SISI WANAWAKE WAPAMBANAJI, HATUNA BAHATI KWENYE MAPENZI
Sisi wanawake wapambanaji hatuna bahati Kwenye mapenzi hata siku Moja Wanasema wanawake sio waaminifu sio kweli, upande wa wanaume na wanawake ni bahati tu kupata mahusiano ya kweli. Wakubwa zetu wanasema usimkatae mwanaume kwa sababu hana kipato, mkatae mwanaume ambae hana malengo nilijikuta naingia Kwenye majaribu nilikua na mahusiano na mwanaume tulipanga malengo mengi
Mwenzangu mtumishi wa serikali mimi mfanyabiashara nina duka na mkulima pia mwenzangu akapata mtihani mimi ndio nilikuwa natoa pesa Zangu kumsaidia. Anawaambia marafiki zake siwezi kupata mwanamke kama huyo nilipambana nae kwenye changamoto mpaka amekaa sawa akaanza kupunguza mawasiliano ukimpigia anakuwa mkali
Mimi nikaaenda shamba kuvuna mazao niliishiwa pesa nimemuomba akanijibu kwa ukali kama hana pesa nimejikuta Nina maumivu kila siku nimekuwa mtu wa kulia marafiki zake wanamuuliza huyo mwanamke mbona kakupa sana msaada anawajibu kwa ukali wasimungilie Kwenye mahusiano.
Amefungua biashara ila hana mpango na mimi marafiki zangu wananiambia nenda sehemu, huenda kuna mtu katikati anawavuruga ila mimi siamini hilo nahisi ni akili zake tu..

