NILIITWA MKE, KUMBE NILIKUWA MCHEPUKO WA KUDUMU
Jina langu ni Zaituni, mkazi wa mkoa wa Morogoro, mji wa kasoro bahari. Kwa miaka kumi na tano, maisha yangu ya mapenzi yamekuwa ni mfululizo wa kudanganywa na wanaume walioolewa. Kila mwanaume aliyekuwa anakuja kwangu, alikuwa akidai kuwa hana mke, lakini punde tu tukiingia kwenye mahusiano mazito, nagundua kuwa ana familia yake.
Nilichoka kuitwa “mchepuko” na nilikuwa natamani sana kuitwa mke wa mtu halali. Nilifikisha miaka 38 nikiwa nimekata tamaa kabisa. Nilihisi nina laana ya kuwa mwanamke wa pembeni maisha yangu yote.
Hofu ya kuchelewa kupata watoto ilinitesa sana, maana nilijua kuwa umri wangu wa uzazi unakaribia ukingoni. Kila nikimuona mwanamke aliyeolewa akiwa na mume wake, nilikuwa nahisi wivu wa ajabu na kulia.
Nilijaribu kwenda kwa waganga wengi hapa Morogoro lakini hakuna aliyeweza kuniondoa kwenye hiyo laana ya kuwa mchepuko. Nilianza kujitenga na watu na kuishi maisha ya siri kwa sababu nilihisi aibu. Nilikuwa naona kama kila mwanaume ananitazama kama chombo cha starehe tu na si mwanamke wa kuwekwa ndani kama mke.
Nilikubali tu kuamini katika Mungu, ndipo niliwaendea Viongozi wa Dini wakanifanyia Dua kadhaa, na hatimaye Nyota ya Ndoa ikang’aa, na sasa mimi ni Mke wa Mtu jamani.

