KIJIJI AMBACHO HAKINA WANAUME, WAMEPIGWA MARUFUKU KUINGIA
Chanzo: TUKO
Kijiji hicho kinaitwa Umoja kinachopatikana katika kaskazini mashariki mwa eneo la Samburu. Historia ya kijiji hicho ni kinatokana na wanawake 15 waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono waliodhulumiwa na wanajeshi wa Uingereza. Lengo kuu la kujengwa kwa kijiji hicho lilikuwa kutoa usalama kwa wasichana waliokuwa wakikimbia ukeketaji (FGM) ambao ni suala kuu la linalozua wasiwasi nchini licha ya kuharamishwa.
Nyumba za kijiji hicho zimezingirwa na miiba na kupakwa samadi sawia na zingine eneo la Samburu ila wanaume hawaruhusiwi kijijini humo. Tangu kuanzishwa kwake, kijiji hicho ni hifadhi kwa wanawake, kutoka kwa jamii ya Samburu na kwingineko, ambao wanakimbia ukeketaji, dhuluma ya nyumbani na ndoa za mapema.
Kulingana na Rebecca Lolosoli, ambaye ni mwanzilishi wa kijiji cha Umoja, wazo la kuanzisha jamii ya wanawake pekee lilimjia wakati alipokuwa hospitalini akipokea matibabu kutokana na kichapo alichopokezwa na kundi la wanaume. Lolosoli alipokezwa kichapo hicho kama onyo ya kuthubutu kuwahamasisha wanawake Wasamburu kuhusu haki zao hatua ambayo ni kinyume na mila za jamii hiyo.
Umoja sasa ni kijiji kilichostawi chenye karibia familia 40 huku wanawake wakijichumia mapato kupitia kwa kuwauzia watalii shanga na kutoka katika kambi iliyoko karibu. “Ninajivunia sana kuishi katika kijiji hiki kwa sababu sasa hakuna anayenisumbua, na mume wangu hatanishambulia hapa,” Lolosoli alisema katika mahojiano na ABC News. Hata hivyo, Kijiji cha Umoja bado kinakabiliwa na changamoto tumbi nzima kutoka kwa wanaume wa eneo hilo ambao huwaibia ng’ombe wao kila mara.
Kando ya ya hayo, Lolosoli hajafanikiwa kabisa kuwafungia wanaume nje ya kijiji chake kwani kuna baadhi ya wanawake ambao bado wanadumisha uhusiano na wanaume kutoka nje ya kijiji. Licha ya changamoto zilizopo, kijiji cha Umoja kinasalia kuwa kijiji cha kipekee nchini Kenya na salama kwa mamia ya wanawake na wasichana wengi wa Samburu.


1 Comment
Hey there are using WordPress for your blog platform? I’m new to the blog world but I’m trying to get started and create my own. Do you require any coding knowledge to make your own blog? Any help would be greatly appreciated!