NJIA SABA ZA KUWA MTU MWENYE KUJIAMINI
Kuongea hovyo pasipo utaratibu na utulivu kunaweza kusababisha uongee mambo yasiyo ya maana ambayo yanaweza kukuondolea hali ya kujiamini.
2. Kuwa mtu wa kusikiliza kwa makini na kutafakari kwa kina kabla ya kuongea. Hakikisha hauingilii mazungumzo ya mtu akiwa anaongea.
Hii itakusaidia kuongea vitu ambavyo vina uzito na maana ambavyo vitakufanya uheshimike na kusikilizwa jambo ambalo litakuongezea hali ya kujiamini zaidi.
3. Ongea vitu ambavyo unavijua sanaaa au una uhakika navyo. Kama vitu hivyo umefundishwa au umejifunza,hakikisha umefanya mazoezi ya kutosha kabla ya kusimama mbele za watu kuongea. Hii itakufanya ujiamini zaidi na uaminike!
4. Zingatia uvaaji wako,ukaaji wako na namna ya kusimama.
Kama ni mwanamke, hakikisha unavaa,unakaa au kusimama kama ambavyo mwanamke anapaswa kuwa, vivyo hivyo kwa mwanaume. Kutokufanya hivyo, watu watashindwa kukusikiliza na kuzingatia sana kutazama namna ulivyokaa,ulivyovaa au ulivyosimama jambo ambalo litakupotezea hali ya kujiamini.
5. Hakikisha unawatazama watu machoni wakati wa kuongea au kuwasikiliza. Kuwatazama machoni kunakufanya uongeze hali ya kujiamini na kuaminika mbele yao.
6. Epuka kuongea kwa hasira au kutumia lugha isiyo na staha. Kufanya hivyo kutasababisha watu washindwe kukusikiliza au kukuamini jambo ambalo litakupotezea hali ya kujiamini kwako.
7. Kuwa na subira (Mvumilivu).
Kitendo cha kuwa mtu mwenye uharaka sana katika kuongea au kusikiliza kunaweza kukufanya kupoteza mantiki au umakini jambo ambalo litapelekea kuongea vitu ambavyo sivyo au havina maana. Ukikosea katika uongeaji wako,kurekebisha ni vigumu unakuwa tayari umepoteza kujiamini kwako na watu kukuamini.