Mambo Matatu Ya Kutisha Kuhusu Nguo Za Mitumba
Wakati nikipitia mitandao ya kijamii asubuhi ya leo nimekutana na picha hii iliyonitafakarisha sana. Kupitia tafakuri hiyo nimejifunza mambo yafuatayo ya kutisha ambayo nimeamua kukushirikisha ili nawe ujifunze pia.
1. Nguo za mitumba ni nguo ambazo zimevaliwa na watu na kuzitupa baada ya kuona hazifai tena kwa matumizi yao(Nalifahamu hilo muda mrefu sana). Hivyo basi, unapovaa nguo ya mtumba tambua kwamba inaweza isiwe salama sana kwako! Magonjwa ya ngozi yanaweza yasiishe kwenye miili yetu kwasababu ya nguo hizi,narudia tena tukiwa tunazivaa na kutamba nazo tutambue kuwa sio salama ndiyo maana zilitumika na kutupwa.
2. Nguo za ndani za mitumba sio salama zaidi! Zilivaliwa kutunza sehemu nyeti sana za miili yetu,baada ya matumizi zikatupwa(zikatelekezwa) baada ya wahusika kuona hazifai tena. Lakini pia, inawezekana waliozitumia baada ya kuzichoka walizitupa mahali pasipo SALAMA. Kwahiyo, sisi wahitaji tukaletewa tuzitumie…hivyo basi, TUNAPOVAA NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA, tutambue kwamba tumekubali kuambukizwa magonjwa ya fangasi sugu sehemu zetu za siri, U.T. I sugu zitatusumbua pia lakini pia hata kansa ya vizazi vyetu tunaweza kuipata huko mbeleni kwasababu ya namna ambavyo nguo hizi zimehifadhiwa na kutumika na wenzetu. Tunapozitumia kwasababu ya umasikini wetu, tutambue kuwa sio salama sana kwa matumizi!
Unaweza kufikiri ni hali ya kawaida kujikuna kila mara huko sirini kwako,kumbe tatizo ni hilo kufuri lako na Boksa yako sio salama! Unaweza kujiona ni kawaida kujikuna chuchu zako mara kwa mara kumbe mchawi ni brazia yako. TUNAPOVITUMIA, tusijisahau sana!
3. Nguo za ndani za mitumba zinaweza zisiwe salama sana KIIMANI NA KIROHO. Kwa sisi ambao tumeishi sana nyumba za kupanga, tunajua sana mambo haya. Anika nguo ya ndani kwenye kamba, wakati wa kuanua unaweza usiikute, wasiokupenda wataichukua na kuipeleka kwa waganga wao wa jadi kukuharibia maisha yako!
Roho chafu, mikosi kuhusu UZAZI unaweza kuvipata kwa kuvaa nguo ya ndani ambayo imevaliwa na mtu wa mwanzoni aliyetanguliwa kuvaa nguo hizi!
TUFANYE NINI SASA NA UMASIKINI WETU?
1. Usivae nguo ya ndani ya mtumba au nguo ya mtumba yeyote au kiatu cha mtumba pasipo kukiosha kwa maji ya Moto. Hii itasaidia kuua vijidudu vienezavyo magonjwa! Nguo za mitumba angalau tutatamba zao kwa kujiamini pasipo hofu ya Magonjwa.
2. Usivae nguo ya ndani ya mtumba au mavazi yeyote au kutumia chochote ambacho tayari kimeshatumiwa na mwingine pasipo kukiombea! Unaweza kupokea mikosi ya ugumba rafiki kwa wewe unayependelea nguo za ndani zilizokwishavaliwa na wengine.
Hata wanaoombea nyumba za kupanga baada ya kuhamia sio wajinga.
Hata wanao kagua magari kutoka Ulaya yanayoingia nchini wanafanya hivyo kwasababu wanajua ni used(yametumika tayari) japokuwa sisi huyaita mapya, kitu kilichotumika hakina uhakika wa usalama KAMWE!Dunia yetu hii ina mambo mengi sana tusioyajua, ni Mungu pekee ndiye anaweza kutuepusha na mabaya hayo!
MWISHO! Muafrika hawezi kuepuka kitu cha mtumba, lakini anaweza kukitumia kwa tahadhari kwa ajili ya usalama wake.