ZIFUATAZO NI SIRI TANO ZA KUISHI MAISHA MAREFU YENYE FURAHA!
1. Puuzia na usipoteze muda wako kwenye vitu ambavyo hauwezi kuvizuia!
KAMWE usiogope kuhusu kitu ambacho hauwezi kukizuia. Hiyo ndiyo maana halisi ya maisha ni FUMBO. Kupoteza muda kufikiria vitu usivyoweza kuvizuia kama vile magonjwa na kifo, utakufa mapema sana ndugu!
2. Jenga tabia ya kucheka(kufurahi) angalau mara moja kila siku!
Hii itasaidia kukuondolea msongo wa mawazo na kukuongezea uwezo wa kujiamini. Ukijiamini, unaweza kufanya jambo lolote chini ya JUA.
3. Wachukie watu kimya kimya, na wafurahie watu machoni pa watu wengine!
Hiyo ni siri nyingine ya maisha ya furaha. Ukimchukia mtu, hakikisha hajui na hiyo ndiyo silaha pekee ya kupambana na adui zako. Hakikisha maadui zako wasijue kuwa wewe ni adui, hata kama wanagombana na wewe jifanye umenyoosha mikono kwao hiyo ndiyo itakuwa rahisi kupambana nao. Lakini pia, Jenga tabia ya kuwafurahia watu mbele za watu, watakupatia vitu ambavyo ni vigumu sana kuvipata kwa juhudi zako ndiyo maana MACHAWA wanafika mbali sana siku hizi, wameweza sana kuitumia farsafa hii. Watu wengi wanapenda kusifiwa mbele za watu na hiyo asili ya mwanadamu yeyote yule!
4. Binadamu hana tabia ya kutosheka na kuridhika hiyo ni asili yake, ndiyo maana ni kawaida sana kumuona tajiri mwenye kila kitu lakini hana FURAHA. Hivyo basi, kamwe hautafurahia maisha yako usipojifunza kuridhika hata kwa kidogo ulichonacho au ulichobarikiwa!
5. Wewe ndiye mwenye wajibu wa kupambania maisha yako kwa asilimia MIA MOJA!
Haupaswi kumtwisha mzigo,
Haupaswi kumtwisha lawama,
Haupaswi kuhitaji huruma,
KWA YEYOTE YULE. Hata Mungu haupaswi kumtwisha mzigo wa maisha yako, yeye hubariki jitihada zako. Siku ambayo utaanza kufurahia maisha yako ni siku ambayo utawekeza jitihada zako zote katika kupambania furaha yako na uchumi wako kwa asilimia mia moja.