SHERIA NANE ZA KUZINGATIA ILI KUONGEZA THAMANI NA HESHIMA YAKO
1. Usijibu meseji back to back!
Mtu akikutumia meseji,ukamjibu halafu akakutumia tena ukajibu akatuma tena ukajibu yaani kuchati na mtu kwa muda mrefu tambua kwamba sio kwamba atakupenda kwa hicho unachokifanya bali atakudharau na kukushusha thamani kuwa hauna kazi za kufanya.
2. Fanya kile ambacho wewe unaamini ni SAHIHI!
Jifunze kuamini kile ambacho kiko kwenye fikra zako ambacho unaona ni sahihi, watu wana tabia ya kuwathamini na kuwaheshimu watu ambao wanaonekana wenye misimamo. Kama wewe ni mtu wa kufuata kila ambacho unaambiwa na wengine, utadharaulika sana milele!
3. Usimpigie mtu simu zaidi ya mara mbili.
Kama mtu asipopokea simu basi yuko mbali na simu au hawezi kupokea simu yako kwa wakati huo. Kuendelea kumpigia mtu huyo ni kushusha thamani yako, muache kwa muda atakapokuta missed call zako atakutafuta asipokutafuta basi tambua hauna thamani yeyote kwake. Jitahidi kuipandisha ili siku nyingine asiache kupokea simu yako kwa makusudi bali yeye ndiye ahangaie kukutafuta!
4. Punguza kuongea sana na chagua vitu vya KUONGEA!
Usiongea sana na hovyo hovyo, jenga tabia ya utulivu kusikiliza wengine wanapozungumza ili utakaposimama kuongea, ongea vitu vyenye hoja ambavyo vitamfanya kila mtu akupigie makofi ya kukuheshimu. Watu wengi wanaoongea sana hovyo hovyo mara nyingi wanadharaulika na wanadamu!
5. Usiache kumshukuru yeyote yule aliyekufanyia jambo jema kwenye MAISHA YAKO!
Hii itakusaidia thamani na heshima yako kuongezeka kwasababu sifa zako za kukumbuka waliokuthamini huko nyuma zitasambaa kila mahali. Siku zote kizuri, chajiuza!
6. Hakikisha unakuwa na vyanzo vya MAPATO vingi kadri uwezavyo.
Hii itakusaidia uwe na misingi imara ya kiuchumi na kifedha. Kwasababu, Binadamu ana tabia ya kumheshimu mwenye fedha. Ukiwa nazo, nawe pia utaheshimiwa!
7. Hakikisha hauruhusu yeyote yule kujua MIPANGO yako au kitu ambacho unapanga kukifanya.
Hii itawafanya maadui zako wakuogope kwasababu watakosa namna ya kukuangusha. Heshima yako itakuwa kubwa zaidi!
8. Usijenge urafiki na mtu kupita kiasi.
Jenga urafiki muhimu kwa watu ambao wana faida kwako tu! Lakini pia, hata urafiki huo ambao ni wa malengo muhimu (mahusiano, biashara au imani) haupaswi kuvuka mipaka na kugeuka sumu. Kila kitu, kinapaswa kuwa kwa kiasi ili maisha yako yawe mazuri!