WAAFRIKA WENGI TULIZALIWA MASIKINI NA TUNAWEZA KURITHISHA VIZAZI VYETU UMASIKINI KWA SABABU ZIFUATAZO!
1. Wazazi wetu walitufundisha Kupenda PESA ni vibaya!
Hii ni tofauti kabisa na watu kutoka Ulaya(wazungu) na Asia( Wahindi pamoja na waarabu). Wao wanawafundisha watoto umuhimu wa pesa kuanzia utoto wao,kuitunza na kuizalisha. Lakini, Waafrika tulifundishwa kuwa kupenda pesa tutakuwa wezi na vibaka. Jambo ambalo sio sahihi!
2. Wazazi wetu walitufundisha kuwa na Watoto wengi na wake wengi ni UTAJIRI !
Wazazi wetu hawakutufundisha kuwa utajiri ni kumiliki mali nyingi zisizohamishika(ardhi,majumba, mashamba) pamoja na utajiri wa kumiliki vitu vingi vinavyokuingizia PESA na vichache sana visivyokuingiza pesa badala yake WALITUFUNDISHA KUWA NA WAKE WENGI NA WATOTO WENGI NDIYO UTAJIRI. Sio sahihi pia!
3. Wazazi wetu walitufundisha uchoyo na ubinafsi!
Baadhi ya wazazi hawataki kuwapatia mitaji watoto wao,wanawataka wajitafutie wenyewe wakati hawakuwafundisha kutafuta kwasababu walidai pesa ni mbaya. Hii ni kinyume kabisa na watu kutoka mataifa ya Asia na Ulaya ambao wanaongoza kwa UKWASI, wao kurithishana vyanzo vya mapato au kufanya kazi kama familia na ndugu wamoja ni kitu cha kawaida! Afrika, ndugu mkishirikiana kwenye utafutaji hatma yake ni kugombana na kurogana.
4. Wazazi wetu hawakutufundisha kuweka akiba ya pesa kwa ajili ya dharula(majanga).
5. Wazazi wetu hawakutufundisha kuheshimu pesa(Kuitumia kwa kuzingatia bajeti na sio hovyo hovyo).
6. Wazazi wetu hawakutufundisha tunapaswa kukopa ili kuzalisha pesa au mali na sio kwa ajili ya kulipa madeni yanayotokana na utumiaji mubaya wa pesa kwenye ANASA.
7. Wazazi wetu walitufundisha kuwa mtaji wa masikini ni NGUVU ZAKE NA SIO AKILI ZAKE!
MTAZAMO huu umezalisha masikini wengi sana ambao wamejikuta wakifanya kazi ngumu na nzito kwa juhudi sana lakini matokeo yake wameishia kwenye umasikini wa kupindukia. Mtaji wa masikini ni namna anavyoitumia akili yake ipasavyo kuzalisha pesa na kuitunza.
Mpendwa, watoto wako hatma ya maisha yao inakutegemea wewe. Wafundishe thamani ya MALI NA PESA ili wasijidharau na kuukumbatia umasikini. YEYOTE YULE ANAWEZA KUWA NA MALI AU UTAJIRI, WAFUNDISHE MAARIFA SAHIHI YA PESA ILI WAKUTUNZE KWENYE UZEE WAKO!