NILIKULA NAULI YAKE MARA TATU KUMBE NI MJEDA
Episode 11
“Vipi shoga hizi pesa unazozoa hapo chini ndo zangu mie π” Tausi aliongea huku akiachia kicheko
“Hebu tulia kwanza usichukue hata hiyo buku π” Nilimshikiria mkono uchu wake wa pesa naujua
“Usitake kunitapeli hata kidogo π”
“Acha kujipa matumaini hapa, huyo bwana hajakuelewa pamoja na uzuri wako huo βhii pesa inaenda kutafuta demu mwingine…..cha kukuhurumia sana nitakupatia shilingi afu thelathini π”
“Jema wewe naujua utapeli wako vizuri π€£ kwahiyo umenileta hapa kama kitega uchumi chako nipe hizo pesa niende kukinyoa vizuri kwa ajili yake”
“Sijui huamini lakini ukweli hajakuelewa π” Nilimuambia rafiki yangu kisha ni kampatia shilingi elfu 30
Sikutaka story naye, niliingia mtaani kutafuta chombo kwa ajili yake…. nilitafuta huku na kule lakini sikupata hata mmoja.
Nikiwa nimechoka zangu nilirudi ghetoni kwangu kupumzika ubaya ubwela bhana kama atanichinja kama mbuzi wa kafara mie sina siogopi π₯±
Nilipanda zangu kitandani kulala, kabla hata sijapumzika zangu vizuri, mlango uligongwa.
Mie huyu nilienda zangu kufungua mlango nikiwa nimevuta mdomo π nikijua ni Khalid
Nilishtuka baada ya kukutana na Mama Monica anayeogopeka hadi na ndege π©
*Kuja hapa mbwa wewe, hili presha lote ni dalili tosha ya ukorofi π₯Ά….kwanini ulimtapeli Kijana wangu na hata ukawa unakuja kwangu kuomba dawa?…kwani hukujua kama mie hapa ni Mama yake β” Mama Monica alinifokea akitaka kuniweka kibao
“Najua tu Tausi ndio amekuambia hizi habari, huyo mbwa hana kifua hata kidogo π©… naomba unisamehe halikuwa lengo langu kumtapeli, kama ningejua ni Kijana wako wala nisingeweza kufanya huu ujinga π”
“Unataka kuwa Kuku wa Mayai au kuku wa nyama π₯΄ naomba ujichagulie mwenyewe”
πππππ Niliangua kilio kwa sababu sikuwa na maneno mengine ya kumuambia Mama Monica
Kabla hajanipatia kitisho kingine, mlango uligongwa.
Nilienda kufungua kwa haraka, kidogo nilitabasamu baada ya kumuona Khalid π
“Ni kitu gani nyie wawili mlikuwa mnazungumza π vipi upo hapa kumpa dawa ili nisahau utapeli alionifanyia?”
“Khalid unafika mbali sasa, Mimi huyu ni shirikiane na huyu mjinga kukutapeli wewe π ni heri nijigeuze kuwa Kuku lakini si hiyo fedheha unayo ni tengenezea “
“Huyu Mbwa kuna namna kanikosea sifurahii kuona akizungumza na wewe, naomba usimuadhibu kwa lolote kwa sababu nitamaliza naye mwenyewe β” Khalid alinilinda
“Sawa, Mimi naondoka lakini ukirudi nyumbani naomba uniombe msamaha kwa kudai na shirikiana na huyu ng’ombe π” Mama Monica aliongea kisha akaondoka
“Vipi kazi yangu umefikia wapi π₯΄”
“Kwani lini unarudi kazini π©”
“Una maanisha nini kusema lini narudi kazini π”
“Ukirudi kipindi kingine nitakuwa nimempata Mwanamke mwenye vigezo unavyotaka”
“Weee cheusi mangara hebu niangalie machoni kwanza β”
Nilimuangalia bila kummaliza, huwa sina aibu kiivyo
“Ulinyimwa vyote ukapewa macho π haya macho yangekuwa ni makalio basi ungetisha”
π€£π€£π€£π€£ Nilijikuta ni kicheka, Khalid pia alicheka
“Mbwa wewe hivi tumeshirikiana kucheka π€” Khalid alinibadilikia
“Nisamehe kwa kushirikiana kucheka na wewe β”
