Nchi tano zilizowahi kuvunjwa kuzalisha nyingine
Dunia ilikuwa na nchi kibao ila nyingine zikaja na kupotea na ndani yake kukaanzishwa nchi nyinginezo nyingi tu.
Tuachane na hizo kibao, hapa tuangalie nchi tano ambazo hazikuwepo ila zilianzishwa kutoka kwa nchi fulani, yaani nchi husika ikapotea na kuanzishwa nchi nyinginezo.
1. Yugoslavia
Hii ni nchi moja iliyokuwa huko Ulaya. Ilianza mwaka 1918 lakini ikafika tamati mwaka 1992. Yaani wakati sisi tunaanzisha mfumo wa vyama vingi, wenzetu walikuwa wanaiua nchi moja na kuzalisha nchi kibao. Ndani yake kukazalishwa nchi saba kama Slovenia, Croatia, Serbia, North Macedonia, Kosovo, Montenegro, Bosnia and Herzegovina.
2.Czechoslovakia
Hii ilikuwa nchi moja kubwa tu huko Ulaya lakini ilipofika mwaka 1992 ikameguka sehemu mbili, ya kwanza ikaitwa Jamuhuri ya Czech na ya pili ikaitwa Slovakia.
3. Austria-Hungary
Hii ilikuwa nchi nyingine ya Ulaya kumeguka. Baada ya vita vya kwanza vya dunia kumalizika, sasa wakaona ulikuwa wakati sahihi wa kuimega nchi hiyo na mataifa mengine kuzaliwa.
4. Prussia
Hii ilikuwa nchi nyingine kumegwa hapo Ulaya. Baada ya vita vya pili vya dunia kumalizika, nchi ikagaiwa kwa mataifa matatu. Taifa la kwanza ikawa Ujerumani, ambayo nayo ilikuwa na Magharibi na Mashariki. Nchi ya pili ikawa Poland na ya tatu Urusi sehemu iitwayo Kaliningrad.
5. Tibet
Hii ilikuwa nchi ya kujitegemea kabla ya kuvamiwa na China. Watu hao wakaamua kuivamia, wakaiteka na kusema kuanzia sasa hakuna nchi inayoitwa Tibet, hii yote imekuwa China japokuwa mpaka leo washikaji wanalilia uhuru wao, wanataka kujitoa mikononi mwa China.