BINTI, JIANDAE KUWA SINGLE MOTHER, UKIWA NA HIZI DALILI
Chanzo: Jamii Forums
Huu ujumbe nawalenga mabinti kati ya umri wa miaka 15 hadi 26 kwasababu ndio ujumbe unaweza kuwasaidia maishani mwao wasije kuingia mkenge wa kuingia mkosi na laana ya kuwa single mother. Sote hadi sasa tunakiri kuwa usingle mother madhara yake ni makubwa sana kwa wanawake wenyewe especially eneo la afya ya akili na mwili lakini pia kwa jamii kwa ujumla, hakuna faida wanayoipata kwa ongezeko la wanawake wanaoishi wenyewe bila wanaume.
Zifuatazo ni dalili ambazo wewe kama binti ukiziona then jua shetani yupo kazini kukuandaa uje kuwa single mother. Na kama utaweza kuziona na kuchukua hatua mapema then kuna uwezekano ukamshinda shetani na kuja kuwa mwanamke ambaye jamii inakutarajia:
1. Ukiona unaishi kwenye familia ya mama tu bila baba kuna uwezekano mkubwa sana wa kuja kuishia kuwa single mother kwasababu ya mfumo wa malezi bila baba huandaa akili yako kukataa mfumo wa familia ya baba,mama na watoto. Kusolve jitahidi kujifunza ni kitu gani umekosa kwa baba kutokuwapo maishani mwako then hakikisha haijirudii kwa watoto wako.
2. Kulelewa na baba mlezi na si mzazi. Kulelewa na baba wa kambo kutakuandaa na mtazamo kwamba ni sawa kuharibu mahusiano na kutafuta mtu mwingine wa kuanza nae upya akulelee watoto. Hiyo zamani iliwezekana kwasababu wanaume walikuwa ma’simp. Miaka hii kuwa na mtoto then ukaolewa ten ani muujiza. Ama sivyo utajikuta nimpira wa kona unagombaniwa na wapenda ngono hadi uchakae ukiwa na watoto 6 kila m’moja na baba yake. Kusolve hii, utakapoingia katika mahusiano kwa jitihada zote uyalinde na kuhakikisha yanafika mbali.
3. Ukiona neno la MUNGU kwako sio maagizo bali ni hobby na vilivyokatazwa kwako vinafanyika bila shida then jiandae kuwa single mother. Wanaume Bible na msaafu upo ndani yad amu zao maana walipewa maagizo na mwenyezi MUNGU ambayo wewe mwanamke hukuwahi kuyasikia. Kosea hata yule mwanaume muhuni atakwambia kwamba hapa unakiuka maagizo ya MUNGU. Suluhu,ukitaka kwenda sawa na wanaume imara, shika maagizo ya MUNGU, sio usubiri umekuwa single mother ndio unaanza kufuata maagizo ya MUNGU.
4. Kabla haujawa single mother kuna vitu ujiulize kabla haujavifanya. Jiulize, je, hiki ninachofanya sasa nitakuwa nakifanya hadi nikifika miaka 60 au 70 huko mbeleni. Ukiona jibu ni hapana then achana nacho, kama jibu ni ndio then kipe priority. Hii itakuepusha na mambo au life trends nyingi sana za foolish age ambazo kuna umri ukifika ukizifanya unaonekana kichaa. Imagine Kajala akichora tattoo, akienda club, akivaa bikini, akibadili wanaume, hivi vitu kwa umri wake ni sawa?
5. Ukiona una matarajio ya kuishi mfumo wa maisha ambao mamlaka ya mwanaume yanakupa wakati mgumu na unahisi maisha ni wewe kuwa na final say bila guidance ya mwanaume kwenye maisha yako then jiandae kuwa single mother kwa nafasi kubwa. Wanaume hawahitaji kuwa kimahusiano na mwanaume mwingine katika mwili wa kike ni aina fulani ya ushoga na wanaume rijali huwa wanachukia ushoga.