“Jiandae twende Casino….kule kuna watoto warembo, naomba ukanisaidie kuchambua…. sifa zote za Bianca unazo naomba usinichezee akili katumie haya macho yako kukodoa vizuri βΉ”
Sikuwa hata na cha kujiaandaa tuliongozana mpaka Casino, kazi yangu ilikuwa ni kutazama mademu wenye sifa kama za Bianca Mnigeria π
“Tafuta vizuri, ukikosa uje usiku K yako ni halali yangu β” Khalid alinitisha π©
Mie huyu nilisikia kuchoka eeeh π
Episode 12
Kila demu niliyekuwa namuonesha alikataa….kuna pisi moja iliingia ilikuwa makini sana lakini hata hiyo aliikataa pia π
“Khalid, mbona muonekano wa Bianca ni wa kawaida sana hawafikii hata pisi nilizo kuonyesha, bhana ee nimechoka kufanya hii kazi wee kama una mpango wa kushambulia K mpaka izeeke hamna shida β na kama utafikisha hii kesi kwa Mama yako niwe Kuku wa Mayai au wa nyama hamna nouma pia π” Nilimvimbia baada ya kuona ni kama ananiendesha hivi bila mpangilio
“Jema umesemaje π”
“Kama ulivyosikia bhana π” Nilijibu hivi ni kijiona mshindi
Khalid hakuzungumza chochote, aliendelea kunywa zake pombe baada ya kumaliza alilipia bill, sikuwa ni kinywa pombe nilimkumbusha alipie bill ya chakula alifanya hivyo β
Sikuelewa kwanini Mwanaume huyu anakuwa mwema kwangu namna hii.
Tulipanda zetu tax nikijua napelekwa nyumbani kupumzika π©
“Tunaenda hotelini kupumzika nataka niifanyie kazi kauli yako ya kushambulie K mpaka izeeke π₯΄”
“Ilikuwa ni hasira bhana kweli na wewe ukachukulia vitu serious namna hiyo π” Nilijichekesha lakini bado Khalid aliendelea kushikiria msimamo wake
Nilijiahidi kuhama Mkoa baada ya siku ya leo kupita. Sijui hata hii ni mara yangu ya ngapi kujipa ahadi lakini ukweli kabisa siku ya leo ikipita ni lazima nihame Mkoa π
Tulifika katika hotel ya Sierra Nevada, ilikuwa ni hotel ya gharama sana.
Sikuamini kama mie Jema cheusi mangara nimeletwa hapa kufanyiwa Shambulizi la K π©
“Kaoge kwanza…” Khalid aliniambia
Niilingia bafuni kuoga huku nikiwaza usalama wangu.
π€ Nilishangaa baada ya kumkuta Khalid amelala tena alikuwa akikoroma kabisa
Heeeh! hii si ndio nafasi sasa ya mie kutoroka π nipo tayari ni kalale stendi pindi kutakapo pambazuka niende zangu Mkoa wowote ule utakao kuwa mbali na Mwanza au Arusha
Nilivaa zangu chapu chapu kisha ni kataka kunyonga kitasa nisepe
“Wee mshenzi rudi hapo ulale π€” Khalid alizungumza
Nilijikuta ni kiogopa zaidi kwa kuongeza makosa π
Nilipanda kitandani kulala, Khalid sijui yukoje bwana, aliniamrisha nilale ukutani β hakuishia hapo aliniwekea mkono wake nisije kukimbia
Wala hata hakuishambulia K yangu kama alivyo niahidi. Sijui hata ilikuaje nilikuja kushtuka nikiwa pekee yangu.
Hakukuwa na dalili zozote za uwepo wake π
Siyo kwamba namjali sana hapana!….nilishika simu nikaanza kumpigia nijue tu mahali alipo.
“Nimepata dharula nipo njiani narudi kazini Arusha. Nikitulia nitakutumia nauli uje….kwaheri nipo busy sana siyo kidogo. Nimepokea tu simu yako kukutoa hofu β” Khalid aliongea kisha akakata simu
π eti anitumie nauli tena pindi atakapo tulia? mbona kama ni changamoto hivi.
Niliendelea kupumzika mahali hapa mpaka nilipojisikia kuamka.
