VIFUNGO VYA KICHAWI BAADA YA KUPEANA TALAKA
Ndoa ni taasisi yenye nguvu kubwa kijamii na kiroho. Lakini pale panapojitokeza kutokuelewana, mara nyingi matokeo yake huwa ni migawanyiko na hatimaye talaka. Katika mazingira mengi, talaka haimalizii tatizo pekee, bali huibua hali mpya ya maumivu, visasi na mara nyingine mashambulizi ya kiroho.
Kuna baadhi ya watu wanadhani kwamba katika Dunia hii ya kisasa, basi uchawi haupo, na kilichobaki ni hadithi tu za kufikirika. Lakini ukweli ni kwamba, uchawi umeongezeka sana miongoni mwa watu kuliko hata zamani.
Baadhi ya wake au waume, baada ya kutalikiana, huchukua hatua za kichawi kuwafunga waliokuwa wenzi wao kimaendeleo. Vifungo hivi huonekana katika sura mbalimbali: mume au mke kushindwa kupata mafanikio ya kifedha, kuzuiwa kupata kazi nzuri, biashara kufa ghafla, au hata kukosa amani ya kimaisha. Hii inatafsirika kama “kifungo cha talaka” ambacho hutokana na hasira, wivu au hamu ya kulipiza kisasi.
Wakati ndoa na talaka zinapaswa kuwa mchakato wa kuamua njia bora za maisha ya baadaye, uchawi unaotumika kama kifungo unageuza talaka kikwazo kwa maendeleo.
Ni bahati mbaya sana baadhi ya wanaume au wanawake wengi hawajalijua hili. Nawasanua, unapoona sintofahamu baada ya talaka, jikague, chukueni hatua.
Hii sio ramri chonganishi. Yapo kwenye jamii zetu na tunaishi nayo. Na hii michezo ya kichawi inatajwa kufanywa mara nyingi na wanawake.
Hata katika haya Mahusiano ya Kimapenzi ambayo siyo ya kindoa, wapo watu ambao huwafanyia uchawi waliokuwa wapenzi (Ma-Ex) wao baada ya kuachana nao.