USIUE KILA NYOKA
Nyoka ni mdudu anaeigwa sana na majini kwahiyo unaweza kuona nyoka lakini hakika akawa si nyoka wa asili. Kwasababu hata majini hujifananisha na nyoka.
Lakini pia nyoka hutumiwa na makundi ya wachawi kama silaha. Kwa maana nyengine nyoka hutoa muonekano wa kiumbe mwenye utisho ndio maana humtumia.
Kwahiyo haishauriwi kuua kila nyoka kama hajaonesha muonekano wa madhara mbele yako. Salama zaidi ni kufukuza nyoka na sio kuua moja kwa moja hasa nyoka ambae hujui mazingira yake yalivyo.
Kuna baadhi ya koo pia hutumia nyoka kama kiwakilishi cha mizimu yao. Hivyo wanapomuona nyoka wa aina fulani humuheshimu kana vile wameona mtu mbele yao.
Cha kujifunza kwenye somo hili, nyoka hapigwi ovyo unaweza kujitumbukiza kwenye mzozo na matatizo na majini maisha yako yote. Kwasababu ukimdhuru mwenzao hushambulia kwa haraka kama chui mwenye njaa.
Chanzo: Abdulrazaki Issa

