VIMEPITWA NA WAKATI LAKINI VINAMPATIA HESHIMA MWANAMKE!
Kuna vitu vingi sana ambavyo sasa vinaonekana ni vya kipuuzi lakini vilimpatia heshima mwanamke. Mwanamke yeyote yule akiamua kuvizingatia vitairudisha heshima yake na kuipandisha juuuuu sana mawinguni!
INASIKITISHA SANA KWA MWANAMKE ANAYEPUUZIA MAMBO HAYA AMBAYO ANAYAITA YA KIPUUZI.
1. Kuvaa Brazia.
Baadhi ya wanawake hawapendi kuvaa Brazia wakidai ni ushamba pasipo kujali kuwa ndiyo heshima ya mwanamke. Mwanamke, utamaduni wa kuvaa Brazia sio wa kuupuuzia, kuyaacha wazi matiti hakumpi heshima mwanamke hata kidogo.
2. Kuvaa nguo ya ndani.
Kuvaa nguo ya ndani kwa mwanamke(chupi) sio utamaduni wa kuupuzia kwasababu humpatia heshima mwanamke lakini pia humfanya atembee kwa kujiamini wakati wote.
3. Kuvaa under skirt!
Huu ni utamaduni wa Bibi na mama zetu ambao wanawake wa sasa wamepuuzia na kuzifanya under skirt kuadimika sokoni kwasababu hazina wateja. Lakini, kuvaa under skirt kwa mwanamke humuongezea heshima na kujiamini, haipaswi kupuuzwa.
4. Kumnyonyesha mtoto.
Wapo wanawake hukwepa jukumu la kumnyonyesha mtoto wakidai wanaharibu maumbile ya vifua vyao. Wanawake wa aina hii ambao huwalea watoto kwa kutumia maziwa ya ng’ombe kwa makusudi ni wapuuzi sana na hushusha thamani yao bila kujua.
5. Kutopenda kujifungua kwa njia ya upasuaji(Kujifungua kwa njia ya kawaida).
Wapo wanawake wapuuzi wenye afya njema hupenda kujifungua kwa makusudi kwa njia ya upasuaji ili kutoharibu sehemu zao za KIKE. Wanawake wa aina hii ni wapuuzi sana na hushusha thamani yao pasipo kujua. Utamaduni wa mwanamke ambaye ni mzima kiafya ni kujifungua kawaida!
6. Kutokuwa na tabia ya Kuogopa UCHUNGU na kutopenda kubeba mimba.
Baadhi ya wanawake warembo ambao ni wavivu wa UZAZI NA WENYE KUOGOPA KUHARIBU MAUMBO YAO huwashawishi waume zao kupandikiza mbegu zao za kike na za kiume kwa mwanamke mwingine ambaye atawazalia mtoto kwa malipo na makubaliano maalumu. Mwanamke huyo aliyekodiwa hupandikizwa mimba kitaalamu na kisha kubeba mimba kwa miezi tisa na kuingia leba wakati ukifika. Akijifungua, hupokea pesa zake na kusaini hati ya kutomdai mtoto kuwa ni wa kwake. Huu ni utamaduni wa kisasa na wa kipuuzi, mwanamke halisi hujenga heshima yake kwa kubeba ujauzito miezi tisa na kuingia leba kwa ajili ya kujifungua.
7. Kutokuwa na tabia ya kutopenda kupika, kufua na kuosha vyombo.
Kuna wanawake warembo ambao hawataki kufanya kazi za nyumbani wakidai kuwa wanaharibu kucha zao ndefu za mikono yao zilizopakwa rangi. Nawaambia kuwa tabia hiyo inawaondolea uanamke na kuwashusha thamani kwasababu mwanamke halisi hawezi kukwepa kupika, kuosha vyombo, kufua na kudeki. Mwanamke acha tabia hiyo mbaya mara moja, ni ushauri tu!
JE, UNAFIKIRI NI UTAMADUNI GANI WA ZAMANI ULIOKUWA UKIMPATIA HESHIMA MWANAMKE LAKINI UMEANZA KUPOTEA?