NILIKULA NAULI YAKE MARA TATU KUMBE NI MJEDA
Hadithi Ya Kweli
Episode 01
Basi mwenzenu mie sikuwahi kufikiria kama ipo siku nitakuja kuwa kubwa la Matapeli π€£
Njaa mbaya sana jamani π sijui hata nilijifunzia wapi huu uhuni ila nilijipata tu nimefungua akaunti huko Facebook kisha nikajiita Madam Jema π.
Kisura changu hiki kibovu sikuta nikianike kwenye mtandao, nilichofanya niliingia kwenye akaunti ya Dada mmoja hivi wa Nigeria ni kachukua picha zake π
Hakuwa wa moto sana, picha zake zilikuwa ni za kawaida tu sema alikuwa na sura, umbo pamoja na rangi wa chocolate π
Jema mie nilikuwa na lisura langu fulani hivi, acheni tu nyie ndio maana nimeamua kuwa tapeli π€
Kila nikipost picha au vijimaneno vyovyote kuna Kaka mmoja jina lake anaitwa Khalid alikuwa anajituma sana kucomment na kulike π
Mie huyu nilipata shauku ya kufatilia kuhusu yeye.
Nilisikia hasira kwa sababu akaunti yake haikuwa na chochote, yaani hata profile yake ilikuwa na picha ya njiwa, jina lake tu ndio lilinifahamisha kuwa ni wa kiume π€
Aliacha kuwa ana comment kwenye picha zangu, yaani zile za Mdada wa Nigeria akaanza kuwa ananichatisha Messenger π
Sikuwa na kaa online mara kwa mara hivyo tulijikuta tukibadilishana namba β
Khalid alihisi mie na maisha mazuri kutokana na muonekano wangu feki π
Aliamini Mimi si mtu wa njaa lakini laiti angejua kila jioni huwa najipitisha kwenye nyumba za starehe kama bar na Macasino makubwa ili nionekana kwa Wanaume hata asingekuwa ananiita tajiri π
“Jema, unafanya kazi gani mrembo” Khalid alinitupia swali kati kati ya maongezi
“Nitafanya kazi gani my wangu tofauti na kupasua vichwa vya binadamu π….mie ni Daktari jamani” Niliongea huku ni kijichekesha
“Okay, una miaka mingapi Mamy “
“Kwa kukadiria naweza kuwa na miaka mingapi”
“Ulivyo na kisura kama cha mtoto nashindwa hata kubahatisha π” Khalid aliongea huku akijichekesha
“Jamani, miaka yangu ni 25 tu π€” Niliongea kwa kuremba sauti, masikini mie na uzee wangu huu wa miaka 28 hadi niliona aibu kujigamba
“Mtoto mdogo kweli halafu mafanikio kishazi…. anyway nimefurahi sana β”
“Khalid unafanya kazi gani”
“Mimi ni Mfanyabiashara tu, leo naweza kuwa Tanzania kesho China au Ufaransa kwa kifupi si mtu wa kutulia”
“Kwahiyo kwa sasa upo wapi”
“Nipo, Arusha….lini utakuwa free nikutumie nauli uje”
Heeee! mie huyu moyo wangu ulishtuka sana baada ya kusikia nauli π±
“Jema mbona kimya Mamy”
“Nilikuwa napiga hesabu hapa, nina kama siku nne hivi za mapumziko hivyo kama utaweza kutuma nauli fanya hivyo, ila mwenzio sipendelei kupanda Basi π” Nilijishaua
“Nauli ninayo tuma ni ya ndege Mamy, kwa uzuri wako huo huwezi banana kwenye Basi kama ndizi kwenye mkungu β…. nitume kwenye hii namba au. Halafu usiwe na shaka nitatuma na pesa ya saluni”
Mie huyu moyo wangu ulisalia kudunda tu badala ya kuzungumza π©
Episode 02
“Jema vipi mbona kimya Mamy? nimeuliza nitume kwenye namba ipi π” Oyaah nyie tapeli Mimi niliulizwa kwa mara ya pili
“Kuna ujumbe nilikuwa nafatilia kwenye simu….okay, tuma kwenye namba hii” Nilijitia sina presha na nauli yake
Tobaaaaa nyie π€ kuna watu wanapesa jamani au ni kwa sababu sijawahi kumiliki laki tano.
“Jema Mamy umeiona pesa niliyokutumia?” Niliulizwa
“Ahsante umetuma laki tano, ngoja nifanye booking ya ndege mapema….kesho nitakuwa hapo Arusha β” Nilimhakikishia
Tulipiga story mbili tatu kisha ni kakata simu.
