Sababu 3 Kwanini Ukifikisha Miaka 27 Unatakiwa Kukata Mazoea na Wanaume wa Watu!
Miaka 27 ni umri wa utulivu, kutambua thamani yako, na kujenga misingi ya maisha ya baadaye kwa hekima. Ikiwa bado una mahusiano ya karibu na wanaume wa watu, huu ni wakati wa kujitathmini na kujiondoa kwa sababu hizi saba.
(1) Wanaume Wote Siriasi Wanaotaka Kuoa Huuliza Kabla ya Kutongoza
Mwanaume siriasi na muoaji akitaka kumtongoza mwanamke kitu cha kwanza atauliza, “Huyu vipi?”
Sasa kama watu kila siku wanakuona na waume za watu, moja kwa moja watamwambia, “Hapana, huyo anadanga.” Ikimaanisha hata kama hujalala naye, hata kama huna mpango naye — ni rafiki tu — lakini jamii inakuona naye, inawezekana hata mke wake analalamika, hivyo kila mtu anakuona mdangaji. Waoaji wote wanakukimbia.
(2) Watu Wanajua Ni Mwanaume Wako
Hivyo Wanakunenea Mabaya
Ukiwa na mwanaume wa mtu, watu wanaokuzunguka wanajua — hata kama hujawahi kusema. Wanakutazama kwa jicho baya, wanakusema nyuma ya pazia, na wanaume wanaokufuatilia wanakata tamaa kwa sababu wanahisi tayari “umeshachukuliwa.”
(3) Unakwamisha Baraka Zako Kwa Kujihusisha Na Ndoa Za Watu Wengine
Ukipandikiza maumivu kwenye ndoa ya mtu mwingine, usitarajie furaha ya kweli. Mateso unayosababisha leo kwa mke halali, yanaweza kurudi kwako kwa namna nyingine. Usihatarishe baraka zako kwa mapenzi ya haramu. Kumbuka hata kama hulali naye lakini ile tu kuwa karibu naye wakati mwingine unakuta mwanaume anamdharau mpaka mke wake moja kwa moja inatengeneza maumivu ambayo yanakuja kukukutabaadaye!

