Mwanafunzi wa Form Four Aanguka na Kufariki Baada ya Kugundua Mpenzi Wake ambaye ni Mwalimu, Ana Mke
Wakazi wa Kaunti ya Kakamega, nchini Kenya, walipatwa na mshtuko na huzuni kubwa kufuatia tukio la kuhuzunisha lililomhusu mwanafunzi wa Kidato cha Nne; inaripotiwa kuwa alianguka na kufariki dunia baada ya kugundua kuwa mwalimu aliyekuwa naye katika uhusiano wa kimapenzi alikuwa tayari ameoa na ana watoto.
Kulingana na taarifa za eneo hilo, msichana huyo alikuwa amejenga uhusiano wa karibu sana na mwalimu huyo, akiamini kuwa uhusiano wao ulikuwa wa kweli na kwamba hatimaye ungesababisha ndoa baada ya yeye kumaliza mitihani yake ya KCSE.
Inadaiwa kuwa alikuwa na matumaini makubwa kuhusu maisha yake ya baadaye, akiamini ahadi alizopewa na mwalimu huyo, ambaye alidhani alikuwa hajaoa na alikuwa na nia ya dhati katika uhusiano wao.