Sikutaka pesa ilale kwenye simu, siku hizi watu wana tabia ya kurudisha miamala β
Niliingia ndani ya kijora changu kisha ni kavaa zangu sendo za mkopo. Siku ya leo sikulichosha tako langu kulitikisa kisa na maana nionekane kwa Wanaume π₯΄
Laki tano niliyotumiwa na Khalid ilinipa kichwa kupita maelezo
“Wewe huyo leo unatoa lakini nne na nusu π³ Dada wa M-pesa aliniuliza
“Mbona pesa ndogo hii my wangu π”
“Hebu nipe hiyo namba ya mganga wako haiwezekani π”
“Mbwa wewe nipe changu mapema ni kapumzike na si kunidhalilisha mbele za Watanzania π”
Nilichukua changu kisha ni kaondoka, pesa iliyosalia kwenye simu ilikuwa ni kwa ajili ya salio si unajua tena tapeli mie sitakiwi kuishiwa bando β
Mida ya usiku niliongea na Khalid kama kawa, nilimhakikishia uwepo wa safari siku ya kesho
“Natamani uje umevaa nguo uliyokuwa umejiachia kwenye picha ya jana π€”
“Sina mazoea ya kurudia nguo ila kwa ajili yako nitafanya hivyo, please naomba nilale sasa ili kesho asubuhi niwahi kuingia kwenye ndege β”
Khalid wa watu ni muelewa, hamuwezi kuamini nilipambana kutafuta picha ya Mwanaume yoyote yule wa kishua huku Facebook nimposti kama marehemu Mjomba wangu π©
Sikutaka kuweka picha za Watanzania ni kihofia kukamatwa. Bahati nzuri nilipata picha ya Mwanaume wa Sudan.
Nilitafuta picha yake moja iliyokaa kitajiri zaidi ni kapost FB “R.I.P Anko wangu mzuri ππππ΅
Nilifanya hivi nikiamini Khalid ataona.
Kulivyo pambazuka tu asubuhi, Khalid alinipigia simu akanipa pole
Mie huyu tena nilibana pua kabisa nionekana na mafua sababu ya kulia
“Ahsante …. naomba ni kupigie baadae π” Nilikata simu nikijitia na uchungu kupita kiasi
Nina muda mrefu sana bila kula chips ya mayai π niliamua kujitoa out. Sikuwa na shobo na hawa Wanaume naowatia machoni.
Kama nitawekeza akili yangu FB nina uhakika nitapata pesa nyingi zaidi ya hapa β
Sikutaka kujisahau hata kidogo, kuiba pesa ya mtu ni dhambi na muda wowote unaweza kupigwa zongo….sikutaka kuvua nguo mchana kweupe.
Baada ya kumaliza zangu kula chips na kasoda kangu ka baridi. Nilipanda bajaji, sikuona shida kusema naenda kwa Mtaalamu mwenyewe anajiita funga funga π
“Pisi kama wewe unaenda kwa Mtaalamu?…ni kitu gani umekosa π₯΄” Dreva bajaji aliniuliza
“Weee Kaka mbona kwenda kwa Mtaalamu ni jambo la kawaida tu….au wewe ni mtoto wa Nabii maana hata kuvaa kwako hauna tofauti na walokole β…..ongeza mwendo kabla sijatumiwa upepo wa kisulisuli ni kashindwa hata kukulipa pesa yako”
ππππ Dreva bajaji alivunjika mbavu. Tulitumia saa zima kufika kwa Mtaalamu.
Ilinilazimu kujitanda ushungi vizuri hasa baada ya kumuona jirani yangu. Mwenyewe ni muongo hatari sikutaka tujuliane hali π
Mtaalamu mwenyewe alikuwa taratibu kama kobe, yaani alitumia muda mwingi kusikiliza Mteja Mmoja.
