Wafundishe watoto wako ustaarabu ufuatao kuhusu CHAKULA wasikuaibishe
Wafundishe watoto wako kuona thamani ya chakula wanachokula kwa kula pasipo kumwaga chini hovyo,kumwaga mezani au kujimwagia chakula na kuchafua mavazi yao. Kuwafundisha watoto kula pasipo kumwaga chini kutawafanya kujua thamani ya chakula kwenye utoto wao na watakapokuwa watu wazima,kwamba chakula kinapatikana kwa jasho kinapaswa kutumiwa kwa umakini kwasababu kuna wengine wanakikosa. Ni ushauri tu!
2. Kula pasipo uharaka, wale taratibu!
Hii itawafanya wawe wastaarabu katika utoto wao na watakapokuwa watu wazima. Lakini pia, watu wakubwa katika nyazifa,utawala au maeneo yeyote Duniani huwa hawapapatikii chakula. Yaani chakula hakiwafanyi kuvurugwa akili na kushindwa kupoteza umakini wao. Kwahiyo,kuwafundisha watoto kula polepole ni kuwaandaa kuwa watu wakubwa baadae. Kula haraka haraka ni ishara ya umasikini, hawapaswi kuzoea tabia hiyo mbaya!
3. Kula na kuramba vidole!
Huu pia sio ustaarabu mzuri. Watu wastaarabu na wakubwa Duniani huwa hawali chakula kwa kuramba vidole vyao. Kuwafundisha watoto wako kula chakula PASIPO KUJIRAMBA VIDOLE VYAO NI KUWAANDAA KUWA WATU WAKUBWA SANA DUNIANI HAPO BAADAE. Kula na kujiramba vidole ni ishara ya umasikini!
4. Kula na kukomba sahani au chombo cha chakula!
Huu pia sio ustaarabu, ni tabia mbaya sana unapokuwa eneo la ugeni utaaibika sana. Kumfundisha mtoto wako kula pasipo kukomba sahani au chombo cha chakula ni kumuandaa kuwa mtu MKUBWA sana baadae. Hakuna tajiri au mwenye nyadhifa kubwa kiutawala anayekula na kuramba sahani. Wafundisheni watoto wenu kuukataa UMASIKINI. Sema Amina.
5. Kula na kuomba UKOKO!
Hii ni ishara ya kutotosheka na kuridhika na chakula ulichokula. Hii ni ishara ya urafi kwasababu ukoko sio chakula! Nakushauri, mfundishe mtoto wako kutokuomba ukoko baada ya kula chakula au kutopenda kula ukoko kwasababu ni ishara ya umasikini (ni kubariki umasikini alionao). Kwahiyo, anapofundishwa kutopenda kuomba ukoko anafundishwa kuwa ukoko sio chakula bali apambane kutafuta CHAKULA HALISI NA KIZURI. Hapo utakuwa unamuandaa kuwa mtu MKUBWA BAADAE. Watu wakubwa katika nyadhifa,matajiri au watu wakubwa Duniani katika maeneo mbalimbali ukoko sio sehemu ya chakula chao. Hawaombi ukoko! Hawali ukoko! Muandae mtoto kuwa mtu mkubwa na sio kuubariki UMASIKINI.
6. Kula na kutokusema asante baada ya kushiba ama kumaliza kula!
Hii ni ishara ya kuthamini aliyemwandalia chakula au kuthamini chakula alichokula. Asante ni ishara ya hekima,ukuu na ustaarabu. Watu wakubwa huwa wanashukuru baada ya kupokea!
USIPUUZIE MAFUNDISHO HAYA. UKIPUUZIA, MTOTO ATAKUAIBISHA SIKU MOJA KWASABABU YA CHAKULA!