6. Kama ndoa kwako ni kitu cha ziada then kwa kizazi hiki jiandae kuwa single mother. Wanaume wanatukuza ndoa kama taasisi muhimu ya kijamii ambayo inawapa validation ya uwepo wao kama viongozi ndio maana wanalipia mamilioni ili kuingia. Sasa wewe ukidharau kitu ambacho mwanaume anakitukuza unatarajia ni mwanaume gani dunia hii atakupa umuhimu au hata tu kukujali kama mwanamke wa muhimu kwenye jamii? Kila sehemu utakataliwa.
7. Ukiona unatazamia kuwa serious na mahusiano kwa maana ya kuchumbiwa na kufunga Ndoa baadae sana yaani kuanzia miaka 30, nakuhakikishia kwa kizazi hiki utakuwa single mother. Wanaume wanajua tofauti ya mwanamke serious na mwanamke serious. Unaweza kufanya biashara katika stage yoyote ya maisha ila kuna muda maalumu wa kuwa mke wa mtu,mama wa familia, hivi vitu ukishafika 30 kutoboa ni mtihani. Kama unabisha jaribu ujionee.
8. Ukiona akili yako inakushawishi kutoa bikra yako kwa mtu ambaye hajakuposa na sio mume wako hata familia haimjui ila tayari umeshaanza kushiriki nae ngono then nakuhakikishia kwa kizazi hiki muda wowote unaweza ingia kundi la usingle mother.
9. Ukiona unawaza kupata mtoto kabla haujajua namna ya kuishi na mwanaume then nisikudanganye, wewe tayari ni single mother mtarajiwa. Kulea mtoto bila baba ni kiungo muhimu sana cha usingle mother.
10. Jitazame wanaume unaotarajia kuwapa nafasi ya mahusiano. Je, unatumia vigezo gani kuwachagua, je ni urefu,rangi, mwili wa mazoezi,pesa na wanachomiliki, familia wanapotokea kipato chao, kabila au uzuri wa sauti yake? Hongera,wewe ni single mother mtarajiwa.
11. Unaamini kuwa miaka kuanzia 16 hadi 26 ni umri wa kula usichana (getting wild and laid) na utakuwa serious kuanzia miaka 30 huko? Kama hii ndio idea yako ya kuishi basi nikushauri tu ukajaze form ya usingle mother mapema ili muda ukifika wa kujiunga na club hii ya masingle mother uwe tayari umeshajaza fomu.
12. Tazama marafiki zako,je, umezungukwa na akina nani? Wadangaji, “single and ready to mingle”,mafeminist, wapenda pesa, wapenda maisha ya gharama, wapenda bata, wasiojua ibada,wanatii amri za MUNGU, kama kikosi chako cha marafiki kina tiki boksi hizi zote au hata baadhi then jiandae muda wowote lolote linaweza kutokea.
13. Unaogopa mwanaume kukutawala na kucontrol ratiba zako kwasababu ni mfumo dume? Vizuri simama na mfumo jike ambao kigezo chake kwa miaka hii ni kuwa single mother. Huko hakuna mtu atakupangia ratiba, utalala na kila umtakae, utazaa na kila umtakae,na utaishi na kwenda popote pale. Utakachokipata kama faida mimi sijui, waulize masingle mother wenzako.
Hitimisho, mwanamke hutengeneza future yake na jamii yake katika umri wa kuanzia miaka 16 hadi 26. Nje ya umri huu ni kutengeneza matatizo huko mbeleni na kutafuta kichaa ambacho hakina ulazima. Ni wajibu wako kama binti kujilinda na kujiweka tayari kuja kukutana na mwanaume ambaye utaweza kujenga naye familia na kupata nae watoto mkiwa ndani ya ndoa lakini muhimu zaidi kuwalea vema kwaajiri ya mustakabali mzuri wa jamii na
taifa.