Nilishusha pumzi baada ya jirani yangu kufikiwa, kidogo niliuachia uso wangu upate upepo π
Huyu hakukaa sana alitoka mapema bila hata kugeuka kushoto wala kulia. Sikumjali, mie huyo niliingia kueleza shida yangu β
Episode 03
“Una matatizo mengi weye kama nitaanza kuyataja yote tutakaa hapa siku tatu β lakini kama upo na haraka kama mwenzio aliyetoka waweza sema hilo moja linalo kutia presha π₯΄” Mtaalamu aliniambia
“Nimekula nauli ya Kaka Mmoja nimekutana naye tu FB, njaa hizi ni mbaya sana Kamanda. Nipo hapa unisaidie kinga nisije patwa na baya π” Niliongea kwa kutia huruma
Nilitarajia huyu Mtaalamu atacheka kama wale wengi cha ajabu alinitazama kwa umakini sana π₯΄
“Huko nje kazi ni nyingi sana, kwanini umechagua kuwa tapeli weye π€…ni kama umejileta mwenyewe hapa nikugeuze kuwa kuku wa mayai βpesa ni ngumu sana acha kuibia watu sitasikiliza shida yako ” Heee! Mtaalamu alinigeuka akataka ashike kibuyu chake anigeuze kuku wa Mayai π
“Unakataa kusikiliza shida yangu kisa mie siyo pisi kali π…. siyo kosa langu kumtapeli wallah sitarudia” Nilibembeleza
“Kwahiyo unataka kusema Mimi huyu nina upendeleo?…mbona una kasirisha mizimu mbwa wewe π€… okay, nitafunika kombe Mwanaharamu apite siku ya leo βfanya kuondoka hakuna jambo litakupata kwa utapeli ulioufanya, natumaini hautarudia tena”
Niliondoka nikiwa na hasira π€ Mtaalamu huyu anajitia Malaika wa mwanga. Sikutaka kusumbuana naye. Mtaani kwetu kuna Wataalamu kishazi β
Nilimkumbuka Mama Monica aliyewahi kumtibia marehemu wifi yangu.
Nilichukua bajaji ni kaenda kwake kujielezea π€. Mama wa watu hakuwa na baya, kwanza huwezi kujua kama ni Mtaalamu kwa jinsi anavyoishi kwenye mjengo wa maana.
Alinipatia dawa ya kuzuia mabalaa, hakuwa na choyo hata kidogo ni kama alikuwa ananibariki kazi iendelee π
Nilimpatia chake kisha mie huyu ni karudi zangu nyumbani. Tobaaa nyie Khalid alikuwa kapiga simu zaidi ya mara tano. Vile ilikuwa silent, isingekuwa rahisi kwangu kusikia
Nilishika simu yangu ni kampigia, moyo wangu ulikuwa una dunda mno bila sababu ya msingi π imagine hata simu haikuwa imepokelewa
“Hello Jema”
“Samahani nilikuwa nimelala ndio naamka π€§” Niliongea kwa kutia huruma huku nikipiga chafya ya uongo
“Nipo Mwanza, nimekuja kwa dharula tu nielekeze mtaa wako nije kukusalimia β”
π΅π΅π΅π΅ Nilisikia kuchanganyikiwa
“Sina nguvu hata za kuelekeza na wala sitaki kumuona mtu yoyote kwa sasa π Mjomba wangu mie ndio alikuwa kila kitu kwangu. Nikikaa sawa nitakuja tu” Niliongea kwa kuomboleza
“Nitakutumia basi picha yangu hata uione tu sura yangu β”
“Usinitumie kwa sasa vile sauti yako inavutia nahofia unaweza kunichanganya moyo wangu ni kashindwa kuomboleza π sitaki unitumie picha pindi msiba utakapoisha nitakuja kukuona, vyovyote utakavyo kuwa Mimi nitakupenda tu…..Kijana au Mzee kwangu sina baya” Niliongea
“Okay kuwa na amani Jema wangu, Mimi sina shida katika hili…” Khalid aliongea kisha akakata simu alidai yupo bize
Ni kama alikausha koo langu kwa maneno yake, nilivaa zangu kijora kisha ni kaelekea dukani kwa Mangi kuchukua soda ya baridi kabisa, si mnajua tena nipo na kibunda π
Mmmmh π leo dukani kwa Mangi kuna Mjeda alikuwa amekaa tena akisoma zake gazeti. Sikutaka shobo naye kabisa kwa sura langu hili hata sikutaka kujidhalilisha
“Baby wangu Mangi nipe soda ya baridi kabisa nipoze koo langu π” Niliongea
“Mmmh wewe huyo leo una kunywa soda basi tutarajie mafuriko π”
ππππ Mie huyu nilichukua soda huku nikiangua kicheko, sijui ilikuaje….soda iliniponyoka ikadondokea kwenye buti la Mjeda ambaye hata sikumsalimia π©
Episode 04
“Sa… samahani π” Niliongea huku ni kijichekesha
Duuh huyu Mjeda hakuwa na story na mie alisogeza tu buti lake kimtindo π kisha akaendelea kusoma zake gazeti.
Mie huyu nilivyo jaliwa jeuri pia niliokota soda yake, niliitikisa kimtindo ni kaona haifai β
“Nipe soda nyingine….”
