HUU NDIO UTAFOUTI WA MWANAMKE NA MWANAUME KATIKA UVUMILIVU!
1. Mwanamke atavumilia maumivu kwa ajili ya urembo wake.
Kuhusu kupendeza. Mwanamke yuko tayari kuvumilia maumivu. Atavaa kiatu cha kisigino kirefu sana chenye kumuumiza ili mradi aonekane mrembo,atakaa chini kwa masaa zaidi ya sita akivumilia maumivu ili tu asukwe msuko wa kisasa, atatoboa pua,masikio au ngozi yake ili mradi apendeze. Mwanamke kuhusu suala la urembo wake, hataki mchezo kabisa yuko tayari kuvumilia maumivu ya aina yeyote ile.
2. Mwanamke atavumilia maumivu kwa ajili ya watoto wake.
Ndiyo, yuko tayari kuteseka na kuumia ili watoto wake wapate furaha. Lakini sio kwa ajili ya mume wake, ndiyo maana ni wanawake wachache sana wanaweza kumvumilia mwanaume asiye na kazi…yaani mwanamke hawezi kuteseka kutafuta chakula na kumlisha mume wake. Atafanya hivyo lakini atawahi kuchoka!
3. Mwanamke atavumilia maumivu kwa ajili ya PESA!
Ndiyo maana anaweza kufanya biashara inayomuumiza au kumdhalilisha ili tu apate pesa. Wanawake wengi kwenye suala la pesa wako tayari kubadili tabia zao halisia.
Lakini je, vipi kuhusu sifa za wanaume kulingana na sifa za wanawake hapo juu?
1. Mwanaume hayuko tayari kuumia kwa ajili ya urembo( KUPENDEZA). Yaani mwanaume hayuko tayari kuvumilia maumivu ili tu apendeze. Suala la kuwa na muonekano mzuri wa sura au mavazi au kujipendezesha halimuumizi kichwa,lakini kwasababu ya utandawazi, wapo baadhi ya wanaume wameanza kufanya mambo haya na kujikuta wakifananishwa na wanawake.
2. Mwanaume atavumilia maumivu kwa ajili ya mke wake anayempenda pamoja na watoto wake.
Mwanaume yuko tayari kushinda njaa watoto wake wale, yuko tayari kutembea peku watoto wake wavae, yuko tayari kumlinda mke wake,yuko tayari kufanya chochote kwa ajili ya furaha ya familia yake. Kama mwanaume mwenye familia hana tabia hizi Basi kuna sababu ambazo zimemfanya awe hivyo alivyo sasa!
3. Mwanaume ni mara chache ataendeshwa na pesa. Mwanaume anaongozwa na ushababi wa kiume na sio pesa…japokuwa wapo baadhi siku hizi wako tayari kufanya chochote kwa ajili ya PESA na ndiyo maana wanajikuta wakibatizwa majina mengi,madume suruali! machawa! Mashonga! Wanawake! Mashangazi! Na kadhalika, hulka ya mwanaume sio kuendeshwa na pesa Bali UANAUME WAKE.
Muelewe mwanaume au mwanamke ujue namna ya kuishi naye VYEMA.
ANYWAY! Kilichoandikwa hapa sio sheria, ni mtazamo wangu na mawazo yangu. Je, wewe unafikiri tofauti hizi ni za KWELI?