujikuta naogopa nikihisi ni tapeli
“Je upo tayari?” aliniuliza
“Sasa si mpaka nifikirie halafu ntakuamini vipi?”
“Usijali, unaweza ingia mtandaoni utakuta maelezo kuhusiana na hotel yetu ambapo hoteli hii imekuwa rafiki kwa watu wengi halafu ukisharidhika na maelezo ya mtandao basi utaweza kunipa taarifa na mi nitakutumia nauli ya kuja Katavi”
“Ok….umesema inaitwaje?”
“SoftHearted Hotel in Katavi”
“Ok”
Mama yule alikata simu nikabaki nikijiuliza ana malengo gani na mimi, ndipo nilipoingia mtandaoni na kuitafuta hiyo Hoteli, kweli ilikuwepo, naye pia alikuwa amepigwa picha ikawekwa pale na majina yakiandikwa vyema “Sophia Mshirakandi” nilisoma maelezo halafu nikamtumia ujumbe
“Kama maelezo ni ya kweli yale basi mimi niko tayari” Nilituma
Haikupita dakika nyingi akapiga “Hallo Nuryat”
“Ndio mama”
“Jiandae kwa safari kesho au kesho kutwa kwani nitakutumia nauli ndani ya dakika 5 kuanzia sasa”
“Sawa” mimi nilijibu kama vile utani halafu nikaendelea kuwahudumia wateja wangu
Bila kuamini, ndani ya dakika 3 tu ziliingia pesa kwenye simu yangu kutazama hivi ni laki na 20, hapo nikajua kweli yuko serious na mimi, akanipigia
“Umeiona?” aliniuliza
“Ndio, but samahani mama, umepata wapi namba zangu?” niliuliza
“Nimetumiwa na mtu wa huko Sumbawanga utakuja kufahamu zaidi ukija
“Ok Mama” nilijibu
**
Baada ya siku mbili nilikuwa kwenye usafiri naelekea mkoani Katavi, pesa niliyotumiwa ilizidi nauli ya kwenda na kurudi, hakika sikuamini na Niliogopa nikihisi sio mtu mzuri kwangu
*
Ikiwa ni usiku niliweza kulala katika hoteli ile lakini asubuhi mama Mshirakandi aliweza kuniambia kitu cha tofauti
“Samahani kwa usumbufu Nuryat” Alisema
“Ndio”
“Kuna tawi la hoteli yetu tumelifungua huko Kasulu hivyo basi ninatamani wewe ukawe kama meneja mkoani Kigoma, aliniambia”
“Oh my God” niliongea
“Jiandae tuondoke wote kwenda kigoma”
“Sawa mimi niko tayari hata sasa hivi”
“Tuondoke”
***
Baada ya siku moja nilikuwa nimeamka nikiwa kigoma asubuhi kabisa, mama alinichukua na kunipeleka hotelini ilikuwa bado mpya
Nilifika ndani ya chumba cha mabosi nikakuta wanaume saba wakiwa wameketi kwenye sofa huku wakiwa wamevaa Suti za dark blue na mashati ya rangi ya light blue huku wakinyonga tai na kuwa sare sare na mwanamama yule ambaye naye alivaa hivyo
“Shikamooni”nilisalimia
“Marahaba karibu”
“Jamani good morning this is a girl i told you about” aliongea mama Mshirakandi
“Ok Thank you mama, we think she is mostly welcome, ingia chumbani ubadilishe nguo zipo tayari” alisema baba mmoja
“Chumba kipi?” Niliuliza
“Hicho hapo” Mama alisea akinyoosha mkono kuelekea mlango Fulani
Nilitembea mdogo mdogo kwa uoga nikasogea mlangoni na kufungua huku nikiogopa “Ingia usiogope” alisema mama
Ilibidi nimtii nikaingia ndani ya chumba kile, nilipoingia hivi ndani, nilikuta chumba kipo empty, hakina kitu chochote zaidi ya mtu mmoja wa kiume mrefu alikuwa amesimama katikati huku akinipa kisogo, pia alivalia suti kama zile za wale watu, Niliogopa lakini sikuona uso wake maana aligeukia ukutani na kuniachia mgongo tu nyuma.
