Baba Askofu na Binti Yake, Wakamatwa Wakiwa Gesti
Majengo, Kaunti ya Vihiga – Drama ilizuka Majengo Jumatatu jioni baada ya mwanamume mwenye umri wa miaka 52, anayeaminika kuwa askofu, kunaswa kwenye nyumba ya kulala wageni na bintiye.
Kulingana na ripoti, mke wa askofu huyo aliarifiwa kwamba mumewe na bintiye walikuwa wameonekana wakiingia kwenye chumba cha wageni. Alikimbilia kwenye nyumba ya kulala wageni pamoja na maafisa wawili wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Hamisi.
Walipofika, tayari umati wa watu ulikuwa umekusanyika nje. Binti huyo, 23, alishutumu vikali umati wa watu na mamake, akihoji ni kwa nini walivamia jumba hilo kwa hasira na kupindukia.
Katika taarifa yake, msichana huyo alieleza kwamba babake alimwomba aende kwenye nyumba ya wageni kwa sababu alikuwa na jambo muhimu la kuzungumza naye. Alisisitiza kuwa hakuna kisichofaa kilichotokea.
Aliendelea kumwita mama yake na polisi “wajinga” kwa kuingilia kati, kuvuruga kile alichoelezea kama kipindi cha kibinafsi cha kujifunza, na kujaribu kumwaibisha baba yake.
Hata hivyo, akizungumza kwa hasira, mke wa askofu huyo alihoji ni kwa nini mumewe alichagua nyumba ya kulala wageni ili kumfundisha binti yao badala ya maeneo mengine salama.
Licha ya utetezi wa binti huyo, askofu huyo alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa madai ya kujihusisha na kitendo kisichofaa na binti yake. Anatarajiwa kufika mahakamani siku ya Jumatano.
Chanzo: vihiga

