SHERIA NANE ZA MAISHA YA FURAHA AMBAZO WASIOKUPENDA HAWAWEZI KUKWAMBIA!
1. Usiibe mali ya mtu mwingine!
Inaweza ikawa pesa, ardhi,mke au mume. Cha mtu sumu,kiepuke hakinaga FURAHA ya kudumu MILELE!
2. Heshimu dini au imani ya mtu mwingine!
Hii itakusaidia kutoingia kweye CHUKI za kidini au kiimani ambazo zinaweza kukukosesha FURAHA. Chuki za kiimani hazinaga MWISHO isipokuwa wanaopigana mpaka wazikwe!
3. Kula chakula ambacho umekitafuta mwenyewe au umeshiriki kukitafuta. Hii itakusaidia kuepuka masimango na manyanyaso kutoka kwa hao ambao wamekutafutia CHAKULA.
4. Usitegemee PESA za mke,mume au ndugu yako yeyote yule!JIFUNZE KUTAFUTA PESA AMBAZO zinatokana na jasho lako!
Hata kama unatumia pesa za mume,mke au ndugu yako zitumie iwapo tu umeshiriki kuzitafuta. Hii itakusaidia kuepuka masimango na manyanyaso kutoka kwa hao ambao unategemea PESA zao ili uweze kuishi.
5. Kamwe hauwezi kupendwa na kila mtu. Lakini pia, usijiskie vibaya unapochukiwa ukawa mtu wa visasi. Badala yake jenga tabia ya kujifurahisha na kujipenda mwenyewe.
6. ISHI kwenye nyumba yako inayotokana na jasho lako au ambayo unailipia kodi wewe mwenyewe. Hii itakusaidia kuepuka manyanyaso na masimango yanayoweza kukukosesha FURAHA kutoka kwa hao ambao wanalipia Kodi ya nyumba au unaishi kwenye nyumba zao.
7. Maadui zako au wanaokuchukia wengi unawazidi akili, pesa,mali au kitu chochote kile ndiyo maana hawakupendi. Hivyo basi,usipoteze FURAHA kuwafikiria wanaokuchukia bali weka nguvu zako katika kufikiria maisha yako. UNAVYOZIDI KUFIKA MBALI ZAIDI, waliokuwa wanakuchukia hawatakua maadui zako tena bali watakusifia na kusema kuwa walishiriki kukuwezesha kufika hapo ulipo. Inafurahisha sana!
8. Tambua chanzo cha FURAHA YAKO yaani unataka nini kwenye HAYA MAISHA. Watu wengi wana Pesa na kila kitu ambacho unahisi ungekuwa nacho wewe ungekuwa mwenye furaha lakini wao hawana furaha. Kwanini? Kwasababu furaha ya kweli inatokana na wewe kujua ndoto zako na makusudi ya uwepo wako Duniani uweze kuzitimiza. Ndiyo maana kuna mtu ni mfugaji mdogo, ni mchungaji au kiongozi wa cheo cha chini kabisa lakini ana furaha, Kwanini? Kwasababu wametimiza ndoto zao ambazo wamezipambania kwa juhudi kufika hapo walipo. Rafiki yangu, hata uwe na cheo kikubwa kiasi gani au mali kiasi gani hautakuwa na furaha kamwe! Kama haujui unataka nini kwenye HAYA MAISHA.
Kama una huzuni, tambua kuna sheria hapo juu HAUJAIZINGATIA. Je, ni sheria gani unawaza kuanza kuitumia kuanzia sasa ili uwe na FURAHA?