“Wacha weee huyo Mwanaume uliyempata utamfilisi π” Mangi aliongea huku akijichekesha
“Wee koma kukariri kila Mwanamke anayekuja hapa dukani kwako ana hudumiwa na Mwanaume, wengine tunajipambania wenyewe kwa akili zetu π”
“Kwa wewe sikatai, maana tangu nije hapa sijawahi kukuona unaongozana na Mwanaume big up sana β”
Tukiwa tunaongea story za hapa na pale, Mjeda mwenyewe aliondoka baada ya simu yake kuita
“Boss usisahau kuniletea lile dude π” Mangi aliongea na hata ni kaona kama anajipendekeza
Mjeda mwenyewe hata hakumjibu zaidi ya kumpungia mkono π kama Mwanasiasa vile.
“Mwanaume kujipendekeza na kuomba omba vitu kwa Wanaume wenzio ni ujinga wa hali ya juu π₯΄” Nilimchana
“Huyo ni Mtoto wa Mama Monica, ni jamaa yangu sana wala siyo kwamba najipendekeza π”
“Mama Monica huyu Mtaalamu wa madawa π”
“Eeeh huyo huyo ndio Mama yake β”
“Sasa ndio avimbe π₯΄”
“Kamvimbia nani?…wewe si ndio umemkuta hapa ulipaswa umsalimie π”
“Akwende zake bhana hata ningemsalimia sidhani kama angeitikia π€”
Baada ya kumaliza zangu kunywa soda nililipia kisha ni kaondoka.
Nikiwa natembea Khalid alinipigia simu. Sikutaka kumpokea kwa sababu nilijua kama nitafanya hivi nitapata presha tena nikiwa barabarani β
Niliiacha simu ikaita mpaka ikakata, wakati nakata kona nilikutana na Mama Mama Monica
“Niambie Jema, umeweza kuona mafanikio hadi sasa π”
“Sijapokea ujumbe wowote wa vitisho kutoka kwake, hii inanipa nguvu aisee π€”
“Endelea tu kula pesa zake hakuna kitu anaweza kukufanya, mie mwenyewe nilivyo kuwa kama wewe nilikula sana nauli za Wanaume π”
“Wewe huyo ulikuwa unakula nauli π”
“Acha tu, ila siku Kijana wangu alalamike kuna Mbwa imekula nauli weee nitamgeuza kuwa barabara π”
“Kijana wako mwenyewe ndio huyo Mjeda nimemuona kwa Kaka Mangi hakuna mtu anaweza kula nauli yake π€£ mwenyewe hacheki”
“Na kweli hachekagi, mie mwenyewe tu huwa hatucheki…. unaenda wapi saizi”
“Naenda nyumbani ni kalale kidogo”
“Usipende kulala sana wewe bado Binti, ukilala lala hovyo bahati zitakupita β, baadae nikampikie mwanangu”
“Haya Mama Monica mwenyewe unaye ogopeka hadi na ndege wa angani π” Nilimwaga sifa
“Wee mtoto una balaa kwaheri bhana π” Mama Monica aliongea akizidi kutembea
Nilipofika ghetoni kwangu ndio nilipata akili ya kumpigia simu Khalid
“Jema kesho narudi Arusha, nilitaka tuonane lakini kwa kuwa umesema upo bado katika maumivu makali nitakapofika nitakutumia nauli, tafadhali naomba tuonane hata kwa siku moja tu. Navutiwa na urembo wako, tafadhali sana π” Khalid alinibembeleza
ππ Jamani nauli nyingine tena inataka kutumwa.
“Sawa ukifika nitumie nauli nitajitahidi kuja, siyo kujitahidi ni lazima nije….utatuma kwa namba hii hii ngoja ni lale kidogo β” Niliongea kwa upole jamani, baada ya Khalid kukata simu sikuamini kabisa.