EP 29
Ilibidi nimtii nikaingia ndani ya chumba kile, nilipoingia hivi ndani, nilikuta chumba kipo empty, hakina kitu chochote zaidi ya mtu mmoja wa kiume mrefu alikuwa amesimama katikati huku akinipa kisogo, pia alivalia suti kama zile za wale watu, Niliogopa lakini sikuona uso wake maana aligeukia ukutani na kuniachia mgongo tu nyuma
Nilitetemeka huku nikijiuliza ni nini kile, nilianza kupata mawazo kwamba wanataka wanifanye nini wale watu jamani, nilianza kujuta nilihisi wanataka kunichezea picha za ngono, nikageuka Nyuma ili nitoke lakini yule mtu aliongea
“Dianaa” Ilikuwa sauti nzito ya kutetemeka yenye kuonyesha kuwa inanifahamu, nilishtuka nikijiuliza nani anafahamu jina langu halisi kule kigoma? Nikamgeukia na kumtazama nimchunguze ni nani
“Kwanini uliamua kuondoka na kuniacha katika hali ngumu hivi lakini?” aliniuliza mtu yule, ubongo wangu ulivyodadavua haraka haraka sauti nikagundua ni ya Franco ile, hivyo nikashangaa
“Francoooo!!!!” Niliita kwa mshangao
Franco aligeuka huku akitoa tabasamu zito nikamtazama sikuamini, ikabidi nimuwahi na kumkumbatia huku machozi yakinitiririka
“Franco” Niliongea kwa hisia huku nikilia na kumpiga piga mgongoni “ninajisikia vibaya” niliongea
“Diana hujui jinsi nimetumia gharama kubwa kukutafuta” Aliniambia
“Franco, usingetumia pesa zako kunitafuta mimi sio wa hadhi yako tena jamani” Nilisema
“Oh my God….siamini umekonda Diana unaonekana una stress”
“Lazima niwe nazo nimepoteza kila kitu Franco sina imani tena”
Franco aliniachia na kunitazama usoni “Nakupenda” aliniambia
“Ok Franco but unajua kilichonikimbiza mjini?” Nilisema ili tu asije akaanza kunilaumu baadaye akija kujua
“Nakijua, lakini siogopi maana wewe sio mtu wa kwanza kufanya hivyo baby” Alisema na kunishika mkono akanitoa hadi nje, nilikuta watu wanatusubiri
Franco alipiga magoti na kutoa pete mfukoni akaninyooshea sikuamini “Please, will you marry me?” aliniuliza mimi nikabaki nalia tu maana nilikuwa nimeshampenda yule mwanaume ila niliogopa sana
“Franco” Nilimuita
“Please, Diana nataka nikuoe” alisema, ikabidi ninyooshe mkono kumkubalia
“Niko tayari Franco” Nilisema
Franco alinivisha pete, watu wote wakashangilia, tulipomaliza alinitambulisha kwa wale watu, wawili ndo walikuwa ndugu zake na wengine ni marafiki wa familia yao tu
*
Penzi lilimea upya, tukaishi kwa furaha mwishowe tulienda singida nikatambulishwa halafu nikakubaliwa nioane naye na alilipa mahari mwishowe tukaoana
Kweli nilianza kufanya kazi SoftHearted Hotel maana alinitafutia yeye
Franco pia sasa tunaishi naye kigoma na tunapendana, nampenda sanaaaa
MWISHO WA SIMULIZI
Hitimisho
Nimeamua kutoa historia hii kwa watu waelewe jinsi maisha ya kupendekeza ngono ili mtu ajipatie mahitaji maalumu, ina madhara makubwa kwani utakuwa mtumwa wa wale wanaokuhudumia.
La haula, jipange kabla ya kuzaa, ili watoto wako wasije wakawa watumwa wa ngono kujipatia mahitaji maalumu.