Niliingia bafuni ni kaoga, siku zote maji ya hotelini yanakuwaga matamu kupita maelezo.
Nilienda kwa Mangi kwanza kupumzika β japp ni muongo lakini huwa ananipa burudani sana kwa maneno yake
“Weee naye imekuaje tena hivyo, yaani Tausi kanisimulia ujinga wako mpaka nimesikia kutetemeka π” Mangi alinicheka
“Nyie wote waongo π….sasa kama kanitangaza kwako si ulipaswa ukae kimya, na atanitangaza sana kama aliniibia bwana wangu mtaa mzima ukajua basi sasa hivi nitakuwa na mtihani β”
“Na utakuwa na mtihani kweli kweli, kasema atapita nyumba moja baada ya nyingine π€£”
“Hebu nipe soda ya baridi nijipoze koo langu β” Nilifunga mjadala kwa namna hiyo
Nikiwa nimechora zangu nne wazungu wanaita four, moyo wangu ulilipuka baada ya kumuona Tausi akiwa na Mama Monica π©
Navyo muogopa huyu Mama sababu ya madawa yake nilihisi mkojo unapita kidogo kidogo
“Wachaa wee naona upo unapoza koo lako ili upate nguvu za kutapeli Watoto wa watu π” Mama Monica hakuniacha salama baada ya kuniona
Kabla sijajitetea kwake simu yangu iliita, hakuwa Khalid ila niliamua kuvunga
“Hello Khalid π” Kusema hivi tu Mama Monica alivunga kama hana ugomvi na mie
Episode 13 & 14
“Okay sawa nikipata muda nitaenda kumfikishia ujumbe lakini ingependeza kama utampigia mwenyewe, poa bye π€” Nyie watu nilivunga kama naongea na Khalid kumbe mtu aliyenipigia simu mwanzo alikata kitambo tu baada ya kuona na zungumza pumba
Siyo Mangiπ³ Siyo Tausiπ³ siyo Mama Monicaπ³ wote walinikodolea macho….
“Kwahiyo ulikuwa unaongea na Khalid” Waliongea kipamoja utadhani waaimbaji wa ya moto bendi π
“Eeh kuna maelekezo alikuwa ananipatia”
“Yananihusu mie π” Mama Monica aliuliza
“Ndiyo….π©” Niliongopa
“Sawa, subiri ni chukue vitu muhimu twende zetu nyumbani β” Mama Monica alichukua vitu vyake kisha akanipa ishara tuondoke
Tausi naye alikuepo nyuma kama mkia
“Weee naye unaenda wapi π Mimi na weye tushamalizana siwezi kukupatia nafasi hata kidogo umkaribie Kijana wangu β” Mama Monica aliachia dongo
Mie huyu niliangua kicheko ndani ya moyo, sikuamini kama Tausi alienda kujipigia debe kisa Khalid π€£
Tausi aliondoka kwa aibu, mie hata sikuwa na habari.
“Huko nyumbani na Wageni hebu tuzungumze hapa haraka haraka, huyo Khalid kakutuma uniambie nini maana simu zangu huwa hapokei ni mpaka ajisikie π”
“Ugomvi wangu na wake usiingilie tofauti na hapo ataacha kabisa kurudi nyumbani π€” Niliongopa, nilimuona Mama Monica kapoaa
“Wala Mimi na wewe hatuna ugomvi, acha niwahi Wageni wangu βila jitahidi kukaa mbali na Tausi ni muongo sana kanisimulia kitabu chako chote ni kasalia nimeshika moyo” Mama Monica aliongea kisha akasepa
Nilishusha pumzi π€ kwa uongo nilio zungumza.
Sikutaka kujipa tabu, nilienda zangu ghetoni kwangu kupumzika
Baada Ya Siku Mbili Kupita β
Khalid alinitumia nauli shilingi milioni mbili π©. Sikuwa na jeuri tena ya kula hela zake. Nilifanya mpango wa kupata visa, mbwa mie sijawahi hata kupanda ndege. Kipindi namrusha roho enzi zile najiita Daktari Jema nilikuwa najiona wa kishua sana ingawa nilikuwa na feki maisha π€
Baada ya kila kitu kukamilika mie huyo nilivaa kijanja zaidi.