Niliamini dawa za Mama Monica zina nguvu kuliko kawaida. Sikutaka kuendelea kulala, nilivaa suruali na tisheti nilishika njia kwenda kutoa ushuhuda π€
Episode 05
“Mama Monica kiboko ya matatizo sugu pita hapa ni kuone, kama ni vyombo vichafu nitaosha, leo nitakuwa Mfanyakazi wako π” Niliongea kwa makelele
π΅ Badala ya Mama Monica kujitokeza alikuja Kijana wake Mjeda tena akiwa kabeba kibegi bila shaka alikuwa anasepa
“Shi….shikamoo Braza π΅” Nilijikuta nikimsalimia
“Marahaba…..” Duuh jitu hili liliitikia kama halitaki hivi kisha likasepa
Mie huyu tena nilibetua zangu midomo π kama ni jeuri mie mwenyewe ni bonge la jeuri, dharau kishazi zimelala kwenye hii kichwa
“Huyo Mtoto ana gubu jamani kitu kidogo tu ananuna….hapo kaenda kulala hotelini kesho anapanda zake ndege anarudi kazini π” Mama Monica alilalamika
“Toto kama hilo si unaroga tu kwanini upate tabu π na dawa unazo”
“Nitaroga wote lakini siyo Kijana wangu…acha akalale zake hotelini π”
“Sikuwahi kujua kama una Mtoto wa kiume, hivi anaitwa nani vile π€”
“Ukiachana na Monica huyo ndio Mtoto wangu wa kwanza, anaitwa Khalid β”
“Kina Khalid wote ni wa pole na watumaji wazuri wa nauli huyu wa kwako alipaswa kuitwa Ngoswe π”
“Acha ujinga nisije kukugeuza msukule π… niambie hilo jambo lililokuleta, maana makelele yako niliyasikia”
“Dawa zako naona zinafanya kazi, kama kesho atatuma nauli nitakuletea pesa ya soda β”
“Bhana eeeh usiniambie anataka akutumie nauli tena π€”
“Anaonekana kuwa na pesa nyingi, acha anisaidie sina kazi hapa mjini ya kunifanya nitambe, hii itakuwa ni nauli yake ya mwisho kuingia tumboni mwangu mie huyu sitaki lawama tena π”
“Kula nauli kadri uwezavyo hakuna mtu wa kukugeuza chura wala mayai ni hofu yako tu π”
Tulipiga story za hapa na pale kisha ni kaondoka, nyie watu saa kumi na mbili juu ya alama shilingi milioni moja iliingia kwenye simu yangu π΅π΅π΅, presha ilipanda aisee
“Jema nimekutumia nauli please naomba usiache kuja π” Khalid aliongea kwa unyonge huyo
“Usijali my wangu nitakuja naomba nilale kidogo…π” Nilimuaminisha sana kupita maelezo ukweli ni kwamba sikuwa na ratiba ya kwenda Arusha.
Kulivyo pambazuka asubuhi nilizima simu, sikutaka kabisa kusumbuana naye. Afadhali hata ningekuwa na maelezo ya kumpea kichwa hiki hakikuwa na maneno π΅
Nilikaa wiki nzima bila kuwasha simu yangu, sikuwa na mtu yoyote wa kuwasiliana naye hivyo sikujipa presha kabisa β
Kila nikilala ndotoni nilijiona nikifukuzwa na mapanga π©, kulivyo pambazuka asubuhi niliwasha simu bila kujali itakuaje,
Nilitarajia kutakuwa na meseji kibao za malalamiko kutoka kwa Khalid lakini haikuwa hivyo π
Nilihisi ni mtandao hivyo nilitoka nje ni kapanda juu ya mti lakini hakukuwa na text π©
Kuna namna nilianza kupata hofu, nilihisi kuna jambo Mwanaume huyu analitengeneza kwa ajili yangu kama si kuokota makopo basi nitaanza kutembea kwa kurudi nyuma π
Nilishika simu ni kampigia, tobaaaaa nyie π simu haikuwa ikipatikana, nilipiga na kupiga lakini simu haikupatikana. Ilikuwa ni wiki ya kwanza, ikawa wiki pili hadi mwezi β.
Nilikaza moyo ni kaachana naye, pengine amekufa nifurahi mie π€Έ au pengine kaamua kuachana na Mimi kabisa π
Asubuhi moja nikiwa nimelala simu yangu ilivamiwa na meseji, nilinyoosha mkono kivivu vivu π₯±
π±π±π± Nilichanganyikiwa baada ya kukutana na shilingi milioni mbili kutoka kwa Khalid
“Pole, nilipata dharula ghafla nikakosa hata muda wa kukuambia usije Arusha. Naomba ufanye juu chini uje tafadhali”
ππ€Έππ€Έππ€Έππ€Έ Mie siyo bingwa wa kuruka sarakasi ila kwa jinsi Khalid alivyo ni furahisha Jema mie niliyekuwa na lala naota na kimbizwa niliruka mpaka ni kaumiza mkono wangu.
Sikutaka kupoteza muda, nilivaa nguo kisha ni kaenda kwa Mangi kununua kreti mbili za bia.
Nilitaka kumshagaza Mama Monica π, mpaka sasa naamini nipo salama kwa sababu yake yeye
Nilifika kwake nikiwa na bajaji
“Mama Monica unaye ogopeka mpaka na ndege wa angani njoo nje Mama yangu weye π” Niliongea huku ni kiachia cheko kubwa
Inaendelea π₯