NIFANYE NINI MAMA MKWE WANGU MTARAJIWA NI MCHAWI?
Mimi ni binti wa miaka 27 sijaolewa ila nina mchumba wangu ambaye kila kitu kishakamilika na mwezi wa 3 Mungu akipenda tunafunga ndoa, sababu ya kuja kwako ni kuhusu Mama wa mchumba wangu, Mama mkwe wangu, watu wananiambia ni mchawi na sijui ni fanye nini. Wiki iliyopita Mchumba wangu alifiwa na Baba yake mzazi, kwakua nishatambulika kwao na ndugu zake tunaelewana vizuri nilimsindikiza.
Tukiwa kwenye msiba kuna tetesi zilikua zikienea kua Mama mkwe wangu ndiyo kamuua Baba mkwe, watu walikua wakiongea namna alivyokua akimtesa kishirikina na mambo mengine mengi. Mimi sikuyatilia maanani kwani nilijua ni kazi ya watu kusema. Lakini baada ya msiba wakati najiandaa kuondoka alinifuata shemeji yake na Mume wangu yani mke wa Kaka yake. Mume wangu kwao wapo saba, wakike mmoja na wanaume sita na mume wangu ndiyo wamwisho kwao hivyo ndiyo wa mwisho kuoa pia.
Yule Dada aliniambia maneno ambayo yalinishangaza na kuniumiza sana mpaka kufikia kutaka ushauri wenu. Alinimbia kama naolewa na ninataka mtoto katika maisha yangu basi nihakikishe nazaa kabla ya ndoa na si baada ya kuolewa. Aliniambia kua kufunga ndoa na wanaume wa ile familia ni sawa na kufunga kizazi kwani huwezi kupata mtoto tena. Nilimuuliza mbona yeye ana watoto akaniambia katika wale watano walioolewa hakuna hata mmoja mwenye mtoto bali watoto wanaowalea ni watoto wakambo.
Anasema yeye analea watoto watatu lakini wote ni wale ambao mumewe kazaa nnje ya ndoa na kumletea kulea. Niliogopa sana na kuamua kuchunguza palepale Kijijini nikaambiwa ni kweli, nikaunganisha na matukio ya nyuma ambayo mchumba wangu alikua akinilazimishiia tuzae kabla ya ndoa lakini mimi nikakataa. Niko njia panda, ndoa wmezi wa 12 kila kitu kishakamilika, je niahirishe, ni bebe mimba kabla ya ndoa vau nimuulize mchumba wangu, niko njia panda ndoa naitaka na mtoto nataka pia!