Nilitamani mtaa mzima wajue kama napanda ndege siku ya leo lakini walikuwa wamelala π
Muda wote nilikuwa na chati na Khalid na hata nilikuwa na mtumia picha kama ushahidi.
Nilifika Jijini Arusha kwa mara ya kwanza, mbwa mie nilishuka kwenye ndege nikiwa sina presha la moyo hata kidogo β
Kabla hata sijapiga simu Khalid mwenyewe alinipungia mkono, nilitembea kwa haraka kumkimbilia sijui nilipatwa na kitu gani niliteleza ni kadondoka chini π©
Episode 15
Niliona aibu nyie, jeje langu jeupe lilishika uchafu π£
“Sasa hapo umejikwaa kwa lipi na huku hakuna kitu cha kujifanya ujikwae π€ na nani kakuambia uvae viatu virefu namna hiyo, kwani ungevaa raba tu ingekuaje π” Khalid aliachia cheko
Mie siyo mtu wa kukasirika hovyo ila kwa cheko lake Ilinibidi ni kasirike
“Karibu Arusha….π€” Khalid aliongea akiwa bado na dalili za kucheka
“Mama Monica ana kusalimia…” Niliongea ili aachane na vicheko vyake
“Utakaa huku wiki moja β” Aliongea akijitia hajasikia kuhusu salamu za Mama yake
Sikutaka kumkumbusha tena, kwa pamoja tuliingia kwenye tax iliyotuijia
Muda wote shingo langu lilikuwa dirishani ni kishangaa mandhari ya Jiji la Arusha β
Nilijikuta ni kianza kupata hofu kutokana na sehemu tuliyokuwa tunapita π©
“Tunaelekea wapi π”
“Naenda kukuchinja, wewe si ni bingwa wa kula pesa za watu, β”
“Huwezi kunifanyia hivyo nina imani na wewe π” Nilijichekesha
“Una imani na Mimi?….na huku siyo Nabii π na kuchinja kweli nimedhamiria mbwa wewe π€”
πππ niliangua kilio baada ya kuona Mwanaume huyu hana utani na Mimi hata kidogo
“Acha kutupigia kelele una mchanganya dreva β” Khalid alinisisitiza
“Basi hata niongee na Wazazi wangu tu kabla hujanifikisha huko machinjioni mbwa wewe π”
“Mie mbwa?….badala ya kunibembeleza unaniita Mbwa π”
“Ni kubembeleze kwa lipi? na kubali nilikula nauli yako lakini na wewe si ulinitumia π kuliko unitishie naomba uniache nirudi Mwanza, hata bila kunipatia nauli nitafika”
Khalid alikaa kimya, hii ilinipa mawazo kwanini Mwanaume huyu kaamua kukaa kimya badala ya kunijibu π€
Moyo wangu ulichanganyikiwa zaidi baada ya kuingia kwenye Kambi ya Wanajeshi
“Kuliko unilete hapa nifanyiwe shambulizi la K na Wanajeshi wote hawa ni heri uniue…π”
Khalid aliendelea kula buyu, dreva tax alisepa zake baada ya kutufikisha.
Mie huyu nilishikwa mkono na Khalid, ni heri hata angekuwa anaongea basi ningejua kuna usalama kati yetu π”
“Hiki ndio kinyumba changu, si unajua tena hapa ni Kambini ni ngumu kumiliki nyumba kubwa β”
“Ndio kusema haunichinji π₯Ί” Niliuliza baada ya kuona anaongea vizuri
“Mjinga kweli wee cheusi mangara Mimi nilikuwa na kutania tu π”
“Utani gani huo fala wewe π” Niliongea huku machozi yakiniporomoka,
“Pole mamy, endelea kupumzika mie bado masaa yangu ya kazi hayajaisha. Nitafurahi kama leo nitakula chakula chako π”
π Niliishia kukodoa macho, imekuaje tena naitwa Mamy na huku nilipewa kibarua cha kutafuta Mwanamke mwenye sifa kama za Bianca
Kilichonitisha zaidi ni pale aliponipiga busu la mdomoni kisha akaniambia baadae π nilijikuta ni kilia kabisa. Kwamba ndio tumekuwa wapenzi tayari au ni nini ana maanisha
Inaendelea π₯